East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

I Think There Is No Need For What They Call First Track, As We People Of East Africa Need To Intermingle And Share Both Our Cultures As Well As Vision.

I Advise Our Leaders To Allow First People To Migrate From One Nation To The Other Untill We Reached A Situation Where The Every Part Of The Block Have The People Of The Same Culture,mindset And Share Some Interest And After That We Can Have A Political Federation Since We Are Together.
But As For Now We Are Not Ready For Political Federation.

Consider A Country Like Tanzania Which Is Politicaly Very Stable And It's Economy Is Getting Stronger With Abundant Natural Resources To Join With A Country Like Kenya With No Enought Natural Resources And Is Experiencing Polotical Instability, It Is Obsiously A Threat To All Tanzanians.
Museveni Question Now, It Is Another Threat For Both Tanzania And Kenya, Look Back The Way President Museveni Has Abused The Ugandan Constitution Just To Run For His Third Term And He Claimed That He Is Aspiring To Become The First East Africa President, You Can Imagine Such Type Of Leader Whom Managed To Change Ugandan Costitution To Be Granted A Role Of Leading East Africa Cooperation Including The Most Beautiful Country Tanzania.

Please It Is So Soon For Political Federation, Let Us Take The Europian Way.

It Me A Concerned East Africa Citizen
 
Hey Waheshimiwa viongozi (decission makers Tanzania)mkumbuke cheo ni dhamana, nataka niwaambie kuwa mmepewa madaraka ya kulinda maslahi ya watanzania waliopo na vizazi vijavyo.Chonde chonde msifikirie maslahi yenu binafsi mtakayoyapata kutokana na huo muungano, ni ya muda mfupi tu na mtawaacha watanzania kwenye matatizo mengi kuliko ya sasa.Mpaka sasa muungano wetu tu unatia shaka,hapo hapo tz ni dampo la bidhaa duni,umaskini ndo kwao,kana kwamba hiyo haitoshi mnataka pia tz iwe dampo la matatizo ya ardhi, ukabila,udini, vita,chuki.JAMANI chonde chonde we need peace.Huu si muda muafaka,ECONOMICALLY are behind,lets have time ,compare and contrast gains and losses, we will get right answer.PLEASE, WE ARE NOT READY TO JOIN EAF!
 
Some 50 people have been killed in the past month in clan violence over land in Kenya's western province, local government officials say.
Spokesman Abdul Mwasera told the BBC more than 30 people had been arrested in connection with the clashes.

Hundreds of families fled to camps after conflict began during a government land allocation programme.

The government has barred politicians and religious leaders from visiting the area accusing them of inciting clans.

"We have arrested 35 members of the Sabaot lands defence force, a group that is claiming responsibility for this recent fighting and the government has deployed enough security personnel to counter these fighters," said Mr Mwasera.

The Sabaot community lives at the foot of Mt Elgon on Kenya's border with Uganda and some displaced families have fled into Uganda.

The BBC's Muliro Telewa in western Kenya says tension remains high in the area as the disagreement among the clans on how land should be divided intensifies.

Seven schools in the area have been closed following the violence.

Reports say trouble started after some families sold their land and benefited from the government's new allocations at a prime settlement scheme leaving the original squatters landless.

The affected communities now want the government to revoke land allocations to 1,732 families.

President Mwai Kibaki's administration has pledged to resolve land problems across the country which have persisted for more than 40 years.

http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/6317255.stm
 
Sasa kwanini waharakishe hilo suala iwapo wanajua fika sie wagema ulimbo hatuna tunalolijua inabidi wachukue muda katika kuelewesha na pia wasisahau kutupa raia wa Bongo vitambulisho ili tuweze kujuana maana bila hivyo tunaweza kusikia bingwa wa Mnanda anatokea Kenya au Uganda
 
Mie naomba faida na hasara za jumuia hii ili niweze kujijua niko kwa anayejua naomba anitumie kwenye e-mail
asanteni
 
naomba mtu yeyote atakayesoma maneno haya ayasome kwa mkandamizo kuonesha ni jinsi gani hatuwakubali wao((( HATUTAKI)))
 
hawa watu hatuwataki na wote wanaowakubali hawa watu uraia wao nina mashaka nao inawezekana wakawa sio watanzania,kuleni kona Rwanda na Burundi
 
Katika tembea tembea yangu leo hii nilikutana na haya :

Kikuyu.com

Jaluo.com

Ubuntu forum

Lugha inayotumiwa zaidi ni kiingereza na makabila yao.

Nikajiuliza hivi hadi leo watu bado tuko nyuma namna hii, samahani tuko mbele namna hii, yaani tunajali ukabila badala ya utaifa. Kwa masikitiko makubwa sikuweza kukutana na Kenya.com lakini kumbe ipo ilikuwa imepooza sana aka topix.net, lakini bado ni ukabila kabila tu kwa wachangiaji. Sasa kweli hawa ndugu zetu tukiungana wataendeleza uluo wao, ukikuyu wao na ukalenjini wao etc. TUWE MAKINI. ugomvi na mauaji kwa ajili ya ardhi na mengineyo yataanza kuhamia kwetu maana hajafa mtu kwa sababu ya ardhi.
 
Je kuna viongozi wetu weshapewa 10% au nanihii?, mbona nao wanapelkwa puta hivyo?.....

Hili swala wala halina hata majadiliano...WE ARE NOT READY!!! sijui kwannini viongozi wetu hawasikii na wanaharakisha hivyo.
 
Tanzania iJIFUNZE KUSEMA 'NO'
Tanzania ijitoe EAC
Umefika wakati wa nchi ya Tanzania kujifunza kuSEMA 'No!' kwa kujitoa kwenye jumuia ya afrika mashariki (EAC) na kusitisha mchakato wa kupokea maoni ya shirikisho la afrika mashariki; vilevile tu kama Tanzania ilivyoSEMA 'No' kwa COMESA.

Mnamo mwaka 1986, Kenya na Uganda, pamoja na Sudan, Somalia, Ethiopia (na baadaye Eritrea) zilianzisha iliyokuja kujulikana kama Jumuia ya Mashariki ya Afrika -- The Intergovernmental Authority on Development (IGAD) ambayo makao makuu yake ni Jiji la Djibouti. IGAD ambayo Kenya na Uganda zilishiriki kuianzisha, ina jumla ya watu milioni 190. Zikiongezeka nchi za Rwanda na Burundi kwenye IGAD, basi idadi ya watu itakuwa milioni 210. Hii ni idadi kubwa ya watu kuliko ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) yenye watu milioni pungufu ya 100. Ni kwa nini Kenya na Uganda ziondoke kwenye IGAD jumuia yenye idadi kubwa ya watu (ngonjera: soko kubwa, utandawazi, ndiyo dunia ya kisasa kuungana kama vile Ulaya), na badala yake zije kwenye EAC ambayo ina watu wachache zaidi? Sasa hivi IGAD ina nchi saba, zikiongezeka Rwanda na Burundi, zitakuwa nchi tisa; kwa nini wasiendelee na Jumuia yao, badala yake wang'ang'anie EAC yenye Tanzania?

Tanzania ipo Jumuia ya nchi za Kusini (SADC). SADC ina nchi wanachama 14, wenye idadi ya watu milioni 235. Watu milioni 235 tulioko SADC ni wengi zaidi ya mara mbili kuliko walioko EAC. Kwa nini Tanzania iondoke SADC na kwenda EAC?
COMESA ambayo Tanzania ilijitoa, ina jumla ya idadi ya watu milioni 405, kwenye nchi wanachama 20, idadi ya nchi ambayo ni mara saba zaidi ya nchi tatu anzilishi EAC. Angalau COMESA ni mmojawapo wa mifano michache inayotia moyo kwamba bado Tanzania ina ubavu wa kusema 'No' kwenye medani za kimataifa.

Zamani, enzi za Nyerere, Tanzania ilikuwa inajua kuSEMA 'No!' Tanzania haikuwa inapokea amri kutoka kokote wala kwa yoyote nje ya Tanzania. Nchi nyingine haikuthubutu kuiamrisha Tanzania kufanya jambo lolote, halafu nchi hiyo ikachekewa tu. Ndiyo maana Tanzania ilikuwa 'mstari wa mbele katika ukombozi wa Kusini mwa Afrika' hata kama nchi za Magharibi zilikuwa hazipendi.

Tanzania, enzi za Nyerere, iliSEMA 'NO!' kwa wanyonyaji na mabeberu. Tanzania 'ikakata mirija' ya mabepari kwa kutangaza azimio la Arusha. Mabepari wakaondoka, na uchumi wa nchi ukawa mikononi mwa nchi na wananchi. Kumbuka thamani ya Shilingi ilivyokuwa! Shilingi tano kwa dola moja, enzi za utoto wa mwandishi huyu. Ndiyo maana sarafu ya shilingi tano ikaitwa "Dala". Mabasi ya binafsi yalipoanza kufanya kazi, yakawa yanatoza nauli ya shilingi tano tano ('dala' 'dala') badala ya shilingi tatu tatu za mabasi ya UDA. Kwa sababu Tanzania iliSEMA "No!" kwa unyonyaji.

Likaja shirika la IMF na masharti yake. Tanzania ya enzi za Nyerere ikaSEMA "No!" kwa masharti ya IMF. Tanzania ilijali utu wake. Ilijali wananchi wake. Haikuangalia 'makunyanzi' ya nchi nyingine bali ililinda utu wake. Wengine wataSEMA Tanzania enzi za Nyerere ilikuwa 'Maskini Jeuri'.

Kusema hivi siyo kwamba sera za sasa za uchumi wa Tanzania zifanyike asilimia mia moja kama zamani, bali jambo kubwa linalosemwa hapa ni kwamba angalau Tanzania zamani iliweza kuSEMA 'No'. Tena iliSEMA 'No' kwa nchi za magharibi, na nchi za mashariki zilipoanza kuleta mambo yasiyoeleweka. Haikukubali kitu chochote mradi tu kimesemwa na 'wakubwa' nje ya Tanzania.

Kati ya SADC, IGAD, COMESA na EAC, nani mwenye uwezo mkubwa wa kupambana na utandawazi? Bila shaka siyo EAC. Kwa vile EAC ni mradi unaofadhiliwa na nchi za magharibi – hivi mtu atakufadhili kukuongezea nguvu za kupambana naye? SADC ilizaliwa kutokana na ushirikiano wa nchi zilizokuwa mstari wa mbele wa ukombozi kusini mwa Afrika. IGAD ilizaliwa kutokana na malengo ya kuunganisha nguvu ya nchi za Kenya, Uganda, Somalia, Ethiopia, Djibouti, Eritrea na Sudan ili ziweze kukabiliana na changamoto mbalimbali. Kwa hiyo muda uliokwisha kupotea EAC unatosha. Tanzania ijitoe EAC, ibakie SADC. Kenya na Uganda zibakie IGAD. Kwa Rwanda na Burundi "zitapendezea" zaidi IGAD kuliko SADC, kutokana na historia ya ushirikiano wa muda mrefu na IGAD.

Utaona wazi kwamba kwa kujiunga na EAC, nchi hizi haziongezi nguvu za "kupambana na utandawazi" kama ambavyo wanataka tuamini. Wala siyo "umoja ni nguvu" -- kwa vile ni kujitoa kwenye jumuia kubwa, zoefu, zenye nchi nyingi na mafanikio ya muda mrefu, pamoja na idadi kubwa ya watu – kigezo ambacho ndicho kibwagizo cha ngonjera za kuanzishwa EAC. EAC ya sasa ni utengano, na wala si umoja. Ili EAC ishamiri, lazima Kenya na Uganda ziondoke IGAD, muungano wenye idadi ya watu milioni 190, ili ziunganike na Tanzania itakayoondoka SADC yenye watu milioni 235, ili kuanzisha EAC yenye watu milioni zisizofika 100.

Kama pana maamuzi yenye matokeo mabaya kuliko yote kwa Tanzania na Watanzania, basi ni hili la kujiunga EAC ya sasa hivi. Hakuna mantiki yoyote ya Tanzania kujiunga na EAC.

EAC ipo kutokana na nchi za Jumuia ya Ulaya (EU). Jumuia ya Ulaya imeziamuru nchi za Afrika kujigawa kwenye mafungu mafungu ("EPA") kama vile jumuia ya afrika mashariki, ili makusudi ziweze kuuza chochote huko Ulaya. Amri hii ni badala ya 'Makubaliano ya Cotonou' baina ya nchi za Afrika na za Ulaya. Hii ni amri. Kwa nchi zenye kujua kuSEMA 'No' bado zitauza vitu vyao Ulaya, lakini si kwa 'mteremko' kama wa zile ambazo zitatii amri bila maswali. Ndiyo maana Jumuia ya Ulaya 'inafadhili' mradi wa shirikisho la afrika mashariki EAC. Lakini hata SADC ni "EPA" inayokubalika kwenye EU. Ni kama vile Tanzania "inaogopa" kuonekana vibaya kwa EU, ndiyo maana inashindwa kusema wazi kwamba haina muda wa kupoteza EAC.

Leo hii upepo umegeuka. Imefikia hatua ya kukubali 'kila kitu' kinachosemwa na nchi za nje. Mashindano ni kupewa sifa nje ya Tanzania, hata kama sifa hizo hazisaidii kitu chochote, wala hazina maana. Kusifiwa nje ya nchi ndio limekuwa lengo kuu. Haiwezekani tena kuSEMA 'No' kwa lolote lile, mradi tu 'Yes' yetu itaongeza sifa nje ya nchi. Lengo, sera, na kila kitu kinakusudia kupata sifa NJE ya Tanzania. Ndiyo maana Tanzania inayumbishwa itoke SADC iliyoianzisha enzi za Nyerere, iende EAC. Siku hizi hatusikii tena "NO!" zikisemwa kwa nchi za nje. "No!" zinazosikika, ni zile zinazopayukwa kwa sauti kubwa kwa Wananchi wa Tanzania. Hizo zitatekelezwa hata kwa mtutu wa bunduki. Lakini si kwa raia wa kigeni (wajiite vyovyote – wawekezaji, wakimbizi, ma-'TX' – jina lolote, hao hawawezi kusikia 'No' yoyote toka kwa watawala Watanzania.

Wengine wanaunga mkono EAC kwa kuogopa kuonekana "wanaabudu" mipaka ya Tanzania ambayo ni matokeo ya mikutano ya wakoloni iliyofanyika Ulaya karne ya 19 katika kile kijulikanacho kama "the scramble for and partition of Africa" ambapo Waafrika hawakupewa fursa ya kushiriki. Wako radhi wapoteze utaifa wao kwa vile tu waonekane "wameendelea" kiasi cha kutaka "kuchora upya" mipaka ya Afrika.
Kama si sababu hiyo, basi wanaunga mkono EAC ili waonekane "siyo waoga", watu wanaoogopa ushindani kwenye shirikisho mbele ya macho ya wanaopigia panda shirikisho la afrika mashariki. Hoja inayopigia mstari kwamba Watanzania ni wavivu, wasioweza kujilinganisha na watu wowote wengine.

Wengine wanaogopa kutoa maoni kwa vile wanasema uamuzi umekwishafikiwa, na maoni yatakayotolewa hayatabadili chochote. Wengine wanadhani kutoa maoni ya kupinga kuhitimisha taifa la Tanzania kwa kujiunga na EAC, maana yake unapingana na Rais wa nchi, unapingana na CCM. Si "mwenzetu" wewe. Yaani mambo ya enzi zile za "zidumu fikra" za watu fulani. Fikra yoyote nyingine haina nafasi. Karne ya 21 bado watu wana mawazo hayohayo. Hawaamini kwamba kuishauri serikali, mawazo tofauti na serikali inavyofikiri, siyo uhaini wala kosa la jinai. Wengine wanajificha kwenye kauli "itolewe elimu ya kutosha kwa wananchi", "muda hautoshi kukusanya maoni", "shirikisho lichelewe kidogo, limeharakishwa mno", au "viongozi tuwe makini kwenye shirikisho", badala ya kusema wazi shirikisho la afrika mashariki halina tija yoyote kwa Tanzania wala Watanzania.

Baadhi wanaunga mkono kwa vile wamekata tamaa kwamba "wenyewe" wameshafikia maamuzi kwa hiyo kusema hakutasaidia kitu. Haifai kukata tamaa kwamba "wameshafikia uamuzi" tayari. Hao waliofikia uamuzi ni akina nani? Japokuwa mwenendo ni kama unaelekea kuwa namna hiyo, lakini fursa bado ipo ya kuliokoa taifa la Tanzania lisiangamie kwa kujitumbukiza kwenye shirikisho la EAC. Kwa hapa Dar es Salaam, Tume "ya kukusanya maoni" imefanya mikutano yake yote ya kukutana na wananchi pembezoni mwa mji. Ile iliyofanyika mjini ilikuwa kwa makundi maalum, ambapo mwananchi tu wa kawaida kama vile mimi na wewe hangeweza kuhudhuria bila kuonekana ameenda kufanya fujo. Yaani ukitaka kujua wananchi wa Dar es Salaam wanawaza nini kuhusu kufutwa kwa taifa lao, maeneo ya kwanza na ya pekee kwenda ni Vijibweni, Chanika na Bunju!? Hiyo ndiyo Tume ya "kukusanya maoni".

Bado yapo mawazo kwamba Watanzania tupo duniani kwa ajili ya kutatua matatizo ya watu wa nchi nyingine. Tuliumbwa ili tuwe mshumaa wa kuangazia wengine huku sisi tukiteketea. Kama jambo lolote litakuwa la manufaa tele kwa watu wa nchi nyingine, lakini hasara tupu kwetu kama hili shirikisho la EAC, basi lazima tulikubali.

Hivi sasa wapo watawala wetu ambao hawaamini kwamba Mtanzania anaweza kitu chochote, au anastahili chochote zaidi ya raia wa kigeni, hata kama Mtanzania huyu yumo nchini mwake. Haiwezekani kuSEMA "NO" kwa raia wa kigeni wanaowinda na kuua wanyamapori. "No" ni kwa wenyeji tu. "No" itasemwa na nani kwa 'wawekezaji' ambao kila kukicha migogoro haiishi kugombana na Watanzania wenyeji?

Kasumba hii imefikia pabaya – hatuamini iwapo Watanzania tunaweza kubakia na Taifa letu la Tanzania, na kujitawala wenyewe – mpaka tufute uhuru wa nchi yetu tuukabidhi wa raia wa kigeni ili watutawale, kupitia kwa 'soko la pamoja' la EAC, au kupitia kwa 'shirikisho la afrika mashariki'.

Hatutaki tena kutambua kwamba JWTZ inatosha kutulinda – bali tunataka ifutwe kwa kuunda Jeshi jipya la Afrika Mashariki, ndani ya shirikisho, ambalo litachanganyika na majeshi ya Rwanda, Burundi, Uganda, Sudan, Kenya, na pengine Somalia.

Kwenye shirikisho, tunategemea kuwarudisha nyumbani mabalozi wote Watanzania, na kuwakilishwa badala yao na wale wa kutoka popote EAC. Watawala wetu hawadhani Watanzania wanastahili kuendelea kuwakilisha Watanzania wenzao huko nje. Ndiyo maana sasa hivi tunapata kigugumizi kuSEMA "NO" kwa shirikisho ambalo maana yake Wizara ya Mambo ya nchi za Nje ya Tanzania itafutwa – badala yake ianzishwe Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa wa EAC.

Mawazo ni ya hivyohivyo kasumba kwa masuala ya fedha, elimu, polisi na mengine ambayo yatakuwa ni ya shirikisho; na bado tunajiuliza iwapo tuseme au tusiseme "No" kwa wazo la kuondolewa mamlaka ya kutawala maswala yote ya fedha, elimu, polisi na mengine yatakayoamriwa kwenye bunge la EAC.

CONTINUES TO PART II
 
Kwenye shirikisho la afrika mashariki Rais wa Tanzania hatakuwa tena Amiri-Jeshi Mkuu – ana jeshi la kuliamrisha ndani ya shirikisho? -- itamlazimu afanane na Rais wa serikali ya wanafunzi au Rais wa TFF asiye na majeshi. Urais ni jina tu au ni yale 'yatokanayo' na jina hilo? Hata kwa hili jamani midomo inakuwa mizito kuSEMA "NO!"?

Kwenye shirikisho la afrika mashariki, bunge la Tanzania litakuwa halina tofauti sana na bunge la watoto ambalo maamuzi yake hayana nguvu yoyote. Spika na wabunge wa Bunge la Mkoa wa Tanzania wakati huo watakuwa sawa tu na wachezao mchezo wa kuigiza. Maneno yote ya kibunge yatakuwa EAC, ndani ya shirikisho. Kwa sasa waheshimiwa Wabunge wetu 'wanapozwa' na maneno laini kwamba Bunge la Tanzania 'litabakia tu vilevile' kwenye shirikisho ili wasithubutu kuSEMA 'No" kwa EAC.

Walioko kwenye chama tawala CCM, wanashindwa kuSEMA "NO" kwa EAC kwa kudhani shirikisho litakapokuja, CCM itabakia kuwa CCM, chama tawala Jamhuri ya Tanzania. Wanasahau kwamba kwa kuanzisha "Jamhuri ya Muungano wa Shirikisho la Afrika Mashariki" maana yake hakutakuwepo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama hamna Jamhuri ya Tanzania, basi maana yake hakutakuwepo na chama tawala, chama cha upinzani, wala cha mageuzi. Siasa litakuwa suala la muungano wa shirikisho. Kama ambavyo si ruksa kuanzisha chama cha siasa upande mmoja tu wa Jamhuri ya Tanzania hivi sasa, ndivyo itakavyokuwa wakati huo. EAC itakuwa ni nchi moja – pasipoti moja, vitambulivyo vya raia vimoja, Rais mmoja – ambaye kwa kuanzia ni Yoweri Museveni. Kwa vile wote tutakuwa raia wa nchi moja, haitawezekana kumzuia raia mwenzio kufanya shughuli za siasa popote kwenye Jamhuri ya Shirikisho la Afrika Mashariki. Hii ina maana Watutsi wa kutoka Rwanda wataruhusiwa kugombea ubunge Dar es Salaam, wakati ambapo Wazaramo wa Dar es Salaam wataweza kwenda kugombea ubunge Rwanda au Uganda. Je, Hayo ni mambo ambayo hatujui iwapo tunatakiwa kuSEMA 'No'?

Kodi inayokusanywa Tanzania, inaweza na bila shaka itatumiwa nje ya Tanzania, lakini ndani ya Jamhuri ya Shirikisho la Afrika Mashariki kwa kuwa Tanzania itakuwa ni kijimkoa tu cha EAC. TRA itakuwa imefutwa na badala yake kuanzishwa mamlaka ya mapato ya EAC. Kodi za wengine nazo huenda zikatumika Tanzania, iwapo wabunge kwenye EAC ya wakati huo watakuwemo wale ambao zamani walikuwa Watanzania, na wakaweza 'kasi mpya' ya kutwangana mingumi bungeni, kama wenzao walivyozoea. Hili nalo ni la kuvuta pumzi kusita kuSEMA 'No'?

Sasa ni wakati wa kuSEMA 'NO! HATUTAKI! hilo halina manufaa kwa nchi yetu na kwa hiyo hatutaki! Tuwe na msamiati wa hapana! Tusikubali kila kitu, mradi tu wameSEMA Wazungu au wamegawa posho za kushiriki mijadala.

Shirikisho ya afrika mashariki ni jaribio kwenye maisha ya Watanzania ambalo wazi matokeo yake yatakuwa mabaya mno kwa Tanzania na Watanzania.
EAC itamsaidia vipi mwananchi wa Tanzania kupata maisha bora? Tumchukulie huyu mwanakijiji aliyeko Nanjilinji, Kilwa.

*
Yeye maisha yake yataboreshwa vipi na shirikisho?
*
Ni kipi ambacho hakipati sasa hivi, nje ya Jamhuri ya Muungano wa Shirikisho la Afrika Mashariki, ambacho atakipata pindi Tanzania ikisitishwa kuwa Jamhuri na kugeuzwa mkoa mmoja wapo wa mikoa / majimbo ya Jamhuri ya Muungano wa Shirikisho la Afrika Mashariki?
*
Pana ulazima gani wa kufanya MAJARIBIO kwenye MAISHA ya mwanakijiji huyu kuona iwapo ataweza KUISHI Maisha Bora au Bora Maisha baada ya kumletea "ushindani" kutoka nje ya nchi kupitia shirikisho la afrika mashariki?

Watu ambao maisha yao hutumiwa kwenye majaribio ni wale ambao huonekana hawana thamani yoyote machoni pa wanaobuni jaribio. Yaani majaribio hufanyika kwa wale wanaotazamwa sawa tu na wanyama ambao wanaweza kutumiwa kwenye majaribio husika. Ni kweli Watanzania tumeshuka thamani kiasi cha kufanya majaribio kwenye nchi yetu na maisha yetu?

Wanaounga mkono jaribio la EAC kwenye maisha ya Watanzania wanatoa hoja kwamba "msiwe waoga" kufanyiwa majaribio haya. Wengine wamefikia hatua ya kuSEMA kwamba Watanzania ni watu wanaojali sana mambo ya nje kuliko ya kwao. Kwa hiyo Watanzania hawajui kuSEMA 'NO'. Ndivyo wadhanivyo. Na kuthibitisha hivyo wamekuja na wazo la kuSEMA "Watanzania hamuwezi, tena hamfai kujitawala wenyewe – lazima mjiunge na EAC." "Hivi kweli Watanzania ninyi mnajua KuSEMA 'No'?" Ndiyo maana Wabunge walipokataa muswada wa Shirikisho, bado Tanzania ilibakia tu kwenye mchakato huo, kwa vile majirani zetu hawaamini iwapo "No!" inayosemwa na Watanzania inamaanisha kweli "NO!". Hoja ikarudi tena kinyemela, na zile sauti za "NO" hazisikiki tena.

Sasa hivi ule mkataba wa EAC uliopo umerudishwa uandikwe upya. Watawala wetu wameridhia uandikwe upya. Chochote kitakachoandikwa humo nani ana uhakika itasemwa "NO" na watawala wa Tanzania utakapofika wakati wa kusaini? Moja ya mageuzi makubwa kwenye kuandika upya mkataba huo ni kutoa uwezo wa kufikia maamuzi ya mwisho EAC kwa watu walioko kwenye ngazi ya uafisa mawizarani – na siyo mawaziri kama ilivyo sasa, au marais kama ilivyokuwa EAC iliyokufa. Umefika wakati wa kuSEMA 'NO' kwa EAC.

Tanzania ijitoe EAC.

EAC ina tofauti ipi na COMESA? Kwa nini tusifanye kweli ya kuSEMA 'NO' kwa EAC, kama tulivyofanya COMESA?
Wale Watanzania wanajipatia rizki zao kwa sasa EAC, pamoja na wale wanaoishi kwa matumaini ya kunufaika binafsi EAC, serikali ya Tanzania iwafidie pesa zote ambazo wanatumainia kuzipata EAC.

Serikali, na hasa Bunge la Tanzania, lianzishe mchakato wa kuitoa Tanzania EAC. Ni wakati wa kuSEMA 'No' kwa EAC. Vyama vya mageuzi vipo nchi hii? Au vinangojea uchaguzi tu? Yaani hata vyama vya upinzani navyo havina msamiati wa kuSEMA 'NO' kwa EAC? Jambo la kutia moyo ni kwamba tayari wameshaanza kujitokeza viongozi wa vyama vya mageuzi kufanya kazi ya KuSEMA 'NO!' kwa EAC.
Burundi, Rwanda, Kenya, Sudan na Uganda, zinaweza kuendelea na shirikisho lao ndani ya EAC au IGAD kwa kushirikiana na Somalia, Ethiopia, Eritrea na Jibuti wakipenda. Tanzania tutaendelea na SADC. Hapa Tanzania wanaweza kuja kupiga stori tu. Mengineyo yote kwao. Kapu la mjanja, mjinga hatii mkono!

Email: mlenge@yahoo.com
Simu: +255 75 4372902
Blogu: http://mlenge.blog.com
 
Nadhani mjadala huu wa kujiunga kwenye jumuiya hii umeharakishwa mno. Sababu hata hii tume ya kuratibu maoni ya wananchi inafanya kazi mbili kwa mara moja. kuwaelezea watu nini jumuiya ya afrika mashariki halafu kuwa shawishi. ni sawa na kumfundisha mwanafunzi somo jipya na baada ya saa moja unampatia mtihani na unategemea ashinde huo mtihani.

Haya maelezo yanayotolewa hayatoshelezi kuwaelezea wananchi juu ya umuhimu wa jumuiya hii ambapo wakati sisi tunahangaika na masuala ya umeme na kushindwa kudhibiti raslimali zetu wenyewe wenzetu bado wanapambana na masuala ya ukabila pamoja na vita za wenyewe kwa wenyewe, sasa tunaungana wapi na wapi hatuungani. tumeshaona mseveni anaonyesha ishara za kutaka achaguliwe kuwa rais wa kwanza wa shirikisho (tamaa!).

Sisi raia tunaoishi pembezoni mwa nchi tunajua adha za kiusalama tunazozipata toka kwa majirani zetu wanyarwanda na warundi. sasa hawa tukiwaruhusu kuwa sehemu yetu wenyewe tunaelekea wapi kama tu wao wenyewe hawaelewani katika nchi zao wakati huo huo wakiendelea kuhatarisha amani kwenye nchi yetu?

Angalia hivi majuzi ni siraha ngapi zimechomwa moto kule kigoma na karibu zote zimetokea huko kwenye mataifa jirani!Tusipoangalia hapa tumechemka!
 
Jamani
kumbe tumeona shirikisho bado harifaii,tusipoteze mda kupiga soga
tuchukueni hatua za makusudi ku block hawa jamaa wasiendelee bila hivyo watatuunganisha
tulioko bongo tufanyeni kongamano la kukataa, ili wajue hatutaki kweli kweli

yani maviongozi yetu utazania yamelogwa
tulizulumiwa ktk ile jumuia ya 1977 bado yanarudia yaleyale
mali zetu zinatangazwa nchi nyingine yanaona na bado yamekaa kimya,
kazi kudaganya wananchi maisha bora yakukaa gizani? au na sisi wananchi tusiwe wenda wazimu tuwa bwatukie au nasi tumelishwa limbwata??

tunataka nasi tutafute tena uhuru kwa mara ya pili kutoka ktk shirikisho kama walivyo serbia,cosovo,Ugoslavia kutoka USSR
Kama jumuia ilimshinda Mwalimu unadhani hawa waruka njia vinyamkela wataiweza??
yani hata hii jumuia ikiudwa haitapita mda risasi zitalia watu wanataka kujiondoa. kama kakundi kana ona kanaonewa ktk nchi ndogo kama wilaya je?kwenye shirikisho
napenda kuwauliza viongozi wetu ni nani aliye waloga? nisisitize kwa ki BBC who be witched you leaders??
mchawi aliyewaloga ameshakufa? si mkamtafute muombe msamaha ??Harafu murudi kwa Muumba Muombe angalau Busara kidogo??tafuteni busara
yani mnavyonikera natamani hata mtemi Mkwawa afufuke leo tuongozwe naye
kuliko hii minyan'gau isiyopenda kusikiliza wana nchi wanataka nini?
mnatulazimisha ili iweje watu wenyewe mda wa kuishi hapa dunia wenu uko very limited
Aisii mnaudhi sana ,watu wenyewe elimu ni vi bachalor mnadhani mna uelewa mkubwa hadi wa kuamlia watu wote aisii mnakera sana
badala yakushughulikia kuinua uchumi wa tanzania yamewashinda sasa sijui mnataka kukwepa aibu kwa kuwaingiza kwenye shirikisho
kama mmeshindwa kutuletea maisha bora ,bora mg'atuke wapo wanaoweza kutuletea maisha bora bila shirikisho
mnaudhi sanaaaaaaaaaa, mnakera sanaaaa
 
Kenya is a ticking time bomb

Kenya is controlled by the “haves”, and the “have nots” have little or no say.

Getting rich is not a crime but getting rich using the wrong means is not right. Still, it’s wrong for a government to support the rich only and do very little for the suffering poor. I don’t support the lazy poor but a system must be developed to handsomely reward the hardworking poor.

We are a capitalist state where almost everything is turning out to be for the rich. Education, good health, housing, food and economic opportunities.

That’s the reason why the Ndungu, Anglo Leasing and Goldenberg reports gather dust on government shelves since the men listed in them are rich and can afford to buy their freedom.

Despite the rush by the common man to invest on the Nairobi Stock Exchange, it remains a rich man’s playground.

However, the power of the ballot is with the common majority.

Let’s use it wisely.

Kinoti Gatobu
via email
 
mazingira ya ushindani wa kibiashara,kisiasa na kijamii yatarudishwa nyuma na mifumo tofaoti inayoendelea katika nchi wanachama. kenya imetawaliwa na ukabila, uganda udikteta, tanzania mpasuko wa muungono na rwanda na burundi machafuko ya kikabila, yote haya yatakua yetu sote! ni vipi jumuiya hii itasonga mbile wakati wana matatizo yasiyofanana? sitaki sio tu kuharakishwa bali hata kuwepo kwa shirikisho lenyewe
 
i don't if we really need it. frankly speaking this federation is beneficial only to our leaders and mainly political leaders.

Please was it a mistake to choose you as our leaders, if yes then may god forgive us for doing such kind of a mistake, but please Tanzania leaders better not let us enter to that hell called east africa community, kindly requesting don't let us regret our patience onto you.
 
EA FEDERATION is good in some aspect but it needs a clear thinking before signing the contract for the mentioned federation. The coutries concern should make sure:
1. Its people are ready to compete for jobs at the National level (EA Federation). I think some of the countries will loose oportunities while others winning the oportunities.
2. Medium of Communication should be uniform.
3. Restructuring training curriculum
4. Etc.

I propose to have what we call Co-federation ( where the five coutries UG, TZ, Kenya, RWAnda, and Burundi) should remain with their president while sharing some issue with other coutries.
 
Kikwete: Kama si Mkapa leo tungekuwa shirikisho

na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete ameshangazwa na hatua ya baadhi ya wanasheria na wanasiasa kumlaumu yeye kutokana na kuanza kwa mchakato wa kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki ifikapo mwaka 2013.

Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na kamati inayokusanya maoni kuhusu uanzishwaji wa shirikisho hilo, Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Wazo la kwamba tuwaachie wananchi waamue kuhusu shirikisho, lilikuwa ni wazo la Tanzania, wenzetu waliona tunapoteza wakati, waliona viongozi wanaweza kuamua tu kuwapo kwa shirikisho. Nawashangaa sana wale wanaosema eti tumekosea kuwashirikisha wananchi,” taarifa iliyotolewa na Ikula jana ilimnukuu Rais Kikwete akisema.

Aliiambia kamati hiyo kuwa, baada ya tume iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria wa Kenya, Amos Wako kuhusu shirikisho kuja na ‘road map’, “sisi Tanzania tulisema ngoja tuwashirikishe wananchi ili tupate uhakika kwamba wananchi wanaridhika kuwa na shirikisho au la.”

Aidha, katika kile kinachoonyesha kuwa kuna nchi wanachama wanalitaka shirikisho kwa udi na uvumba, Rais Kikwete aliwaeleza wajumbe wa kamati hiyo kuwa, kuna nchi moja (hakuitaja) ilifikia hatua ya kuandaa rasimu ya muundo wa shirikisho bila kuzishirikisha nchi nyingine, achilia mbali wananchi.

“Tulipogundua hili, Rais Mkapa alinituma mimi, wakati huo nikiwa Waziri wa Mambo ya Nje, kwenda Kenya na Uganda, tukawaeleza wenzetu jamani hapana, hivi sivyo tunavyotakiwa kwenda, tukawapa somo, hatimaye wenzetu wakatuelewa. Lakini wenzetu waliona kuwaachia wananchi waamue ni kama vile viongozi tunajivua madaraka,” alisema.

Akionyesha kuwa uamuzi wa kuwashirikisha wananchi hauna lengo la kuwa ghiliba, Kikwete alisisitiza kuwa, maoni yatakayotolewa na wananchi yataheshimiwa, kuzingatiwa na kupewa umuhimu unaostahili.

Akizungumzia kuhusu nafasi ya Zanzibar katika shirikisho, alisema hakuna maslahi ya nchi kama nchi, na kwamba jambo la msingi la kujadili ni namna ya kuisaidia Zanzibar kukuza sekta yake ya uzalishaji ili iwe na bidhaa za kuuza katika soko la Afrika Mashariki.

“Muundo wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki si sawa na ile iliyovunjika ambayo angalau kulikuwa na maslahi kama nchi, hii ya sasa inazungumzia zaidi soko. Tusipoteze muda kujadiliana nani atafaidika vipi na namna gani. Tujadili namna gani tutaisaidia Zanzibar iwe na viwanda, izalishe bidhaa,” alisema.

Alisema suala la msingi la kujadili ni kuwa Tanzania inaingiaje katika ushirikiano huo chini ya muundo wa muungano wake.

Kuhusu hofu ya wananchi wengi kupoteza ardhi na ajira, Kikwete alisema masuala hayo hayatakuwa katika shirikisho, bali yatadhibitiwa na nchi husika.

Rais Kikwete alitoa maelezo hayo licha ya majuzi kukataa kulizungumzia suala hilo, alipoulizwa na wahariri akisema kwa kuwa suala hilo bado lipo kwa wananchi, ni vema wakaachiwa watoe maoni yao kabla ya yeye kulisemea.

Ili kuhakikisha kuwa kamati inakusanya maoni kutoka kwa watu wengi, Rais Kikwete aliitaka kuhakikisha inakutana na watu wengi kadiri inavyowezekana.

“Ningependa pale mtakapofika kwenye makundi kama vile vyama vya siasa, hakikisheni kwamba mnawapata wanachama wengi wa vyama hivyo, badala ya kukutana na viongozi peke yao,” alisema na kubainisha kuwa, lengo liwe ni kupata mawazo mchanganyiko.

Akitoa ripoti ya kamati hiyo, mwenyekiti wake, Profesa Samuel Wangwe, alisema kazi imekwenda vizuri, ingawa kuna changamoto kubwa kutokana na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu suala zima la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema uelewa mdogo, ambao umeonyeshwa hata na wasomi, umeifanya kamati hiyo kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja; kuwaelimisha wananchi na kisha kukusanya maoni na kusababisha ionekane kana kwamba inafanya kazi ambayo si yake.

Utetezi huo wa rais unakuja wakati makundi ya wanasiasa na wanasheria yakionyesha waziwazi kutofautiana na mchakato huo, na kupinga kitendo cha Rais Kikwete kuruhusu hoja ya kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki.

Wengine wamefikia hatua ya kuhoji uhalali wa kikatiba uliompa nguvu Rais Kikwete kuteua tume ya kukusanya maoni kuhusu suala ambalo hatimaye litasababisha kufa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Sasa nataka nimuulize kikwete
kwa mjibu wako kikwete umetuambia viongonzi wenzako
1. Ni madikiteta
2. vi Miungu mtu vya kuona kuwashirikisha wananchi ni kujishusha
kibaya zaidi kuna nchi kati ya Kenya au Uganda inaona viongonzi wa nchi nyingine ni bomu hadi pekee ikaandaa map road
3.kuna nchi piga ua garagaza wanalihitaji shirikisho
Je wewe kama Raisi uko tayari kushirikiana na madikiteta,vi miungu mtu na je?umefanya uchunguzi kugundua kwa nini nchi hizo zinalihitaji kwa udi na uvumba?

kwa maelezo yako yanatosha kufahamu hata wewe una uwalakini wa shirikisho hilo kwanini upoteze mda na pesa nyingi kuunda kamati??
kwa makosa hayo waliofanya viongozi wenzako kwa nini wewe huoni ni sababu tosha kwa kutowangunisha watu wako??

Je umejiuliza kwa nini wanaitaka tz iwemo ndani ya shirikisho??shirikisho si lazima tz, zipo nchi nyingi zingine na si liwe lazima la nchi za afrika mashariki

Jamani kiongozi wetu tumeteseka vya kutosha sasa upuuzi hatutaki na wala kupoteza mda kujishebedua huku na kule walakini ukijua kinagaubaga kuwa

viongozi wenzako ni mafisadi na hawana nia nzuri.
Achana na upumbafu huo tafutia wananchi wako maendeleoa,ulikua umeanza vizuri kweli kweli hadi kimataifa ulianza kupata ujiko sasa hili litakuporomosha mpaka jehanamu
Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom