East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

Number 1: I support kuwa na Shirikisho la East Africa.

Matatizo YOOTE ya EAC ilokufa, iwe ni platform to redress and ensure Tanzanian interest are taken care of this time around.

Sijafuatilia details za ndani kujua what we are bargaining for as Tanzanians, but kutokana na hii debate hapa, my views ni kuwa we MUST get in there and negotiate mapema, otherwise it will come a time when sweeping changes will simply push us in. We need to get in there and bargain our corner.

We have our positives as a Nation with track records za kujivunia, which we MUST take into the Federation and get our model in there - kuna UTAIFA bila ukabila, kuna lugha ya Kiswahili - si madogo hata kidogo haya mjue!! Kuna hulka zetu za AMANI and calmness. Lakini kuna mengi we need to learn from them as well. Mfano, hawa jamaa wako mbali kwa kimbinu za kibiashara. We need to adapt fast to be able to fit and flourish. Kujitoa na kulalalmika hakutusaidiii in a long run.

Why are we debating about nchi ya Kenya au Uganda au Tanzania (Zan and Tanganyiaka) in a first place. Jamani, hizi nchi ziliundwa tangia year 1885 by that Berlin Conference. Tanzania yetu ya Leo ni ya 1964 chini ya Nyerere na Karume na ajabu wapo watu wanataka ivunjwe! Sasa history is giving us chance to become 1 watu mnapiga kelele za nyuma za kung'ang'ania model ya Utawala tuliorithishwa na Mkoloni?? Let us create our own thing - hii ni 21st century!

We need progressive politics ndugu zangu.

Let us embrace change and get what we MUST have on the table to bargain so that we end up with all what we have, and get more from the union. Tusipofanya hivyo, kuna uwezekano we end up with all that we dont want to have.

Embrace change. It is a good thing.

Taasisi.
 
Taasisi

Well said, but where is our negotiators? Sio hawa ambao ni wezi na wala rushwa? Kwa nini wasichaguliwe watu waliobobea au upeo kwenye nyanja hii ya miungano? Vipi muungano wetu na Zanzibar? Kwa nini watu wanaendelea kuuwana wakati wa uchaguzi? Je ni kosa la nani?
 
Ole,

Agreed. You have highlighted some problems. I would suggest we deal with the problems but we shouldn't make it that the problems should stop us getting the Federation/Union/Muungano.

Mfano ni kuwa, perhaps if we make it very clear

Issues/Matters:
1.
2.
3.
4

The above are non negotiable and we MUST get them into the Union.

Good to have
5.
6.
7.
8.
That will be a good start.

Matatizo ya Nchi yete, we deal with them but we shouldn't scare the Public that Muungano ni kitu kibaya na Wakenya , Waganda will do this or that. We have to be in to take the Lead on this.
 
Jamani watanzania wenzangu imefika wakati wa kuangalia mambo kwa upana na kujua dunia yetu inakoenda. Katika historia ya maendeleo ya nchi yeyote duniani leo hakuna nchi inayo kataa wasomi! mfano Canada wana program ya kuwapa uenyeji wasomi na watu wengi wamehamia huko, vilevile hapa marekani kuna program za wasomi walimu wa shule na manesi wanapewa permanent residency or green card.

Tanzania inatakiwa invest sana kwenye education ya juu na nina maana education ya chuo. Kwa sasa tunaogopa wakenya na waganda ni vizuri kuogopa lakini solution siyo kuwazuia bali ni kuongeza wasomi Tanzania. Nchi yetu wamegundua gas, investment za gold zinaongezeka n.k kazi zitakuja lakini zitataka elimu ya juu. Kama kuna kitu kikwete atafanya cha maana ni kuivest kwenye elimu ya juu, hata hapa marekani wasingependa kuleta wasomi kutoka nje lakini solution ni kuinvest kwenye education.

Watu wengi watasema education inachukua muda lakini ukweli ni kwamba nyuo vikuu ni miaka mitatu au minne tu, serikali inatakiwa iongeze idadi ya wanafunzi wa nyuo vikuu. Rafiki yangu amechukua P.H.D kwenye area ya uchumi wa Tanzania na future yake hapo MS aliniambia tatizo kubwa kwenye statistics ni human resources au wafanyakazi hasa wenye skills. Kama nchi yetu haita invest kwenye elimu tutakuwa kama Botswana nchi tajiri lakini wananchi hawajasomo hivyo inategemea wataalamu kutoka nje hasa Tanzania na Nigeria.

Serikali inatakiwa kuchukulia hii swala kama tatizo na kuliombea msaada, JK waeleze wadhamini ukweli kwamba watu wanaomaliza vyuo ni wachache sana na ongeza nafasi za wana vyuo hii issue ni emergence. Mtashangazwa na kitu kimoja uchumi wa Tanzania utakuwa sana muungano utakapo anza lakini wasomi wa nchi nyingine watajaa Tanzania kama hakutakuwa na watanzania wakufanya kazi.

Mimi kwa mawazo yangu naona watu waliosoma wasiogope watapata kazi lakini kwa wale ambao hawana elimu watakuwa na wakati mgumu sana. Lakini tuache kulalamikia wasomi wasomi hata kama ni wa nje wananyanyua nchi sana tatizo ni kama huna wasomi inamaana pesa nyingi itaenda nje.

Hivyo solution ya hili swala la EAF kwa kikwete ni Education, waeleze wananchi kwamba utawapa kazi na training program zitakazo wawezesha kucompete na watu wa nchi nyingine. Vilevile Encourage wasomi wa nje warudi Tanzania inawasomi wengi sana nje.
 
Kamundu
ndio maana tunalikataa shirikisho kwa sasa mpaka pale atakapokuja mwenye upeo na kuwaandaa wa tz ku compete
kwa sasa kuingia EAF na kuwaua watz.

Angalia saizi baada ya serikali kusupport wanafunzi wa chuo kikuu pamoja na uchache wao ,ndio kila siku wanashinda barabarani wana andamana
serikali inawataka wachangie asilimia 40 hii asilimia si mchezo kwa mtz kwa hesabu za kawaida ni karibu milioni 1.2

kwa wa tz watakumbuka kimbembe kilichotukumba kulipia sh elfu arobaini tu za secondary sasa leo asilimia 40.jiulize wangapi watasoma ?? na wakati huohuo tuingizwe kwenye shirikisho
hapa unaona kabisa viongozi analao jambo
 
Admin i wrote a good topic about EAF but is deleted why? i used proper words and the message was about education why are you bias?
 
Am I bias? Hii ndo shukrani yako?

So nice to see this complaint. Am the one who merged your thread to the EAF Main thread. I love this kind of conversation either. Even this' not a TOPIC and needs to be merged to EAF main thread.

You know what, hili ni tatizo la wengi... You need to recheck before complaining. Hakuna mwenye hamu ya kufuta thread yako na wala hanufaiki nayo labda kama ni tangazo la ngono etc LAZIMA litaondolewa.

Kumradhi, usiwalaumu na ujumbe unaotakiwa kwenda PM nitumie PM si huku kwenye ukumbi.

Anytime bro...
 
Kamundu, good point!

Tatizo siyo kwamba hatutaki jumuia, tatizo ni muda na tuingieje ili kulinda maslahi yetu. Huu unaitwa ushirikiano lakini ndani yake kimsingi imejificha vita ya kiuchumi. Naamini kwamba unahitaji kujitayarisha kabla ya kwenda vitani. Na vitani watu huenda kwa mategemeao ya kushinda. Usiingie vitani kama huna tegemeo la kushinda, au angalao kutoka dorooo!

Tunahitaji muda kujiweka sawa!
 
Hi!
Kwa upande wangu mimi sioni sababu ya sisi *(Tanzania) kujiunga na hili shilikisho kwa kipindi hiki na wala sidhani kama utakuja muda ambao tutakua tayali kujiunga nalo.
Zifuatazo ni sababu zangu kuu;
1. Hatuna mlingano wa kiuchumi kati yetu sisi na hao wenzetu, hili litatuletea matatizo katika soko letu la bidhaa hasa za viwandani.

2. hatuna mlingano wa uwiano wa idadi ya wasomi. wenzetu KE & Ug, wanavyuo vingi ukilinganisha na vyetu,hivyo idadi ya wahitimu wa elimu ya juu kwa wenzetu iko juu kulinganisha nasi.

3. Maendeleo ya kiviwanda, maendeleo ya kiviwanda yetu yapo chini kulinganisha na wenzetu
 
Hi!
Kwa upande wangu mimi sioni sababu ya sisi *(Tanzania) kujiunga na hili shilikisho kwa kipindi hiki na wala sidhani kama utakuja muda ambao tutakua tayali kujiunga nalo.
Zifuatazo ni sababu zangu kuu;
1. Hatuna mlingano wa kiuchumi kati yetu sisi na hao wenzetu, hili litatuletea matatizo katika soko letu la bidhaa hasa za viwandani.
2. hatuna mlingano wa uwiano wa idadi ya wasomi. wenzetu KE & Ug, wanavyuo vingi ukilinganisha na vyetu,hivyo idadi ya wahitimu wa elimu ya juu kwa wenzetu iko juu kulinganisha nasi.
3. Maendeleo ya kiviwanda, maendeleo ya kiviwanda yetu yapo chini kulinganisha na wenzetu

Wrong!

Maendeleo ni uchumi na uchumi unahitaji watu, na shirikisho ni la watu, watu watakuwa wengi, hivyo soko linaongezeka. Kwa hiyo shirikisho, kwa sababu hiyo ni muhimu. Swala ni kwamba tunahitaji kuingia humo katika muda muafaka!
 
Kwa mawazo yangu muda bado lakini hatutaweza kuzuia wasomi ni kuendeleza wasomi wetu. Je ni lini tutakuwa tuna wasomi? kwa sababu kampuni ikija ku invest sasa hivi na inahitaji geologist na hakuna Tanzania je watafanyaje?. Tanzania inahitaji vitu vifuatavyo kabla ya muungano. Mimi siogopi idadi ya viwanda Tanzania

1. Tuanhitaji kuwa na ID kwa Watanzania wote.
2. Tunahitaji kuwa na sera sawa za rushwa mfano adhabu na seriousness.
3. Tunaijahi kuwa na monetary policy sawa kwa sasa tuna pesa tofauti hivyo itacomplicate any business.
4. Tunahitaji kuwa invest kwenye education na training kama tunaona degree program ni expensive then tuige mode ya US ya community college kwa training.
 
Mtukwao

Maendeleo ni uchumi na uchumi unahitaji watu, na shirikisho ni la watu, watu watakuwa wengi, hivyo soko linaongezeka. Kwa hiyo shirikisho, kwa sababu hiyo ni muhimu. Swala ni kwamba tunahitaji kuingia humo katika muda muafaka!

Wingi wa watu sio hoja, waafrika tupo wengi mbona hadi leo bado bara la Afrika ni masikini? Botswana population ni less than 2 million angalia wako wapi? Angalia GDP za top 20 African countries :http://www.joinafrica.com/Country_Rankings/gdp_per_capita.htm

Kwa hali hiyo maoni yako ni kuongeza matatizo na nchi kama Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda. Haya matatizo tuliyonayo hayawezi kutatuliwa na Nchi jirani ni sisi wenyewe.
 
Ukahaba wakithiri Kenya
Wengi wapoteza bikira katika umri wa miaka 16

NAIROBI, Kenya

WENGI wa wasichana nchini hapa wanapoteza ubikira wao kabla ya kufikisha umri wa miaka 16, imefahamika.

Kwa mujibu wa uchunguzi, mbali ya hali hiyo, wasichana wengi wamekuwa wakijihusisha na mapenzi ya watu wa jinsia moja yaani 'kusagana'.

Ilifahamika zaidi kuwa wasichana wengine wa kati ya umri wa miaka 18 na 25 wamekuwa wakitumia vifaa bandia katika kujiridhisha na hamu ya mapenzi na wengine kufanya mapenzi kwa makundi.

Utafiti huo umebaini kuwa matumizi ya dawa za kulevya ni jambo linachangia kwa kiasi kikubwa kushawishi wasichana hao kujihusisha na tabia ambazo ni kinyume na maadili ya Kenya.

Wakati matokeo ya uchunguzi huo yakitangazwa na vyombo vya habari, baadhi ya wazazi na viongozi wa dini wamepinga hatua hiyo.

Viongozi wa dini na wazazi walisema kugundulika kwa hali hiyo ni jambo la kutisha sana na kwamba jitihada za makusudi hazina budi kufanyika ili kukabiliana na hali hiyo.

Kwa mujibu wa uchunguzi, asilimia 56 ya wasichana waliohusika na uchunguzi huo walikutwa wamepoteza bikira zao wakiwa na umri wa miaka 16.

Hata hivyo, kuna matumaini kuwa asilimia 30 ya waliohusika na uchunguzi huo walikutwa na bikira zao na wakiwa na umri wa miaka 16.

Asilimia nane ya wasichana waliohusika na uchunguzi waligundulika kujihusisha na vitendo vya usagaji na matumizi ya vifaa bandi kwa ajili ya kujiridhisha kimapenzi ambao ni asilimia 16.

Wanaojihusisha na usagaji, walisema wamefikia hatua hiyo baada ya kufundishwa wakiwa shuleni au vyuoni.

Asilimia nyingine 47 ya wasichana waliohojiwa walisema wameshiriki kutoa mimba ili kuepuka ujauzito.
 
Tanzania tutaburuzwa , kutokana na uoga wetu na tabia ya kukosa ujasiri kwa wageni, na hatuwezi kuepuka hiyo ndivyo tulivyo, kwa kuliepuka hilo bora tusijiunge, Asante.
 
Shirikisho la Afrika Mashariki Halitufai Watanzania kwa sasa kwani Kwanza Mimi Naamini Mtoto wa simba ni simba kwahiyo Idd Amin Bado Yupo kwa njia tofauti tu! na pia Naamini bado mbegu ya uadui na sababu zilizosababisha Vita vya Kagera bado hazijaondoka kwa kila mhusika!.Pia Wenzetu walioko Magharibi mwa nchi yetu Siamini kama ni watu wakuamini kwa Amani kwani kama chuki zao zimekaa kwa karne je kitakachozifanya ziiishe sasa ni nini?

Naamini Kuna (values) zilizojengwa na Waasisi wa Taifa hili ambazo ndizo zinaifanya Tanzania mpaka leo iwe hivi ilivyo ambapo wenzetu wengi waliotuzunguka zimewashinda kwahiyo ni risk kubwa sana kujichanganya nao kwawakati huu.Shirikisho la kiuchumi sawa lakini kisiasa Jamani Watanzania Tunajitumbukiza kwenye Kiza kinene kilichobeba majanga Je Tutakimbilia wapi?
 
Hi

Leo sina muda mreafu wa kuchangia hapa. Nitarudi kufafanua kwa undani nitakayo andika hapa. Nitarudi tena..

Chukua vitoto vya chui na simaba vikiwa ana siku 1 au 2 mbili tangu vizaliwe.

Vilete nyumbani kwako. Vilee pamoja na vitoto vya Paka wako. Ni kwa kipindi tu, tofauti zitakuwa hazionekani. Muda muafaka ukifika...Utashaangaa...!

Utalijua JIJI!

Pale kila kiumbe kitakaponza kuonyesha kuwa Paka ni nani, chui ni nani na simba ni nani!

Lakini mlivyowabishi hamtanisikiliza ..lakini ninaadika ..ili siku Utakapo kuja kumjua Museni vizuri mbele ya makucha yake..utambue kuwa ni Yule yule Dictotor aliyesomea CCP Moshi kwa jina la Idd amini dada ni lakini huyu Musen yyeye ni wa kisasa...alisomea Chuo kikuu Dar Es Salaam.

Najua sintazikilizwa..lakinina mimi kwa ujasiri wa Ki_Baba wa taifa..ninaandika.. lakini Tutalijua jiji pale tutakpokuja kugundua kuwa hatuingii kwnye shirikisho na ushirika na Paka ..ila..Simba Saba kama Jina lilinavyoonyesha ..M_SABA Au kwa ligha ya huko kwao M_SEVEN au M_7

Wanachi wa Uganada na Watanzania ..na wa Kenya...Wachukue wafuge ..Pamoja..siku itafika..Utalijua jiji... pale mwanchi wa Uganda atakapokuwa anachotakiwa kuwa..Ukifikiri nimwanachi..kumbe ni Simba ..tena Simba saba katika mmoja.....mwanchi wa Kenya atukwa chui na mwanchi wa Tz anabakia Paka kwani ..ndio asilizao..Kilichotokea hapo..Ilishasemwa.. Utakachopanda ndio utakachovuna...ni muda tu..mbegu zitajonyesha..hivyo hiyo muda utatuonyesha asili ya kila mwanachi. Soma mada "Afya ya tanzania" au Hisia hasi toka "Tanzania yenye Neema" uone asili ya Watanzania...!

Mwanchi wa uganda ..itakuja kugundulika hawezi kuishi Bila Dictotor. Hivyo hata . Kwa asili yao lazima wamtengeneze mmoja kila mara wa kuwaongoza...! Hata wewe unayesoma hapa nenda kawe raisi wa uganda . Ni mwaka ujao kama sio ule mwingine utaanza kuongea Ki_ Idd Amini yaani ueshaanza kuiva..bado kuepuliwa tu uanze kula nyma za watu. Utaanza kuongea ..unataka kuwa Raisi wa maisha..unataka kuwa kiongozi wa shirikisho..na ujinga wote wa kidictotor..., utaanz akusahau kumtambulisha Rais wa tanzania mbele ya Ma_Rais wengine na mbele ya umati mkubwa ...yaani unaanza kupiga Mkwara..na wanchi wake wakiona..Ili Tugope...???? Usituchezee!!! leo sintaongea sana..lakini hali ilivyo...Maoni haya hayanakazi..Mbele ya yule dictoror Wa kampala...atawatia mfukoni paka na chui ..na atautwaa...URais wa milele wa Shirikisho..huo ni mfano tu..ukiwa na dukuku duku...niulkizeni nitafafanua...Lakini ..Nakuhakikishia ..TUTULIJUA JIJI MBELE YA IDD AMINI DADA WA PILI! Tutaliwa nyma au tutaliwa ...Almasi na Dhadu..kazile zinazovuwa DRC???

Bora Amri mkuu Wa JWTZ..aaanze kuandaa vikosi...Tutawachakaza...mpka SUDAN..leo hii tunaubavu...Nakuambia ..tutalijua jiji...!!!!
 
ikitokea tukajiunga
mimi nitasema hakuna raisi Mjinga na mpumbavu kama JK
maana wakati tunaibiwa ndege zote na kenya NA IKABIDI MSUMBIJI watuazimishe ndege na meli ya victoria kufanywa BUFFET na kungolewa kule kisumu.

Pia ile vita ya Kagera nadhani huyu JK alikua tayari Mfunga buti(mjeshi) hivyo anafahamu habari hiziz bara bara, sasa akitu unganisha sitokaa nione raisi mwingine mpumbafu kama huyo.

Kurubuniwa na akina M -7,waliobaki(k-back)da yani atakua mpumbafu wa kutosha kama anataka mali ni kheri JMK na kilanja wake mkuu EGL watuibie kama walivyofanya richmond watuachie nchi yetu wakati ukifika watupishe walio na machungu na nchi
 
habari za kazi Watanzania

kuundwa kwa shirikishisho si tatizo ili inabidi serikali yetu ijipange kwa kukabiriana na changamoto hii, kabla ya makubaliano ni vizuri tuwe katika angalizo la kwa mda wa miaka kama kumi kwanza ili tuangalie kama kuna manufaa ambayo watanzania wanapata, si kuingia kichwa kichwa baadaye tuje kujuta, na pia inabidi kuangalia kama kuna faida yeyote.

hiyo mikataba wanayotaka kuingia serikali ni bora watulie mpaka mwafaka utakapofanikiwa.

asanteni

maleva kaduma
malevakaduma@yahoo.com
 
Ndugu Watanzania wapendwa,
naomba kuchangia machache katika huu mjadala!
Kwanini tukimbillie ku establish hii federation bila ku plan on a longterm basis?

Muuungano wa nchi hizi si kitu kibaya ila the whole process na time frame ambayo imeamuliwa ni mfupi mno. Tuna hitaji mda mrefu sana, sisi kama watanzania kuwa na ufahamu wa issues zote ambazo ziko entailed katika hii federation ni 'must'. Iliichukua Europe muda mrefu sana kabla hawajafika hapa walipo leo hii! Na mpaka leo hii miaka 50+ bado wanashindwa kukubaliana baadhi ya mambo!!! Sasa unapomwambia mwanachi wa kawaida atoe mawazo kwenye jambo ambalo hana hata idea! wot is it all about? sio sawa.

Watanzania wengi tu wa kule vijijini hata na wale walio mijini hawaelewi vitu vingi kuhusu mambo ya federation zaidi ya kuku ambia tu kwamba itatuletea umoja! umoja for wot? Tunahitaji fair playing ground ili tuweze kushiriki kikamilifu kwenye muungano huu, until then, bora tubakie kama tulivyo, tu sort matatizo tuliyo nayo badala ya kuji ingiza kwenye matatizo mengine.

Sio kama hatuwapendi wenzetu wa Kenya na Uganda la! nadhani imefikia wakati kwa sisi Watanzania kuonyesha UTAIFA na UZAWA kwa kutetea vile vilvyo vyetu! labda ni kutokana na hili ndo kunako wafanya baadhi wenzetu watuone wakorofi,ma-racist kwa kuwa walishatuzoea kuwa ni watu wa 'sawa ndugu'!!!!!
Faida kubwa mojawapo ya kuwepo huku ughaibuni (UK) sio elimu niliyo ipata bali ni Uzawa na maongezeko ya machungu ya nchi yangu na kwa hili nina uhakika siko peke yangu, tuko wengi sana, exposure tuliyoipata imetoa mwamko huu mkubwa na nina uhakika pia,itasaidia kuwa induce hata wale walio nyumbani sooner or later kutofautisha kati y mchele na pumba!!!!!!

MY fellow EA plz expect more of the same!!!!! this is just a start !!


MBONGO MZAWA
 
Back
Top Bottom