East African Federation (EAF) public Views

Salaam kwa wote:

Naomba niwarudishe katika mambo ninayofikiri ni ya msingi.
Naamini kwamba lengo ni kwa watanzania kuwa na maisha bora (hii inatakiwa kuwa ni Matakwa ya kitaifa - national interest), hii ni pamoja na

kuwa na mahali bora pa kuishi
kuwa na chakula bora cha kutosha, ikiwemo maji safi na salama,
kuwa na elimu ya ujuzi na yakuwezesha kufanya maamuzi bora kwa ujumla
kuwepo usafiri bora wa kuwezesha kutoka sehemu moja hadi nyingine
kuwa na umeme
kuwa na huduma bora za afya etc

swali, ni namna gani shirikisho hili la afrika mashariki linaweza kusaidia kuwafikisha watanzania katika malengo hayo. kwa kweli kama lengo sio kuwawezesha watanzania basi hakuna haja, hata kidogo ya kulizungumzia swala hili (kwa sababu kutakuwa hakuna matakwa ya kitaifa)

Sijui sababu hasa ni kwanini Tanzania pamoja na kuwa na mali nyingi na watu wa kutosha, imeshindwa kufikia malengo ya hapo juu lakini baadhi ya sababu nafikiri ni;

-kukoseka na kwa muongozo (katiba) sahihi kwa watanzania na,
-kukosekana kwa uongozi wenje ujuzi wa kutosha wa kuweza, angalau, kuweka msingi wa kufikia malengo hayo.

SIONI NI JINSI GANI SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI LINAWEZA KUTIMIZA LENGO HATA MOJA KWA WATANZANIA IWAPO KILA NCHI KIPEEKEE IMESHINDWA!!

hivyo nafikiri, wabongo turudi kwenye maabara (drawing board) tufanya uchunguzi wa matatizo makubwa yanayotukabili.

asanteni.
 
EAC States to introduce common work permits

Who is really deciding our destiny? KENYANS I WONDER!
 
EA fast-tracking fiercely opposed

2007-01-12 11:00:55

SOURCE: Guardian http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2007/01/12/82164.html
 
Ni vyema tukawa na Shirikisho, ila wasiwasi wangu ni juu ya hii "fast tracking" ya uanzishwaji wa hili shirika!

Nadhani bado tuna maswali kadhaa muhimu ya kujiuliza. Baadhi ya hayo ni kama:
1. Nini itakuwa hatma ya taifa kama Tanzania baada ya shirikisho?
2. Je, sababu zilizoiua Jumuiya ya Afrika Mashariki (1977) ambayo kimsingi ingepelekea kuwa na Shirikisho haziwezi kujirudia?

3. Ni nini itakuwa hatma ya nchi majirani (Rwanda & Burundi) ambazo zimekubaliwa kuingizwa kwenye mchakato wa uanzishwaji wa Shirikisho wakati hatukuwa sambamba toka awali? Hawatakuwa wanaburuzwa?

4. Je, tofauti za mifumo ya utawala katika nchi wanachama hazitakuwa na athari zozote kwa shirikisho?
Na mambo mengine mengi.
Mi nadhani ni vyema Watanzania na wengine wote tukajiuliza sana maswali haya, lakini tuyapatie majibu ndiyo tuamue ama kuendelea na mchakato "fast tracking" ama twende polepole (ngazi kwa ngazi).
Tuangalie mifano kadhaa: Umoja wa Ulaya na Muungano wa Nchi za Marekani. Tuna yapi ya kujifunza kutoka huko?

Nina wasiwasi sana na tume ya Mwalimu wangu Prof. Sam Wangwe kama kweli itaweza kupata maoni halisi ya Watanzania juu ya "fast tracking" ya Shirikisho la Afrika Mashariki. Je, Watanzania wanaelezwa ukweli ama wanaburuzwa?
------------------
Mwanaharakati
 
Sikubaliani na Muungano wa Africa Mashariki kwa mitizamo miwili mikubwa..

1. Kiuchumi - Hatuko sawa na hatutaweza kuwa sawa na wananchi wakafaidika na kitakachotokea ni majirani kuzidi kukuza uchumi wao kwa rasilimali zilizopo Tanzania kwa sababu wao wanauzoefu tayari na walishaona madhara ya kile sisi ambacho tunataka au tunakifanya sasa hivi (Yaani wao walishafanya na wakaona madhara na faida zake mapema)

2. Kielimu - Tumeshaona wenzetu walivyo tuzidi makazini kwa sisi tilioajiriwa au tulio kwenye ajira, Makampuni yaliyo mengi hapa kwetu yameajiri wakenya katika taaluma mbali mbali ikiwemo Masoko na uongozi wakati wazalendo pia wanaweza kufnya kazi hiyo tena kiufanisi lakini hatujaweka wazi sheria ya kuwaajiri majirani zetu wa Jumuiya Ya Africa Mashariki matokeo yake wanasema itakibiza wawekezaji, Wenzetu wameshaanza kuwekeza hapa kwetu wakati sisi hatuna hata ndoto ya kuwekeza hivi sasa kabla ya Muungano (Je shirikisho likipitishwa Watanzania walio wengi hawatapata)

MFANO miezi miwili iliyopita Wakenya waligoma kufanunya kazi kwa vile nchini mwao mavamiwa na madereva wageni wa magari makubwa wanaolipwa mishahara midogo na kusababisha wao kukosa ajira (Wengi wao walikuwa ni Watanzania na ni lini watanzania wamegoma kisa ajira zinapewa wageni? serikali haioni? Je baada ya shirikisho itakuwaje?)
 
Apart from some few people in Rwanda, less than 1% of Rwandans speak English.I think to tell the truth, Rwanda should not hide in our Community because of justice.

How a country can be accepted in english speaking countries because ONLY the president speaks english!!!!!!!!!!!!!! SHAME

President Kagame must first face justice about planning and executing genocide in his country and not hide in commonwealth.

He is a super lier, he killed three presidents in less than two years: Rwandan say that he killed president Ndadaye of Burundi, and killed President Habyarimana of Rwanda and another President of Burundi after shooting down the plain.

If you back him in commonwealth, you back the problem because he is a potential terror.
 
EAC States to introduce common work permits


Who is really deciding our destiny? KENYANS I WONDER!


Exactly.Now that's a fact u got to live with an there is little u can do to change anything.It's up to u to decide.The freeway or the hard way.Oh dear Tanzania.i cry for u.
 

Get the hell out u cow.u got nothing against Rwanda. u just mad with ur own country which definitely is Tanzania.U don't get it why Rwanda in just a decade has moved from genocide to glory.The best performing economy in eastern Africa.As a Kenyan i'm cool with the fact that the 1% Rwandans who speak English do it rather well as opposed to the 100% Tanzanians who speak English in a very sick way.

What's up with u pple.One day, u so anti-English,the next day u claim u invented the language.Is it that bad in Tanzania?Do u folks know about a great invention-the compass:lets u know where is north,south,east an west.
 
nadhani maoni haya unaweza kuyasambaza kwenye mtandao


‘Woga ni silaha dhaifu katika maendeleo’
* Tumezidi kulalama


na manyerere jackton

WATANZANIA tupo kwenye mjadala, tukitafuta njia, na kasi sahihi ya kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki.

Kwa bahati nzuri, nimepata bahati ya kupita katika mikoa takriban yote. Nimesikia maoni ya wananchi. Nimejua furaha na karaha wanazotarajia baada ya kujiunga. Wengine wana hofu. Wengine ni majasiri, wanalitaka Shirikisho lianze hata kesho.

Wengine wanajadili Shirikisho kana kwamba kuna swali la “je, mnataka shirikisho, au hamlitaki?” Hakuna swali la aina hiyo. Swali lililopo, ni “je, twendeje kwenye shirikisho? Twende pole pole, au twende haraka?”

Kwa maana nyingine, tutake tusitake, shirikisho litakuja. Shirikisho kwa lugha nyingine, ni mwilingiliano. Utandawazi ni mwingiliano. Kinachoweza kukataliwa na Watanzania ni neno au msamiati, lakini ushirikiano lazima uwepo.

Baadhi ya Watanzania wanalikataa shirikisho kwa kutoa hoja dhaifu. Kwa mfano, wanasema tukishirikiana, Wakenya watachukua (watamaliza?) kazi zetu! Rais Yoweri Museveni anataka urais, atakuja kututawala! Shirikisho la nini wakati Wakenya wameshashika kazi zote katika hoteli, asasi na kwingineko?

Watanzania hatuna elimu kama Wakenya na Waganda- tutatawaliwa! Hatujui Kiingereza- tutashindwa kwenye usaili! Hatuna viwanda vingi! Thamani ya pesa yetu ni ndogo. Kenya wanatuudhi, wanajitangazia Mlima Kilimanjaro kuwa uko kwao!

Kwa ufupi ni kwamba zinatolewa hoja nyingi ambazo zikichunguzwa, ni hoja dhaifu. Kwa mfano, Mwalimu wa shule au chuo anaposimama na kusema elimu ya Watanzania ni ndogo, maana yake ni nini? Wanafunzi wamweleweje? Huko ni kujitukana.

Tujadili hoja moja baada ya nyingine. Tuanze la hili la Wakenya kuteka kazi za Watanzania. Wakati Watanzania wanaogopa kupoteza kazi kwa Wakenya baada ya kuanza kwa Shirikisho, mambo ni kinyume. Kazi zimeshatekwa. Kwa nini zimetekwa? Zimetekwa kwa sababu sisi Watanzania hatuna uzalendo. Idara ya Uhamiaji ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiongozwi na Wakenya wala menejimenti ya kigeni. Ni Watanzania wanaoiongoza. Wanaoruhusu wageni hawa kuja kuchukua kazi hata za kufua shuka, ni Watanzania. Vinginevyo tuambiwe kwamba wote waliopo Uhamiaji ni wageni, wanawapendelea wageni wenzao.

Saluni katika miji ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya na kwingineko, zimeshikwa na Wakenya, Warundi na Wakongo. Nani kawakaribisha? Je, udhaifu wa Uhamiaji, ambao ni udhaifu wa Watanzania, ni kigezo cha kulichukia Shirikisho la Afrika Mashariki?

Tunalalamika kuwa Wakenya wanautumia Mlima Kilimanjaro kujinufaisha! Hivi sisi tulitarajia nini? Kama tunathamini usingizi na kujisahau kujitangaza nje ya mipaka? Tunalalamika Kenya kutangaza Kilimanjaro ipo kwao, tunasahau kuwa hata hapa hapa nchini, Arusha wanajitangaza kuwa Mbuga ya Serengeti ipo Arusha! Wakazi wa Mkoa wa Mara kama hawaoni sababu ya kuukanusha uwongo huo, nani awasaidie kuifanya kazi hiyo? Kila kitu kinanunuliwa Arusha, Mara wamelala, nani awaamshe? Ukilala utaibiwa tu.

Rais Museveni kawa gumzo. Watu wanapoteza muda wanasema, “hatutaki shirikisho kwa sababu Museveni ametangaza kwamba anataka awe rais wa kwanza wa shirikisho”. Huku ni kupoteza muda. Nasema hivyo kwa sababu bado hakujawekwa vigezo na sifa za rais wa Shirikisho. Yawezekana sifa ikawa kwamba rais wa kwanza wa shirikisho lazima awe mwanamke! Au Rais wa kwanza wa shirikisho, lazima awe ni rais mstaafu kama Mzee Mwinyi, Moi, Dk. Salmin na kadhalika. Hivi kweli Museveni kutangaza nia tu ya kuwa rais ndiyo sababu ya kuchukia ujio wa shirikisho?

Hoja ya kwamba Watanzania tutashindwa ndani ya shirikisho kwa sababu ya kutojua Kiingereza, hiki nacho ni kioja. Hizi ni hoja dhaifu mno. Tena zinatolewa na wasomi, wakiwamo wa vyuo vikuu na wahadhiri.

Kwanza, Watanzania wangapi wanajua kwamba kidato cha sita Tanzania ni sawa na mwaka wa pili katika Chuo kikuu nchini Kenya? Wangapi wanajua kuwa mwanafunzi aliyehitimu sekondari Kenya, hawezi kupokewa chuo kikuu Uingereza hadi apate miaka kadhaa ya kupigwa ‘msasa’? Nani anayejua kuwa pale Tunguu, Zanzibar Wakenya hawapokewi hadi kwanza wasome ili elimu yao iwafikishwe kwenye kiwango cha kukubaliwa kujiunga chuo kikuu? Haya tunayajua, au tunasema tu elimu ya Tanzania ni ndogo kwa hisia? Ni hatari sana kujadili mambo kwa hisia.

Sijui ni nani alituloga, hadi tukaamini kuwa Kiingereza ndiyo chanzo cha shibe, maisha bora, dawa, ondoleo la dhambi na mambo mengine kama hayo?

Kama Watanzania tu wavivu, Kiingereza kitatufaa nini?
Hivi kweli tunahitaji kujua Kiingereza ndipo tuweze kulima kwa njia za kisasa na kupata ziada? Kule Sumbawanga ambako mahindi yanaoza kwa kukosa wanunuzi, wanalima sana kwa sababu wanazungumza Kiingereza?

Pemba ambako nyanya chungu zinaagizwa kutoka Tanga, ilhali ardhi ipo, wanafanya hivyo kwa sababu hawajui kuzungumza Kiingereza? Umasikini wa Pemba unasababishwa na Kiswahili? Je, si kweli kwamba uvivu na kutotaka kubadilika ndiyo sababu kuu?

Hoteli zetu zinatoa huduma mbaya zisizo na mfano. Wahudumu hawazingatii maadili ya kazi zao. Glasi chafu. Majibu mabaya. Hakuna unyenyekevu. Haya yako karibu sehemu zote za Tanzania. Je, hali hii ni kwa sababu hatujui Kiingereza?

Na kama tuliolaaniwa, Kiingereza tunakililia kwa sababu moja tu-kwenye usaili! Hivi nani kasema kwenye shirikisho, bila kupata kazi inayohitaji usaili, hatuwezi kushindana? Ujasiriamali utawezekana vipi kama tutaendelea kuwa na fikra za aina hii? Kwa nini kila mtu anawaza kuajiriwa, badala ya kuajiri?

Nani anaweza kufuga kuku 100,000; kisha akashindwa kuuza mayai Kenya kwa sababu hajui Kiingereza? Nani atakayevumbua dawa ya kutibu ukimwi, kisha akose wateja kwa sababu hajui kuzungumza Kiingereza? Mbona wakarimani tunao. Wataajiriwa na nani? Tunakuwa wavivu wa kuzalisha, kisha tunasingizia lugha.

Mhitimu wa VETA Kenya aliyefundishwa kutengenza gari au dirisha kwa Kiingereza au Kinandi, ana tofauti gani na wa Tanzania aliyefundishwa kwa Kiswahili au Kikurya?

Kenya hawalali. Malori yanasafiri usiku na mchana. Usiku mabasi yako barabarani. Sisi ni tofauti. Pale Mombo wilayani Korogwe, kulikuwa na kituko. Kiongozi mmoja, kwa wivu tu wa mkewe, alizomoka na kupiga marufuku kina mama kuuza vyakula kwa wenye malori nyakati za usiku! Kina mama wale wameamua kujiajiri. Wameamua kuukosa usingizi, lakini kiongozi kwa wivu wake tu wa kimapenzi, anapiga marufuku biashara hiyo. Hapa tukidhibitiwa na Wakenya tutamlalamikia nani?

Nchi gani iliyoendelea kwa kuhamasisha watu wake kuuchapa usingizi? Nchi gani iliyoenelea ambayo watu wake wanafanya kazi kwa saa 12 tu? Je, udhaifu huu ndiyo tunaujengea hoja ya kulikataa shirikisho?

Wapo wanaopinga shirikisho, wakidai kwamba hatutajiandaa! Wengine wanasema kwa kuwa kuna mtafaruku kaskazini kwa Uganda; Kenya, Rwanda na Burundi ni wakabila; na Muungano wa Tanzania bado una dosari, basi tusubiri kwanza matatizo hayo yamalizike ndipo tuungane!

Kama Watanzania wanahofu kuambukizwa ukabila kutoka Kenya, Rwanda na Burundi, kwa nini wasiwe na ‘hofu’ ya kuambukiza amani, upendo, utulivu na mshikamano katika nchi hizo?

Madai ya kwamba tusubiri kwanza tofauti kwenye Muungano zimalizike ndipo tuingie kwenye shirikisho, ni ya kuchangamsha baraza. Hao Wamarekani, au Waingereza walioungana mamia ya miaka iliyopita, tangu lini wametulia? Je, hatusikii chokochoko za kila mara kwa Waingereza?

Mbona mwaka 1961 tulijitawala bila kuwa na wasomi na wataalamu wengine? Mbona mambo yalienda vema hadi wasomi wetu walipoanza kuiharibu nchi? Hawa wote wanaoruhusu wageni kuja kuajiriwa kwa kazi zisizostahili, walionunua rada, waliosaini mikataba ya kipuuzi kwenye madini, waliobariki ujio wa Net Group Solution, IPTL, Richmond, waliotuwekea mezani mapanki, si ni hawa hawa wasomi baada ya Uhuru?

Je, ni kweli hatuna wasomi, au wapo lakini wengi wao ni wazandiki, mafisadi, wachumia tumbo na wasiokuwa na huruma kwa makabwela waliogharamia elimu zao?

Udhaifu huu wa kukosa uzalendo, uzandiki, ufisadi na uchumia tumbo, ndizo hoja zinazotumiwa kulipinga shirikisho?

Kama ni wasomi, Tanzania ina wasomi wengi, tena wenye uelewa wa hali ya juu. Kinachowakwaza baadhi ya wasomi wa Tanzania, kwanza ni kukosa uzalendo, na pili ni ubinafsi. Hawafanyi mambo kwa ajili ya Tanzania ya leo na ijayo. Wanafanya kwa ajili ya matumbo yao. Ndiyo maana wako radhi kugawa rasilimali za nchi bila soni, alimradi tu wahakikishiwe mlo.

Pale wasomi waliposimama kutetea maslahi ya Tanzania, mafanikio yalionekana, lakini pale walipoamua kutuweka kwenye mabalaa kama ya mikataba ya madini, maumivu tumeyashuhudia.

Tumekosa ujasiri. Tunajitahidi kutafuta vi-jisababu visivyo vya msingi, kuhalalisha udhaifu wetu.
Nasema hivyo kwa sababu Shirikisho si fomula kama ya hesabu. Si kwamba kila shirikisho lazima liwe 2+2=4. Shirikisho la Afrika Mashariki linaweza kuwa na mfumo wake mzuri, utakaolinda maslahi ya kila nchi.

Kwa mfano, suala la ardhi hilo linaweza lisiwe ndani ya masuala ya shirikisho. Ardhi ya Watanzania itaendelea kuwa mali ya Watanzania. Kwa namna gani hilo na mengine yatawezekana, ndilo suala la Watanzania kulijadili. Tutafute fomula.

Je, Zanzibar na visiwa vingine, vitakuwa katika nafasi gani ndani ya Shirikisho? Hayo ndiyo mambo ya kujadili na kuyapatia fomula inayofaa.

Changamoto kubwa inayotukabili Watanzania, ni kufunguka akili na kuingia katika ushindani wa maendeleo. Tujifungue akili, tusafiri kwenda huku na kule duniani kote. Tufanye biashara kwa juhudi. Tujaze ndege za Dubai kama wanavyofanya Wakenya na Waganda.

Tuzaliwe upya. Tuwe wazalendo. Tuipende nchi yetu. Kila Mtanzania katika nafasi yake, ahakikishe anafanya jambo kwa manufaa ya nchi yake. Uhamiaji wanapoachia kazi zote zishikwe na wageni, watambue kuwa wanawaumiza Watanzania wenzao. Tuzalishe zaidi, tufanye kazi kwa juhudi, maarifa na uadilifu. Bila kubadilika, kamwe tutabaki kuwa mabingwa wa kulalama, ilhali wenzetu wakizidi kuchanja mbuga kuelekea kwenye maendeleo.

Udhaufu wetu wenyewe, tusiuingize kwenye hofu ya kuundwa kwa shirikisho. Mkazi wa Mtwara, Abdallaha Chiwaula, amewahi kusema: “Woga ni silaha dhaifu katika maendeleo” Nani nasema bila kubadilika kwa hiari, wakati utatubadili kwa nguvu!


manyerere@hotmail.com
0713 335 469



.tamati…
 
Muda muafaka wa shirikisho bado. Soko la pamoja na sarafu moja na kuimarisha eac na vyombo vyake kwanza.

Kwa upande mwingine, uganda bado ina vita vya wenyewe kwa wenyewe. Maelfu ya watu bado wanakufa kutokana na vita hivyo kasikazini mwa uganda. Lra bado iko inayumbisha uganda. Je, tanzania haitahusishwa na gharama za vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini uganda? Rais museveni kashindwa kuituliza uganda na bado hataki kuachia ngazi. Anabadili katiba kila kukicha ili aendelee kutawala uganda. Sasa anataka shirikisho ili awe raisi wa kwanza wa shirikisho. Je, katiba ya shirikisho haitayumbishwa na rais kama huyu? Vile vile, "bahima empire" iko akilini mwake. Je, tanzania iko macho na hii "bahima empire?" demokrasia nchini uganda bado kabisa. Utawala wa mabavu bado upo.

Rwanda nayo bado haijatulia kutokana na "genocide" ya 1994. Bado mashitaka yanaendelea, na hata rais wa nchi hiyo naye anakabiliwa na shutuma za mauwaji ya raisi wa zamani. Tena rais kagame anashutuma za kutaka utawala wa "bahima empire" katika nchi za maziwa makuu. Tanzania itasalimika na utawala huu? Vile vile, ukabila wa u-tusi na u-hutu bado unaendelea wakati tanzania ukabila ni historia. Demokrasia nchini rwanda bado kabisa. "dictatorship" imeshika usukani.

Nchini burundi nako mambo bado. Fnl na serikali bado zinavutana na mauaji ya raia yanaendelea. Silaha nyingi sana bado ziko mikononi mwa watu isivyo halali, kitu ambacho tanzania inapambana kukisafisha. Ujambazi na utekaji magari ya abiria na hata ya mizigo unatokana na silaha hizo zilizozagaa ovyo. Raia wa tanzania wanataka usalama wa maisha yao na mali zao. Kwa hiyo,tanzania isibebeshwe mzigo mwingine kabla haijamaliza wa kwake. Uhuru na demokrasia burundi bado kabisa.

Kenya nako "pilitical instability" bado inang'ang'ana. Mwisho haujulikani ingawa kuna jitihada ukilinganisha na uganda na rwanda. Kenya kuna nafuu kwani utawala wa sheria una sehemu yake.

Tanzania nayo haijamaliza muafaka wa cuf na ccm. Nyufa za muungano zizibwe kwanza ili watanzania wawe wamoja kisiasa; kusiwe na wanzanzibara na wanzanzibari kabla ya kufikiria shirikisho. Tanzania ina demokrasia na utawala wa sheria ukilinganisha na nchi zote zinazotaka shirikisho.

Shirikisho la afrika mashariki litakuja tu pindi kila nchi ishamaliza au kupunguza matatizo yake ya kisiasa. Tusikimbilie shirikisho litakalo leta madhara kwa watanzania. Rwanda na burundi ndiyo tu wamejiunga na eac. Mafanikio na/au madhara ya kujiunga kwao na eac bado hayajatathiminiwa. Inakuwaje kukimbilia shirikisho kabla ya tathimini ya eac? Demokrasia na utawala wa sheria ni vitu muhimu na vya lazima kabla ya shirikisho.

Mwisho kwa leo.
 
I have been keenly following the discussions on the formation of EA Federation, particularly the admission of Rwanda and Burundi into the EAC. It is an obvious fact that most Tanzanians are xenophobic and they are so hypocratic when you meet one and gives a smile and a seemingly warm Karibu; you might think they are nice people until you leave with them!

It's a pitty how misinformed and biased they are. For example saying that Rwandese do not speak English is ridiculous! Atleast 80% of Rwandese who have studied up to High School can speak and understand both English and French (perfectly by the way). Being an "Anglophone" is not simply because a country was colonised by the British; for God's sake, Tanzanians DO NOT KNOW English!

Other people talk about Rwandan and Burundi having problems and therefore watawambukiza wengine in the Community; that's a very illiterate analysis that can obviously only be made by Tanzanians! Rwanda is progressing very well in all sectors, check out World Bank Reports, read international political forum comments; check out the awards that country is getting in IT, Good governance and economic development! You should try to go out of your borders and cheap talks at Brake Point, Rose Garden, Msasani Club and other iddlers places and get the right information.

Now these two countries are already in the EAC, if Tanzanians are allergic, you move to the SADC. Since you are a very special country with very special people, maybe you will find other specials elsewhere!

Shame on you.
 
Man, you are sick, if English is the only thing you can be proud of, you are doomed! You can definately do better than this!
 
St**** kenyan, why don't you go back to your country.


Obviously they hate u - nenda kwenu!



how different are u?



you know what, you are full of shit, i don' know why i'm wasting my time responding to this 'thing'.
 
Unregistered,
This is exactly the picture we paint aof Rwandese, and trust me- You proved to be!...
Guess what, we better stick with SADC.... we fed you Refugees for years! and this is what you pay us back!.... Nyamukeras!
 
Waganda wateka vijiji Kagera
Oscar Mbuza, Bukoba

Tunayataka haya?
 
Naona bado hao waGanda wana jinamizi la Idd Amin Dada. Sasa tuki Unite si ndo watateka hadi kule Arusha, I wish I could be in Tz this time to witness it.
 
Unregistered,
This is exactly the picture we paint aof Rwandese, and trust me- You proved to be!...
Guess what, we better stick with SADC.... we fed you Refugees for years! and this is what you pay us back!.... Nyamukeras!

See, how can you then deny that Tanzanians are miopic? Not all Rwandese have been refugees in Tanzania, revise your history (if definately you have ever read one!). They hate me so I should go kwetu? Idiot, who told you I fancy being in Tanzania? If I ever go to Tanzania, it's for a visit to a few friends who can think (Not all Tanzanians are idiots like you!), so some of your countrymen can think and I relate with them!

By the way, even Rwandese who came to Tanzania as refugees ended up being job-creators for you guys, you hate them because they are smart and hard-working.

Lastly, you hate them or not, you won't move Rwanda or any other neighbouring country to the Middle East, they are there to stay and you will keep talking nonsense, they will keep developing...and if you don't stop majungu and go to school, they will develop at your expense!

Wake up!!!
 
Unregistered

It seems you do not read between the lines. Tanzania is not your mother or father. We are tired of other peoples problems; we you are developed so what? Leave us alone with our poverty - Period!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…