East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

Hakuna cha Mseven wala Msix,
shilikisho la mara hii hakieleki kitu, walivyotufanyia ile jumuia mara hii tunakambana roho.

Mkenya na wengine hiyo kenya airways kama hujui ilikuwa hivi-

Kenya walisubiri ndege zote na meli zote zimetua kenya wakazikamata na wakatangaza kujitoa kwenye community yani kuivunja,sisi Tz ilikosa ndege hata moja mpaka tukaenda kuazima ndege msumbiji meli hiyo mv victoria ilyopo hapo mwanza mlifanya BUFFET pale Kisumu tugawapigia magoti mkatupa hako kameli mmekakongorowa, ndege mkakatalia zote tukakubali matokeo tukajikongongoja mpaka leo hapo tumefika. Hii kwa mtz inamuuma sana ndio maana hataki kusikia neno KENYA

sasa mmekula mlizotuibia mmemaliza mnakuja na nyimbo zile zile safari hii haikieleweki kitu hata mpige kelele TUTAZIKANDAMIZA na huyu Kikwete mnaojitahidi kumlaghai hata akikubali kitu haikieleweki bado kama mnataka shirikisho na eneo kubwa la biashara kwa nini msing'ang'anie kuungana na ndugu zenu wasomali, wasomali ni wakuu wa jeshi la polisi la kenya, wasomali ndio washika nyazifa kenya kwanini msiungane na hao????

Na tunamwabia kikwete akitaka tz pageuke kuwa IRAQ basi atuunganishe na wakenya, baganda, banyarwanda na barundi

Tanzania ni Kaanani ila kuna watu wachache wanapafanya kuwa Misri
 
Mkamap,

Hiyo ni kweli kuhusu Kenya airways, nikiwa na wakati nitajibu kufafanua zaidi vile ilvyo fanyika hapo kesho, sasa hivi nakimbia kuwachukua watoto wangu shuleni.

Dua, please be sober like Mkamap, real issues!!! not anger!!! or may i say "anger".
 
Mkenya
Una fahamu maana ya anger wewe? Hawa viongozi wanafikiri wanaweza kutuendesha sisi katika karne ya 21, wajiulize tena na nyinyi Kenya mnajiona mko mbele na mnafikiria mtafanikiwa. Mwalimu JK Nyerere (RIP) pamoja na kupenda shirikisho hata kabla ya uhuru aliamua kufunga mpaka wa Tanzania na Kenya, unafikiri ni kwa nini? Mshukuruni Edward Moringe Sokoine (RIP) aliyeweza kumshawishi tena na mpaka ukafunguliwa. Sasa vidonda hata havijapona mnataka kuleta huu ujinga mwingine. Tatizo lenu hamuelewi sisi Tanzania tuliathirika vipi na mnafikiri haya ni mambo rahisi ya kukurupuka.

Usione vinaelea vimeundwa.
 
Kabla ya uhuru, Nyerere, Kenyatta na Obote walijadiliana kuunda shirikisho la Afrika ya Mashariki, nadhani wakiwa kwenye mkutano wa PAFMECA kama hatua za kwanza za kuelekea Muungano wa Afrika nzima. Kwa vile Tanganyika ilikuwa imepiga hatua sana kuelekea uhuru wake, Nyerere akashauri kuwa wakubaliane nchi zote zipate uhuru kwa pamoja siku moja na kuunda federation siku hiyo hiyo, huku akitaka Kenyatta awe Rais wa federation na Nyerere mwenyewe awe waziri wa mambo ya nje. That was a very honest and sincere plan of Nyerere. Mwanzoni Kenyata alikubali lakini baada ya kukutana na watu wake, wakampinga hivyo akajitoa kuua plan hiyo. Tanganyika ikaendela kupata uhuru wake mwaka mmoja mbele ya Kenya na Uganda.

Baada ya uhuru, bado Nyerere hakuishia hapo, aliendelea kuwashawishi wenzie hadi mwaka 1966 wakakubalina kuunda Jumuia ya Afrika Mashariki ya kiuchumi tu siyo federation ya kisiasa. EAC ikaundwa mwaka 1967 nadhani. Hata hivyo Kenya walikubali hii EAC kwa shingo upande (nakumbuka kuwa Mwai Kibaki mwenyewe aliipinga sana wakati huo akiwa mbunge wa sehemu moja huko ukikuyuni). Ni kutokana na Kenya kutoitaka EAC ndiyo maana walikuwamo very strategically na pale ilipoonekana kuwa mazingira ni mazuri kwao kupora faida za EAC miaka kumi baadaye wakapora na kuondoka.

Baada ya somo hilo la EAC na somo tulilojifunza kwenye muungano wetu wenyewe, sidhani kama kweli watanzania tuko kwenye nafasi yoyote ya kushangilia muungano wa aina hii tena. EAC ilituachia matatizo mengi ambayo hatuhitaji kukumbushwa tena. Ni afadhali tuendelee na mfumo huu huu tuliona sasa wa kiuchumi, na kama utafanikiwa, ndipo tuanze kuuangalia tena baada ya miaka kumi hivi.
 
Kichuguu, Dua na Mkenya,
Kusema kweli katika EA Watanzania tu wavumilivu zaidi. Halafu eti wanawake wetu warembo na wapole sana! Wanawake wa Kitanzania mali sana Kenya na Uganda! In the Inter- Univeristy Exchange programme- kuna mwaka 1996 or 97 yaani 60% ya waschana watu walioenda kusoma Unganda na Kenya hawakurudi- waliolewa kule! Sii mnajua jinsi walivyo warembo! Ingawaje pia walikuwepo waschana toka Uganda na Kenya walisoma Law hapo UDSM- wote baada ya kusoma walirud makwao- ni wakali mno! Wamaume Watanzania waliwaogopa!
I dont know how to address this imbalance- naomba mawazo!
Jamani tunavyoongea ushirikiano EA. kuna maeoneo mengi- naona kama hili la intermarrieges linasahaulika!
 
NMB yaporwa m.230/-, polisi, jambazi wauawa


Yohanes Mbelege na Marta Fataely, Moshi

UPORAJI wa mamilioni ya pesa na mauaji ya kinyama ya askari Polisi ni vitendo ambavyo vimeukumba mji wa Mwanga mjini, huku Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Bw. Jordan Rugimbana, akitimua mbio kuwafuatilia majambazi hao.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 1.40 usiku katika benki ya NMB ya mjini humo, ambapo majambazi waliivamia benki hiyo na kupora zaidi ya sh. milioni 230.

Katika tukio hilo, pia Polisi walimuua mmoja wa watu hao, Bw. Peter Mbugua (37), raia wa Kenya na mfanyabiashara wa Karuri nje kidogo ya Jiji la Nairobi nchini humo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Lucas Ng'oboko, alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kwamba askari aliyeuawa kwa risasi na majambazi hao ni namba E6829 Konstebo Michael.
Katika tukio hilo, licha ya kumuua Bw. Michael pia walimjeruhi askari mwenzake namba F6973 Konstebo Naftal na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini hapa.

Habari kutoka eneo la tukio zilidai kuwa awali majambazi hao walimteka Meneja wa Benki hiyo, Bw. Robert Marandu na Meneja wa Operesheni, Bibi Salome Matemu, na kuwaamuru watoe funguo za chumba cha kuhifadhia fedha katika benki hiyo.

"Kwanza walimteka Bw. Marandu wakati akiingia kwa gari nyumbani kwake, kisha wakamteka na huyu mwenzake huku wakiwatishia kuwaua iwapo wasingetekeleza amri yao na pia familia zao zote ziliwekwa chini ya ulinzi," alisema Kamanda Ng'oboko.

Ilidaiwa baadaye majambazi hao waliingia katika benki hiyo na kumuua askari huyo na kumjeruhi mwingine kwa kipigo, ambapo baadaye waliingia ndani ya benki na kuwaamuru Bw. Marandu na Bibi Matemu wafungue chumba cha kuhifadhia fedha nao wakatii amri hiyo.

Alisema katika chumba hicho cha fedha, majambazi hao walichukua fedha zote zilizokuwamo ambapo pia waliiba bunduki zote walizokuwa nazo polisi na hatimaye kutokomea.

Wakati majambazi hao wakiondoka, walipishana na Bw. Rugimbana, ambaye alianza kuwafukuza kwa nyuma akitumia gari lake alilokuwa ametokanalo safarini Butiama mkoani Mara.

Ilielezwa kuwa baadaye taarifa zilifika Polisi ambao nao walianza kuwafuatilia majambazi hao na baada ya kufika eneo la Kiboriloni mjini hapa, polisi waliwaona majambazi hao na kuwafuatilia, katika magari mawili, moja likiwa aina ya Toyota Land Cruiser ambalo namba zake hazikujulikana.

Hata hivyo, jambazi aliyeuawa akiwa ndani ya Toyota Corolla T979AMY kabla aliwamiminia risasi polisi ambao walikuwa wakiwafuatilia na kupasua magurudumu ya gari hilo la Polisi.

Kutokana na majibizano ya risasi, polisi walimuua jambazi huyo akiwa katika eneo la YMCA mjini hapa, ambapo hati yake ya muda ya kusafiria inaonyesha aliingia nchini kupitia Namanga Juni 18.

Hata hivyo, majambazi waliokuwamo kwenye gari lingine walitokomea na fedha huku pia wengine waliokuwa katika gari la jambazi aliyeuawa walijichanganya na watu na kutoweka.

Baada ya kumuua mmoja wa majambazi hao, polisi walifanya upekuzi na kumkuta akiwa na bastola aina ya Bereta mali ya Jeshi la Jimbo la Michigan, Marekani, ikiwa na risasi saba.

Aidha, walikuta magazini ya bunduki aina ya SMG ikiwa na risasi 38, bunduki aina ya SMG na risasi 18, magazini ya bastola yenye risasi nane, risasi nane za SMG alizokuwa ameficha kwenye soksi na hati ya kusafiria.

Vyanzo vingine vya habari vilidai kuwa kuna mtu jana alijitokeza Polisi mjini hapa akidai kuwa gari aina ya Toyota Land Cruiser linalodaiwa kutumika kutorokea na majambazi hao aliporwa wakati akiwa Arusha.

"Huyu aliyeuawa alikutwa na simu ambayo hadi jana watu mbalimbali waliokuwa wakitumia namba za Kenya walikuwa wakimpigia na hivyo tunawasiliana na wenzetu wa Kenya kuupata mtandao wao," alisema Kamanda.

MKENYA,
WIZI MABENKI TANZANIA SASA NI MAJAMBAZI TOKA NAIROBI.
JE HUU NDIYO AINA YA USHIRIKIANO TUNATAFUTA HAPA AFRIKA MASHARIKI? THIS IS THE FREE MOVEMENT OF PEOPLE?
NI AFADHALI TUKAE KAMA ZAMANI
 
Mzalendo, Dua, et al..

Crime is everywhere and including Kenya, we do not condone crime and criminals!, i think its unfortunate that some people here will justify some previous actions by our leaders to seal the borders. Kenya and Tanzania share an almost 1,300km border no country has the required resources to seal it against criminals i.e (US/Mexico border) unless of course we are at WAR in which case land mines could be used.

What needs to be done is for close corporation between the 2 countries security institutions, we cannot conclude that all the crime happening in Tz is due to Kenyans and Kenyans alone NO!, however, i must admit that we have a higher prevalence of crime than Tz, and of which it is important for Tz to study the causes very keenly as this will eventually affect its citizens ultimately, such reasons as Social/Economic inequalities etc...

Among the East Africa countries, Kenya has had the longest uninterrupted Capitalism ideology which has come with some positive i.e modest industrialization as well as negativity such as high social/economic inequalities, corruption etc.., which are presently being addressed accordingly, such lessons are very important for other E. A countries mostly Tz.

I have had an opportunity to travel to Tanzania regularly in the last 2 years and i have observed increasing social economic disparities, you have a very vibrant middle class but the only way of telling is the latest SUV's they drive, Most of these people are NOT investing in Tanzania, they are investing on other countries S.A, Kenya, Middle east etc.., this eventually will lead to high unemployment, in brief the rich richer the poor poorer!!.

The Minute the low level citizens realize that there are some people who have accumulated enormous wealth within a short time will also instill an "urgency" for the poor to shoot to wealth which other way is possible than to commit crime, its all open, look at Richmond, BOT, ATC, flawed contracts etc.. these are signs of things to come... Tanzania is creating some billionaires overnight, who would otherwise invest in the country but alas they are converting the TSH's to US$/Euro and taking it out!!. Look at the Tshs is plummeting fast...

These are some of the lessons Tz should have learnt from their brothers in the north. So do not sit and wish for the status quo, with statements like "Kama ilivyo kuwa Zamani" etc.. Globalisation is here mpende msipende, yaliofanyika kale itufunze tutakavyo ishi in the future, lets break out of these cocoons. Let us learn through others mistakes...

A small example, Scientists took more than 200 years to discover cure for some bacterial diseases i.e penicillin, It may have taken 3ys after invention for the penicillin to come to Tanzania and treat the Sick, Some of you here would opt to wait for 200 mores yrs to allow such an important invention to help you..

My thoughts.....
 
Mkenya,
Unajua sisi Watz hatujazoe fujo- my concern is "Imported Crime from Kenya" ambapo pia askari wetu huuwawawa!
Sisi tumezoea kuishi kwa amani. My point is angalia all recent robberies in Moshi (waliiba 5.6 Tshs billion NBC, Wakaiba over 100 Trust Bureau de Change- wakiba tena Chase Bureau de Change). Wakauwa watu na askari. Juzi wakaiba zaidi Tshs 200 m- pia wakaua askari!
Hii mbegu mbaya- haswa ya kuua watu- na Tanzania, waizi wapo ila hatuuani namna hii! This is our point!
 
Not turn aroud
which grobal->neo-colonilism? the time for propagada is gone.

first u must think deep down before u act-> u africans who be whitched u?? why don't u want real liberation???
The grobal song->is nothing but colonialism ,u know what,these whites can't come physically to colonialise u instead they fix u out by the word grobal.
how far sure ur that people of mathare can compete with usas or europeans not even vietnamese->usiwe mtumwa wa akili hii ni mbaya zaidi kuliko utumwa wa mwili

Kwanini mnakubali kuimbishwa nyimbo na wazungu na ninyi mnazipokea na kuzitia vipambio->????
hawa watu hawaji tena kukutawala physically na badala yake wanakuambia soko huria wanajua wewe muafrika huwezi kupambana nao na watachukua kila kitu hii sio ukoloni?????
We Mkenya when u think always is advisable think BIG

unahabari hata Scotland wanataka kujitenga kutoka United Kingdom(U.k)
hizo nchi tz ,kenya,uganda zinauwezo wa kuendelea zikiwa in (discretine) zikijitegemea ->ikiwa hao akina Raila,MUrungaru,Mrungi,uhuru->wakiwa wakereketwa wa nchi yao
ndivyo ilivyo kwa tz pia uganda.
Mie nalipinga hilo shirikisho kwa nguvu zote maana linaundwa makusudi ama kudidimiza nchi hususani ama kuvuruga amani ktk nchi kusudiwa ili wajichotee mimali kama wanavyobeba mafuta BARGDAD.

Sisi waafrika kama bado tunabeba silaha kuingia madarakani ndio advantage yao hawa jamaa wa wanayotumia___->angalia uchaguzi wenu hapo mwaka huu mtauana je? ukijumlisha nchi kadhaa itakuwaje?
Before u know ur finished.

Mkenya from now on i will give u five if and only if u will establish a group in kenya to protest this terible movement->the said EAF ->thx 4 ur + respond
 
Watanzania wakataa shirikisho Afrika Mashariki
*Asilimia 76 hawataki liwepo kabisa

*Kikwete asema maoni hayo yataheshimiwa

Na Ramadhan Semtawa

KAMATI ya kukusanya maoni kuhusu uharakishwaji (fast tracking) wa uanzishwaji wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki, imewasilisha ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete, huku asilimia 75.9 ya Watanzania, wakipinga mpango huo.

Ripoti hiyo inaonyesha jinamizi la kero za muungano bado linaitafuna Tanzania, kwani idadi hiyo iliyopinga, imetaka kwanza kero hizo zitatuliwe kabla ya kukimbilia kwenye shirikisho.

Wakati hao wakipinga baada ya kuulizwa, wengine asilimia 3.3, bila ya kuulizwa, walituma maoni yao kukataa kabisa kuwepo kwa shirikisho hilo.

Akiwasilisha ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati ya kukusanya maoni kuhusu mpango huo, Profesa Samwel Wangwe, alisema asilimia 20.8, waliunga mkono mpango huo kasi.

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa jumla ya Watanzania 65,000 walipata fursa ya kutoa maoni yao katika mikoa na wilaya zote, ambazo kamati ilifika.

Ripoti hiyo ambayo imegawanyika katika vitabu viwili pamoja na mkanda wa video, imegawanwa katika makundi mawili ambayo ni kisiasa na jamii.

Inaeleza kwamba Watanzania waliopinga shirikisho wamekuwa na sababu mbalimbali, ambazo moja ni ya kisiasa, kwamba hawalifahamu shirikisho hilo.

Sababu nyingine ni pamoja na demokrasi na utawala bora, ambapo Watanzania wana shaka kama vitu hivyo viwili vipo katika nchi nyingine.

Watanzania hao pia wameangalia suala la ulinzi, usalama na amani na tofauti za kiitikadi na pia walipinga kutokana na tofauti ya maendeleo ya kiuchumi kati ya nchi hizo na Tanzania hasa kulinganisha na Kenya.

Sababu nyingine ni kutaka kwanza, Tanzania itatue kero zake za muungano na Zanzibar kwani hadi sasa hazijamalizwa.

Akizungumza sababu za kuchelewa kuwasilisha ripoti hiyo, Profesa Wangwe, alisema kamati ilichukua maoni kwa njia mbalimbali ambazo ni pamoja na vyombo vya habari, kujaza dodoso na mtandao wa kompyuta kwa ajili ya kuwezesha hata Watanzania walio nje kupiga kura.

Rais Kikwete akizungumzia suala hilo, alisema maoni hayo ya Watanzania yataheshimiwa.

Alisema ingekuwa ni tatizo kama Watanzania hao wangesema hawataki shirikisho, lakini kwa kuwa hawataki liharakishwe, yeye haoni kama ni tatizo.

Rais Kikwete alisema ripoti hiyo itapelekwa katika ngazi ya Baraza la Mawaziri, ili ifanyiwe kazi na kisha kupelekwa katika wizara husika ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuendelea na mchakato.

Kama maoni hayo yatazingatiwa, mchakato wa kuundwa kwa shirikisho utakwenda kama ilivyoelezwa katika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Tayari hadi sasa nchi za EAC, zimeanza kutumia mfumo mmoja wa forodha (Customs Union), huku makubaliano mengine kama soko la pamoja (Common Market), sarafu ya pamoja (Monetary Union) na shirikisho la kisiasa (Political Federation) yakiwa bado hayajakamilika.

Tume hiyo ilianza kazi yake Oktoba 13 mwaka jana na imekabidhi ripoti yake Julai 13, ikiwa ni zaidi ya miezi sita imepita tangu ripoti hiyo ilipotakiwa kuwasilishwa.

kikwete hapa asitake kutuhadaa hapa ,ni kwamba hututaki shirikisho baada ya miaka kama mia mbili hivi ndio lifikirike sio kama walivyopanga wao
 
Wabongo wamelikataa shirikisho la A. Mashariki!

Watanzania wakataa shirikisho Afrika Mashariki

*Asilimia 76 hawataki liwepo kabisa
*Kikwete asema maoni hayo yataheshimiwa

Na Ramadhan Semtawa

KAMATI ya kukusanya maoni kuhusu uharakishwaji (fast tracking) wa uanzishwaji wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki, imewasilisha ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete, huku asilimia 75.9 ya Watanzania, wakipinga mpango huo.

Ripoti hiyo inaonyesha jinamizi la kero za muungano bado linaitafuna Tanzania, kwani idadi hiyo iliyopinga, imetaka kwanza kero hizo zitatuliwe kabla ya kukimbilia kwenye shirikisho.

Wakati hao wakipinga baada ya kuulizwa, wengine asilimia 3.3, bila ya kuulizwa, walituma maoni yao kukataa kabisa kuwepo kwa shirikisho hilo.

Akiwasilisha ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati ya kukusanya maoni kuhusu mpango huo, Profesa Samwel Wangwe, alisema asilimia 20.8, waliunga mkono mpango huo kasi.

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa jumla ya Watanzania 65,000 walipata fursa ya kutoa maoni yao katika mikoa na wilaya zote, ambazo kamati ilifika.

Ripoti hiyo ambayo imegawanyika katika vitabu viwili pamoja na mkanda wa video, imegawanwa katika makundi mawili ambayo ni kisiasa na jamii.

Inaeleza kwamba Watanzania waliopinga shirikisho wamekuwa na sababu mbalimbali, ambazo moja ni ya kisiasa, kwamba hawalifahamu shirikisho hilo.

Sababu nyingine ni pamoja na demokrasi na utawala bora, ambapo Watanzania wana shaka kama vitu hivyo viwili vipo katika nchi nyingine.

Watanzania hao pia wameangalia suala la ulinzi, usalama na amani na tofauti za kiitikadi na pia walipinga kutokana na tofauti ya maendeleo ya kiuchumi kati ya nchi hizo na Tanzania hasa kulinganisha na Kenya.

Sababu nyingine ni kutaka kwanza, Tanzania itatue kero zake za muungano na Zanzibar kwani hadi sasa hazijamalizwa.

Akizungumza sababu za kuchelewa kuwasilisha ripoti hiyo, Profesa Wangwe, alisema kamati ilichukua maoni kwa njia mbalimbali ambazo ni pamoja na vyombo vya habari, kujaza dodoso na mtandao wa kompyuta kwa ajili ya kuwezesha hata Watanzania walio nje kupiga kura.

Rais Kikwete akizungumzia suala hilo, alisema maoni hayo ya Watanzania yataheshimiwa.

Alisema ingekuwa ni tatizo kama Watanzania hao wangesema hawataki shirikisho, lakini kwa kuwa hawataki liharakishwe, yeye haoni kama ni tatizo.

Rais Kikwete alisema ripoti hiyo itapelekwa katika ngazi ya Baraza la Mawaziri, ili ifanyiwe kazi na kisha kupelekwa katika wizara husika ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuendelea na mchakato.

Kama maoni hayo yatazingatiwa, mchakato wa kuundwa kwa shirikisho utakwenda kama ilivyoelezwa katika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Tayari hadi sasa nchi za EAC, zimeanza kutumia mfumo mmoja wa forodha (Customs Union), huku makubaliano mengine kama soko la pamoja (Common Market), sarafu ya pamoja (Monetary Union) na shirikisho la kisiasa (Political Federation) yakiwa bado hayajakamilika.

Tume hiyo ilianza kazi yake Oktoba 13 mwaka jana na imekabidhi ripoti yake Julai 13, ikiwa ni zaidi ya miezi sita imepita tangu ripoti hiyo ilipotakiwa kuwasilishwa.

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=476
 
Big ‘no’ to speedy federation

Daily News Reporter
Daily News On Saturday; Saturday,July 14, 2007 @00:02

SEVENTY six per cent Tanzanians are against fast-tacking East African federation for political, economic and social reasons, a report of the Presidential committee on the matter has shown.

The report, which was handed to President Jakaya Kikwete at State House in Dar es Salaam yesterday by committee chairman, Professor Samuel Wangwe also indicated that only about 21 per cent Tanzanians supported the idea.

“You have done your job. What remains now is for the government to work on the report and liaise with our East African Community partners,” President Kikwete told Professor Wangwe.

The committee interviewed a total of 65,000 people from all 26 regions, on the mainland and the Isles. Many others participated in the exercise through the media and public debates.

Professor Wangwe said it took longer to collect views because of the sensitive nature of the matter and the need to adhere strictly to the committee’s terms of reference given by the president himself.

Bound in two volumes and on video tape, the report is in two categories identifying political as well as economic and social reasons. Lack of awareness about the intended federation was the dominant political reason for rejection of the idea.

After discussion by the cabinet, the report will be given to the Minister for East African Co-operation, Dr Ibrahim Msabaha who will also share similar reports with fellow East African counterparts.

The report will also find its way to the East African Community secretariat and not doubt to a future summit of the now five member regional economic bloc after Burundi and Rwanda were admitted last month.

The idea to fast-track East African federation was endorsed at a special summit in Nairobi in August, 2004, which “resolved to expedite the process of integration so that the ultimate goal of a political federation is achieved through a fast track mechanism”.

The federation is dead and buried.
 
Congrats to all Tanzanians who voted against the fastracking EAF,

We here in Nairobi have welcomed your "NO" to fastracking,but before we get response from other EAF members let us use this honorable platform to analyze the reasons as to why there was overwhelming 76% NO vote. But again please remember it is the fastracking that you voted for, and not the EAF which has already been acceded to by all countries, ask JK.

I think we in Kenya do not want the "Fastracking" because of the following reasons:-

1. Levels of Economic development

2. Political development "real" and "imposed" Democracy

3. Social cultural influences i.e Crime etc..

4. Educational disparities etc......

" Dua la kuku limempata mwewe"

Dua , finally your job is safe from maruading Kenyans. joke🙄

lets bring up the real issues that will help foster the EAF in future, what lessons have we learnt with the fastracking etc.. are you going to call JK ask him to revoke the EAF agreements? or Mr. Mbowe of Chadema to raise the issue in Parliament.

What is the next move for Tz?, was there any other options for the Mwananchi? option of walking out of EAF?.

Your Sober views please!!!




Big ‘no’ to speedy federation



The federation is dead and buried.
 
I asure u Mkenya the said EAF will never be formed<=>(sign meaning if and only if)Tz must be included,either EAF will be formed excluded ->Tz.
why->the former EAC had vey big impacts to Tzns and was the one of the major factor for our today's poverty not only still it is believed was puposely there to finish out TZ
even Kikwete knows ->anawapiga changa la macho tu other members
hataunganisha ng'ooo.
namnukuu kikwete"kama isingekuwa Mkapa shirikisho lingekuwa limeshaundwa na baadhi ya nchi zilikuwa zimeshakuja na loadmap ya shirikisho bila kushirikisha nchi zingine na mimi nikiwa kama waziri wa mambo ya nje Mkapa alinituma kuwaeleza wenzetu kuwa hatuendi hivyo na tulipokutana mie nikiwa rais kuna marais walisema tuunde haraka hilo shirikisho lakini mimi niliwaambia hapana lazima tuone maoni ya wananchi wanasema je? lakini marais hao walisema kutafuta maoni ni kujishusha chini ya madaraka na badalaka yake wakataka tutumie madaraka yetu kuanzisha shirikisho mie nikasema viongozi wanakuja na kupita lakini wananchi wapo siku zote na wazo hili la kutafuta maoni limetoka TZ".
sasa mkenya hilo ni ri-ru-ngu la mwisho kama wtz wamepiga kura no ndio mwisho labda liundwe na nchi nyingine
CU byee
 
Tunajivunia kuwa East Africans..

See the medals table at the just concluded 5th IAAF World Youth Championships in Ostrava, Czech Republic

http://www.iaaf.org/WYC07/results/medals.html

39793_W400XH600.jpg
 
Be Frank,

I normally congratulate my Kenyan friends for those medals, and they also do accept it. There is nothing like EA flag or EA national anthem. Whenver they get a metdal it is a Kenyan flag that flies and a Kenyan National Anthem is played. You have every reason to be proud of that achievement and and we do understand your excellence in athletics, but we don't want to be fooled that those medals also belong to Tanzania.
 
I have been preach over and over that EAC is not going to be like EU. This people who initiate this are insane, and they are in big illusion dreams. This countries have a lot of differences from Political, Economical and Social.
Uganda is practice dictatorship, Kenya still in tribalism and Tanzania is suffer in Economic and social standard. So, Mkapa and his team were sick in the head when they initiate this bull crap. We don't want it, I hope Kikwete will listen Tanzanian voices that shout to him don't do it. Or we will call for changes of Katiba so we can see possibility of impeaching his government.
 
I have been preach over and over that EAC is not going to be like EU. This people who initiate this are insane, and they are in big illusion dreams. This countries have a lot of differences from Political, Economical and Social.
Uganda is practice dictatorship, Kenya still in tribalism and Tanzania is suffer in Economic and social standard. So, Mkapa and his team were sick in the head when they initiate this bull crap. We don't want it, I hope Kikwete will listen Tanzanian voices that shout to him don't do it. Or we will call for changes of Katiba so we can see possibility of impeaching his government.
Mungu atupe nini Watanzania kwa kuukataa huu upuuzi wa hawa jamaa na tamaa zao za uongozi,umoja wenu huu watanzania tunasema hatuutaki soma zaidi hapa kama wewe ni mpenda nchi hii http://www.habaritanzania.com/articles/3988/1/Wananchi-robo-tatu-hawataki-Shirikisho
 
Tanzania.How long do u have to exploit,lord over,ravage, this East African paradise known as Zanzibar. If Zanzibar wasn't part of Tanzania it would be as advanced as Mauritius, Seychelles.

Thanks to the Mabwenyenye at Dar who just wanna sip Mnazi all day an complain about mt. Kilimanjaro, Zanzibar is stuck with ya an they don wanna be part of ya. Tanzania, if u great as u think u are,u don need the Zanzibar. Let the Zanzibaris be an independent sovereign nation. U Tanzanians are always whining about aliens in ur country.U have no clue about the number an status of aliens living in Kenya. Even one personality of international repute lamented that it wouldn't be surprising if Osama was spotted shopping at river road Nairobi whilst the duke of York was throwing a party at the Stanley hotel Nairobi.

Kenyans are a universal people.We cuss each other all day but when it comes to dinner tyme we sit at the same table an pass the salt around. Being tolerant is a Kenyan ideal.The Ugandan army oftenly crosses the border,kills Kenyans an confiscates their property. Kenyans on the north are consistently raided by Ethiopian invaders.Somali to the east have literary invaded the country.

They have carved their own Somali within Kenya eg Eastleigh. Rwandans, Sudanese, Ethiopians most of whom are undocumented, live an rock in Kenyan towns. Are Kenyans complaining? No an they never will.Why? Coz we know who we are,we didn't choose to be Kenyans.

We were branded to be so by some supposedly very superior aliens who think of us as uncivilized, diseased, poor dark, skinny elements whose desperation makes they the self proclaimed saviors of Africa feel like gods.

So u Tanzanian, call me a Kenyan an ban me from ur country. I don care. But at least why force yourself onto a relationship with Zanzibar who wanna be just Zanzibaris an not Tanzanians.
 
Matatizo,

Mimi sijua kama Z'bar wangekuwa wenyewe wangekuwa kama Ushelisheli au Maurishazi. Mbona Comoro choka mbaya na wamekuwa wenyewe ndugu yangu? Na Madagaska je?

Umoja siku zote ni kitu kizuri- mimi nafikiri kwa EA tumechelewa sana kuwa nchi moja- ndo maana tuko nyuma kimaendeleo! Haya mambo ya mimi Mkenya, mimi Mganda, mimi Rwanda, mimi Mtamzania.... yataisha lini? Je yanatufanya tuwe na maisha bora zaidi? Mimi naona yanazidi kuturudisha nyuma- katika hii dunia nani atakutambua kama wewe ni Mkenya ukiwa peke yako? na ndo maana tunaendelea kunyonywa na Mataifa mengine.

Sisi tu wamoja, tuungane mapema tuweke watu wetu mbele na maslahi ya ubinafsi wa viongozi nyuma!

Hapa Afrika tunazungmzia nchi 53 zenye uchumi kidogo sana-(ukitoa S.Afika)-katika SSA GDP inafikia nchi moja ya Ubeligiji! Na bado tunawasiwasi wa kuungana! Tukubali tuu -tuungane au tuendelee kuwa nyuma!

MzalendoHalisi
 
Back
Top Bottom