EATV awards 2016 nominees: Hatua ya kupiga kura

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
TUZO za EATV zimeanzishwa mwaka 2016 na kampuni ya East Africa Television na Radio, zitafanyika kwa mara ya kwanza tarehe 10/12/2016 jijini Dar Es Salaam,Tanzania.

Tuzo hizi zinashirikisha wasanii wa muziki na filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki na zitakuwa zikifanyika kila mwaka, huku vipengele vya tuzo vikiongezeka kila mwaka kutoka vipengele kumi vinavyoshindaniwa mwaka huu.

Kuanzishwa kwa tuzo hizi kuna lengo la kuthamini wasanii na kuleta ushindani kwenye sekta hii ya sanaa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Kwenye tuzo za mwaka huu kutakuwepo na jumla ya vipengele kumi. Vipengele sita vitashindaniwa na wasanii wa muziki, Vipengele vitatu vitashindaniwa na wasanii wa filamu na kipengele kimoja kitakua ni tuzo ya heshima.

Vipengele hivyo kwa upande wa muziki ni mwanamuziki bora wa kiume, mwanamuziki bora wa kike, mwanamuziki bora Chipukizi, kundi bora la mwaka, Video bora ya mwaka na Wimbo bora wa mwaka.
Kwa upande wa Filamu vipengele vitakavyoshindaniwa ni Filamu bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Kiume na Muigizaji Bora wa kike.
Tuzo za EATV 2016 zinafanyika kwa udhamini wa Coca Cola na Vodacom Tanzania .

Utofauti wa tunzo hizi na zingine ni kwamba kwenye hizi msanii mwenyewe ndio anajipendekeza kuwania tunzo fulani kwenye kipengele fulani huku akiambatanisha na kazi yake.
Pia msanii anayefuzu kushiriki tunzo hizi lazima awe amesajiliwa na Basata au bodi ya sanaa ya nchi husika africa mashariki.
EATV Awards imeanza na vipengele 10 ambavyo ni:-

1. Mwanamuziki bora wa kiume

2.Mwanamuziki bora wa kike

3. Mwanamuziki bora chipukizi

4. Kundi bora la muziki

5. Video bora ya muziki

6.Wimbo bora wa mwaka

Kwa upande wa filamu ni

7. Muigizaji bora wa kiume

8. Muigizaji bora wa kike

9. Filamu bora ya mwaka

Jana yaliwekwa wazi majina ya wasanii kutoka vipengele viwili ambayo yamepita kuwania tuzo husika kila kipengele wamepita wasanii watano ambao watakwenda kupigiwa kura nayo ni Muigizaji bora wa kiume wa kiume na Msanii bora chipukizi.

1.MUIGIZAJI BORA WA KIUME
Nominees:

  • Meya Shabani Hamisi - Facebook Profile

  • Salim Ahmed (Gabo) - Safari ya Gwalu

  • Daudi Michael Tairo (Duma) - Mfadhili Wangu

  • Dotto Hussein Matotola - Likichwa Lala

  • Saidi Ally Mkukila - Ndugu wa mume



2.MWANAMUZIKI BORA CHIPUKIZI
Nominees:


  • Amani Hamisi (Man Fongo) - Hainaga Ushemeji

  • Feza Kessy - Sanuka

  • Rukia Jumbe (Rucky Baby) - Give me some more

  • Mayunga Nalimi (Mayunga) - Nice Couple

  • Rashid Said (Bright) - Nitunzie
3.MUIGIZAJI BORA WA KIKE
Nominees:

  • Chuchu Hansy - Laura

  • Rachel Bitulo Njingo - Nimekosea wapi

  • Frida Kajala Masanja - Hii ni laana

  • Khadija Ally - 3 Days
4.FILAMU BORA YA MWAKA
Nominees:

  • Facebook Profile

  • Safari ya Gwalu

  • Mfadhili Wangu

  • Hii ni Laana

  • Nimekosea Wapi?
5. KUNDI BORA LA MWAKA
Nominees
. Navy Kenzo

.Mashauzi Classic

.Team mistari(Kenya)

.Sauti sol (Kenya)

.Wakali Wao

6.VIDEO BORA YA MWAKA
Nominees
. Namjua-Shetta

.Njongereza-Navio

.Aje-Alikiba

.Don Bother- John Makini

.Ndindindi-Lady Jayeed

7. MWANAMUZIKI BORA WA KIUME
  • Alikiba
  • Ben pol
  • Mwana FA
  • Sheta
  • G nako.
8 MWANAMUZKI BORA WA KIKE
  • Vannesa Mdee
  • Lady jaydee
  • Lina Sanga
  • Rubi
  • Lilian Mbabazi(Uganda)
9 .WIMBO BORA WA MWAKA
  • Moyo Mashine-Ben pol
  • Aje-Alikiba
  • Ndindindi-Lady jaydee
  • Don Bother- John Makini
  • Kamatia Chini-Navy kenzo.
NB: ukiona msanii wako hayupo kunaweza kuwa kumesababishwa na sababu zifuatazo
  • Inawezekana hakutaka kushiriki hivyo hakuchukua fomu
  • Inawezekana hajasajiliwa BASATA hivyo hana vigezo vya kushiriki
  • Inawezekana hakukidhi vigezo vya kuwa kwenye hivyo vipengele.

Baada ya kutangazwa kwa vipengele hivyo tayari zoezi upigaji kura limefunguliwa kuanzia leo saa sita usiku. unaweza piaga kura yako kwa njia ya simu kwa kutuma code ya msanii kwa kipengele husika kwenda namba 15777 pia kuana njia ya mtandao kupitia tovuti ya eatv.tv/awards.
 
Dah! Ama kweli Mungu si Babu Tale manake kulikuwa na hatari ya mwaka kukatika bila King kuonja tuzo! Ama kweli katika maisha haipaswi kukata tamaa... ukiona mlango mmoja unafungwa basi mitatu mingine inafunguka!
 
hah
Dah! Ama kweli Mungu si Babu Tale manake kulikuwa na hatari ya mwaka kukatika bila King kuonja tuzo! Ama kweli katika maisha haipaswi kukata tamaa... ukiona mlango mmoja unafungwa basi mitatu mingine inafunguka!
ahahahahahha ashindwe yeye sijui safari hii anaweza singizia kuwa wadhamini ni coca cola na vodacom ndio wameleta hujuma.
 
Wasije nao kuwa kama Kili Award huko mbeleni.
 
hah

ahahahahahha ashindwe yeye sijui safari hii anaweza singizia kuwa wadhamini ni coca cola na vodacom ndio wameleta hujuma.
Ayah! Hapo kweli lazima wasizingizie Vodacom na Coca Cola... tena usishangae siku ya siku wakaacha kushiriki kwa kisingizio cha "kutokuwa na imani na wadhamini...!" Let's wait and see. Tena na hapo ndipo nimeuelewa huo utaratibu wa msanii mwenyewe kutuma maombi ya category ipi ashiriki!
 
Sasa huyo Feza Kessy ataendelea kuwa chipukizi hadi lini?! Faiza,popote ulipo nitafute bhana... yaani hadi leo bado chipukizi tu!!
 
usipomuona kiba ujue kasusa
 
Sasa huyo Feza Kessy ataendelea kuwa chipukizi hadi lini?! Faiza,popote ulipo nitafute bhana... yaani hadi leo bado chipukizi tu!!
hahahahhaha
 
Gabo anachukua tuzo ya muigizaji bora wa kiume,
 
Imeendelea leo Karume CBD

MUIGIZAJI BORA WA KIKE
1. Chuchu Hansy - Laura
2. Khadija Ally - 3 Days
3. Frida Kajala - Hii ni Laana
4. Rachel Bithulo Njingo - Nimekosea Wapi
5. Khadija Ally - Penzi la Baba

FILAMU BORA YA MWAKA
1. Hii ni Laana - Frida Kajala
2. Nimekosea Wapi - Rachel Bithulo
3. Safari ya Gwalu - Daniel Manege
4. Mfadhili Wangu - Daniel Michael Tairo
5. Facebook Profile - Meya Shabani Khamis
 
Imeendelea leo Karume CBD

MUIGIZAJI BORA WA KIKE
1. Chuchu Hansy - Laura
2. Khadija Ally - 3 Days
3. Frida Kajala - Hii ni Laana
4. Rachel Bithulo Njingo - Nimekosea Wapi
5. Khadija Ally - Penzi la Baba
Mbona naona kuna tatizo la kiufundi hapo? Hao ni watu wawili tofauti au ni one and the same?! Kama ni mtu mmoja; sasa hapo watakuwa wanatafuta Muigizaji Bora wa Kike au Filamu Bora Iliyochezwa na Mwanamke? Can you crosscheck please? Au mimi ndo SIELEWI?
 
Mkuu mimi nimeweka kama nilivyopokea. Wahusika wanaweza kutolea ufafanuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…