EATV awards 2016 nominees: Hatua ya kupiga kura

EATV awards 2016 nominees: Hatua ya kupiga kura

Huo mkataba unawahusu nini wakina hormonize na wenzie???
Haijapendeza kujitenga na shuhuli ya home tena hawa ambao ndo wanatoka
Jamani mbona kila baya mnawapa WCB? huwajui wabongo harmonize na raymond wangeshiriki wakashinda ungesikia matusi kama bosi wao ndio ameshawishi wapewe!
Nafikiri kwa hili wametumia busara sana kuziacha halafu mwakani ndio washiriki
By the way wengi sana na waliofanya vizuri hawapo mfano Baraka da prince,nick wa pili,joh makini
Ila nafikiri utaratibu wa kujipendekeza ndio mbovu
 
Wasanii kutoka WCB wote hawakutaka kushiriki
Diamond ni baloza wa vodacom na vodacom ndo wadhamin wa hizi tuzo
Jamaa kijiweka pembeni kuzuia maneno ya kuleta upendeleo kwake
Umeenda Mbali sanaaaaa.....!!!! Hizi tuzo ni za kujaza Form Diamon na WCB nZIMA wapo Buzy na Show watajaza Form sa Ngapi???? Msanii anajipendekeza hiyo ndo nini yupo bzy na Africa Tour!!! Wenye uchu na ambao hawana ya kufanya walipata mda wa kujipendekeza
 
wasanii wengi wakubwa kupuuza tuzo za ndani ya nchi kuna jambo la kujifunza.....any way inaweza kuwa mwanzo mzuri
Hamna aliepuuza sema utaratibu uliotumiwa na eatv sijawah kuusikia sehemu yeyeto ile duniani, yani eti wasanii watume wenyewe majina yao na kazi wanayotaka iwe nominated huo si upuuz kabsa kwann wasingekaa wenyewe eatv na kuchagua kazi nzur na iwe nominated then waseme watu wapige kura kupata mshndi, utaratibu mbovu ndo umepelekea hayo
 
sasa msanii bora akiwa diamond
wale team kuonewa si watatukana eatv kila siku
Msanii Bora Tanzania na Afrika Mashariki anajulikana!!!

Sisi shule msingi alie kuwa anashika nafasi ya kwanza kila mtihani basi Siku ya mtihani akiumwa na asifanye yule anayemfuata alikuwa anafurahia sanaaaaa!!!! Kwasasa tanzania hamna video bora Bora kama KIDOGO! HAMNA MSANII BORA KAMA DIAMOND OVER!

ASIE TAKA ANYE
 
Kuna kigezo kimoja kinasema kazi yako unaoipambanisha inabidi iwe imetoka ndani ya kipindi flani kitu ambacho wengi wa wasanii wa wasafi hawafit. nyimbo zao nyingi nzuri ni za hivi karibuni mwaka huu
 
Huo mkataba unawahusu nini wakina hormonize na wenzie???
Haijapendeza kujitenga na shuhuli ya home tena hawa ambao ndo wanatoka
EATV ndo walikosea wao ilitakiwa Wadau wa mziki wapendekeza majina nani anafaa wapi na kwanini sio Msanii aanze kujaza Formu kama anafaNya Registration
 
Kuna kigezo kimoja kinasema kazi yako unaoipambanisha inabidi iwe imetoka ndani ya kipindi flani kitu ambacho wengi wa wasanii wa wasafi hawafit. nyimbo zao nyingi nzuri ni za hivi karibuni mwaka huu
sio kweli harmonize bado ilitoka mwezi wa tatu kama sijakosea akafuata raymond huku kwetu ilikua kabla ya mwezi wa sita

Ila kwa mtazamo wangu wametumia busara kuziacha kwa mwaka huu ,kama ingetokea wote wakawa nominated matusi yasingekosekana
 
UTABIRI WANGU:
-Mwanamuziki KE..Vmoney
-Mwanamuziki ME..Ali Kiba
-Wimbo bora..Ben pol moyo mashine
-Video bora..Lady JD ndindindi
-Kikundi bora..Navy Kenzo
-Chipukizi..Man fongo
-Muigizaji ME..Gabo
 
WCB sahv hawataki tuzo za kichoko kabisa.......

Kama wangechukua fomu hapo asingepona mtu kabisa........

NI MTAZAMO WANGU......
 
EATV WASAFI AWARDS IMOOOOOOOOOOOO....................................!!!!!!!!!!!!!!!!! 😱😱🙄😛😀🙁😡
 
Wasanii kutoka WCB wote hawakutaka kushiriki
Diamond ni baloza wa vodacom na vodacom ndo wadhamin wa hizi tuzo
Jamaa kijiweka pembeni kuzuia maneno ya kuleta upendeleo kwake
Kweli maana Angekimbiza Tuu wabongo Tungngeanza Mboyoyo Mingi kama Kawaida Yetu
 
TUZO za EATV zimeanzishwa mwaka 2016 na kampuni ya East Africa Television na Radio, zitafanyika kwa mara ya kwanza tarehe 10/12/2016 jijini Dar Es Salaam,Tanzania.

Tuzo hizi zinashirikisha wasanii wa muziki na filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki na zitakuwa zikifanyika kila mwaka, huku vipengele vya tuzo vikiongezeka kila mwaka kutoka vipengele kumi vinavyoshindaniwa mwaka huu.

Kuanzishwa kwa tuzo hizi kuna lengo la kuthamini wasanii na kuleta ushindani kwenye sekta hii ya sanaa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Kwenye tuzo za mwaka huu kutakuwepo na jumla ya vipengele kumi. Vipengele sita vitashindaniwa na wasanii wa muziki, Vipengele vitatu vitashindaniwa na wasanii wa filamu na kipengele kimoja kitakua ni tuzo ya heshima.

Vipengele hivyo kwa upande wa muziki ni mwanamuziki bora wa kiume, mwanamuziki bora wa kike, mwanamuziki bora Chipukizi, kundi bora la mwaka, Video bora ya mwaka na Wimbo bora wa mwaka.
Kwa upande wa Filamu vipengele vitakavyoshindaniwa ni Filamu bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Kiume na Muigizaji Bora wa kike.
Tuzo za EATV 2016 zinafanyika kwa udhamini wa Coca Cola na Vodacom Tanzania .

Utofauti wa tunzo hizi na zingine ni kwamba kwenye hizi msanii mwenyewe ndio anajipendekeza kuwania tunzo fulani kwenye kipengele fulani huku akiambatanisha na kazi yake.
Pia msanii anayefuzu kushiriki tunzo hizi lazima awe amesajiliwa na Basata au bodi ya sanaa ya nchi husika africa mashariki.
EATV Awards imeanza na vipengele 10 ambavyo ni:-

1. Mwanamuziki bora wa kiume

2.Mwanamuziki bora wa kike

3. Mwanamuziki bora chipukizi

4. Kundi bora la muziki

5. Video bora ya muziki

6.Wimbo bora wa mwaka

Kwa upande wa filamu ni

7. Muigizaji bora wa kiume

8. Muigizaji bora wa kike

9. Filamu bora ya mwaka

Jana yaliwekwa wazi majina ya wasanii kutoka vipengele viwili ambayo yamepita kuwania tuzo husika kila kipengele wamepita wasanii watano ambao watakwenda kupigiwa kura nayo ni Muigizaji bora wa kiume wa kiume na Msanii bora chipukizi.

1.MUIGIZAJI BORA WA KIUME
Nominees:
  • meya.png

    Meya Shabani Hamisi - Facebook Profile
  • gabo1.png

    Salim Ahmed (Gabo) - Safari ya Gwalu
  • duma.png

    Daudi Michael Tairo (Duma) - Mfadhili Wangu
  • dotto.png

    Dotto Hussein Matotola - Likichwa Lala
  • mkukila.png

    Saidi Ally Mkukila - Ndugu wa mume



2.MWANAMUZIKI BORA CHIPUKIZI
Nominees:

  • manfongo.png

    Amani Hamisi (Man Fongo) - Hainaga Ushemeji
  • feza.png

    Feza Kessy - Sanuka
  • rucky.png

    Rukia Jumbe (Rucky Baby) - Give me some more
  • mayunga.png

    Mayunga Nalimi (Mayunga) - Nice Couple
  • bright.png

    Rashid Said (Bright) - Nitunzie
3.MUIGIZAJI BORA WA KIKE
Nominees:
  • chuchu.png

    Chuchu Hansy - Laura
  • rachel.png

    Rachel Bitulo Njingo - Nimekosea wapi
  • kajala.png

    Frida Kajala Masanja - Hii ni laana
  • khadija_0.png

    Khadija Ally - 3 Days
4.FILAMU BORA YA MWAKA
Nominees:
  • facebook_3.png

    Facebook Profile
  • gabo.png

    Safari ya Gwalu
  • mfadhili.png

    Mfadhili Wangu
  • laana.png

    Hii ni Laana
  • wapi.png

    Nimekosea Wapi?
5. KUNDI BORA LA MWAKA
Nominees
. Navy Kenzo

.Mashauzi Classic

.Team mistari(Kenya)

.Sauti sol (Kenya)

.Wakali Wao

6.VIDEO BORA YA MWAKA
Nominees
. Namjua-Shetta

.Njongereza-Navio

.Aje-Alikiba

.Don Bother- John Makini

.Ndindindi-Lady Jayeed

7. MWANAMUZIKI BORA WA KIUME
  • Alikiba
  • Ben pol
  • Mwana FA
  • Sheta
  • G nako.
8 MWANAMUZKI BORA WA KIKE
  • Vannesa Mdee
  • Lady jaydee
  • Lina Sanga
  • Rubi
  • Lilian Mbabazi(Uganda)
9 .WIMBO BORA WA MWAKA
  • Moyo Mashine-Ben pol
  • Aje-Alikiba
  • Ndindindi-Lady jaydee
  • Don Bother- John Makini
  • Kamatia Chini-Navy kenzo.
NB: ukiona msanii wako hayupo kunaweza kuwa kumesababishwa na sababu zifuatazo
  • Inawezekana hakutaka kushiriki hivyo hakuchukua fomu
  • Inawezekana hajasajiliwa BASATA hivyo hana vigezo vya kushiriki
  • Inawezekana hakukidhi vigezo vya kuwa kwenye hivyo vipengele.
Zoezi la kupiga kura litafunguliwa leo saa sita nitawaweke utaratibu wa kupiga kura na maelezo mengine..
itaendelea....
Kwa hiyo Kiba kachukua fomu kwenye shindano hili??!!
Kweli Kiba kachanganyikiwa
 
Jamani mbona kila baya mnawapa WCB? huwajui wabongo harmonize na raymond wangeshiriki wakashinda ungesikia matusi kama bosi wao ndio ameshawishi wapewe!
Nafikiri kwa hili wametumia busara sana kuziacha halafu mwakani ndio washiriki
By the way wengi sana na waliofanya vizuri hawapo mfano Baraka da prince,nick wa pili,joh makini
Ila nafikiri utaratibu wa kujipendekeza ndio mbovu
labda...
 
Kwa hiyo Kiba kachukua fomu kwenye shindano hili??!!
Kweli Kiba kachanganyikiwa
huo ndio ulikuwa utaratibu ilikuwa wewe mwenyewe unachukua fomu na si kiba pekee ni kila msanii aliyeshiriki humo alichukua fomu.
 
hakika
UTABIRI WANGU:
-Mwanamuziki KE..Vmoney
-Mwanamuziki ME..Ali Kiba
-Wimbo bora..Ben pol moyo mashine
-Video bora..Lady JD ndindindi
-Kikundi bora..Navy Kenzo
-Chipukizi..Man fongo
-Muigizaji ME..Gabo
 
Hamna aliepuuza sema utaratibu uliotumiwa na eatv sijawah kuusikia sehemu yeyeto ile duniani, yani eti wasanii watume wenyewe majina yao na kazi wanayotaka iwe nominated huo si upuuz kabsa kwann wasingekaa wenyewe eatv na kuchagua kazi nzur na iwe nominated then waseme watu wapige kura kupata mshndi, utaratibu mbovu ndo umepelekea hayo
lakini mbona wasanii wengine wamechukua fomu kwani inapunguza nini?
 
Back
Top Bottom