Bado tv na radio station zinanguvu dunia kote sio tz tu hawa si ndio wanaolia nyimbo zao zipigwe MTV base urban TV na nyingine nyingine halafu leo wanakunya nyodo kweli masikini akipata matako hulia mbwata
Kaka Kauli ya Diamond haihitaji uwe na Degree ili uielewee kama utakuwa tayari kuelewa tutakuelewesha ......Kwanza Diamond Hajasema kuwa Hategemei kabisa Radio na TV hiyo moja! Pili diamond kaongea kwa kuangalia sahizi maisha yanavyokwendaa...
Nianza hivi Diamond bado anategemea media kusambaza kazi zake na Social networks kusambaza kazi zake alichosema sasa ni kuwakutumbusha tu watu wa Media kuwa sio RADIO NA TV tuu ndio zinauwezo wa kusambaza kazi zake ikiwa na maana Hategemei Radio na TV tuu hapana Hata social netwks nazo pia anazitegemea!
Ukweli wa alicho kiongea upo wazi kabisa kabisa....zamani ilikuwa msanii ukitoa wimbo wako ili uchezwe kwenye Radio au TV ilikuwa ni lazima Uende na kazi yako kwenye kituo husika cha TV au RADIO ukaitambulishe Kazi yako hapo ndio wataicheza napo wakiamua ndio maana kukawa na Media tour au mtu anatoka mkoa Kuja Dar kuleta kazi yake mfano Diamond alikuwa anaenda hadi IRINGA?, Ruvuma huko kupeleka kazi zake kwenye vituo vya Radio ili waicheze lakini kadri siku zinavyozidi kwenda mambo yanabadirika sahzi sio kama zama hizo sahizi Diamond anaweza kutoa wimbo akaweka Link kwenye account yake Ya instagram au Twitter na Asilimia 99 ya media za Bongo wataucheza huo wimbo wake baadae! Nafikiri unaona tofauti
Radio na TV ZOTE zinazo cheza kazi za Diamond nje ya Tanzani si dhani kama diamond anapeleka kazi zake huko kote,hao wote wanaona kazi za diamond kupitia Mitandao ya kijamii.....na hasa ukurasa wake wa Insta au twiiter .....fikiria tuu kwa akili ya kawaida hivi diamond huwa anaenda Australia kupeleka kazi zake? Kaenda uingereza na ulaya kwa ujumla kupeleka kazi zake? Ghana je kaenda? Nasehemu zingine za Afrika? Kama hajaenda kazi za diamond mpya wanazipata wapi?
Ni vile tuu watanzania hatujataka ukweli tukiambiwa wala Mabadiliko hatuyataki.....ila huo ni ukweli kama Mtu una Followers MILLIONI 3 INSTA una followers Twitter na Ufollowers Facebook bado utategemea tuuu Radio na TV? Mkitaka kama nyinyi mnavyosema means Diamond asiwe ana post kazi zake kwenye mitandao ya kijamii ila awe anapeleka tuuu kwenye Radio na Tv halafu wale wa kwenye mitandao ya kijamii watasikia huko unadhani inawezekana?
Jiulize kitu kidogo cha msingi! Ishu ya Makonda na Vyeti Feki sahizi inaongelewa Tanzania nzima! Wewe uliisikia kwenye TV au RADIO kwa mara ya kwanza? Kama Sio mitandao ya Kijamii hicho kitu kingesikika hivyo? Huo ni mfano mdogo tuu kuonesha ni kwa kiasi Gani mitandao ya kijamii ina nguvuu??
Jamani ukweli ubaki kuwa ukweli Now mtu aliepo kwenye mitandao ya kijamii hana haja Ya kusikiliza Taarifa ya Habari iwe kwenye TV au kwenye Radio kwasababu yote yatakayo ongelewa huko alisha yaona muda mrefu kwenye MITANDAO ya kijamii!!
Ifike muda twende na wakati sahizi sio zama zile mambo yanabadirika! Mbona Vituo vingine havijakasirika iwe EATV tuu kwanini? Wao ndio wana uchungu sana?
Think umenielewa!
-Danya-