EATV na EA radio wamjia juu Diamond , kisa kusema hategemei redio na Tv pekee

EATV na EA radio wamjia juu Diamond , kisa kusema hategemei redio na Tv pekee

Kumbe kisa tuzo hahahahahaha hata ingekuwa mm siwezi kupeleka jina langu eti niwe nominated aaaaah waendelee tu kumchunia
 
kwenye kipindi cha planet bongo watangazaji wa Dullar na juma junior wametokwa na povu baada kusikia kauli ya diamond aliosema sasa hivi akitoa nyimbo hategemei radio na TV pekee kusambaza mziki wake Bali a natumia mitandao ya kijamii kuhakikisa mziki wake unafika kwa mashabiki kwa ukubwa alionao, tofauti na zamani redio na TV zilikuwa na nguvu kumshusha msanii
Dullar amesema diamond amekosea kutoa kauli hiyo na ametoa boko na angesema hivo kabla hajawa Diamond wakati anatoa mbagala
Huku juma junior akisema diamond ametoa kauli ya kijiweni na ya kijinga.

Ikumbukwe diamond na EA media wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu kiasi hawachezi nyimbo za Diamond kwenye vituo vyao.
Ilibuka upya baada ya diamond kugoma kushiriki tuzo za EATV awards ,diomond hakuchukua form za kushiriki.
Hao EATV &EA RADIO na Dimond wote wapuuzi.
Vituo vyao havichez nyimbo zake sasa shida iko wapi?Diamond kama haamini katika TV na redio nae asipeleke hizo nyimbo zake?Asiseme maneno hayo kwa sababu yeye ni ndio CEO wa wasafi, akisema yeye ndo image ya WCB je hizo media zikiwapotezea hao wasanii wadogo wa WCB itakuaje?Kibiashara anaichafua brand ya kampuni yake,asidhani yeye ni Diamond, now ana kundi la watu wanaotembea kwa nyota yake, aseme hayo akiwa na redio na tv yake yenye ushawishi
 
Kama Diamond kasema hivyo basi nikweli kakosea sana

Mashabiki ndo wanaopromote bifu
 
Bado tv na radio station zinanguvu dunia kote sio tz tu hawa si ndio wanaolia nyimbo zao zipigwe MTV base urban TV na nyingine nyingine halafu leo wanakunya nyodo kweli masikini akipata matako hulia mbwata
Kaka Kauli ya Diamond haihitaji uwe na Degree ili uielewee kama utakuwa tayari kuelewa tutakuelewesha ......Kwanza Diamond Hajasema kuwa Hategemei kabisa Radio na TV hiyo moja! Pili diamond kaongea kwa kuangalia sahizi maisha yanavyokwendaa...

Nianza hivi Diamond bado anategemea media kusambaza kazi zake na Social networks kusambaza kazi zake alichosema sasa ni kuwakutumbusha tu watu wa Media kuwa sio RADIO NA TV tuu ndio zinauwezo wa kusambaza kazi zake ikiwa na maana Hategemei Radio na TV tuu hapana Hata social netwks nazo pia anazitegemea!

Ukweli wa alicho kiongea upo wazi kabisa kabisa....zamani ilikuwa msanii ukitoa wimbo wako ili uchezwe kwenye Radio au TV ilikuwa ni lazima Uende na kazi yako kwenye kituo husika cha TV au RADIO ukaitambulishe Kazi yako hapo ndio wataicheza napo wakiamua ndio maana kukawa na Media tour au mtu anatoka mkoa Kuja Dar kuleta kazi yake mfano Diamond alikuwa anaenda hadi IRINGA?, Ruvuma huko kupeleka kazi zake kwenye vituo vya Radio ili waicheze lakini kadri siku zinavyozidi kwenda mambo yanabadirika sahzi sio kama zama hizo sahizi Diamond anaweza kutoa wimbo akaweka Link kwenye account yake Ya instagram au Twitter na Asilimia 99 ya media za Bongo wataucheza huo wimbo wake baadae! Nafikiri unaona tofauti

Radio na TV ZOTE zinazo cheza kazi za Diamond nje ya Tanzani si dhani kama diamond anapeleka kazi zake huko kote,hao wote wanaona kazi za diamond kupitia Mitandao ya kijamii.....na hasa ukurasa wake wa Insta au twiiter .....fikiria tuu kwa akili ya kawaida hivi diamond huwa anaenda Australia kupeleka kazi zake? Kaenda uingereza na ulaya kwa ujumla kupeleka kazi zake? Ghana je kaenda? Nasehemu zingine za Afrika? Kama hajaenda kazi za diamond mpya wanazipata wapi?

Ni vile tuu watanzania hatujataka ukweli tukiambiwa wala Mabadiliko hatuyataki.....ila huo ni ukweli kama Mtu una Followers MILLIONI 3 INSTA una followers Twitter na Ufollowers Facebook bado utategemea tuuu Radio na TV? Mkitaka kama nyinyi mnavyosema means Diamond asiwe ana post kazi zake kwenye mitandao ya kijamii ila awe anapeleka tuuu kwenye Radio na Tv halafu wale wa kwenye mitandao ya kijamii watasikia huko unadhani inawezekana?

Jiulize kitu kidogo cha msingi! Ishu ya Makonda na Vyeti Feki sahizi inaongelewa Tanzania nzima! Wewe uliisikia kwenye TV au RADIO kwa mara ya kwanza? Kama Sio mitandao ya Kijamii hicho kitu kingesikika hivyo? Huo ni mfano mdogo tuu kuonesha ni kwa kiasi Gani mitandao ya kijamii ina nguvuu??

Jamani ukweli ubaki kuwa ukweli Now mtu aliepo kwenye mitandao ya kijamii hana haja Ya kusikiliza Taarifa ya Habari iwe kwenye TV au kwenye Radio kwasababu yote yatakayo ongelewa huko alisha yaona muda mrefu kwenye MITANDAO ya kijamii!!

Ifike muda twende na wakati sahizi sio zama zile mambo yanabadirika! Mbona Vituo vingine havijakasirika iwe EATV tuu kwanini? Wao ndio wana uchungu sana?

Think umenielewa!

-Danya-
 
Oyaa, kubali yaishe Diamond hapaswi kutamka hayo maneno kwa biashara anayoifanya.

Unazidiwa upeo wa kufikiri hadi na watu wenye akili fupi ya shule ya msingi tu.
Alipaswa kusemaje? Hivi hapa bongo vituo vikubwa ni Cloud na EATV hawa EATV wanao taka kusambaza kazi za Diamond kwa Siku wanacheza mara ngapi kazi zake kwenye Radio na TV tuanzie hapo
 
Ifike muda twende na wakati sahizi sio zama zile mambo yanabadirika! Mbona Vituo vingine havijakasirika iwe EATV tuu kwanini? Wao ndio wana uchungu sana?

Think umenielewa!

-Danya-

Watu wanabishana huku ukweli wanaujua, maana ndogo ya tafsiri "Sitegemei Radio na TV PEKEE", neno PEKEE wameamua waliondoa kwa manufaa yao binafsi.
 
Mondi ana cheti cha lasaba kweli?

Okay,uwezo wake wa kufikiri unaishia hapo
 
EATV na EA radio wana muda sana hawapigi nyimbo zake..wala huwa hawaandiki chchtr kizur kuhus diamond labda kiwe kbaya..
sa povu la nn???
 
EATV na EA radio wana muda sana hawapigi nyimbo zake..wala huwa hawaandiki chchtr kizur kuhus diamond labda kiwe kbaya..
sa povu la nn???
Ndo maana wamepovuka wamejishtukia dongo linawahusu
 
Hivi mi naona woooote humu mnatoka povu tuuuu bureeee kwa story za kutunga....na hao EATV ndo mabogaz kabisaaaaa yaaan wameonyesha kuwa majamaa sio profesional kabisa na kazi zao..hawana tofauti namii nnaeshinda mitandaoni kusoma umbea kila siku...ATAKAELETA USHAHIDI HAPA KWAMBA DIAMOND ALITAMKA HAYO MANENO POPOTE PALE BASI NA ALETE... Otherwise msituchoshe na maporojo yenu,na hao EATV ni mbururaaaaz!!!!!
 
Video hii hapa ya watangazaji wa EATV
MOD naomba uipandishe juu
 
Uwepo WA TV na Radio ndio umewatoa wasanii wengi hususa na yeye pia.

Kauli aliotoa kiufupi hailidhishi... Je ulishawahi kuwaza kuwa Radio na TV visinge kuwepo, Wasanii Na Vipaji kiujumla tunge vitambua kwa namna gani. Zaidi Sanaa ingejawa na Ubinafsi usio pingika.
 
Hebu leteni iyo interview tusikilize wasitafute kiki kupitia mondi kwanza hayo maelezo kibaya kaongea nn kunaubaya ukisema hutegemei tu radio na tv bali na social media hao EATV waache ubashite afu wamemkomalia mondi kivipi au kisa alisusia tuzo uchwara zao si wanamsanii wao pendwa waendelee nae WCB hatutoi kiki mfyuuu[emoji57]
 
Back
Top Bottom