Ebu niambie unapoona hii kitu unamkumbuka nani katika mahusiano

nilimwandikia barua,kesho yake nakuta barua yangu imebandikwa nyuma ya mti wa kengele,aibu shule nzima.
 
nilimwandikia barua,kesho yake nakuta barua yangu imebandikwa nyuma ya mti wa kengele,aibu shule nzima.

huyo alikuwa anakuchukia mpaka anakuogopa yaani pole lakini.
 
Nakumbuka pale Ubungo Kisiwani
kulikuwaga na watoto wakali kweli
yaani ila mm nilimpenda sana
ILUMINATHA jaman maana yule
mtoto wakichaga ni shida. Kwanza mrefu,mwembamba wastani,ana
boflo kijungu (kalio la wastani)
,macho yake bwana hajakuita
umeitika cha mwisho sasa mtoto
alikuwa na sauti nzuri yenye
rafudhi ya kichaga akiongea mtoto wa mwanamke mwenzie huku hoi
unaambiwa. Jamani natamani
niludi shule ya msingi jaman
 
Simkumbuki kwa mazuri Mwalim Njiku Bomani Primary School Kiomboi Iramba yule mwalimu alinitesa sana nikiwa Std VII kila inapofika kipindi chake ananitoa darasani nasimama nje ya darasa na jua kali hadi anamaliza kipindi hata kama siku hiyo ni double, kisa ati nimemkataa wakati kusema kweli nilikuwa hata siijui hiyo biashara. Sitomsahau ktk maisha yangu ni kama imeniathiri hivi. maana alikuwa akiingia tu ananitoa nilikuwa naumia sana sana.
 
Mhhh nA nyie yaani tangy while ya msingi mnafanyA mambo hayooo wengine had tunamaliza kidato cha NNE hatujui kidato cha tank siku nimefanyaaa nimeumiAaaa he nikasema sirudiii tens nikajaribu tena na tens hehehehedh labda halo nimkuMbuke huyo mtumzima mwezangu he he
 
Niliwahi fumwa na barua nikiwa std v. Nilipewa mbakora za haja mpaka nikala kiapo kuwa mapenzi ni kichapo nikazila kabisaaa. Nilipomaliza f.vi nyumbani wakaniuliza unampango gani mbona hatukusikii, nikawaambia sitaki si mlinichapa? Ilikuwa kichekesho maana walianza kunipa hela za kuanza kudate tena, lakini nikawa nakunywa na washikaji. Miaka miwili baadaye baada ya kukalishwa sana ndo nikawa na mahusiano kwa mara ya kwanza.
 
\Namkumbuka my Friend Erotica

please come back tunamiss michango yako sana
 
Last edited by a moderator:
mi nakumbuka nilikuwa nampenda mtoto mmoja tulikuwa tunalingana umri lakini alikuwa na utoto kuliko mimi. alikuwa mzuri na msafi na alikuwa anaishi makazi bora soweto. Siku hizi ni mtangazaji wa radio one anaitwa kwa fujo. Wakati mi nampenda kwa fujo nilikuwa napendwa na kijana alikuwa akiitwa jolvadi. Huyu alishabalehe kabisa na alikuwa na vigimbi ila hatukuwa tunathubutu kumtania maana alikuwa na maguvu. Siku ya siku akaniandikia barua akampa kijana mwingine mkubwa alikuwa akiitwa godlove. Nilipoisoma niliogopa sana na nikawa namkwepa. Tukiwa darasani nikimwangalia ananikonyeza. Mara akaanza kunichukia. Siku ya kufunga shule nikapata taarifa toka vyanzo vya kuaminika kuwa jolvadi anataka kufunga shule na mimi na kwa fujo (kwa wale wa dot com mtu kufunga shule na wewe ni kukupiga kipigo cha mbwa mwitu mkishatoka eneo la shule). Basi nikaogopa nikaenda kushtaki lakini hakuitwa badala yake nikaambiwa niondoke mapema na mwalimu milinga (mama bonii). tulivyofungua shule yakawa yameisha. huyu jolvadi niliskia alikuwa mererani, sasa hivi sijui yuko wapi.
 
Uwanja wa dhambi Itetemya s/msingi Tabora.Ukichokoza mtu unapelekwa mkasulubiane mwee hatari sana utoto!
 
Yaani huku watu wengine wanajaribu kutoa reminds zao za primary wewe umetoa short and clear kwamba hao woooote wa kitambo hicho now ni makoloni yako kitu ambacho nadhani ukweli wake ni asilimia kumi 10%,...sio hii tu post nyingi huwa hujichoshi yaani we unadondoka simple and clear..
salute broh!
 
Enzi hzo

KWAKO NIKUPENDAYE,
S.L.P NATA NIWE WAKO,
NAKUPENDA SANA.
12/3/2005

Kwako ni kupendaye

Nimatumaini yangu wewe ni mzima wa afya kabisa utakapo kujua hali yangu nami ni mzima sanaa
Barafu/lengo/epo la balua hii ni kutaka kukwambia kuwa wewe amina mimi nimetokea kukupenda sana ningeomba niwe nawe kimapenzi tusiachane hadi ndoa,yaani usiku si lali nakuota wewe unaniumiza sana amina naomba unikubalie mwenzako,napo kunywa maji kwenye gilasi nakuona amina umetokea kuutesa moyo wangu naomba usiende kunisemelea kwa mwalimu wala kwa mama ako atanichapa tutakuwa tunafanya kwa siri sana amina
Nimatumaini yangu ombi langu litakubaliwa naomba unirudishie majibu na majibu mpe alie kupa balua hii

Ndimi nikupendaye sana
Unautesa moyo wangu


Enzi hizo ni shida na mwandiko mbaya karatasi chafu wakumtuma mpaka umnunulie bagia demu akipokea tu barua humuongeleshi
 

duh! mkuu hataki kujichosha
 
mmmmh kipindi hicho hii kitu sikua hata naijua

kwanza ilikua ukiwa na mtu unaonekana muhuni tulikua tunawatenga wavulana kabisa

anyways ...maisha ya sasa yamebadilika kitoto cha chekechea kina boy
Ni kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…