Edgar Kibwana: Mayele inabidi ajifunze sana kwa Kagere

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Mchambuzi wa kipindi cha michezo cha Clouds Fm, Edgar Kibwana akichambua mechi ya jana ya Simba dhidi ya Namungo, amesema mshambuliaji wa Yanga mkongomani Fiston Mayele ana mengi ya kujifunza kwa mshambuliaji wa Simba Meddi Kagere!

Edgar Kibwana aliendelea kufafanua zaidi, " Mayele ambaye ameanza mechi nne na kucheza dakika nyingi mpaka sasa ana magoli mawili sawa na Kagere ambaye yeye huanzia benchi na kucheza dakika chache nae ana magoli mawili"

" Mayele amezungukwa na wachezaji bora wengi lakini bado anasuasua katika ufungaji wa magoli tofauti na Kagere ambaye timu yake kwasasa haichezi vizuri" Edgar Kibwana aliongeza zaidi.

Kwahyo Edgar Kibwana akahitimisha kwa kusema, ni wakati sasa wa Fiston Mayele kujifunza zaidi kwa mkongwe Kagere kwenye ufumaniaji wa magoli ili awe bora zaidi!!

NB:
Namuunga mkono Edgar kwani Fiston anacheza soft soft sana anahitaji kupambana zaidi
 
Vile vitu havifundishiki ule ni uwezo binafsi na nishasema mpaka msimu unaisha hakutakuja kuwa na heading matata kama ya kagere

Mayele ni upepo tu na ndio maana hata magoli yake anashangilia saaana as if ye mwenyewe haamini (mbahatishaji)

Kinachomponza zaidi ni kulewa sifa, jamaa anavimba sana anajikuta ni mchezaji tegemezi kila time camera inammulika yeye tu. Hiyo tuliiona kwa aucho lakini taratibu tunaona uelekeo wa upepo ni tofauti, mechi ya juzi sijui hata kama bechi alikuwepo
 
Hayo ni mawazo ya mchambuzi, Kama anamuona Kagere ni Bora kuliko Mayele huwezi kumpinga. Mwisho wa msimu kila kitu kitakua hadharani. Huitaji misuli ya shingo ikutoke kumtetea mchezaji, Kazi yake itaongea.
 
Mtu akileta hoja ya kitaalamu na wewe ukachangia ushabiki utaonekana mbangaizajk Tu.
Mleta mada ana hoja nzuri lakini kusema Mayele anacheza soft sijui kwako ulifumdishwa nini maana ya Soft. Mayele mshambuliaji mgumu ambaye tatizo lake ni moja tu, converting rate yake iko chini na hachukui jitihada kuiinua.
 
Ndio nakubali hata mm Fiston Mayele na Yanga yake wanapenda misifa mingi wakati ligi ndo kwanza inaanza, ngoja tuone nani atakua mkali wa kufumania nyavu kati yake na MK 14
 
Aucho akipata minor injury ndiyo maana alipumzishwa
 
Uko sahihi magoli yote ya Kagere ni uwezo binafsi ,kama goli la jana mazingira kama yale ngumu sana kufanya maamuzi yale,angalia magoli waliyokosa kibu na bocco
 
Kwa hiyo na wewe huna tena lawama kwa wachambuzi wa clouds, kwani mlikuwa mnawapigia umbea sana hapa
 
Mkuu umechangia thread kishamba sana,punguza nongwa kama kushangilia ata akina Ronaldo et all wanashangiliaga kwa nguvu sana as if wamebahatisha la hasha ni uwezo wao binafsi jana Mr Kagere lile goli nilimkubali sana mimi kama mpenda mpira wa miguu na sio shabiki wa mpira Kagere alionyesha ukomavu na uwezo binafsi katika soka as a pro,relax na penda mpira achana na ushabiki itakushushia heshima hapo ulipo its my hope mashabiki wenzie wasiopenda mpra watakusapoti..kila la heri hapo ulipo.
 
Nchi ina uhuru sana wa kila mtu kutoa mawazo yake ila naona kama wachambuzi uhuru wao unapitiliza natoa ahadi kwa kushirikiana na GSM hili jambo tutaliweka sawa
 
Yanga hawatengenezi chances nyingi za kufunga kama Simba.

Lakini pia Fiston ni mchezaji daraja la chini kuliko Kagere namfananisha na Michael Sarpong tu.
 
Yanga hawatengenezi chances nyingi za kufunga kama Simba.

Lakini pia Fiston ni mchezaji daraja la chini kuliko Kagere namfananisha na Michael Sarpong tu.
Wewe siyo wa kuongea maneno ya kiwango cha chini kama haya labda kama umeandika ukiwa baa.
 
Ndio usoft wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…