SoC01 Edgar Lungu Ameonesha Njia, Tuige Kulinda Amani

SoC01 Edgar Lungu Ameonesha Njia, Tuige Kulinda Amani

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 22, 2021
Posts
7
Reaction score
5
Na Nkuruma wa Karne ya 21.

Imekuwa kawaida kwa mataifa ya Afrika kuongozwa na Chama kimoja mfululizo huku chaguzi zikifanyika kuwahalalishia watawala mipango yao ya kudumu madarakani na kuachiana ndani ya Chama chao kama wanavyotaka.

Mambo haya yamekuwa yakilelewa na jamii yenyewe kupitia mfumo unaowekwa na watawala wa kuiandaa jamii kutokujihusisha na masuala ya siasa ya nchi na badala yake kuwafanya wawe wafuasi wao tu ili wao (waliopo madarakani) waendelee kutawala na kufanya mambo yao bila bughuza.

Hii imefanya katika jamii za Kiafrika hasa hili ni kubwa zaidi, kwamba uchaguzi siyo njia ya wananchi kuamua Nani wawe viongozi wao bali ni kitendo cha kupitia madhila ya vurugu, vipigo kwa wasio na hatia na watawala kujitangazia ushindi mnono hata kama kura zilizopigwa na wananchi hazikuwatosha kuwapa ushindi huo. Na hiki ndicho chanzo kikubwa Cha machafuko katika jamii nyingi za Kiafrika, wanasiasa wabinafsi wasiokuwa tayali kukabidhi madaraka kwa hiari kwa kuheshimu kura za wananchi.

Lungu Edga, ameionesha dunia kuwa jambo hili linawezekana kabisa katika jamii za Afrika, ameitafsiri Demokrasia kwa vitendo na maneno ya kishujaa Sana kufuatia uamzi wake wa kuachia madaraka kwa hiari na kutoa kauli zenye kuunga mkono ushindi wa mpinzani wake wa muda mrefu aliyeshinda uchaguzi huo kwa njia ya kura za wananchi.

Lungu Edga, ambaye amekuwa madarakani akiongoza Taifa la Zambia tangu Mwaka 2015, amepoteza kiti hicho baada ya mpinzani wake Hakainde Hichilema kushinda uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa.

Hakainde Hichilema ameishika nafasi hiyo kupitia uchaguzi huo ikiwa ni Mara yake ya sita katika kuwania nafasi ya Urais katika Taifa hilo ambapo historia inaoeleza kuwa amewahi kuwania Urais Mara tano hapo awali lakini hakuwahi kufanikiwa kutimiza ndoto yake ambayo imekuja kutumia mwaka huu 2021.

Hata hivyo, mapito yake hayatofautiani Sana na maisha wanayoyaishi wapinzani wa Kisiasa Afrika kwani amekuwa akikabiliwa na madhila Mara kadhaa ikiwemo kuswekwa magerezani na misukosuko mingine ya namna mbalimbali.

Hatua ya kuingia Ikulu mpinzani huyu aliyegombea Mara tano bila mafanikio na hatimaye kutimiza ndoto hiyo katika awamu ya sita inatoa funzo kubwa kwa watawala wa Afrika ambao bado wanaamini kuwa wanaweza kujiapiza kutawala milele katika mataifa yao.

Wanapaswa kutumia mfano wa Zambia na hatua aliyoichukua Rais Edga ya kuachia ikuli na kukabidhi nchi kwa Mpinzani wake aliyempitisha katika madhila kadhaa huko mwanzo kama ni somo linalotufahamisha kuwa ipo Siku yaja nayo itatimia kuwa yule unayemtesa leo atakuja kuwa juu zaidi ya ulipo wewe na wewe itakuwa chini zaidi ya alipo yeye leo.

"Demokrasia hai na inayofanya kazi ni ile ambapo sauti za wananchi zinaweza kusikilizwa bila bughuza" ni maneno ya kishujaa aliyoyatoa Edga Lungu akitangaza uamzi wake wa kuyaunga mkono matokeo ya Urais ambayo talimpa Ushindi Mpinzani wake Hakainde Hichilema.

Kwa somo hili, Waafrika, wanasiasa wa Afrika na wanaharakati wafuasi wa siasa, ipo haja ya kujifunza kuyatii maamzi ya wananchi kwa mustakhabali mzima wa amani na maendeleo ya nchi.

Vitendo vya watawala kujiapiza kutawala milele katika mataifa yao wakidhani wao ndio wenye hati miliki ya Uongozi wa Taifa hilo, matumizi mabaya ya vyombo vya dola, majeshi, polisi, magereza na mahakama kulazimisha watawala waendelee kudumu ikilu hata kama hawakubaliki na waliowengi matokeo yake huwa ni kuchafua amani ya jamii husika.

Kama alivyowahi kueleza Nelson Mandela, Rais wa Zamani ya Afrika Kusini kuwa njia pekee iletayo amani na watawala kudumu madarakani kwa amani Ni maridhiano ya amani kwa kuheshimu maoni ya wananchi, Mandela alitahadhalisha kuwa Matumizi ya nguvu kwa kutumia polisi, magereza na mahakama, ama tume za kihuni za uchaguzi hakuwafanyi watawala wadumu mamlakani Bali, japo kwa kupitia maumivu makali Sana huwaandaa wananchi nao kutumia nguvu inayofanana na hiyo ya watawala ili kudai mageuzi wanayoyataka. Na hapo ndipo amani hupotea.

"Wale wanaobeza maridhiano ya amani katika kutafuta changamoto za watu, hulazimisha matumizi ya nguvu katika kidai haki yasiepukike" ni moja ya kauli alizowahi kuzitoa Nelson Mandela akiwaonya watawala dhalimu wanaotumia hila kwa raia ili wadumu madarakani hata kama hawakubaliki na jamii zao.

Nami Mwana wa Lufunga nasisitiza, Afrika yenye siasa Safi za upendo, kuvumiliana na kupokezana mamlaka za uongozi kwa mujibu wa sheria na kwa kutii matakwa ya wananchi inawezekana, na kwakufanya hivyo, Afrika patakuwa mahali Safi pa watu wastaarabu kuishi kwa amani na si mahali pa waovu kufurahia huku wema wanaojaribu kudai yaliyo sawasawa wakipata taabu na madhila ya kitengenezwa kihuni dhidi yao ili kutimiza mipango binafsi ya wenye mamlaka, hayo hutishia amani ya Kesho Maana mioyo ya watu hufika mwisho wa uvumilivu. Kumwachia mpinzani Ikulu ikiwa ameshinda kihalali siyo udhaifu, Zambia na Edga ameionesha njia, tuige mema ili tuishi vema.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom