Makamu wa Raisi aliyewashuhudia Maradona na Pelle anakwambia MESSI ni habari nyingine wewe ambaye hata Supersport ni hadi uende kibandaumiza na jero lako unabisha hadi mishipa inakukakamaa
Kiukweli kizazi hiki tuna bahati ya kumshuhudia King Messi maana wachezaji wa sampuli yake huzaliwa kila baada ya miaka 2000
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mkuu unafahamu kama yeye kama mtaliano na mshabiki wa Ac milan ana maadui hawa wawili.
1. Timu ya Taifa Brazil ambayo ilikuwa ikizionea Timu za ulaya including Italy
2. Napoli,Timu ndogo iliokuja kuchukua ubingwa wa Italy na kuwabwaga ma giant kama Ac milan.
Pelle anatoka Brazill na Maradona ni wa Napoli,
Maelezo ya huyo mtu sidhani kama yana credibility hapa.
Ni kama umuulize Dalgish kama ronaldo ama Cantona alikuwa mchezaji mzuri.
Maradona kati ya 84 mpaka 91 alikuwa anachezea Napoli na katika prime yake miaka 4 makombe ya ligi italy 2 na nafasi ya 2 mara 2.
Timu ndogo kama Napoli kwa Effect ya mchezaji mmoja iliwachachafya sana vigogo wa Italy.
Huu ni.msimamo wa ligi Nafasi ya Napoli 1983 kabla ya maradona kutua
Sasa fikiria mchezaji mkubwa Duniani club kubwa zinamtaka anaondoka club kama barcelona na kwenda club inayokaribia kushuka daraja ya Napoli,then anawapa ubingwa tena mara mbili, na wakikosa ubingwa wanakuwa wa pili, hizi ndio sifa za wachezaji wazuri wa zamani.
Leo hii mtu kama Messi,ronaldo neymar etc hawaendi timu ndogo hata kwa ndumba, na siku zote watachagua wachezaji wazuri wawazunguke, siku messi akienda Argentina anakuwa wa kawaida sababu kule hawawezi kusajili. Maradona na hio hio average argentina aliipa Kombe.