hiram
JF-Expert Member
- Aug 1, 2013
- 266
- 393
Solidarity Rule ni sheria ya Fifa inayosema kwamba kama mchezaji atauzwa kwenda klabu ya ligi kubwa duniani basi asilimia 5 ya mauzo ya mchezaji huyo itagawanyishwa kwa timu zote alizochezea akiwa na miaka 12 hadi 23.
Hata klabu ya Simba itanufaika na sheria hiyo ambapo African Lyon, TP Mazembe na Simba zitahesabika kama klabu alizochezea Samatta akiwa na miaka 23 kushuka chini; kunifaika kwa Simba na African Lyon hakutokani na umakini wa viongozi wao bali sheria hii inalazimisha timu hizo kulipwa asilimia tano hizo.
Katika makala ya Jicho la Mwewe ya mwanaspoti 27/01/2020 mwandishi huyu alidai kuwa iwapo Msuva angeuzwa kwenda Benfica basi Yanga isingepata hata senti tano huku akijaribu kuutupia lawama uongozi wa Yanga hata hivyo anachokisema siyo kweli Iwapo msuva atauzwa kwenda benfica basi Yanga itanufaika na Fifa solidarity rule.
kuna vitu viwili mwandishi anavichanganya kwanza kuna hiyo 5% ambayo ni kama fidia ya kumlea mchezaji katika umri mdogo lakini pili kuna mkataba ambao klabu inaweka kwamba mchezaji huyu tunakuuzia na ukimuuza tutahitaji asilimia 20 ya mauzo, huu ndiyo mkataba waliouweka simba na mazembe na mkataba huu uliishia pale Mazembe tu
kutoka Genk kwenda Aston Villa ni Solidarity rule tu ndiyo inawabeba Simba kama itakavyo wabeba Yanga iwapo Msuva ataenda Benfica.
Waandishi wetu wajaribu kuwa makini