Ubaya Ubwela
JF-Expert Member
- Jul 24, 2024
- 1,353
- 3,060
Mtangazaji wa kipindi cha Jana na Leo kutoka Wasafi Fm, Edo Kumwembe amesema angekuwa mshauri wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe angemshauri kujiondoa katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti kisha atangaze kumuunga mkono mpinzani wake Tundu Lissu
Edo amesema “ningekuwa mshauri wa Mbowe ningemwambia Mbowe ajiondoe kwenye kinyang'anyiro na ajiondoe kable ya boksi la kura na atangaze kumuunga mkono Lissu”
Soma: Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA
Edo ameeleza sababu ya yeye kuwaza hivyo ni kutokana na Lissu kuungwa mkono na watu wenye ushawishi na nguvu katika siasa za upinzani hasa CHADEMA.
“watu ambao wanatangaza kuwa upande wa Lissu ni watu wazito sana kwa CHADEMA, John Heche Heche na ana kanda yake, Lema kwa kaskazini lema na kama angesema anamuunga mkono Mbowe kidogo watu wangeyumba, Lissu hao wote ni watu wazito sana kwenye hicho chama”
Ameongeza kuwa kama Mbowe atashinda atakuwa na wakati mgumu kuongoza bila uwepo wa watu hao watatu “fanya Mbowe umeshinda unaongozaje bila hao makamanda, na hao makamanda wana vitu moyoni ukiwasikiliza kulikuwa na mipango ya kuwaondoa kutoka kwa Freeman aweke watu wengine”
Pamoja na hayo amejaribu kuelezea namna watu hao walivyopambania CHADEMA kwa kukaa jela pamoja na kupigwa na polisi wakati mwingine.
Aidha amekumbusha kuwa moja ya pigo alilopata Mbowe ni kushinda kwa Wakili Deogratius Mahinyila Adv Mahinyila kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA ambapo pia anamuunga mkono Lissu