Edo Kumwembe: Ningekuwa mshauri wa Mbowe, ningemshauri ajiondoe katika kinyang'anyiro

Edo Kumwembe: Ningekuwa mshauri wa Mbowe, ningemshauri ajiondoe katika kinyang'anyiro

Uchaguzi wowote wa kidemokrasia ni kwenye sanduku la kura, uimara wa chama utatokea iwapo chama kitapitia kwenye njia za kidemokrasia kuweka viongozi wake madarakani. Chadema kikipita salama kwenye uchaguzi huu kwa njia ya kidemokrasia basi kitakuwa chama imara kuliko siku zote.
 
Mbowe kwenye hili Amefeli sana hata yeye ameshaliona hilo japokuwa it's too late. Mfumo umemuweka kati waliochoshwa na mfumo nao wamemuweka kati. Aikaeli wajina wangu watch out before its more than too late.
 
Mtangazaji wa kipindi cha Jana na Leo kutoka Wasafi Fm, Edo Kumwembe amesema angekuwa mshauri wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe angemshauri kujiondoa katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti kisha atangaze kumuunga mkono mpinzani wake Tundu Lissu

Edo amesema “ningekuwa mshauri wa Mbowe ningemwambia Mbowe ajiondoe kwenye kinyang'anyiro na ajiondoe kable ya boksi la kura na atangaze kumuunga mkono Lissu”

Soma: Godbless Lema: Namuomba Mbowe apumzike, amuachie Lissu afanye kazi ya Uenyekiti CHADEMA

Edo ameeleza sababu ya yeye kuwaza hivyo ni kutokana na Lissu kuungwa mkono na watu wenye ushawishi na nguvu katika siasa za upinzani hasa CHADEMA.

“watu ambao wanatangaza kuwa upande wa Lissu ni watu wazito sana kwa CHADEMA, John Heche Heche na ana kanda yake, Lema kwa kaskazini lema na kama angesema anamuunga mkono Mbowe kidogo watu wangeyumba, Lissu hao wote ni watu wazito sana kwenye hicho chama”

Ameongeza kuwa kama Mbowe atashinda atakuwa na wakati mgumu kuongoza bila uwepo wa watu hao watatu “fanya Mbowe umeshinda unaongozaje bila hao makamanda, na hao makamanda wana vitu moyoni ukiwasikiliza kulikuwa na mipango ya kuwaondoa kutoka kwa Freeman aweke watu wengine”

Pamoja na hayo amejaribu kuelezea namna watu hao walivyopambania CHADEMA kwa kukaa jela pamoja na kupigwa na polisi wakati mwingine.

Aidha amekumbusha kuwa moja ya pigo alilopata Mbowe ni kushinda kwa Wakili Deogratius Mahinyila Adv Mahinyila kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA ambapo pia anamuunga mkono Lissu
kwani edo hajui kuwa chadema ni chama cha ukoo?
 
Jinsi upepo unavyovuma ndani ya CHADEMA kwa asilimia kubwa Mhe. Mbowe hana chake tena. Mhe. Mbowe kubali yaishe na ujitoe kwenye uchaguzi wa tarehe 21.1.2025. Wanachama bado wanakupenda na utaendelea kupendwa kwa sababu umekitoa CHADEMA mbali.
unadhani Mbowe hajui nini kinaenda kutokea hyo tarehe 21.1.2025? Unadhani kwanini ameng'ang'ania?Hapo tutadanganywa eti anafuata Democrasia sio kweli ngoja tusubili hyo democrasia yake baada ya uchaguzi halafu tuilete humu kuijadili.
 
Inakera sana mtu kujifanya kila kitu ni mjuwaji.

Yeye ni mchambuzi wa soccer, awaachie wachambuzi wa siasa wachambuwe nyege tu zinamsumbuwa.
Kwa sababu amesema usilotaka kusikia,kuwa mchambuzi wa mpira hakumzuii kuchambua siasa na hii siyo mara yake ya kwanza kuchambua mambo ya siasa ameshaandika makala nyingi tu juu ya siasa za Chadema, na huyu ni mshabiki wa Chadema na inawezekana kabisa ni mwanachama pia. Hajavunja sheria yoyote ile kutoa maoni yake.
 

Attachments

  • GfMNLpyXYAA8ucg.jpeg
    GfMNLpyXYAA8ucg.jpeg
    58.9 KB · Views: 1
Hilo tukio lilinifurahisha lakini kiukweli nilihuzunika sana, Mbowe sio wa kufikia hatua ile.

Mbowe anatupa wakati mgumu wa kumkataa kwa heshima aliyoijenga juu yetu.
Mi najiuliza zile busara za mbowe zumeenda wapi??
Mbona kwa hapa ilipofikia haihitaji sayansi ya siasa kuona kwamba nyakati ni mbaya kwake hivyo anakwenda kuaibika tarehe 21?
Atafute namna abadili gia hewani atunze heshima kubwa aliyoijenga kwa miaka mingi kama mwamba wa siasa za upinzani hapa nchini kwa kujitoa kwenye uchaguzi huu.
MBowe akishindwa uchaguzi itakuwa ni fedheha kubwa sana kwake!!.
 
Back
Top Bottom