Edo Kumwembe: Simba ile ile, wachezaji wale wale, michuano ndio tofauti

Oldmantz

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
704
Reaction score
1,457
KAMA bao la penalti laini ya Saido Ntibazonkiza dhidi ya Asec Mimosas lingesimama kwa dakika zote tisini si ajabu mashabiki na viongozi wa Simba wangerudi katika dunia yao ya njozi kwamba bado wana timu bora kwa ukanda huu wa Afrika mashariki.

Si ajabu pia wangeendelea kuota ile njozi maarufu kwamba wao wanakuwa kitu tofauti linapokuja suala la michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Safari hii walikumbushwa tu kwamba timu yao ni ile ile tu ya kawaida ambayo wamekuwa wakiishuhudia katika miaka ya karibuni.

Ilianzia katika pambano dhidi ya Yanga. Lilikuwa ni suala la muda tu kabla Simba haijapokea kichapo kile cha mabao matano kutoka kwa mtani. Kibinadamu kama wachezaji wa Simba wangehisi kwamba wamewaangusha mashabiki wao basi wangejibu mapigo katika pambano lililofuata dhidi ya Namungo kwenye uwanja wa zamani wa Taifa.

Mwanaspoti
 
Amesahau na ROSE MHANDO kule Manungu, Wajelajela na Walima alizeti.
 
Jwaneng Galaxy ndio watathibitisha ukweli huu.
 
Huko ni kusumbuliwa na Simba kiakili.Hakuwa na timu ingine imuumizayo moyo?Kwa nini asiijadili hata Rayon Sports?Au hakuna wa kumlipa akiijadili Rayon?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…