Edo Kumwembe: Simba inaweza kuachana na Bwalya

Edo Kumwembe: Simba inaweza kuachana na Bwalya

IAmShedeOne

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2015
Posts
202
Reaction score
385
EDO: SIMBA WANAWEZA KUACHANA NA BWALYA

Rally Bwalya? Huu ni mtihani.

Kipaji kipo kwa Bwalya lakini hajawahi kuikamata Simba kama inavyotakiwa. Hata walipoondoka Luis Miquissone na Clatous Chotta Chama watu wengi walitazamia Bwalya avae viatu vyao lakini hakuvaa kama inavyotakiwa.

Bwalya anacheza soka laini, hana kasi, hana uamuzi wa haraka lakini pia ameshindwa kufunga mabao mengi au kutoa pasi nyingi za mwisho kama ilivyokuwa inadhaniwa.

Simba inapotawala mechi basi na Bwalya anakuwa miongoni mwa mastaa. Inapokuwa na mechi ngumu basi na Bwalya anapotea. .

Kwa mtazamo wangu Simba ikipata kiungo mwingine mzuri zaidi katika eneo la ushambuliaji basi wanaweza kuachana na Bwalya. Kama atahitaji pesa nyingi kwa ajili ya kusaini mkataba mwingine wa miaka miwili nadhani wanaweza kutulia kwanza na kutazama jicho lao kwingine.

Hauwezi kulaumiwa na mashabiki kwa kuachana na Bwalya.” - Edo Kumwembe.

#KanunguJR

sportsarena_tz~p~CbtyC2wqdNa~1.jpg
 
siku zote mbumbumbuuuu fc hawawajui wachezaji wazuri, kama tulivyo taka kufanya kwa sakho, mkijichanganya tuu tunamwai pale terminal 3
 
Pale Simba wakuachwa ni wengi tu ,anzia Medi,Mugalu,Nyoni ,Muzamiru,yule Babu Onyango
,Boko.
Simba watulie ili walete ingizo jipya lenye tija kwa timu.
 
Bwalya Jina kubwa- uwezo mdogo, toka amekuja Simba hakuna kitu kikubwa amefanya. Chama kaondoka- karudi kafanya mambo makubwa kuliko Bwalya aliekuwepo muda wote, mipira yake mingi anarudi nyuma- wamuache tu kwa kweli!
 
Mzamiru mtu na nusu wewe...anaachwaje kwa mfano!?
Hamna kitu pale mdhamiru....
Anacheza holding za kizamani .... Timu ikiwa inafanya buildup ya Attacking anakua ziro kabisa...
Pass accuracy 40%
Maamuzi 45℅
Anakaba vizuri .... Lakini akikamata mali ndo ohooo !!! Unapomkataa

Sent from my FTE171A using JamiiForums mobile app
 
Wabongo aisee kwa kubadilika kama vinyonga. Huyu kuna kipindi aliimbwa sana kuwa bonge la fundi hata chama hamfikii. Na jina mkamtungia kuwa mzee wa soft tachi. Leo hii mnamuona kihande
Uko sahihi Mkuu, alipewa mpaka aka Magician left footer
 
Back
Top Bottom