IAmShedeOne
JF-Expert Member
- Jul 2, 2015
- 202
- 385
EDO: SIMBA WANAWEZA KUACHANA NA BWALYA
Rally Bwalya? Huu ni mtihani.
Kipaji kipo kwa Bwalya lakini hajawahi kuikamata Simba kama inavyotakiwa. Hata walipoondoka Luis Miquissone na Clatous Chotta Chama watu wengi walitazamia Bwalya avae viatu vyao lakini hakuvaa kama inavyotakiwa.
Bwalya anacheza soka laini, hana kasi, hana uamuzi wa haraka lakini pia ameshindwa kufunga mabao mengi au kutoa pasi nyingi za mwisho kama ilivyokuwa inadhaniwa.
Simba inapotawala mechi basi na Bwalya anakuwa miongoni mwa mastaa. Inapokuwa na mechi ngumu basi na Bwalya anapotea. .
Kwa mtazamo wangu Simba ikipata kiungo mwingine mzuri zaidi katika eneo la ushambuliaji basi wanaweza kuachana na Bwalya. Kama atahitaji pesa nyingi kwa ajili ya kusaini mkataba mwingine wa miaka miwili nadhani wanaweza kutulia kwanza na kutazama jicho lao kwingine.
Hauwezi kulaumiwa na mashabiki kwa kuachana na Bwalya.” - Edo Kumwembe.
#KanunguJR