Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Sikubaliani na wewe hata kidogo kwani kuna namna nyingi sana kumjibu adui yako kakaa kimya ni njia moja wapo!
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Magufuli na Polepole.

Hawa watu wawili walitushambulia sana eti mafisadi yamewakimbia na yamehamia Chadema. Sisi kweli kama Chadema tulibanwa sana kuhusu Lowassa ila tulijikongoja tuu. Kiuhalisia mwaka 2015 tulipoteza uhalisia wetu kichama ingawa Lowassa kweli alikuwa mtu wa watu. Tulilazimika kuwafanya wengine kukaa kimya maana kama chama tuliua agenda zetu kuu. Hatimaye sasa tutapumua.

Nimeshangazwa sana na mapokezi ya kifalme aliyopewa Lowassa huku serikali kuu zaidi ya nusu wakihamia Lumumba kwenda kumpokea mkubwa yule. Ni kwa mara ya kwanza kuona mtu akipokewa na viongozi wote wakuu wa chama na serikali. Mtu ambaye watu hao hao walidai kawakimbia! Leo wao ndiyo waliomkimbilia! Mbaya zaidi Magufuli anampokea Lowassa huku akiwa kasimamiwa na zee la mipango aka Rostam Aziz. Dah kweli dunia ina mambo.

Lowassa najua amerudi CCM ili kulinda fursa zake kibiashara pamoja na hatima yake ya uzeeni. Ni hayo tu.

Nasubiri kuona sasa mapovu ya kina Polepole na Bashiru baada ya madon kujihakikishia kuwa sasa wamemzunguka mkubwa wao. Acha kabisa siasa hizi za kibongo. Pia nasubiri neno la Slaa (Najua hatosema chochote maana anatumikia)
 
Nasubiri kauli ya chadema pia, wimbo wa ufisadi utarejea?
 
Bila shaka habari inayo-trend kwa nguvu sana mitandaoni kwa hivi sasa ni aliyekuwa mwanachama wa Chadema na mgombea wa urais kwa mwaka 2015, kwa tiketi ya Ukawa, Mzee Lowassa kurejea CCM.

Sishangazwi sana na uamuzi wake huo wa kurejea kwenye chama chake cha awali, kwa kuwa najua hiyo ni haki yake kikatiba

Ninachojiuliza Mimi ni sababu zipi zilizomfanya Lowassa arudi CCM tena kwa wakati huu??

Je ni kweli kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa anaridhika na juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuliletea maendeleo Taifa hili??

Je yeye Lowassa haoni namna Magufuli anavyominya demokrasia nchini mwetu hadi kuleta tafsiri ya kuwa kiongozi wa upinzani nchini kwetu kuwa ni sawasawa na kujitangazia kosa la uhaini??

Yeye Lowassa haoni namna viongozi wa Chadema wanavyofunguliiwa kesi mfululizo za uchochezi hadi kiongozi mkuu wa upinzani nchini, mheshimiwa Freeman Mbowe kusota katika gereza la segerea kwa zaidi ya miezi 3 hivi sasa??

Watanzania wote tunajua kuwa sababu kuu iliyomtoa CCM mwaka 2015 ni kutokana na jina lake "kukatwa" kuwa miongoni ya wagombea wa CCM mwaka 2015 bila sababu za msingi

Swali la pili ninalojiuliza hivi sasa kama CCM walimkata jina lake kwa sababu za ufisadi, je ufisadi wake "umeyeyuka" hivi sasa, hadi CCM wampokee tena??

Ni dhahiri kuwa hilo suala la propaganda zilizokuwa zilitumiwa na chama cha CCM mwaka 2015 ili "kum-disqualify" mheshimiwa Lowassa kugombea Urais mwaka 2015, hivi sasa zimeyeyuka!

Nimekuwa nikijiuliza pia ni sababu zipi ziizomfanya Lowassa arejee CCM hivi sasa baada ya utawala wa "mkono wa chuma" wa Rais Magufuli kutamalaki??

Kama ni kuona juhudi za Rais Magufuli, je juhudi hizo ameziona Leo Mheshimiwa Lowassa na hakuziona mwaka Jana wakati amefanya kikao cha "siri" pale Ikulu??

Jibu pekee ninalolipata Mimi ni kwanini Mheshimiwa Lowassa amerejea CCM hivi sasa na hakufanya hivyo hapo kabla ni sababu moja tu, ni tegemeo lake la kugombea urais kwa tileti ya Chadema/Ukawa kwa hivi sasa kufifia sana!

Tukumbuke pia ni hivi karibuni Tundu Lissu ametangaza kuwa yupo tayari kugombea urais kwa tiketi ya chama chake cha Chadema iwapo kitaridhia afanye hivyo

Vile vile ni jambo la wazi kuwa hivi sasa nyota ya Tundu Lissu kisiasa ndiyo inayong'ara kuliko mwanasiasa mwingine yeyote kwa upande wa upinzani

Tukumbuke pia habari hii iliyotolewa na mwanasiasa Tundu Lissu ya kugombea kwa tiketi ya Chadema itakuwa haijamfurahisha sana Mheshimiwa Lowassa, kwa kuwa yeye aliamini kuwa ni yeye pekee ndiye anayefaa kugombea urais mwaka 2020 kwa tiketi ya Chadema/ Ukawa

Kwa maana hiyo Tundu Lissu kutangaza kutaka kugombea urais mwaka 2020 ndiyo sababu pekee iliyomfanya Mheshimiwa Lowassa arejee "nyumbani kwake" CCM
 
Bongo taifa lililojaa mang'ombe kuanzia juu hadi chini
 
Dr Slaa alisimamia anachoamini hadi sasa kuhusu ufisadi na utaratibu mbovu uliotumika kuwapokea hawa jamaa. Ameachana na siasa kwasababu hii ili kulinda heshima yake.

Mambo mengine mimi na wewe tunaopiga soga humu hatuyajui kiundani hivyo soga zetu zina mipaka! Ila muda utaongea kwenye mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, comment yaako naitunza, yaweza kua reference hapo baadae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule mzee ni afadhali tu acheni aende bhna mana mtu mwenyew ata kutembea hawezi ^hakua na msaada wowote kwetu bora katupunguzia mzigo [emoji58]
Nitasema kuhusu Lowasa baadaye, Nina mengi ya kusema kuungana na yako na mengine kupingana na wewe. Lakini kwangu bado Lowasa anabaki Lowasa.


(Fursa)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatumia mantiki moja tu ya kuhama vyama lakini hutaki kuangalia tofauti kati ya Dr Slaa na Lowasa status zao wakati wanahama.

Btw najua unaelewa vyema lakini unafanya spinning tu kwa wenye akili ndogo. Hivi unalinganisha kumpokea adui wa chama kwa miaka zaidi ya kumi akiitwa fisadi kuu na kumpa kijiti agombee urais na mgombea ubunge muadilifu kama Dr Slaa? Unalinganisha nini we mzee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani Lipumba huyu anayetumiwa yeye na genge lake kupora CUF. Hivi unawezaje kukejeli hesabu za kisiasa za kina mbowe na maalim Seif. Cuf bara kwa mara ya kwanza kwenye historia ilipata wabunge 10,halmashauri 3 na madiwani zaidi ya 300. Na huo mtaji wa kura za chadema mil. 6. Na kule Zanzibar CUF kuongeza mtaji wa kura za urais Hadi Jecha alipotumika kuisaidia CCM. Oneni aibu
 
Dr Slaa si mwanasiasa tena hivyo hayana impact kwake. Alafu kumbe mlikuwa mnajua hizi blunders lakini mlivyokuwa mnamtetea sasa! Tukiwaita wanafiki tunakosea mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliona ataingia kwenye list ya kupewa ubunge kwa vile ni mke wa mtu fulani ndani ya chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…