Bila shaka habari inayo-trend kwa nguvu sana mitandaoni kwa hivi sasa ni aliyekuwa mwanachama wa Chadema na mgombea wa urais kwa mwaka 2015, kwa tiketi ya Ukawa, Mzee Lowassa kurejea CCM.
Sishangazwi sana na uamuzi wake huo wa kurejea kwenye chama chake cha awali, kwa kuwa najua hiyo ni haki yake kikatiba
Ninachojiuliza Mimi ni sababu zipi zilizomfanya Lowassa arudi CCM tena kwa wakati huu??
Je ni kweli kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa anaridhika na juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuliletea maendeleo Taifa hili??
Je yeye Lowassa haoni namna Magufuli anavyominya demokrasia nchini mwetu hadi kuleta tafsiri ya kuwa kiongozi wa upinzani nchini kwetu kuwa ni sawasawa na kujitangazia kosa la uhaini??
Yeye Lowassa haoni namna viongozi wa Chadema wanavyofunguliiwa kesi mfululizo za uchochezi hadi kiongozi mkuu wa upinzani nchini, mheshimiwa Freeman Mbowe kusota katika gereza la segerea kwa zaidi ya miezi 3 hivi sasa??
Watanzania wote tunajua kuwa sababu kuu iliyomtoa CCM mwaka 2015 ni kutokana na jina lake "kukatwa" kuwa miongoni ya wagombea wa CCM mwaka 2015 bila sababu za msingi
Swali la pili ninalojiuliza hivi sasa kama CCM walimkata jina lake kwa sababu za ufisadi, je ufisadi wake "umeyeyuka" hivi sasa, hadi CCM wampokee tena??
Ni dhahiri kuwa hilo suala la propaganda zilizokuwa zilitumiwa na chama cha CCM mwaka 2015 ili "kum-disqualify" mheshimiwa Lowassa kugombea Urais mwaka 2015, hivi sasa zimeyeyuka!
Nimekuwa nikijiuliza pia ni sababu zipi ziizomfanya Lowassa arejee CCM hivi sasa baada ya utawala wa "mkono wa chuma" wa Rais Magufuli kutamalaki??
Kama ni kuona juhudi za Rais Magufuli, je juhudi hizo ameziona Leo Mheshimiwa Lowassa na hakuziona mwaka Jana wakati amefanya kikao cha "siri" pale Ikulu??
Jibu pekee ninalolipata Mimi ni kwanini Mheshimiwa Lowassa amerejea CCM hivi sasa na hakufanya hivyo hapo kabla ni sababu moja tu, ni tegemeo lake la kugombea urais kwa tileti ya Chadema/Ukawa kwa hivi sasa kufifia sana!
Tukumbuke pia ni hivi karibuni Tundu Lissu ametangaza kuwa yupo tayari kugombea urais kwa tiketi ya chama chake cha Chadema iwapo kitaridhia afanye hivyo
Vile vile ni jambo la wazi kuwa hivi sasa nyota ya Tundu Lissu kisiasa ndiyo inayong'ara kuliko mwanasiasa mwingine yeyote kwa upande wa upinzani
Tukumbuke pia habari hii iliyotolewa na mwanasiasa Tundu Lissu ya kugombea kwa tiketi ya Chadema itakuwa haijamfurahisha sana Mheshimiwa Lowassa, kwa kuwa yeye aliamini kuwa ni yeye pekee ndiye anayefaa kugombea urais mwaka 2020 kwa tiketi ya Chadema/ Ukawa
Kwa maana hiyo Tundu Lissu kutangaza kutaka kugombea urais mwaka 2020 ndiyo sababu pekee iliyomfanya Mheshimiwa Lowassa arejee "nyumbani kwake" CCM