Hii picha haingii akilini hata chembe. Nianze kwa kuuliza .''HUU KAMA SIYO UNAFIKI WA WATANZANIA ULIOPITILIZA NI KITU GANI...???
Kwamba Watanzania wote wako kwenye musiba mzito wa kifo cha Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa CMG marehemu Ruge Mutahaba anajitokeza Edward Ngoyai Lowassa kutangaza kuhama CHADEMA na kurudi CCM inakuwa ni tukio muhimu zaidi kuliko musiba....!!!Rais wa JMT Mhe. John Joseph Magufuli ame-tweet kwenye mtandao wa tweeter kuelezea masikitiko ya kifo cha Ruge lakini hajafika nyumbani kwao na Marehemu Ruge kuwapa pole wafiwa.
Lakini baada ya Lowasa kutangaza kurudi CCM pale Lumumba Rais Magufuli yuko mbele kushangilia na kusherekea kurudi kwa Lowassa. Makada wa CCM wanashangilia na kufurahi katikati ya musiba mzito wa kijana Mtanzania ambaye amegusa nyoyo za Watanzania wengi.
Je, hili limepangwa au ni bakti mbaya? Kama CCM walikuwa wamepanga Lowassa arejee CCM tarehe ya 1 March, 2019 wameshindwa nini kuahirisha sherehe hiyo ambayo haina tija yoyote kwa Watanzania? Je, haya ni maksudi ya kuumiza nyonyo za Watanzania hasa Wana-media na wale wa vyama vingine vya siasa hususan CHADEMA? Maswali ni mengi kuliko majibu....!!
Nihitimishe kwa kusema hivi, kama Taifa, Tanzania tumeshapoteza mwelekeo wa mambo ya msingi ambayo tuliachiwa na mwasisi wetu Baba wa Taifa JK Nyerere(rip). Ni ubazazi wa hali ya juu kuimngiza siasa katikati ya musina mzito kama huu. Matukio haya mawili: KIFO CHA RUGE MUTAHABA na KUREJEA KWA LOWASSA CCM kwa hakika kimeonesha UNAFIKI WA HALI YA JUU usiozingatia UTU, HESHIMA na USTAARABU katika jamii ya walio HAI na WAFU. CCM wamekuwa ni mafundi sana wa kutengeneza PICHA ZA KINAFIKI ambazo kuna siku zitaleta matokeo HASI ambayo Wanasiasa hasa wa CCM hawajawahi kuzitarajia.
Hivi Rais Magufuli haoni aibu? Rais Magufuli amedhihirisha unafiki wake kwa Lowasa. Hivi yale maneno na kauli aliyoitamka siku ile kuwa WALE WAJUMBE WOTE WA MKUTANO MKUU WA CCM WALIOKUWA WAKIIMBA WANA IMANI NA LOWASSA ANGELIWAPOTEZA ZAIDI YA NUSU YAO... ameyafuta lini? Wahenga walisema ukitaka kuwa mwongo na mnafiki mzuri usiwe msahaulifu...!Je, waliokuwa wanashangilia, kuimba na kusherekea kurudi kwa Lowassa CCM jana pale Lumumba basi Magufuli atuambie atawapoteza wangapi?
Tafakuri.