Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Huyu propesa ni malaya wa kisiasa mwingine hana tofauti na mafisadi ndani ya ccm au fisadi lowassa na sumaye. Mtu alijiuzulu halafu anatumia nguvu ya dola kutaka kupora CUF!


Umalaya ni kuhama chama wapi prof amehama chama? Kama issue ni kujiuzuru wadhifa katika chama au serikali huo ni uwajibikaji na hata mzee mwinyi aliwahi kujiuzuru, siasa hamuiwezi kaeni pembeni mtakufa kwa vihoro bure kushabikia matapeli.
 
Kurudi kwa lowasa ccm kuna impact gani katika vyama vya ccm na upinzani?
 
Mkuu El alisafishwa na chadema kwamba ni mtu safo,kea hiyo sehemu ye yote atakayo kwenda anakwenda na utakatifu kutoka chadema.
Kea vile wamezoea kula matapishi,anzeni Tena kumtukana.
Oooh ndiyo maana serikali yote ilitoka kumpokea. Kweli Chadema ni wasafisha dhambi.
 
Acha kuandika pumba. Kama huna la maana la kuandika kaa kimya badala ya kuonyesha ujuha wako hadharani. Matapeli kwanini hawakamatwi? Kuna mwizi nchi hii kama kubwa la majizi dhalimu na dikteta magufuli? Nyumba za Serikali hasara zaidi ya trillions 3, ufisadi wa kivuko 8 billions, kukwapua hazina 2.4 trillions. China huyo dikteta wangeshamtandika risasi miaka mingi kwa wizi na ufisadi wake.




Umalaya ni kuhama chama wapi prof amehama chama? Kama issue ni kujiuzuru wadhifa katika chama au serikali huo ni uwajibikaji na hata mzee mwinyi aliwahi kujiuzuru, siasa hamuiwezi kaeni pembeni mtakufa kwa vihoro bure kushabikia matapeli.
 
Binafsi kabla kuvamiwa clouds na polisi, sikuwa namjua Ruge ingawa jina lake nimewahi kulikia vaguely. Nilikuwa nadhani ni msanii/actress kama wema au wolper. Baada ya clouds kuvamiwa ndiyo nikajua kumbe huyo ruge ni dume.
 
Hii picha haingii akilini hata chembe. Nianze kwa kuuliza .''HUU KAMA SIYO UNAFIKI WA WATANZANIA ULIOPITILIZA NI KITU GANI...???
Kwamba Watanzania wote wako kwenye musiba mzito wa kifo cha Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa CMG marehemu Ruge Mutahaba anajitokeza Edward Ngoyai Lowassa kutangaza kuhama CHADEMA na kurudi CCM inakuwa ni tukio muhimu zaidi kuliko musiba....!!!Rais wa JMT Mhe. John Joseph Magufuli ame-tweet kwenye mtandao wa tweeter kuelezea masikitiko ya kifo cha Ruge lakini hajafika nyumbani kwao na Marehemu Ruge kuwapa pole wafiwa.

Lakini baada ya Lowasa kutangaza kurudi CCM pale Lumumba Rais Magufuli yuko mbele kushangilia na kusherekea kurudi kwa Lowassa. Makada wa CCM wanashangilia na kufurahi katikati ya musiba mzito wa kijana Mtanzania ambaye amegusa nyoyo za Watanzania wengi.
Je, hili limepangwa au ni bakti mbaya? Kama CCM walikuwa wamepanga Lowassa arejee CCM tarehe ya 1 March, 2019 wameshindwa nini kuahirisha sherehe hiyo ambayo haina tija yoyote kwa Watanzania? Je, haya ni maksudi ya kuumiza nyonyo za Watanzania hasa Wana-media na wale wa vyama vingine vya siasa hususan CHADEMA? Maswali ni mengi kuliko majibu....!!

Nihitimishe kwa kusema hivi, kama Taifa, Tanzania tumeshapoteza mwelekeo wa mambo ya msingi ambayo tuliachiwa na mwasisi wetu Baba wa Taifa JK Nyerere(rip). Ni ubazazi wa hali ya juu kuimngiza siasa katikati ya musina mzito kama huu. Matukio haya mawili: KIFO CHA RUGE MUTAHABA na KUREJEA KWA LOWASSA CCM kwa hakika kimeonesha UNAFIKI WA HALI YA JUU usiozingatia UTU, HESHIMA na USTAARABU katika jamii ya walio HAI na WAFU. CCM wamekuwa ni mafundi sana wa kutengeneza PICHA ZA KINAFIKI ambazo kuna siku zitaleta matokeo HASI ambayo Wanasiasa hasa wa CCM hawajawahi kuzitarajia.

Hivi Rais Magufuli haoni aibu? Rais Magufuli amedhihirisha unafiki wake kwa Lowasa. Hivi yale maneno na kauli aliyoitamka siku ile kuwa WALE WAJUMBE WOTE WA MKUTANO MKUU WA CCM WALIOKUWA WAKIIMBA WANA IMANI NA LOWASSA ANGELIWAPOTEZA ZAIDI YA NUSU YAO... ameyafuta lini? Wahenga walisema ukitaka kuwa mwongo na mnafiki mzuri usiwe msahaulifu...!Je, waliokuwa wanashangilia, kuimba na kusherekea kurudi kwa Lowassa CCM jana pale Lumumba basi Magufuli atuambie atawapoteza wangapi?

Tafakuri.
Kwa Hiyo ulitaka walie
 
Barrick na Acacia are not stupid kumpa asiye na uwezo. Sio tender za serikali au CCM. Advantage aliyokuwa nayo ni kwamba yeye ni major supplier wa heavy machinery za mining.
Barrick haijawahi kutoa kandarasi ya uchimbaji kwa Caspian zaidi ya kandarasi ya kuchimba kibwawa cha plant pale bulyanhulu, supplier wa heavy machine wa barrick kwa pale bully ni sandvik, kwa buzwagi ni komats'u na north Mara ni atlas copco.
 
Ruge ni muhimu kwa watu wa mziki
Mkulima au mapori pori kama Hana umuhimu wowote
Juzi jna leo mme Gara Gara kwa kulia kesho tu mtasahau maisha yataendelea

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kurejea kwa Lowassa ndani ya CCM na kupokelewa na uongozi wote wa juu wa nchi na chama tawala, ni ishara ya ushindi mkubwa sana kwake juu ya tuhuma za ufisadi alizokuwa akishambuliwa nazo sana na vyama vya upinzani hasa CHADEMA ambapo mashambulizi ya tuhuma hizo kutoka upinzani yalizima baada ya kujiunga na CHADEMA ili kugombea urais baada ya kutemwa CCM. Ghafla CHADEMA wakabadili kauli kuwa Lowassa hakuwa fisadi.

CCM kuona hivyo wakaibeba ajenda ya CHADEMA kuwa wao wamemtemba kwasababu ya ufisadi na sasa amepokelewa na CHADEMA hivyo ni wapinzani ndio wanao unga mkono ufisadi. Mgombea wa CCM akaenda mbali na kusema kuwa fisadi mkuu amemkimbia na kujiunga na upinzani na akahahidi kuwa akiyakwaa madaraka ataunda mahakama maalumu ya mafisadi lengo likiwa ni kumshughulikia Lowassa. Baada ya kushinda ni kweli aliunda mahakama hivyo lakini hakuna fisadi yeyote aliyepelekwa huko wala Lowassa hakuguswa matokeo yake tuka shuhudia akialikwa ikulu. Kabla ya hapo viongozi mbali mbali wa CCM na vijana wao walipiga kelele kubwa kuwa Lowassa ni fisadi hivyo CHADEMA impoteza mwelekeo kwa kumpokea Lowassa.

Kurudi kwa Lowassa sasa ni wazi mashambulizi ya akina Pole pole, Makonda na rais mwenyewe kuwa Lowassa ni fisadi yamefikia tamati. Lowassa sasa ni safi. Amesafishwa na upinzani ulimtuhumu kwanza na sasa amesafishwa na chama tawala chenyewe kilicho mtema na kumshutumu pia kwa ufisadi. Aidha Lowassa amerejea CCM na rafiki yake mkubwa Rostam ambaye kwa pamoja ndio waliomuweka madarakani JK. Ni wazi huu ni mkakati wa kumasaidia JPM kwa 2020. Lakini kubwa kuliko yote ni kuwa Lowassa ameshinda vita ya ufisadi. Si Mbowe, Lissu, Msigwa, Silaa, Lema, Polepole, Makonda au Rais watako inua midomo yao tena kusema Lowassa ni fisadi. Hongera sana Lowassa!

sasa kama Lowasa hatogombea chochote kuna haja gani kumsema? mtu anapogombea uongozi ndiye anayepigwa madongo
 
Woga tu,Lowassa aliogopwa na watu wengi,si sababu ya ufisadi bali msimamo wake usioyumba.
Ukianzia kwa Mwl.Nyerere akidai Lowassa ana mali nyingi,lakini hiyo sio sababu ya moyoni alitaka watanganyika waamini hivyo.Yeye alitaka Mkapa

Kikwete hakuwahi kujitokeza hadharani kumpa za uso Lowassa lakini alimchimbia kaburi huku akimtayarisha Membe.

Vivyo hivyo Chadema chini ya Dr Slaa walimshutumu Lowassa kama walivyokuwa wanaelekezwa na serikali ya CCM Bungeni.

Hata pale Lowassa alivyojiunga na Chadema walimkubali haraka haraka awe mgombea wa uraisi.
Kama alikuwa fisadi na bado wakamgangania ili awe mgombea uraisi kwa tiketi ya Chadema,basi chama hicho ni ndumila kuwili.
 
Lowassa anatosha kuwa mwanachama. Lowassa hatoshi kuwa rais. Hilo ndo swala, na limefanikiwa.
 
You have no idea mining industry in operate vipi dogo. Waingie tena kununua vifaa? Tender za heavy machinery ni competitive sana. Barrick wanajua kama wanapigwa au la.
Sio tender za serikali hizo. You have to deliver. Siri ni kuwa na capital kubwa. Unaagiza mapema. Wakihitaji, una supply immediately.
unajua kusifia ujinga na ushabiki hauna mbele wala nyuma, kwa barrick kununua wala si kitu kikubwa sana..kikubwa kwao ni maintenance na vipuri vya equipments ndiyo maana wananunua kwa manufacturer, KOMATSU siyo manufacturer???
 
Kwa hiyo mtoa mada una wasiwasi huenda ikatokea kama ile ishu ya Kafulila? Baada ya yeye kuunga mkono juhudi na kuukwaa u Ras wa Songwe, Kamanda Jesca Kishoa amekomaa mpaka kesho na kugoma kabisa kuunga mkono juhudi.
 
Waliposema CCM ina wenyewe bila wao itaanguka,na hiki ndio kimefanyika.
Lowassa karudi ili KULETA MSHIKAMANO NDANI YA CHAMA CHA CCM
Na kweli Kaskazini,Kusini pammoja na nyanda za juu kusini walishajitoa.
 
Back
Top Bottom