Wengi na hasa ndani ya CCM wanadhani kuondoka kwa Lowasa CHADEMA ni pigo kwa chama hicho kwa hilo wana jidanganya.
Ukweli una baki pale pale kuwa watu wameichoka CCM, hawa jamaa wametawala kwa muda mrefu bila ya mafanikio yoyote ya maana zaidi ya kuiba fedha za walipa kodi maskini wa nchi hii.
Hivyo kazi hii ya kutafuta Uhuru ndani ya nchi ambayo ukandamizaji na unyanyasaji ndio vimegeuzwa kuwa Sera ya taifa hakika ni kwamba asingeweza , nchi ambayo una lazimishwa kukiunga chama dola mkono kwa nguvu na usipo fanya hivyo ujue kama ulikuwa na biashara yako nayo ndio imefikia mwisho, kama ulikuwa na mashamba yako ujue wazi kuwa utanyang'anywa.
Hii ni kazi ambayo inafanywa na vijana wa kitanzania wachache wanao jitambua kuwa kuna haki zao za msingi kabisa wanazo dhulumiwa,tena ni vijana wasomi ambao unatambua kuwa elimu aliyo ipiata hamruhusu kujipendekeza pendekeza ili mradi tu apate kajitonge ka ugali kwa siku moja na kuacha kukabiliana na zuio la njaa ya muda mrefu, vijana wazalendo ambao hawaachi kupaza sauti zao wanapo ona upotoshaji na wizi ukitokea ndani ya nchi yetu.
Vijana wa aina hii utawakuta nje ya CCM, vijana wasio kuwa na uoga wa aina yoyote kwenye kusimamia wanacho kiamini kuwa ni haki ya msingi ndani yaTaifa lao, vijana ambao wamesha jitolea na kuona kuwa mahakama na jela ni sehemu ya maisha ya wapigania Uhuru.
Kazi hii Lowasa asingeiweza yeye alikuja kupata farijiko baada ya kunyanyaswa na wezi wenzake alio shirikiana nao kwa muda mrefu kuliibia taifa letu.
Rai hii iwafikie wapigania Uhuru wa kweli kama akina Mh Halima Mdee, Godbles Lema , Mch Msigwa, Lissu, Ruyagwa Kabwe, Ally Saleh, Salum Mwalim, Mnyika, Esther Matiko, Lijualikali, J. Mbilinyi, Suzzy Kiwanga, Suzzy Lyimo, J. Haule. Na wengine wengi sitaweza kuwataja wote, ukweli ni kwamba jitihada zenu za kutafuta Uhuru ndani ya nchi huru unafahamika hadi huko ndani ya chama la wizi.
Hongereni na safari hii upinzani utapata kura nyingi hadi watapata aibu.
Mungu ibariki Tanzania tupate Uhuru 2020.
Sent using
Jamii Forums mobile app