Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Ndio siasa ilivyo hakuna adui au rafiki wa kudumu hili nalo litapita na maisha yataendelea kama kawaida
 
Kila mmoja ana maamuzi yake, ila siasa ni mchezo mbaya sana

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Nimesoma waraka wa Lissu kuhusu Lowassa na mashinikizo yanayo mkabili hadi kuamua kufunika USO Kwa aibu na kufanya lile lisilo tegemewa na kurudi kule kule waliko mtukana matusi ya nguoni wakati wa kampeni na baada ya kampeni.
Ukiacha mashamba na ranchi zake kutishiwa kunyang'anywa, TRA na mafao yake kubwa zaidi ni kusota jela kwa mume wa binti yake Sioi miaka mitatu sasa na binti sio ajabu anaangua kilio kila siku Nyumbani kuwa kama sio wewe baba kuwa Chadema mume wangu asingesota jela.
Pengine anaulizwa na binti au mama Regina kuwa hivi Sioi angekuwa mkwe wa Warioba, Salimu au Msuya angesota namna hii Kwa kesi isiyo kichwa wala miguu?
Mwanamume yeyote ukipima hali hiyo ya Lowassa unapata jibu kuwa alifikia wakati wa kuchagua kuwa na family na sio hao wapiga kura milioni sita.
Tumwambie Lowassa tumekuelewa, aende na akae kimya asilete matamshi kama Waitara maana atawatibua nyongo watu na makombora ya majibu atakayo pata yanaweza kumuua kabisa.
Kila lakheri Ngolay, ukituheshimu tutakuheshimu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo maana Lissu katoa sababu za kiistarabu kabisa na ninadhani hakuna mtu anayetukana kama walivyofanya CCM.Ninachojiuliza CCM wanamtaka Lowassa wa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo maana Lissu katoa sababu za kiistarabu kabisa na ninadhani hakuna mtu anayetukana kama walivyofanya CCM.Ninachojiuliza CCM wanamtaka Lowassa wa nini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanajiandaa kuiba kura kwa kishindo hiyo 2020, sasa wamemchukua ili wakiiba kura ionekane kura za Magufuli zimekuwa nyingi kwakuwa kapata na za Lowassa
 
Naye ni binadamu anadamu na nyama ,wanavyoumia wengine na yeye hivyo hivyo msijali huyu amefungua mpango wa Mungu ccm na cdm nyie subirini tu mtaelewa .
 
Rostam Aziz kufika ikulu wiki haikumaliza mdogo wake kaachiwa huru kesi yake siisikii mpaka leo. Sioi wiki ijayo usishangae nae akatoka rumande, hivi yule kijana msukule(Polepole) mbona yupo kimya sana kulikoni.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Sio CCM ya Magufuli mkuu.Ameona mambo hayaendi South Africa.Ujuaji juaji kule na vidili vya kijinga jinga kama bongo ni unacceptable na out of place.

Tueleweshe mkuu CCM zipo ngapi? Ipo CCM ya Magufuli na zingine za akina nani?
 
Ni vema kupambanua kati ya kumpokea
Mheshimiwa Lowasa Chadema na kumteua kuwa mgombea wa Urais. Kumpokea chamani halikuwa kosa, lakini kumpa nafasi ya uongozi lilikuwa kosa kubwa sana.

Kuna mhimili wa maadili unaosema "the end does not justify the means". Lilikuwa kosa la msingi kwa Chadema kutaka kuchukua Urais kwa njia yoyote. Kumsimamisha mtu ambaye walikuwa wanadai ni fisadi kulitoa ujumbe kwamba wao hawana msimamo hata kidogo.

Kosa kubwa huleta madhara makubwa. Chadema ilijiimarisha kwa "narative" ya kupinga ufisadi. Baada ya kumtaka yule waliyekuwa wakidai ni fisadi papa kuwa mgombea wa Urais, wamejibomolea hiyo narative. Hawana narative sasa. Matokeo yake ni msambaratiko ambao uko sasa.

Unajidanganya ,hujui au vipi?
 
Ukiweka ushabiki pembeni hutasita kuona uzito wa uhamaji Lowasa kuanzia 2015. Hakika CDM ilipata kura milioni 6 kutokana na mvuto WA Lowasa 2015. Hakika Lowasa aliitikisa CCM 2015 japo CCM ilijitahidi kuonyesha hakuwatikisa. Ukweli huu utabaki kuwa kumbukumbu ya kihistoria katika siasa za nchi yetu. Ilikuwa mara ya kwanza CCM kukabiliwa Kwa kiwango kile katika uchaguzi. Makovu yaliyotokana na kuhama kwake bado yangalipo. Usaliti unaoendelea ndani ya CCM asili yake kubwa ni mhamo ule. CCM itapaswa kutafakari kwa kina namna ya kudhibiti makada wenye nguvu kuhama haswa kipindi cha kampeni za uchaguzi. Kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa. Na ikiwa kweli Lowasa 'karudi nyumbani" kwa moyo mkunjufu basi anapaswa kuomba chama radhi kwa kukisababishia makovu. Na ashiriki kutibu makovu yaliyobaki hapa na pale. Mfano Lowasa anatakiwa avunje kambi yake rasmi maana bado ipo. Hapo ndipo "mtoto mpotevu" atakuwa amerudi nyumbani kwao! Lakini pia itamsaidia yeye na CCM kama atatangaza rasmi kuachana na dhamira ya kwenda Ikulu. Awe Mzee mstaafu wa chama chake. Atarejesha sehemu kubwa ya heshima aliyoipoteza.

Lakini hakuna walioumia kwa kuhamahama Kwa Lowasa kama CHADEMA. Wanaweza kujibaraguza na kumdhihaki. Na hapo ndio yanapoanzia maumivu ya CHADEMA. Kumbeza LOWASA Kwa sasa kutawachafua mno kwa makundi muhimu. Kundi la Kwanza ni la wanachama ambao tangu Alfa walipinga ujio wa Lowasa wakapuuzwa. Mbowe aliwaita "watu wasiopima mambo kwa kina"! Leo wao ndio wamedhihirisha walipima mambo kwa kina. Ile Imani "kamanda Mbowe" hakosei inatoweka. Kundi hili litataka kuonyesha lilikuwa sahihi.

Kundi la pili ni wafadhili na mataifa ya nje. Watajiuliza ikiwa kiongozi waliyempokea Kwa mbwembwe na kumtambulisha "waziri mkuu mstaafu" yamemshinda lazima kuna udhaifu. Mara kadhaa Lissu amesikika nje akisifia "mawaziri wakuu wastaafu" kuondoka CCM! Kimataifa athari ya kuondoka Lowasa kwao ni kubwa mno. Sema inahitaji akili ya ziada kuliona hili. Hili ni swali watakalokumbana nalo Kwa mabalozi na vyombo vya habari vya nje. Hawawezi kudai kanunuliwa maana wimbo huo hautaendana na sherehe!

Hasara nyingine ambayo CHADEMA itajutia ni kumpa Lowasa ujumbe wa Kamati Kuu. Kamati Kuu ya Chama chochote ndiyo yenye kuidhinisha mikakakati (halali na haramu) na kupokea taarifa za utekelezaji. Ni taasisi inayotunza siri nzito za Chama husika. Inajadili matumizi ya fedha na Mali za Chama Kwa hiyo inajua nani mbadhirifu. Siri zote hizo SASA ziko mikononi mwa Lowasa. Bila Shaka kaenda nazo CCM. CHADEMA hawawezi kujitetea kuwa hajui! Kama Kamati Kuu haijadili haya basi ina maana Kamati Kuu ya CHADEMA ni kanyaboya? Hakika lazima CHADEMA iingie hofu. Hauwezekaniki Lowasa asijue nani haswa alimshambulia Lissu! Lazima Lowasa anajua ni kwa nini dereva alitoroshwa! Lazima Lowasa anajua ukweli kuhusu Ben Saanane! Haiwezekani Lowasa asijue nini haswa kiliwafika Chacha Wangwe na wengine waliopoteza maisha katika MAZINGIRA ya utata. Lazima Lowasa anajua waliolipua Bomu Arusha. Lowasa anajua nani waliendesha mauaji Rufiji. Hofu imetanda ndani ya CHADEMA ila wanachama hawajui.

Hasara inayowasubiri CHADEMA ni 2020. Zile kura milioni 6 zitarudi zilikotoka. Ni huyu Lowasa watu walimuita raisi wa mioyoni. Ni huyu Lowasa watu walipiga deki lami asipate mafua. Ni huyu Lowasa watu waliapa ALIPO NA WAO WAPO! Hawa hawakupigia Kura CHADEMA. Walimpigia Lowasa!

Mtihani wa mwisho Kwa CHADEMA ni huu: Lowasa alienda CHADEMA na waliokuwa "TEAM LOWASA" alipokuwa CCM. Hawa bado wapo CHADEMA tena wengine wako matawi ya juu. Je CHADEMA itawafukuza? Itawatoa matawi ya juu? Hakutatokea mpasuko kati ya "wakuja" na "wazawa"? CHADEMA inathubutu kwa mfano kumtenga Sumaye na Mahanga? Hapohapo inaweza kuwaamini kuliko walivyomuaminia Lowasa? Leo hii Baraza na Kamati Kuu CHADEMA zikikutana zitathubutu kuongea mambo nyeti wakati Sumaye na Mahanga wamo kikaoni? Au watawatoa nje?

Huu ndio uzito wa hamahama ya Lowasa. Unaweza ukachukia au ukafurahi ukipendezewa!

Ushauri wangu Kwa Lowasa: usijibizane na wao. Waache wahangaike na msiba wa kujitakia.
IMG-20190302-WA0020.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi na hasa ndani ya CCM wanadhani kuondoka kwa Lowasa CHADEMA ni pigo kwa chama hicho kwa hilo wana jidanganya.
Ukweli una baki pale pale kuwa watu wameichoka CCM, hawa jamaa wametawala kwa muda mrefu bila ya mafanikio yoyote ya maana zaidi ya kuiba fedha za walipa kodi maskini wa nchi hii.
Hivyo kazi hii ya kutafuta Uhuru ndani ya nchi ambayo ukandamizaji na unyanyasaji ndio vimegeuzwa kuwa Sera ya taifa hakika ni kwamba asingeweza , nchi ambayo una lazimishwa kukiunga chama dola mkono kwa nguvu na usipo fanya hivyo ujue kama ulikuwa na biashara yako nayo ndio imefikia mwisho, kama ulikuwa na mashamba yako ujue wazi kuwa utanyang'anywa.
Hii ni kazi ambayo inafanywa na vijana wa kitanzania wachache wanao jitambua kuwa kuna haki zao za msingi kabisa wanazo dhulumiwa,tena ni vijana wasomi ambao unatambua kuwa elimu aliyo ipiata hamruhusu kujipendekeza pendekeza ili mradi tu apate kajitonge ka ugali kwa siku moja na kuacha kukabiliana na zuio la njaa ya muda mrefu, vijana wazalendo ambao hawaachi kupaza sauti zao wanapo ona upotoshaji na wizi ukitokea ndani ya nchi yetu.
Vijana wa aina hii utawakuta nje ya CCM, vijana wasio kuwa na uoga wa aina yoyote kwenye kusimamia wanacho kiamini kuwa ni haki ya msingi ndani yaTaifa lao, vijana ambao wamesha jitolea na kuona kuwa mahakama na jela ni sehemu ya maisha ya wapigania Uhuru.
Kazi hii Lowasa asingeiweza yeye alikuja kupata farijiko baada ya kunyanyaswa na wezi wenzake alio shirikiana nao kwa muda mrefu kuliibia taifa letu.
Rai hii iwafikie wapigania Uhuru wa kweli kama akina Mh Halima Mdee, Godbles Lema , Mch Msigwa, Lissu, Ruyagwa Kabwe, Ally Saleh, Salum Mwalim, Mnyika, Esther Matiko, Lijualikali, J. Mbilinyi, Suzzy Kiwanga, Suzzy Lyimo, J. Haule. Na wengine wengi sitaweza kuwataja wote, ukweli ni kwamba jitihada zenu za kutafuta Uhuru ndani ya nchi huru unafahamika hadi huko ndani ya chama la wizi.
Hongereni na safari hii upinzani utapata kura nyingi hadi watapata aibu.
Mungu ibariki Tanzania tupate Uhuru 2020.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kawaida mbaazi ikikosa maua unakuwa na hekawa hizi hizi ila wenye upeo na akili timamu waliwaambia haya yote kabla hajawalangua
 
Zilikuwepo tawala katili, jeuri na hata za Kidikteta na Leo hii zimebaki kuwa historia....Hata hii ya CCM nayo itapita na kusahaulika kabisa....Its a matter of time !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rostam Aziz kufika ikulu wiki haikumaliza mdogo wake kaachiwa huru kesi yake siisikii mpaka leo. Sioi wiki ijayo usishangae nae akatoka rumande, hivi yule kijana msukule(Polepole) mbona yupo kimya sana kulikoni.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Kesi haipo tena alitozwa faini awezayo kulipa akajiondokea huku anacheka! Hiyo ndio nguvu ya mafisadi kwa rais wa "wanyonge" ambaye naye ni mnyonge.
 
Sote runakumbuka Vividly wakati Lowassa alipogamia CHADEMA tuliambiwa huku watu wakiapa viapo vya Miungu yao bila hata ya aibu Usoni

Hayaaa hayo yalipita Ping imekuwa Pong je Lumumba nayo Karudi Kwa kiasi gani?

Huko nyuma tuliambiwa Ooh!! Mwenyekiti Mhe Freeman Aikaeli Mbowe Kavuta Billioni sita Kaenda kuzichimbia Dubai na kwamba Dubai ana akaunti kibao kwa hiyo CHADEMA ni SACCOs yake Binafsi...Mara Ooh!..yeye na BAmkwe wake.

Mambo yameshadhihirika kwa wananchi CCM ilikuwa ikiwalisha Shubiri Mwitu wakishushia na juisi ya Matango Pori..

CCM kimeishiwa Mbinu na Uongo na huwa wanaamini ili Upate Uongozi lazima uwe Muongo.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimesingiziwa mengi ila sasa ni zamu ya wananchi kutafakari kura zao walizipoteza kwa kuitumbukizia CCM mimi Binafsi najuuuta ba Kusaga Meno kwanini niliitumbukizia CCM

Ila Never Again!
Peoples Power
Azimio la Zanzibar 2 ni lini litafanyika tunalisubiri kwa hamu.
 
Back
Top Bottom