Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo maana Lissu katoa sababu za kiistarabu kabisa na ninadhani hakuna mtu anayetukana kama walivyofanya CCM.Ninachojiuliza CCM wanamtaka Lowassa wa nini?Nimesoma waraka wa Lissu kuhusu Lowassa na mashinikizo yanayo mkabili hadi kuamua kufunika USO Kwa aibu na kufanya lile lisilo tegemewa na kurudi kule kule waliko mtukana matusi ya nguoni wakati wa kampeni na baada ya kampeni.
Ukiacha mashamba na ranchi zake kutishiwa kunyang'anywa, TRA na mafao yake kubwa zaidi ni kusota jela kwa mume wa binti yake Sioi miaka mitatu sasa na binti sio ajabu anaangua kilio kila siku Nyumbani kuwa kama sio wewe baba kuwa Chadema mume wangu asingesota jela.
Pengine anaulizwa na binti au mama Regina kuwa hivi Sioi angekuwa mkwe wa Warioba, Salimu au Msuya angesota namna hii Kwa kesi isiyo kichwa wala miguu?
Mwanamume yeyote ukipima hali hiyo ya Lowassa unapata jibu kuwa alifikia wakati wa kuchagua kuwa na family na sio hao wapiga kura milioni sita.
Tumwambie Lowassa tumekuelewa, aende na akae kimya asilete matamshi kama Waitara maana atawatibua nyongo watu na makombora ya majibu atakayo pata yanaweza kumuua kabisa.
Kila lakheri Ngolay, ukituheshimu tutakuheshimu
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo maana Lissu katoa sababu za kiistarabu kabisa na ninadhani hakuna mtu anayetukana kama walivyofanya CCM.Ninachojiuliza CCM wanamtaka Lowassa wa nini?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio CCM ya Magufuli mkuu.Ameona mambo hayaendi South Africa.Ujuaji juaji kule na vidili vya kijinga jinga kama bongo ni unacceptable na out of place.
Ni vema kupambanua kati ya kumpokea
Mheshimiwa Lowasa Chadema na kumteua kuwa mgombea wa Urais. Kumpokea chamani halikuwa kosa, lakini kumpa nafasi ya uongozi lilikuwa kosa kubwa sana.
Kuna mhimili wa maadili unaosema "the end does not justify the means". Lilikuwa kosa la msingi kwa Chadema kutaka kuchukua Urais kwa njia yoyote. Kumsimamisha mtu ambaye walikuwa wanadai ni fisadi kulitoa ujumbe kwamba wao hawana msimamo hata kidogo.
Kosa kubwa huleta madhara makubwa. Chadema ilijiimarisha kwa "narative" ya kupinga ufisadi. Baada ya kumtaka yule waliyekuwa wakidai ni fisadi papa kuwa mgombea wa Urais, wamejibomolea hiyo narative. Hawana narative sasa. Matokeo yake ni msambaratiko ambao uko sasa.
Kesi haipo tena alitozwa faini awezayo kulipa akajiondokea huku anacheka! Hiyo ndio nguvu ya mafisadi kwa rais wa "wanyonge" ambaye naye ni mnyonge.Rostam Aziz kufika ikulu wiki haikumaliza mdogo wake kaachiwa huru kesi yake siisikii mpaka leo. Sioi wiki ijayo usishangae nae akatoka rumande, hivi yule kijana msukule(Polepole) mbona yupo kimya sana kulikoni.
Ndukiiiii 🏃♂️🏃♂️🏃♂️