Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Labda kama ukiniambia ww ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema unaweza ukawa nauhakika kwamba lowassa ajawa na mchango wowote kwenye chama baada ya uchaguzi.kwamba alipokuwa chadema hata Rais mwenyewe alikuwa bado anamuogopa hapo siwez kukaataa ndio maana hata juz chama na serikali nzima imempokea kwa kurudi kwake.mimi mwenyewe nimefurahi lowasa kurudi CCM na wala haijaniumiza kabisa kwa sababu inatoa mwanya zaid ya kina LISSU na wengine kutumia fursa.lakin sibez hata kidogo maamuz ya chama kumchukua lowasa

Naheshimu kutofautiana mawazo maana ndio afya ya mijadala.
 
Huu mwandiko ukiusoma kwa makini zaidi unaweza kujiwa na hisia kuwa Mzee mwanakijiji ni Dr Slaa mwenyewe . Hisia hizi zimetokana na baadhi ya hoja kwenye hili andiko kuwa ni hoja za kujitetea lakini zisizo na misingi yoyote.

Kwa mfano Mwanakijiji anasema eti Dr Slaa ni mwanasiasa bora kuliko mwanasiasa mwingine yoyote kwa sasa ,hii ni hoja dhaifu sàna . Ni hoja ya kihisia na kijipendelea zaidi kuliko uhalisia mwenyewe.


Hoja nyingine anasema eti kuwa balozi si lazima uwe mwana ccm ,hii ni hoja kituko kabisa . Tangu lini ccm ikachagua mpinzani wa kweli kuwa balozi. eti Dr Mkumbo alikuwa mpinzani na akachaguliwa kuwa katibu wa wizara ,hiki nacho ni kichekeho tangu lini Mkumbo alikuwa mpinzani?

Tatu Mwanakijiji anasema kuwa hajaona tatizo lolote kwenye awamu hii . Hii inashangaza sana . Kwani kwa hali ilivyo sasa katika sekta zote hata mtoto wa darasa la saba anajua kuwa liko tatizo.

La mwisho kabisa naomba nikubaliane na baadhi ya hoja za Mwanakijiji( Dr Slaa) kwa mfano ni kweli kabisa Chadema lazima wawe makini zaidi linapokuja swala la kupokea wageni kutoka upande wa pili. Nadhani tukio hili la mzee wetu kurudi nyumbani kwao limeacha fundisho kubwa kwa upinzani.

Hongera mzee wetu . Uwe na mapumziko mema huko nyumbani kwako , maana upande huu wa pili umejaa mateso na mahangaiko mengi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee mbona maneno mengi ,kuondoka kwa Lowasa Hakuna hasara yoyote ile zaidi ya faida ,Mzee hebu Fanya formative and summative evaluation , acha ushabiki .
 
Mzee mbona maneno mengi ,kuondoka kwa Lowasa Hakuna hasara yoyote ile zaidi ya faida ,Mzee hebu Fanya formative and summative evaluation , acha ushabiki .
 
Nilichonote hapa

1. Bado mwanakijiji haoni sababu ya kutomuunga mkono Magufuli.

2. Anaona CHADEMA walikosea kumpokea lowassa hivyo wawaombe radhi watz

3. Mbowe awajibike kwa kumpokea Lowassa.

4. Kuondoka kwa Lowassa upinzani ni uthibitisho kuwa CHADEMA walikosea kumpokea.

4. Anaamini ELna RA ni wachafu na mafisadi.

5. Haoni kama ukaribu wa RA na EL kama utamcorrupt Magufuli maana anaamini Magufuli ni strong enough kuwa collapsed.

6.Anaamimi JPM amefanya mabadiliko makubwa, amebaki njia panda kwenye iwapo JPM atafanikiwa kuibadilisha CCM.

7. Anaamini kuna majeraha Lowassa ameyaacha upinzani, wakati huohuo anakiri kuwa Lowassa hajawahi kuwatetea upinzani.

At this juncture ninakubaliana na Mzee Mwanakijiji kwenye hoja moja tu nayo ni kuhusu kujiuzuru kwa Mbowe au kutogombea maana mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi chamani na kama sikosei wapo ngazi ya mkoa. Mbowe asigombee siyo kama ishara ya kuwajibika bali kama ishara ya kusadifu ile demokrasia inayoimbwa CHADEMA hivyo tu basi.

Pia nimpongeze Mwanakijiji kwa kuendelea kumuunga mkono JPM na kukiri hilo waziwazi. Tofauti na watu kama chahali and the like ambao mwaka 2015 walikuwa kwa JPM sahizi wanajifanya wanatunafkia eti wapo upinzani. Kisingizio eti walimsapoti JPM sababu ya Lowassa. This is absurd, Lowassa anaweza kuwa sababu ya wao kutosapoti upinzani lakini hawezi kuwa sababu ya wao kumsapoti JPM waache kujificha kwenye visingizio wabaki huko na JPM wao.

Mawazo mengine ya Mzee Mwanakijiji siyapingi moja kwa moja lakini yanahitaji kuwa substantiated enough to convince any reasonable person. Nitapoint out mkanganyiko wa mawazo yake hapa chin.

i. Mzee Mwanakijiji hajaeleza kuondoka kwa Lowassa kunakuwaje uthibitisho wa kuwa CHADEMA (au mbowe kama anavyodai) alikosea kumpokea Lowassa? Hivi kuna uhusiano wa "Kupokelewa" na "kuondoka". Kama kuondoka ni uthibitisho wa kuwa walikosea kumpokea je inamaana CHADEMA walikosea kumpokea Kafulila kutoka nccr maana naye ameondoka? Je wasira alipokelewa upinzani kimakosa ndiyo maana akaondoka? Similar facts are to be treated equally. Mwanakijiji ameshindwa kueleza uhusiano uliopo hapa na kwamba je ili umpokee mtu unatakiwa ujiulize atadumu muda gani? Na je chama kina option ya kumnyima kadi mtu kwa sababu yoyote ile?

Na kama ni kumpa mtu ugombea je ukipewa kugombea Urais unatakiwa usiondoke? Vipi tuna guarantee gani kuwa akigombea Lissu au mbowe hataondoka baada ya uchaguzi? Na akiondoka ni uthibitisho kuwa tulikosea kumpa kugombea?

2. Hoja kwamba Lowassa ameacha majeraha CHADEMA wanayotakiwa wayatibu imekuwa conflicted na hoja yake Mwanakijiji mwenyewe kuwa Lowassa hakuwahi kuwa mpinzani wa kweli hivyo kwa maoni yake alikuwa mzigo maana hakuwatetea wapinzani. Mwanakijiji anmeshindwa kuondoa mgongano katika hoja hii.

3. Mwanakijiji ameshindwa kueleza ni kwa jinsi gani anatuguarantee kuwa JPM ataweza kudhibiti (mafisadi kwa mujibu wake Mwanakijiji) akina EL na RA wanaomkaribia kwa karibu. Na ameshindwa kueleza je kuna ulazima gani CCM na mtu (credible kwa mujibu wa Mwanakijiji) kama JPM awe karibu na "mafisadi" aache kazi zake ofisini aende Lumumba uongozi mzima wa chama kumpokea "Fisadi". Hii inamaana gani na wana umuhimu gani hawa Mwanakijiji anaowaona siyo "wasafi" kupewa heshima kubwa na "msafi" (asiyedanganyika kwa mujibu wa Mwanakijiji)?

4. Kuhusu mabadiliko na utendaji wa JPM ni very subjective inategemeana unatazama kutokea angle gani. Mwanakijiji ameshindwa kuonesha ni angle gani anayomtazama Magufuli maana wapo wanaomtazama kama Rais wa wizara ya "miundombinu na uchukuzi" pekee.

Nawasilisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
Shikamoo mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very good counter attack arguments....

Hata hivyo, alichokiandika MwanaKijiji hakiwezi kuwa ni "facts" bali yatabaki kuwa ni "maoni" yake tu....

Hii ni kwa sababu na kama ulivyosema, inategemea sana unayatazama mambo haya katika engo gani kwa kuzingatia siasa zetu za Kiafrika na hususani za Bongo yetu hii....

Na kwa mtazamo wangu, issue ya Mbowe kujiuzulu eti tu kwa kuwa alifanya kosa hili la kumpokea EL kwa mazingira na siasa zetu hizi za Kibongo, binafsi sikubaliani nalo 100%....

Bado naona kabisa kuwa, kwa mazingira tuliyo nayo ingalau kwa kipindi hiki, Freeman Aikael Mbowe ndiye Mwenyekiti anayestahili kuendelea kuongoza harakati za mapambano hayo kwa CHADEMA....

Nakuhakikishia kuwa, likifanyika kosa la Mbowe kutangaza kuwa anaachia ngazi kwa sababu hii iliyotajwa na Mzee MwanaKijiji, ndiyo itakuwa mwisho wa CHADEMA na hakuna jambo muhimu lenye kuashiria kuua rasmi upinzani kabla 2020 wanalosubiri CCM kwa hamu kutokea upesi na kwa haraka isipokuwa mambo matatu haya yafuatayo:

1. Tundu Lissu kupotezwa kabisa ktk siasa za Tanzania aidha iwe kwa KIFO rasmi cha roho na mwili na cha aina yoyote ile ama asije kabisa Tanzania awe mkimbizi wa kisiasa huko huko aliko...

2. Freeman Aikael Mbowe haendelei kuwa M/kiti na Mbunge wa CHADEMA iwe kwa mbinu yoyote ama hata kwa KIFO cha mwili cha kawaida ama hata kisicho cha kawaida.....!!

3. Maalim Seif Sharrif Hamad na CUF ya Zanzibar wanapotezwa kisiasa kabisa iwe kwa KIFO cha kawaida ama hata kwa njia zozote zile. Rejea marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa juzi kati. Lengo ni hili hili.......

• Si ajabu maandiko haya ya kina Mzee Mwanakijiji yaliyoandikwa kwa mpangilio wa dizaini ya "Kimalaika wa nuru" kumbe ndani yake ni " utekelezaji wa kiapo cha ushetani na mkakati wa kufuta upinzani kabla ya 2020" mtupu.....

Soma tu ndani between lines utaligundua hili mara moja na utadhani kuwa ni full chembechembe za "nia njema", kumbe it's part of the strategic plans to lead the opposition to the road heading to hell before 2020 general Election...!!

Kama wanabisha, wanaopewa ushauri huu wenye "nia njema", wajaribu kuutekeleza waone impact yake....

In my opinion, acha Lowassa aende zake. Na nakubaliana kabisa na Mh. Freeman Mbowe, kuwa haya maisha yawe ktk nyanja ya kisiasa ama dini nk hayako "constant" kwamba ikiwa hivi basi inakuwa vilevile.....

It's like a Train Safari to Kigoma whereby on the way there will be get off and get in passengers....!!

Wanaoshuka hawawezi kuzuia Gari Moshi kuendelea na safari hadi mwisho wa Reli Kigoma....


Na haiwezekani kumshusha abiria kwa nguvu njiani mahali ambapo siyo Kituo chake cha kushukia....

Kumlazimisha Mbowe ajiuzuru kwa sbb ya EL, ni kumlazimisha abiria mwenye tiketi ya hadi mwisho wa safari - KIGOMA achukie Tabora junction na kumhadaa kuwa hapa ndo Kigoma .....!!
Nikiri wazi Mkuu kuwa Umenenena Vyema Na Nakubaliana Na Mawazo yako,unajua Hawa Kenge Aina Ya Mzee Mwanakijiji wamekuja Na Makala Ndeefu ambazo Mtu Ukizivamia Kwa Pupa unaweza Ukadhani Jamaa Wamekuja Na Recovery Plan Kwa ajili ya Upinzani Kujikwamua na Mkwamo Uliopo Sasa ila naomba nikuhakikishie Ndg.kitaturu Upo Sahihi 100% tangu Lini Magamba Kama Mzee Mwanakijiji wakautakia Mema Upinzani?? Waache Kutuhadaa Aisee kila Mtu apambane Na Hali ya Kwenye Chama Chake..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tz kuna wapinzani watatu kuwahi kutishia ccm...

Wakwanza ni Maalim Seifu
Wapili ni Dr Slaa
Watatu ni Tundu Lissu...

Sasa kabakia Lissu, sema walichompatia ni kumvunja miguu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 


NB: Makala hii pia nimeiambatanisha chini.

Na. M. M. Mwanakijiji
Kurudi kwa Lowassa CCM kumewagusa watu kwa namna mbalimbali. Wapo ambao wameshtuka na kuumizwa hasa wale ambao walifurahia kuhamia kwake Chadema wakati wa mbio za uchaguzi mkuu wa 2015 na upande mwingine wapo ambao wameshukuru kurudi kwake “nyumbani”. Wapo ambao wanajisikia hasira na kuona kama wamesalitiwa na wapo ambao wanashukuru kwa sababu wanaona kama hakuwa kweli “mwenzao” na sasa ametoka. Yote tisa, kuondoka kwake kumeacha maswali mengi kwa wengi.
Toka juzi nimepokea simu na messages nyingi zikiwa na maswali na mijadala mingi na kutoka na hilo nimeonelea nijaribu kuyajibu maswali haya mbalimbali na yatokenayo nayo katika kuelezea hili na mawazo yangu.

1. Swali: Unachukuliaje kurudi kwa Edward Lowassa CCM?
Mimi: Kurudi kwake hakukunishtua au kwamba sikukutarajia. Toka alivyoondoka CCM baada ya jina lake kufyekwa kule na kutaka kujaribu bahati yake CHADEMA jambo moja lilikuwa wazi; kama angeshindwa kupata Urais angerudi tu CCM. Kitu ambacho kimenishangaza zaidi ni kuwa ameweza kudumu ndani ya upinzani kwa miaka mitatu na nusu hivi. Hili nitalifafanua kidogo baadaye. Lakini niseme tu kuwa Lowassa sasa ana Amani na ni itakuwa makosa kumtukukana au kumkebehi.

2. Swali: Ina maana basi Lowassa hakuwa mpinzani kweli kweli?
Jibu: Lowassa hakuwa kiongozi wa upinzani kwa maana inayoeleweka. Alikuwa ni “mgombea wa Urais wa upinzani”. Ili kuwa kiongozi wa upinzani ni lazima mtu ajithibitishe kifikra, kiutendaji na kimkakati kuwa anataka kukiondoa chama tawala madarakani. Lowassa aliingia upinzani kwa sababu moja na sababu moja tu – kujaribu kuupata Urais ili kutimiza ndoto yake ya kuwa Rais. Hakuwahi kuonesha kujali yanayotokea upinzani, hakuwa kuunga mkono hoja za upinzani na hajawahi kuwatetea wapinzani muda wote kabla ya kuingia kwake upinzani. Kwa hiyo, kurudi kwake CCM si pigo kubwa au lenye maana sana kwa upinzani wa Tanzania.

3. Swali: Sasa hili linaiacha vipi CHADEMA? Huoni kama CHADEMA imejiweka kwenye wakati mgumu?
Jibu: Kwa kiasi ni lazima wakubali huu wakati mgumu na wakubali kuwa uamuzi wao wa kumchukua Lowassa ulikuwa ni wa mahesabu ambayo mojawapo ya jumla zake ilikuwa ni hatimaye Lowassa kurudi CCM. Kama walidhania kabisa kuwa Lowassa atakuwa mpinzani wa kudumu pamoja nao katika shida na raha basi walijionesha udhaifu mkubwa zaidi kuliko ambayo niliwafikiria. La maana ni kuwa huu si wakati wa kulia; ni wakati kuganga majeraha yao na kusonga mbele.

4. Swali: Huoni kama uongozi uliompokea Lowassa unahitaji kuwajibika?
Jibu: Mojawapo ya udhaifu mkubwa wa upinzani wa Tanzania ni kuwa hauna ujasiri wa kuwajibika. Yaani, watu wanaweza kuvuruga na kuvurugana lakini bado watu wale wale wanataka waendelee kuongoza kwa sababu wanaamini hawatovuruga tena au kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza kuchukua nafasi zao. Matokeo yake upinzani wetu bado unaelekea kuangalia kundi la watu unaoweza kuwahesabu kwa vidole kuwa ndio “viongozi wa upinzani” na hawa hawawajibiki, hawawajibishwi na wito wowote wa kutaka wawajibike utaonekana ni kutaka kudhoofisha upinzani.

5. Swali: Sasa ungetaka wawajibike vipi?
Jibu: Kwanza kabisa na kubwa zaidi ningependa kuona Kamati Kuu ya CHADEMA inakaa chini na ikimaliza kikao inakuja na tamko la kukubali makossa na kuwaomba radhi wa Tanzania kwa kuvuruga upinzani mwaka 2015. Hili ni lazima lifanywe. Ni lazima waseme kuwa walikosea; walitaka kutumia njia ya mkato kushinda Urais na walikuwa tayari kusalimu kanuni na misimamo yao ili tu waweze kuingia Ikulu. Waombe radhi.
La pili ni kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ni lazima ajiuzulu nafasi yake ile kufuatia kurudi kwa Lowassa CCM. Yaani, hawezi, hapaswi, na hatakiwi kabisa kuwa mtu wa kuiongoza CHADEMA kuelekea 2020. Si kwa sababu ni mtu mbaya, si kwa sababu simpendi (nina heshima ya pekee sana kwa Mbowe na mchango wake kwa upinzani) lakini kila jambo lina matokeo; bahati nasibu aliyocheza 2015 sasa imelipa; ameliwa. Kama kiongozi na mwanademokrasia wa kweli ni lazima yeye awajibike kwani ndio kiongozi mkuu wa chama. Anaweza kuendelea na nafasi zake nyingine lakini Chadema mikononi mwake tena haiku salama. Mbowe ni lazima ajiuzulu.

6. Swali: Huoni kuwa Lowassa alileta mchango mkubwa katika upinzani kuliko ule ambao ungeletwa na Slaa kwa mfano?
Jibu: Miaka mitatu baadaye lazima swali liulizwe mchango gani? Sasa hivi upinzani umepoteza hata majimbo uliyoyapata kwa haki. Sasa hivi haiwezi hata kujivunia kuwa “Lowassa kaongeza majimbo”! Wanaweza kusema walipata kura nyingi za Urais kuliko mgombea yeyote wa upinzani kabla. Lakini kura hizo zimewasaidia vipi? Je, zilikuwa ni sababu ya CHADEMA au sababu ya Lowassa; kama ni za Lowassa kwa kurudi kwake CCM hizo kura bado zimebakia CHADEMA? Ukweli ni kuwa mchango wa Lowassa ulikuwa ni wa kwa uchaguzi tu wa 2015 na si nje ya hapo au zaidi ya hapo. Kurudi kwake kumefuta (negate) mchango wowote wa maana kwa maoni yangu.

7. Swali: Unataka kusema Lowassa hakuwa na mchango wowote?
Jibu: La hasha! Mchango wa Lowassa ulikuwa wa muhimu kwa kiasi tu cha kwamba walikuwepo watu ambao walitaka Lowassa awe Rais mwaka 2015. Hawa ni wale waliokuwa kwenye yale makundi makubwa mawili. Makundi ambayo sasa hivi yako njia panda.

8. Swali: Makundi gani hayo?
Jibu: Kwanza kulikuwa na kundi kubwa la “Ulipo Tupo” ambao ni wale wana CCM ambao walizunguka na Lowassa kutafuta udhamini na ambao walijitokeza kwa maelfu kila alikopita kuunga mkono ugombea wake. Ni kundi la wana CCM ambao hawakuona shida kuimba “Tuna Imani na Lowassa” mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM. Kundi la wana CCM walioumizwa na kukatwa kwa jina la Lowassa. Hawa walienda na kumpigia kura alikokuweko na naweza kusema hata angeenda chama cha Wakulima wangemfuata maana walikuwa hawafuati sera bali sura!
Na kundi la pili sasa ni la wazungusha mikono wa “Mabadiliko-Lowassa”. Hili lilikuwa ni kundi la wanachama na viongozi wa upinzani ambao walifikiria wamepata hirizi (amulet) ya kuiengua CCM madarakani. Katika ngazi ya chini kabisa hawa ni wale waliodeki barabara na kutandaza kanga njiani ili “masiha” wao apite kuelekea Yerusalemu! Hawakujali alikuwa nani, alisimamia nini, na alitaka kufanya nini; wao walichotaka ni kumuona anaubeba upinzani mgongoni kwake na kuwahakikishia nafasi mahali pema peponi! Katika ngazi ya juu yake walikuwa viongozi wa juu kabisa wa Chadema ambao walijigeuza na kukubali kuuza kanuni zao, misingi yao na ndoto zao ili Lowassa naye awabebe wao pale wao waliposhindwa. Wote wakajikuta wamebadilisha mabadiliko kuwa ni mtu hata kama mtu huyo ni miongoni mwa watu waliosababisha watake mabadiliko hayo! Inanikumbusha kisa cha mbuzi waliolalamika kuliwa na chui mara kwa mara; wakaandaa maandamano makubwa ya kutaka “mabadiliko”. Siku moja mbuzi na wana mbuzi wakajiunga na maandamano hayo na wao wakaimba “mabadiliko”! Halafu mbuzi wakamchukua chui kuongoza mabadiliko hayo!!

9. Swali: Inaonekana kweli CHADEMA walikutibua sana Mwanakijiji?
Jibu: Hawakunitibua mimi hasa; walitibua yote tuliyokuwa tumeyapigania kwa karibu miaka ishirini. Kilichotokea kinaweza kuitwa “Usaliti Mkuu” wa harakati zote za mabadiliko. Ndio maana hata sasa hivi wanapolalamikia serikali na Magufuli binafsi sijawapa uzito unaostahili; kwa sababu sijui kama wanamaanisha, wanatania au wanatafuta tu mahali pa kusimamia.

10. Swali: Huoni kuwa labda upinzani ulilazimika kumchukua Lowassa kwa vile hawakuwa na namna nyingine ya kuweza kushinda uchaguzi?
Jibu: Hapa ndio mgongano mkubwa tuliokuwa nao. Chadema na washirika wake waliamua kutafuta njia ya mkato kushinda uchaguzi. Walitaka kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na chama kingine cha upinzani duniani – wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu kumchukua kiongozi toka chama tawala mwenye tuhuma za ufisadi kuwa mgombea wake wa Urais. Ni kweli walitaka kushinda lakini si kwa gharama hiyo! Na kurudi kwake CCM ndio kunathibitisha ni kwa kiasi gani ule ulikuwa ni uamuzi mbaya sana. Maisha ya watu wengi sana yaliharibiwa, ndoto za wapinzani wengi zilivurugwa, matarajio ya wale waliopigwa na polisi, waliouawa, waliojeruhiwa kwa kutaka mabadiliko. Yaani, hili ni zaidi ya Lowassa na Slaa, hili ni zaidi ya CHADEMA na CCM; lilihusu maisha ya watu. Kuna watu kurudi kwa Lowassa CCM kumewaumiza zaidi kuliko kuingia kwake CHADEMA! Kwamba, baada ya kejeli zote zilizorushwa dhidi yao kwa kumkataa Lowassa leo amerudi kule kule alikokuwa na kuiacha Chadema kwenye mataa yaliyozimika!

11. Swali: Vipi kuhusu CCM na wao kumpokea Lowassa mtu ambaye walimnanga na kulikata jina lake kama kuchinja kibudu; huoni kuwa wao sasa ndio wanaonekana wamekumbatia “mafisadi” kweli kweli?
Jibu: Kwanza kabisa ieleweke kuwa CCM kwa kumpokea Lowassa hawakupoteza kitu. Lowassa kwa kwenda CHADEMA alipoteza kila kitu. Kurudi kwake CCM basi ni bora zaidi kwa Lowassa kuliko hata kwa CCM. Lakini, kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa amerudi “nyumbani” na ni kweli amerudi nyumbani. Sasa kama alikuacha nyumbani kubovu na amerudi amekukuta kubovu tatizo siyo yeye bali ni wale walioachiwa nyumbani. Na kama atarudi na kuendelea na nyumba mbovu kwa vile wengine hawataki itengenezwe hilo litakuwa la kwake na wenzake.

12. Swali: Vipi kuhusu ufisadi naona unazungumza kwa misemo tu; CCM wamekumbatia mafisadi?
Jibu: CCM kama chama hakijabadilika. Mojawapo ya vitu ambavyo nimekuwa nivikirudia rudia toka kuchaguliwa kwa Rais Magufuli ni kuwa CCM ni “ile ile”. Ninaposema hili nina maana ya kuwa sera zake hazijabadilika, mtazamo wake kuhusu kutawala haujabadilika, na linapokuja suala la ufisadi katika mfumo wa kiutawala bado makubwa hayajafanyika.

13. Swali: Makubwa gani unafikiri hayajafanyika hadi hivi sasa?
Jibu: Nikianza kuyaorodhesha naweza kuandika kitabu. Kwa ufupi ni kuwa matatizo ya kimfumo bado yapo. Lakini matatizo ya kimfumo yanatoka na matatizo ya kisheria na matatizo ya kisheria yanatokana na matatizo ya kisera. Sera hutangulia mabadiliko ya sheria, na sheria hutangulia mabadiliko ya mifumo na mifumo ndio hutangulia mabadiliko ya jinsi watu wanafanya kazi. Hadi hivi sasa hakujatokea mabadiliko ya kisera ambao ndio msingi wa mabadiliko yote mengine. Na ndio maana nasema CCM ni ile ile.

14. Swali: Unataka kusema kuwa Magufuli hajafanya kitu chochote cha kubadilisha nchi?
Jibu: La hasha! Mabadiliko yote ambayo tunayaona sasa hivi ni kwa sababu ya Magufuli. Ni yeye mwenyewe; ndio maana wakati anawaapisha mawaziri hawa wapya juzi anahoji mambo yanayofanywa na Polisi na usishange siku mbili au tatu baadaye Polisi wanakuja na kitu. Tumeliona hili kwenye mambo ya bandari, TRA, Magereza n.k. Watendaji wanasubiri kuumbuliwa hadharani na Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Na tumeona hata baadhi ya mawaziri hawajui au hawaoneshi kama wanajua nini wanatakiwa kufanya kiasi cha Rais Magufuli kuwatengua! Sasa haya ni mabadiliko ya Magufuli; lakini kwa vile yanategemea mtu yanatumia nguvu kubwa zaidi. Ni sawasawa na mtu ambaye ameamua kusukuma gari ambalo amelitoa kwenye matope lakini badala ya kuliwasha liende anaamua kuendelea kulisukuma. Litakwenda lakini halitakwenda kama inavyopaswa kwenda kama likiwa limewashwa. Magufuli anajitahidi kusukuma gari na kwenye mteremko linaweza kufikia spidi nzuri tu; lakini lazima ifike mahali gari liwashwe na liende kwa kufuata kanuni za kimekaniki (mechanical laws).

15. Swali: Vipi kuhusu Dkt. Slaa ambaye alirudi CCM na sasa Lowassa ameenda huko huko CCM. Siyo kwamba aliondoka CDM kwa sababu ya Lowassa?
Jibu: Nisiwe mzungumzaji wa Dkt. Slaa kwani anaweza kujisemea mwenyewe. Lakini kwa vile ni rafiki yangu na ninamheshimu labda kuliko mwanasiasa mwingine yeyote Tanzania kwa hivi sasa naweza kusema mambo mawili. Kwanza, Dkt. Slaa hakurudi CCM; aliamua kuachana na “siasa za vyama” kama alivyoelezea katika hotuba yake pale Selena Hoteli. La pili ni kuwa kinyume na watu wengine wanavyochukulia utumishi katika serikali ya Tanzania – ukiondoa nafasi zinazotokana na kuchaguliwa haulazimishi mtu kuwa mwana CCM.

16. Swali: Unafikiri Magufuli anaweza kuteua mtu ambaye si mwana CCM kuwa Balozi?
Jibu: Siyo tu anaweza amefanya hivyo tayari. Na amethubutu kufanya yale ambayo siyo Mkapa wala Kikwete waliwahi kukifanya kwa kiasi hiki nacho ni kuteua watu kutoka upinzani kushika nafasi kubwa za kiuongozi. Kuteuliwa kwa Kitila na kwa Anna Mgwira ni mifano tu. Na siwezi kushangaa au kushtuka akiteuliwa mtu kutoka upinzani kuwa Mkuu wa Mkoa au hata Waziri. Kati ya vitu vingi ambavyo nimevielewa ni kuwa anataka mtu anayeweza kutekeleza kile ambacho Rais anakitarajia.

17. Swali: Lakini Dkt. Slaa hajawahi kurudishi kadi ya CCM na bado anaimilikia na hivyo yeye bado ni mwanachama, sivyo?
Wenye kutoa hoja hii wameamua tu kujitoa ufahamu. Katiba ya CCM (kama zilivyo katiba nyingine za vyama) imeelezea namna gani uanachama wake unakoma. Ibara ya 13:1 ya Katiba hiyo imelieleza hili. Kwa hiyo isipokuwa kama kuna mtu atakuwa ana uthibitisho kuwa a. Dkt. Slaa ameendelea kulipia ada ya chama na kutimiza masharti ya uanachama au b. alipoteuliwa kuwa balozi aliomba uanachama wa CCM tena. Nje ya hapo; kwa kadiri nijuavyo Dkt. Slaa hajarudi kuwa mwanachama wa CCM. Na kwa kadiri ninavyomjua kama ikitokea anataka kurudi CCM atafanya hivyo wazi na akianisha sababu zake za kufanya hivyo. Kujiunga na chama cha siasa ni haki ya kila Mtanzania isipokuwa wale ambao hawaruhusiwi kisheria.

18. Swali: Siwezi kukuachilia bila kukuuliza kuhusu mtu mwingine; Rostam Aziz. Tumemuona Rostam akijitokeza mara mbili hizi tena na Magufuli unachukuliaje hilo hasa kwa vile Rostam alihusishwa sana na ufisadi CCM na pia kuwa karibu sana na Lowassa?
Jibu: Nilisubiri uniulize hili. Kuna mambo kadhaa ambayo yanahitaji kuwekwa vizuri na sijui kama nitakuwa na muda wa kutosha kufafanua kila moja. Kwanza, kama Lowassa alikuwa arudi CCM asingeweza kurudi bila kuungwa mkono na Rostam Aziz. Lakini pia jambo moja kubwa ambalo kutoka na vyanzo vya kuaminika sana ni kuwa Lowassa kweli kabisa hakutaka kurudi CCM. Miezi michache tu nyuma Lowassa alikuwa amejiridhisha kumalizia siasa zake upinzani. Lakini Rostam au RA kama baadhi yetu tunavyomuita amethibitisha kitu kimoja ambacho kinahitaji kufikiria – bado ana nguvu ya ushawishi. Kuna vitu (factors) ambazo vimemfanya Lowassa aamue kurudi CCM – soma jibu langu la mwisho kudokeza mojawapo ya mambo yanayoweza kuwa yamemsababisha Lowassa kurudi CCM kwa ushawishi wa rafiki yake.
Jambo la pili ni kuwa Rostam ana nguvu na ushawishi wa kuweza a. kwenda Ikulu baada ya ndugu yake kuwekwa pingu akatoka huko alikokuwa na b. yeye naye alikuwa ametangaza kuachana na siasa za “majitaka” na akavua vyeo vyake vyote ndani ya CCM. Hivyo, kuonekana kwake hivi juzi kuna tuma ujumbe mmoja mkubwa – kwamba bado anaweza kupiga mluzi na watu wakaitika. Hili ni wazo la kutisha sana.

19. Swali: Unataka kusema RA amemuweka Magufuli almaarufu kama “jiwe” mkononi?
Jibu: Kuna watu wanaweza kuona hivyo na yeye mwenyewe anaweza kufikiria hivyo au kuwafanya watu waamini hivyo. Lakini nitakuambia kitu kimoja kuhusu Magufuli na hili nina uhakika nalo wa asilimia 100; Magufuli si mtu wa kuweza kufikirika amewekwa mkononi; umdharau kwa maangamizi yako mwenyewe. Kuna sababu kwanini Magufuli amemleta karibu Lowassa na Rostam na wengine wameshasahau – na Apson Mwang’onda vile vile. Hawa watatu kuja upande wa Magufuli ni kufanya kile ambacho msemo wa Kiingereza unakielezea – keep your friends close, but your enemies closer yaani weka marafiki zako karibu lakini maadui zako karibu zaidi! Lakini pia nafikiri kuna kitu Magufuli anakitaka kutoka kwa hawa watatu na nadhani naweza kukisia ni kitu gani hasa na wengine wanaweza kuwa tayari wamekikisia.

20. Swali: Ni kitu gani unafikiri Magufuli anakitaka kutoka kwa hawa?
Jibu: Siwezi kulisema kwa sasa.

21. Swali: Unaonaje sasa katika mazingira ya sasa kuelekea 2020 hasa baada ya kurudi kwa Lowassa?

Jibu: Lowassa kwa kweli siyo tishio kuelekea 2020. Angeendelea kubakia upinzani na kuendelea na hoja za upinzani angeweza kuwa ni ‘credible’ figure; yaani mtu wa kuaminika. Sauti yake ingekuwa na nguvu sana. Kwa sasa sioni kama kura za CCM zinaweza kugawanyika jinsi ambavyo zingegawanyika 2015. Hii ina maana kibarua kikubwa mwakani hakitakuwa kwa CCM bali kwa upinzani.

22. Swali: Utamuunga mkono Magufuli kama ulivyofanya 2015 na hasa Lowassa akiwa CCM?
Jibu: Hadi hivi sasa sijaona kwa kiasi kikubwa sababu ya kutokumuunga mkono Magufuli. Tatizo kubwa la CCM bado lipo na hivyo ni namna gani kutafuta uwiano wa mambo haya mawili. Sijui ni kwa kiasi gani Magufuli anaweza kuibadilisha CCM kwa sababu CCM ni ngumu sana; na kama watu wanafikiria kuwa Magufuli ameidhibiti CCM subirini muone wakati utakapofika kumaliza muhula wake wa pili. Mnyukano utakaotokea CCM utakuwa ni wa kukumbukwa! Isipokuwa tu kama kutatokea kitu kikubwa sana 2020.

23. Swali: Una maana gani?
Jibu: Nilisema mwanzoni kuwa ndogo za Lowassa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimekufa. Nimesema hapo juu kuwa ujio wa Rostam Aziz sasa hivi na kumrudisha rafiki yake CCM una maana yake. Kumbuka mwanzoni mwa miaka ya 2000 RA alijulikana sana kama “the King Maker” yaani mtu anayewapatia watu “mfalme”. Vipi kama ndogo ya Lowassa kugombea Urais itakuwa ni kama ya viongozi wale waliokuwa tayari kutawala kwa mhula mmoja tu; vipi kama wanaweza kufanya kama kilichofanywa Urusi? Na yakatokea mabadiliko ambayo ndio wameyapigia mahesabu; vipi kama ndogo ya Lowassa kuwa mgombea wa Urais ni ya 2020? Magufuli amekuwa akilalamikia sana ugumu wa kazi ya Urais na ni jinsi gani umekuwa mzigo mkubwa sana kwake kiasi kwamba niliwahi kuandika Makala kuwa kama kweli anaona ni mgumu hivyo Katiba imeweka njia za yeye kuutua; vipi kama tayari ameanza kufikiria kuutua mzigo huo mara moja kwa sababu unakuja na lawama nyingi sana? Hili wazo ukiliendeleza kwa mbali zaidi unaweza kushtuka sana. Labda ndoto ya Lowassa haijazimika kabisa.

24. Swali: Hapa unaenda kuzua mijadala mingine. Vipi kuhusu nafasi ya Lissu maana hatujazungumza lolote kuhusu Lissu na yaliyotokea na nafasi yake kuelekea 2020?
Jibu: Sasa hapa tutaanza mjadala mwingine; hili niulize tena wakati mwingine nina majibu mengine ya kufikirisha. Jambo hili halijaweza kuangaliwa vizuri sana linaangaliwa kishabiki, kihamasa na kihisia zaidi. Kuna mambo mengi.
MWISHO

Huna jipya
 
Ccm bana wanapenda siasa nyepesi eti, wameandaa maandamano kesho ya kuuga mkono kutoka Lowasa kuondoka sebuleni kuhamia chooni
 
Back
Top Bottom