Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo. Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally. Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim n.k
.
Sikushangazwa na taarifa hii.
Akili ya binadamu ni kama komeo la mlango.
Linafunga na kufunguka.
Yaani, "human mind is a flip-flop structure."
Katika wakati T1, endapo angalau 50.1% ya ushahidi inaonyesha kwamba P, na ushahidi ulio chini ya 50% unaonyesha kwamba sio-P, basi unafungamana na upande wa P, mpaka hapo katika wakati T2, ambapo mizania ya ushahidi itakabadilika.
Mwaka 2015 ni T1 na mwaka 2019 ni T2. Kauli P, yaani tamko kwamba, "CDM ni bora kuliko CCM" likikuwa sahihi mwaka 2015. Na kauli ya sio-P, yaani tamko kwamba, "CCM ni bora kuliko CDM" liko sahihi mwaka 2019. Usahihi unapimwa kwa uwiano wa asilimia ya ukweli.
Hiyo ndio tafsiri yangu ya uamuzi wa Mhe. Lowassa.
Bila shaka atapata nafasi ya kutwambia ni kwa nini mwaka 2015 aliona kuwa "CDM ni bora kuliko CCM" na mwaka 2019 ameona kuwa "CCM ni bora kuliko CDM"
Tunasubiri.
Mama Amoni.
PICHA YA MHE. LOWASA AKIPOKELEWA LUMUMBA DAR, MAKAAO MAKUU YA CCM