Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

1551454442096.png
 
Yeye na Sumaye wote Maboya tu na maji siku zote hufuata mkondo, hivyo fisadi moja limerudi nyumbani kwa mafisadi wenzie.

Nilikuwa nikijiuliza Lowassa yuko Chadema ila kimuonekano kama yupo CCM yaani yupo kimya vyama vya upinzani visiludie tena kosa kama hili walitumia nguvu kubwa kumsafisha.
 
Ni jambo jema mzee wa watu aende kusafishwa na matusi yote aliyotukanwa na CCM kuwa alijinyea stand ya chato, ni lofa na mpumbavu, fisadi aliyekimbilia CHADEMA.
 
Walaaaaa

Mzee hata hujui analysis yoyote about opposition...

Maalim na Lowassa hawana intersection wewe!

Lowassa amerudi humo,ile mamba haijafa,itamgeuza Jiwe kitoweo,subirini!
huko kwa ccm watajipanga wenyewe,, minazungumzia,, maono ya lipumba kwa ed low,, hawezi mtu akapewa nafasi ya kugombea urais kwa ukawa kwa kuhonga hela,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa tu. Hakuwa na lolote ndani ya CDM, aliwatanguliza wenzake warudi CCM akijua na yeye atafuata.
 
Kwa hili unaweza kumkufuru Mungu ukahisi kweli sisi wafirika tumelaaniwa!!
Mbona siamini kama kweli hili jitu limerudi ccm!!!!! Hili ndilo liliimbwa kwenye kampeni za ccm kama ni fisadi, haliwezi kutakata hata kwa omo! Mahakama ya mafisadi ilifunguliwa kwa ajili yake, linaumwa ule ugonjwa ambao mimi siwezi kuutaja isipokuwa Pena alitaja!
 
Leo siyo fisadi tena?
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim n.k



View attachment 1035375View attachment 1035381

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums


In God we Trust
 
Fisadi mwingine huyo yeye na Sumaye yalikuwa makosa makubwa sana kuwakaribisha Chadema mafisadi hawa wawili. Hawana impact yoyote ile ndani ya Chadema.
Sumaye anasubiri nini yeye kuondoka wakati walienda wote cdm

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Siasa ni Si hasa.

Unachoamini ni kweli kumbe sicho.
Bado miezi 20 tu tufanye uchaguzi babu yetu ameamua kurudi nyumbani.

Imenivunja moyo kama mpenda maendeleo, Mpenda ushindani, mpenda changamoto.

Sidhani na siamini kama 2020 kuna atakaetoka Madarakani.

Kwangu mimi ni habari mbaya, Mbaya Mnoo. Ila yote kheri maisha lazima yaendelee.

Tuombe tu uzima.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo. Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally. Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim n.k
.
Sikushangazwa na taarifa hii.
Akili ya binadamu ni kama komeo la mlango.
Linafunga na kufunguka.
Yaani, "human mind is a flip-flop structure."
Katika wakati T1, endapo angalau 50.1% ya ushahidi inaonyesha kwamba P, na ushahidi ulio chini ya 50% unaonyesha kwamba sio-P, basi unafungamana na upande wa P, mpaka hapo katika wakati T2, ambapo mizania ya ushahidi itakabadilika.

Mwaka 2015 ni T1 na mwaka 2019 ni T2. Kauli P, yaani tamko kwamba, "CDM ni bora kuliko CCM" likikuwa sahihi mwaka 2015. Na kauli ya sio-P, yaani tamko kwamba, "CCM ni bora kuliko CDM" liko sahihi mwaka 2019. Usahihi unapimwa kwa uwiano wa asilimia ya ukweli.

Hiyo ndio tafsiri yangu ya uamuzi wa Mhe. Lowassa.

Bila shaka atapata nafasi ya kutwambia ni kwa nini mwaka 2015 aliona kuwa "CDM ni bora kuliko CCM" na mwaka 2019 ameona kuwa "CCM ni bora kuliko CDM"

Tunasubiri.

Mama Amoni.

PICHA YA MHE. LOWASA AKIPOKELEWA LUMUMBA DAR, MAKAAO MAKUU YA CCM

1551457575475.png
 
Back
Top Bottom