Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Baada ya kwenda na kurudi Ikulu ...na kupewa masharti magumu naona leo mzee kaamua"kusurrender"...
wanaachiwa kwa NOLLE muda wowote, kuwa DPP hana nia y'a kuendelea na kesi, au wataomba wakumbushwe shtaka, then wanakubari wanapigwa faini habari imekwisha,

LOWASA amejishushia heshima, ni bora angestaafu siasa tu yule baba
 
Perfect time lets see wangapi mtajishughulisha na uchaguzi wa serikali za mitaa na wa 2020, Lowasa mbinguni huendi
 
Baada ya kwenda na kurudi Ikulu ...na kupewa masharti magumu naona leo mzee kaamua"kusurrender"...
Ni kweli mkuu damu ni nzito kuliko chama wataachiwa na kufutiwa kesi, sishangai nililitegemea ili lakini ameacha mtaji mkubwa. Ninachoshauri wanachadema msimtukane kama ccm walivyomtukana sasa sijui aibu wataziweka wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za Tanzania ni ajabu akiya mama yani lowasa kawamwaga kweupeew hahah hataki shida ....wanasema mpira umeludi gorini,,,cjui mpira umeludi kwa kipa,,cjui kipa kaludi kwa mpira eeee vyovyote ilimladi mpira umeludi

am better here
 
Kuondoka kwa EL chadema nadhani kumewarahisishia tu viongozi kutua mzigo ambao kwa kiasi fulani ulikua umewazidi nguvu. Sasa watapumua maana walikua wamefungwa mikono. Bila shaka hawatarudia tena wakati mwingine. Wajifunze sasa kuandaa wagombea wao badala ya kusubiria makapi kutoka ccm.
 
Ka form four failure kanakojiita la saba sijui katamwangalia vipi huyu Mzee ,ila hili li chama kwa unafiki kinaongoza tutakashudia kanavyompongeza bila haya Mara vikao vya bunge la bajeti litakavyoanza ,yeye na wanafiki wenzie .
 
Umenena umemaliza,Lowasa kasoma upepo upinzani hawezi simama, heri alinde mali na soon mkwe atatoka maisha yaendelee, ni shinikizo LA mda mrefu,anaeweza kupambana na Iisu ni lowasa au Membe 2020 ili chama kisife, ccm iwatumie hao wanakubalika kote kote ccm na upinzani. Huyu ccm mpya hana Kazi ngumu sana kupenya kupambana na Lisu maana kavuruga si mjini si vijijini hauziki zaidi kwa wachumia tumbo na wenye nasaba kama zake.Hoja anazozitegemea ni SGR, bomberdia na stirls goerg ambapo kwa layerman ni msamiati mkubwa ukimwambia SGR,bombardia atadhani ni majina ya Dawa.Lowasa Membe wana nyota za pesa ndani ya mwaka tu nchi itajaa pesa,Lowasa aliinua elimu hii iliyokufa.
 
th
Walipokutana Mwembe Yanga tarehe 15 Septemba, 2007 wakiwa na orodha ya mafisadi papa nchini akiwamo waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa, wapinzani walisahau kitu kimoja au viwili. Kwanza, walikuwa wanaandaa kifo cha Lowassa kisiasa ndani ya CCM na Tanzania. Pili, walikuwa wamemtendea kosa ambalo asingeweza kulisahau maishani mwake bila kulipiza kisasi. Kwa wataalamu wa mambo, tulijua fika kuwa Lowassa alipojiunga na upinzani alisukumwa na sababu kuu tatu yaani:
Mosi, hasira baada ya kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais.
Pili, imani kuwa angeweza lau kushinda kupitia upinzani hata kushindwa bila kupoteza lolote zaidi ya upinzani.
Tatu, alitaka kulipiza kisasa kwa namna upinzani ulivyombomoa na kumtangaza kuliko mafisadi wengine uliotaja.
Tatu, alitaka kuukomesha upinzani na kujijengea nafasi maalumu kwa CCM ambayo, nayo bila shaka, ilijua kuwa alichokuwa akifanya kada wake huu kingeisaidia kwenye uchaguzi husika. Sababu ziko nyingi. Ila hizi tatu ndizo zingemfanya mchambuzi yeyote mahiri kutabiri kurejea tena kwa Lowassa CCM siku moja kama ambayo amefanya leo. Kimsingi, kama kuna aliyeuua upinzani si mwingine bali aliyeushauri kumpokea Lowassa.
Sasa Lowassa ametimiza malengo yake yote. Kuna haja gani ya kubakia upinzani? Kujua tulivyoliona hili tangu siku ya kwanza, SOMA LINK HIIhttps://mpayukaji.blogspot.com/2015/11/when-bongo-politics-became-nastily.html
 
Back
Top Bottom