Nyie mlipomchukua alikuaje ? Labda tuanzie hapo.
Hili pigo la leo pale ufipa ni kama bomu la nyuklia vile.
Hii nchi inaongozwa na ccm toka mwanzo, maendeleo huyaoni?Then wasiporudi bungeni wewe na jamii yako mtapata maendeleo gani??
Watu wa Mungu habari zenu..
Tetesi za ndani za CDM ni maumivu makali baada ya Mh Lowassa kurudi nyumbani kumenoga..!! Yaani ni sawa kuvunjika kwa uti wa mgongo, haiwezi tena kujitutumua hata kidogo kisiasa..!! Poleeeeni..!
CCM haishindwi chochote huwa nasema hivi kila mara.. Sasa mmeona na kudhibitisha..! Chezea kitu kingine sio CCM..!! CHADEMA leo bado wako ktk maruweruwe hawajui nini kimetokea, hawaamini bado..!! Siasa mchezo mchafu sana..!! 😜😂😂
Karibu tena nyumbani.Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.
Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.
Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k
Habari zaidi...
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.
Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.
Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.
Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.
Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.
Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.
Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.
View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448
Unaweza soma pia:
Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums
Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums
Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums
ila Lisu hawezi itikisa CCM ni mwepesi kama karatasi..hakuna aliyewahi kuwa naye Karibu kwenye mfumo. .Lowasa alitikisa na bado hakufurukuta..Kwa upande wa chadema anefaa kw sasa inaonesha kuwa ni Lissu ndo mwenye mvuto wa kisiasa na ameonesha nia ya kugombea 20/20 soo upepo haupo kw lowasa kw sasa na ameona hawez kumzuia lissu kugombea badala yake emeona arudi alikotoka. Pengine chadema walifanya makosa kumpokea na kumpa nafasi ya kusimama kama mgombea urais. Siwalaumu chadema kwani hili ni funzo kwao
Sent using Jamii Forums mobile app
Lowassa ni fisadi au sio fisadi?
My sweet tuachane na siasa ,bora tufanye yetu lolHili gamba fisadi linajali tumbo lake tu na si maslahi ya Watanzania.
Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa vinataka mgombea wa kitaifa awe amejiunga na chama zaidi ya mwaka. Hivyo muda mwafaka wa wanasiasa kuhama ndio huu kama wana nia ya kuteuliwa kugombea nafasi yoyote ya kitaifa na chama husika.Mwacheni Lowassa ahamie CCM ni haki yake ya kikatiba. 2020 kuna mtu atarudi tena Chadema.
Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi Lowassa leo ametakasika au bado ni mchafu?Makamanda mnatapatapa.
ila Lisu hawezi itikisa CCM ni mwepesi kama karatasi..hakuna aliyewahi kuwa naye Karibu kwenye mfumo. .Lowasa alitikisa na bado hakufurukuta..
Unaniumiza kichwa ujue mbili haikai moja inapotea,unakuja na kupotea hahahaha, sikubali nakufata ulipo!!!!Watu wa huku JF nimewavulia kofia maana wanajua kufukua makaburi humu na wakikudaka utajuta kuzaliwa. Bora ku lay low tuu. Wasalimie mama zangu wadogo wote nimewamiss sana ila wasipotee sana[emoji4]
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwenye ile hotuba nzuri Dkt.Lowassa ya leo aitupie tafadhali...
Nasikia kamwaga nondo za kufa mtu.