Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Tatizo wanajua kucheza na upinzani hawajui kucheza na wanainchi.

sisi wanainchi lowasa au mbowe kuhamia ccm kwetu sio jambo kubwa. kwetu sisi tunataka nafuu ya maisha. tufanye biashara vizuri tulime tusipangiwe kwenye uuzaji.
 
Ni ufinyu mkubwa wa akili kudhani kwamba kuondoka kwa fisadi lowassa chadema imevunjwa uti wa mgongo. Hakuwahi hata kwa sekunde moja huyu fisadi kuwa uti wa mgongo. Acha UZUSHI wa kuandika pumba humu. Hebu twambie positive impact ya huyu muongo mkubwa na fisadi aliyekubuhu katika miaka mitatu na ushee akiwa chadema, ambaye kipindi kirefu alikuwa kimya.



Watu wa Mungu habari zenu..

Tetesi za ndani za CDM ni maumivu makali baada ya Mh Lowassa kurudi nyumbani kumenoga..!! Yaani ni sawa kuvunjika kwa uti wa mgongo, haiwezi tena kujitutumua hata kidogo kisiasa..!! Poleeeeni..!

CCM haishindwi chochote huwa nasema hivi kila mara.. Sasa mmeona na kudhibitisha..! Chezea kitu kingine sio CCM..!! CHADEMA leo bado wako ktk maruweruwe hawajui nini kimetokea, hawaamini bado..!! Siasa mchezo mchafu sana..!! 😜😂😂
 
Ruge huyu jamaa itakuwa ameuwawa na sumu kali sana sana kama polonium-210 tena itakuwa alikula, aliivuta au alikunywa huenda ilikuwa ni dozi ndogo aliyopewa na mtaalam wa hali ya juu. Mazingira yanaonyesha kabisa maana tangia mwaka jana alipoanza kujisikia vibaya akiwa kwenye hafla fulani.

Dalili za kupewa sumu ndo hizo kujisikia vibaya kuharisha, kutapika na baadhi ya organ za mwili kushindwa kufanya kazi vizuri na mwishowe kifo. Anyway hii inaonyesha serekale tuliyonayo ni ya aina gani.

Kwenye kumuaga Ruge kuna watu watalia sana kuliko wenye msiba ila ili ku shift attention wakaona wafanye wanamleta mzee Lowassa ila watambue CCM makada ipo siku watakuwa wakimbizi. Waanze kuandaa sehemu z kukimbilia maana sasa mambo yamekwiva

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k

Habari zaidi...

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.

Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.

Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.

Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.

Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.

Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.

Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums
Karibu tena nyumbani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
siasa ni mchezo wa hovyo sanaa nakumbuka wale waliokuwa wakiimba siku ile dodoma ktk ule ukumbi wao walikuwa wakiimba '' ninaa imaniii na Lowasaaaa nina imaniiii na Lowasaaaaa '' ss sijui itakuwaje
 
Kwa upande wa chadema anefaa kw sasa inaonesha kuwa ni Lissu ndo mwenye mvuto wa kisiasa na ameonesha nia ya kugombea 20/20 soo upepo haupo kw lowasa kw sasa na ameona hawez kumzuia lissu kugombea badala yake emeona arudi alikotoka. Pengine chadema walifanya makosa kumpokea na kumpa nafasi ya kusimama kama mgombea urais. Siwalaumu chadema kwani hili ni funzo kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
ila Lisu hawezi itikisa CCM ni mwepesi kama karatasi..hakuna aliyewahi kuwa naye Karibu kwenye mfumo. .Lowasa alitikisa na bado hakufurukuta..
 
Mwacheni Lowassa ahamie CCM ni haki yake ya kikatiba. 2020 kuna mtu atarudi tena Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa vinataka mgombea wa kitaifa awe amejiunga na chama zaidi ya mwaka. Hivyo muda mwafaka wa wanasiasa kuhama ndio huu kama wana nia ya kuteuliwa kugombea nafasi yoyote ya kitaifa na chama husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr slaa cyo ccm.
mbowe anapaswa kuwajibika kwa aibu lake hili.
tulimwonya akakaidi haya ndyo matunda yake yakutema big g kwa karanga ya kuonjeshwa
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania kimesema kuondoka kwa mwanachama wake, Edward Lowassa na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) hakutakuwa na madhara yoyote.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Machi 1, 2019 na Katibu Mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania, Dk Vicent Mashinji alipozungumza na Mwananchi muda mfupi baada ya Lowassa ambaye ni waziri mkuu wa zamani kutangaza uamuzi huo.

“Tunamtakia maisha mema huko aendapo, yeye ni mtu mzima anajua anachokifanya,” amesema Dk Mashinji.
Alipoulizwa iwapo uamuzi wa Lowassa unaweza kukitetelesha chama hicho kikuu cha upinzani Dk Mashinji amejibu kwa kifupi “It will never happen"(haiwezi kutokea).

Na Tausi Mbowe, Mwananchi
CHADEMA YAFUNGUKA LOWASSA KUREJEA CCM..."YEYE NI MTU MZIMA ANAJUA ANACHOKIFANYA"

Neno la Sumaye baada ya Lowassa kurejea CCM

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye ameeleza maoni yake baada ya kusikia Edward Lowassa kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Sumaye amesema "Mimi haunipi shida, mtu akiamua kuhama chama na kwenda kingine ni uamuzi wake,” alisema Sumaye.

"Kama kaamua acha aende, sisi tutaendelea kujenga chama na hicho unachokisema cha kuhama ni ndoto ambayo haipo,” amesema Sumaye alipoulizwa kama na yeye ni miongoni mwa watakaorejea CCM.

Edward Lowassa alijiunga CHADEMA Julai 2015 baada ya jina lake kuenguliwa kwenye mchakato wa kutafuta mgombea wa Urais ndani ya CCM


Neno la Sumaye baada ya Lowassa kurejea CCM - MUUNGWANA BLOG
 
Mwenye ile hotuba nzuri Dkt.Lowassa ya leo aitupie tafadhali...

Nasikia kamwaga nondo za kufa mtu.
 
Watu wa huku JF nimewavulia kofia maana wanajua kufukua makaburi humu na wakikudaka utajuta kuzaliwa. Bora ku lay low tuu. Wasalimie mama zangu wadogo wote nimewamiss sana ila wasipotee sana[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaniumiza kichwa ujue mbili haikai moja inapotea,unakuja na kupotea hahahaha, sikubali nakufata ulipo!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom