Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.
Kazi ipo kwa wale wafia siasa 😀
 
😁😁😁😁😁shikamoo Siasa,Japo dirisha la usajili lilifungwa na TFF wameibeba timu yangu ya Yanga na kufungua TMS kwaajili ya former Pm kuupdate kadi yake
 
😁😁😁Hii nchi raha sana,alipokuwa upande ule alifutwa Kwenye list of shame,kaondoka upande ule wameupdate list ya mafisadi,akirudi tena huko?
 
Itakuwa faida kwa upinzani 100%....

Nilishapiga kelele sana hapa kuhusu Lowassa na Sumaye....

Hawa ni watu walioshiriki kila aina ya ufisadi ndani ya ccm .

Angalia sasa tamaa ya mbowe sijui na Dr slaa uso wake atauweka wapi?....

Niwakati wa Lissu kapewa chama na kumshawishi Bi Fatuma karume wagombee 2020 tuchukue nchi mapema...

Fukuzeni na Sumaye kwenye chama ungana na Zitto awe waziri mkuu baada ya uchaguzi hapo tutawapigania kwa hali na mali.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hao uliowataja kabisaaa ndo wawe first families,unaota mkuu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Beshe ana simama upande wa aliye mlea ndio maana leo Rostam kaonekana Lumumba


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Msiba wa Ruge?

Hapana. Hakuna sababu ya msingi kwa Lowassa "ku-divert attention ya Watanzania kutoka kwenye msiba wa kitaifa wa Ruge."

Hata hisia kuwa "kuna mkono wa mtu kwenye kifo cha Ruge" hazijapata umaarufu kiasi cha kupelekea Lowassa akurupushwe leo ili "azime" suala hilo.

Kuwatenga waliomtosa Lowassa?

Uwepo wa Rostam Aziz katika tukio unaweza kuwa ishara ya uhusika wake katika uamuzi wa Lowassa kurejea CCM. Na uhusika wake unaweza kumaanisha kuwa "mapacha wawili kati ya watatu" wa MTANDAO wa JK (JK mwenyewe, Lowassa na Rostam) sasa wapo kwa Jiwe.

And where does that leave JK? Well, he was the major force behind kutoswa Lowassa. With him were Mkapa na Mwinyi. Sio siri kuwa wote watatu have fallen out of favour with Jiwe.

Nadhani katika hili labda tuache muda uongee.

October surprise?

Katika siasa za uchaguzi huko Marekani, "October surprise" ni tukio la makusudi linalolenga ku-influence matokeo ya uchaguzi.

Ninaazima political jargon hiyo kumaanisha kuwa huenda tukio hilo la leo linalenga ku-preempt tukio jingine kubwa ambalo "mtu flani" anatarajia linaweza "kupozwa" na ujio wa Lowassa huko CCM pindi tukio hilo likitokea.

Ugumu wa kuongelea tukio hili kama ule uliojitokeza katika kujadili uwezekano wa Lowassa kurejea CCM. Kila baadhi yetu tulipofungua mdomo sio tu kubashiri kuwa Lowassa angerudi CCM bali pia kumtuhumu kuwa huenda anakihujumu chama hicho, tuliishia kutukanwa



Kwahiyo to be on the safer side, si vema kuongelea kitu ambacho huenda kikatafsiriwa kuwa ill wish if not sedition. But something is indeed cooking.

Nafsi inakataa sio kuamini kuwa kweli Lowassa karudi CCM (lilikuwa suala la when na sio if) bali kuamini kuwa kurudi kwake CCM LEO ni kwa vile "leo ni siku kama nyingine."

Time will tell.




Sent using Jamii Forums mobile app
Haa,Kumbe hata Hama ya Kingu ilikua kuzima kifo Cha Mzee wa "APEDOMIA"!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo ndio nimeamini kuwa shida kubwa iliyoko ndani ya CCM ni wizi wa kimfumo.
Si ni huyu Lowasa aliye sababisha mpaka zika anzishwa mahakama za mafisadi ?
Na si ni huko huko CCM ndio walipo akina Tibaijuka wa Escrow, Change au jina jingine nyoka wa makengeza, William mwana Ngeleja , au mahakama ya mafisadi ilikuwa kwa Abinda Singh, na Rugemalira.
Ama kweli CCM sasa leo nimeamini kuwa mchawi anaye iroga Tanzania ili isipate maendeleo ni Chama cha mafisadi CCM

Sent using Jamii Forums mobile app

na bado CDM ya Lissu na mbowe ikamchukua

kaa kimya
 
Broo ban***gi haijawahi kukuacha salama
Chadema wao walimnunua kwa kiasi gani?? Mapovu tuu. Kwa taarifa yako Lowassa ameona hakuna faida ya kuendelea kukaa kwenye chama mfu ukitilia maanani sheria ya vyama vya siasa imepita hivyo ulaji wa ruzuku umebanwa sasa anakaa Chadema kwa lipi? Na 2020 kuna uwezekano Chadema wakupata wabunge wawili ama watatu tu. Amerudi nyumbani kumenoga!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom