Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Leo nitakesha kwenye bar kwa furaha ya Lowassa kuondoka cdm. Alaaniwe Mbowe na genge lake kupokea hela ya Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais.
Mbowe nafasi ya Uenyekiti anaifanyia biashara , inabidi tumng'oe

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
Lowassa katumia uhuru wake ambao upo katika katiba ya Tanzania.

Tatizo wapinzania hasa Mbowe alipaswa kumsikiliza Dr Slaa lakini kwa mapenzi yake na pengine uswahiba wake kwa Lowassa alisahau chama kilihitaji kufuata misingi yake na kuheshimu wanachama waliokipigania chama miaka mingi nyuma tena wengine hata walimwaga damu.

Hakika hili ni funzo kubwa sana kwa upinzanisijui kama kuna funzo lingine zaidi ya hili.
 
Dr Slaa alikuwa very right.Kwa kweli Mbowe anastahili lawama kubwa sana.
Wengi hamjui magumu anayopitia huyo mzee, Hiyo ndio njia pekee ya kumuokowa mkwe wake Sioi Sumari, na kumpa faraja binti yake Pamela na mke wake pia, kuna wakati binadamu unakosa option zaidi ya family first, bahati nzuri mimi naelewa kifamilia anapitia wakati gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Dr Slaa ata ondoka CCM kwakua fisadi karudi? kwa hisani ya twitter
 
Kila la heri mzee Lowassa ni haki yako kikatiba japo umeumiza walio wengi waliojitoa kukusapoti wewe na kiukweli kama vijana tuliamini kuwa wewe ndiyo rais wa mioyo ya watanzania na hao uliowafuata walikutangazia hata kufa ndiyo hao waliokuchafua kwa madai umejinyea jukwaani ila vijana na makamanda wa kweli tulijitahidi kulipigania hili kulinda utu na heshima yako ila nachoamini Chadema itasimama na wale walioanzia ndani ya chama, nenda mzee Lowassa nenda kapige push up

Sitegemei kuona viongozi wangu wa chama cha demokrasia na maendeleo wakikusemea mbovu zaidi ya kukutakia heri huko ulikorudi ila tambua CHADEMA itaendelea kusimama na kuimarika kila leo

Wambie kesi ya uchochezi na uhaini wakufutie ila Mbowe na viongozi wote wa chama hawatakatishwa tamaa na kurudi kwako
"
 
Ujio wa Lowasa CCM kwa sasa una faida gani katika uimara wa chama hicho? Je, ni upi mtizamo wa viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama hicho?

Je, kwa chadema Leo hii kuondokewa na Lowasa ni faida au hasara? Alikuwa na ushaeishi?

Kwa Mahakama na serikali, ujio wa Lowasa CCM hauwezi kuwa na viashiria vya rushwa hasa pale yatakapotolewa maelekezo ya kuhitimishwa kwa kesi ambazo zinawahusu ndugu na jamaa zake?

Kama ujio wake CCM utapelekea baadhi ya watu kutoka magereza, je haitaleta picha kuwa tumewaweka watu kwa sababu za kisiasa na hivyo kumfanya jaji mkuu na muhimili wake kuonekana unatumika kuwakandamiza wananchi wenye mrengo tofauti na serikali au chama tawala?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenye ccm wameanza kurudi ( lostam + lowasa) waliokuwa wameshika nafasi zao matumbo joto
 
mapambano bado yanaendelea comrades
lowasa hakua na influence chadema alkua tuu kama picha
off course niliimisi chadema ya harakati maana jiwe bila harakati halita toka

membe akija chadema naomba asigombee, chama kirudi kwa wenye chama
Lowasa kaathiri sana siasa za Chadema haswa kuhusu ufisadi, ukumbuke hii miaka 3 CDM imemtetea sana Lowasa na Sumaye kuwa siyo Mafisadi ili hali CCM ilikuwa ikijinadi kuwa mafisadi wamekimbilia CDM,
Nasubiri kumwona Polepole na siasa zake kuhusu Lowasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fisadi Rostam kamrudisha Fisadi mwenzie. Rostam anawachezea sana akili CCM anawaona mabwege na wao wanashindwa kujua hilo.
 
Kwa hiyo Lowasa sio fisadi tena eeeee Siasa nzuri jamani
 
Lowasa karudi Fisiem kesho tutegemee Shilingi yetu kupanda thamani zidi ya dollar

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom