Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Mabadiliko haya ni kumnusuru mkwewe Lowasa -SIOI SUMARI , unbailable offence of money laundering, mtu akikuahidi kuwa nitafuta kesi, if it were you, what will be your option!?
Hopeless thread!!
 
Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.
Lowasa ni fisadi.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums



Mzee kwa kucheza bembea anaweza sana, ikiwezekana sasa ziwekwe kamba za waya badala ya manila

Na wakati wa uhamisho havai kama wale wanaompokea, ni kama vile anatega mitego
 
Mimi bado naisubiri siku idadi kubwa ya Watanzania itakuwa ni watu wenye upeo wa kutafuta mifumo thabiti inayohakikisha uongozi wa maana nchini zaidi ya kuishia kufikiria kukabidhi matumaini yote kwa binadamu fulani fulani na kuishia kuwaabudu. Yaani tufikie upeo kama uliopo Marekani ambapo mfumo unampa raisi madaraka na nguvu zote za kuwa kiongozi wa taifa kubwa duniani lakini unamuondolea "kitu kujisahau" na kujifikiria mungu.

Leo Watanzania na shule zetu tunahangaika na Magufuli, Lissu, Slaa, Membe, Nchemba, n.k. Tunatafuta masiha ambaye tutamkabidhi madaraka yote kisha tumuachie atumie utashi wake kuamua chochote kutuhusu! Halafu jamaa akiamuru jeshi likabangue korosho au akitoa ndege kuzika "mswahili" nyuzi zinaanzishwa kwa fujo JF kama vile hatukuhusika na maauzi ya aina hiyo! How minimal Tz politics have become, sad! Anyway, let me continue living the dream. At times, it really feels good heading the opposite direction of the crowd.
 
Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.

Balanced..
Hiyo chorus itakuwa mfu.
 
We unadhani ukitokea uhaba mkubwa wa CONDOMS tz Rais ataacha kutafuta mbinu ya kuwaokoa wa kwao huko CHATO...

Cha kwanza katika siasa ni
1.Maslahi
2.Maslahi
3.Sifa
4.Historia
5.Maendeleo ya watu yenye maslahi yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ilivyo kawaida, endapo atajitokezza kiumbe kumkashfu au KUMSEMA vibaya Lowasa Basi ajiandae kupambana na jeshi la polisi.

Awali maneno yake yalikuwa ya uchochezi ila leo Mhe. Dingilai kasema amefutiwa dhambi zake na amekuwa mpya.

Usimtamkie mabaya mzee wetu, Msukuma yule jamaa yako uliyemtusi amerudi kwao Sasa jiandae kumfanya rafiki ukigoma acha chama.

Nape mzee karudi so jiandae kumsujudia,

Makonda jiandae kumsalimia kwa heshima mzee baba la sivyo utapoteza ukuu wa mkoa.

Ridhiwan baba karudi, ulimkejeli Sasa amerejea jamvini

Sent using Jamii Forums mobile app
Tutafika tuu kule tunapotaka kwenda kwa miondoko yote ya hapa duniani chadema songambele hata kwa jasho na maumivu makali
 
Back
Top Bottom