Msiba wa Ruge?
Hapana. Hakuna sababu ya msingi kwa Lowassa "ku-divert attention ya Watanzania kutoka kwenye msiba wa kitaifa wa Ruge."
Hata hisia kuwa "kuna mkono wa mtu kwenye kifo cha Ruge" hazijapata umaarufu kiasi cha kupelekea Lowassa akurupushwe leo ili "azime" suala hilo.
Kuwatenga waliomtosa Lowassa?
Uwepo wa Rostam Aziz katika tukio unaweza kuwa ishara ya uhusika wake katika uamuzi wa Lowassa kurejea CCM. Na uhusika wake unaweza kumaanisha kuwa "mapacha wawili kati ya watatu" wa MTANDAO wa JK (JK mwenyewe, Lowassa na Rostam) sasa wapo kwa Jiwe.
And where does that leave JK? Well, he was the major force behind kutoswa Lowassa. With him were Mkapa na Mwinyi. Sio siri kuwa wote watatu have fallen out of favour with Jiwe.
Nadhani katika hili labda tuache muda uongee.
October surprise?
Katika siasa za uchaguzi huko Marekani, "October surprise" ni tukio la makusudi linalolenga ku-influence matokeo ya uchaguzi.
Ninaazima political jargon hiyo kumaanisha kuwa huenda tukio hilo la leo linalenga ku-preempt tukio jingine kubwa ambalo "mtu flani" anatarajia linaweza "kupozwa" na ujio wa Lowassa huko CCM pindi tukio hilo likitokea.
Ugumu wa kuongelea tukio hili kama ule uliojitokeza katika kujadili uwezekano wa Lowassa kurejea CCM. Kila baadhi yetu tulipofungua mdomo sio tu kubashiri kuwa Lowassa angerudi CCM bali pia kumtuhumu kuwa huenda anakihujumu chama hicho, tuliishia kutukanwa
Kwahiyo to be on the safer side, si vema kuongelea kitu ambacho huenda kikatafsiriwa kuwa ill wish if not sedition. But something is indeed cooking.
Nafsi inakataa sio kuamini kuwa kweli Lowassa karudi CCM (lilikuwa suala la when na sio if) bali kuamini kuwa kurudi kwake CCM LEO ni kwa vile "leo ni siku kama nyingine."
Time will tell.
Sent using
Jamii Forums mobile app