Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lianziapo ndipo liishiapomcha mago hanywele hwenda akawia papo!!
The ikadhibitishwa na amri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama pale viwanja vya jangwani wakati akizindua kampeni 2015-Nilichofunzwa tu na siasa za bongo ni kuwa Sheria na magereza zipo kwa ajiri ya wanyonge wawe chadema ama ccm ukishakuwa mnyonge kweli kunyongwa ni haki yako-Tuendelee tu kupeleka sifa na utukufu kwa mwenyekiti maana anafanya kazi nzuri,mafisadi wamefungwa na utendaji serikalini umeboreshwaLakini CHADEMA ndiyo walianza kumuita Lowasa fisadi, baadae akahamia kwao na akapokelewa kwa heshima kubwa kama mkombozi, gia zikabadilishwa angani,
Kwani Mbowe kaoa kwa Lowassa?Lowasa kwa sasa sio chaguo la upinzani,hata yeye anausikia upepo wa Lissu na Zitto jinsi unavyovuma,kwa sasa hao vijana wawili ndio chaguo la upinzani kwa sasa.
Lowassa mali zake zinachukuliwa ,Mkwe wake kafungwa jela.
Mwanae anaishi kama mjane wakati Baba akirejea ccm mme wake ataachwa huru.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini unawashangaa akina Polepole kufanya kilekile walichofanya Chadema 2015? Hivi kati ya CCM na Chadema ni nani aliyemuita Lowassa fisadi kwa muda mrefu zaidi? Nitakusaidia jibu: Chadema walianza kumuita Lowassa fisadi mwaka 2006 na waliendelea kufanya hivyo hadi Julai 2015, yaani miaka tisa mfululizo.Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Magufuli na Polepole.
Hawa watu wawili walitushambulia sana eti mafisadi yamewakimbia na yamehamia Chadema. Sisi kweli kama Chadema tulibanwa sana kuhusu Lowassa ila tulijikongoja tuu. Kiuhalisia mwaka 2015 tulipoteza uhalisia wetu kichama ingawa Lowassa kweli alikuwa mtu wa watu. Tulilazimika kuwafanya wengine kukaa kimya maana kama chama tuliua agenda zetu kuu. Hatimaye sasa tutapumua.
Nimeshangazwa sana na mapokezi ya kifalme aliyopewa Lowassa huku serikali kuu zaidi ya nusu wakihamia Lumumba kwenda kumpokea mkubwa yule. Ni kwa mara ya kwanza kuona mtu akipokewa na viongozi wote wakuu wa chama na serikali. Mtu ambaye watu hao hao walidai kawakimbia! Leo wao ndiyo waliomkimbilia! Mbaya zaidi Magufuli anampokea Lowassa huku akiwa kasimamiwa na zee la mipango aka Rostam Aziz. Dah kweli dunia ina mambo.
Lowassa najua amerudi CCM ili kulinda fursa zake kibiashara pamoja na hatima yake ya uzeeni. Ni hayo tu.
Nasubiri kuona sasa mapovu ya kina Polepole na Bashiru baada ya madon kujihakikishia kuwa sasa wamemzunguka mkubwa wao. Acha kabisa siasa hizi za kibongo. Pia nasubiri neno la Slaa (Najua hatosema chochote maana anatumikia)
Tena wewe ndiye MNAFIKI NAMBA MOJA. Hebu fuatilia thread zako humu ulizokuwa unaziandika kuhusiana na Lowassa!Dr Slaa si mwanasiasa tena hivyo hayana impact kwake. Alafu kumbe mlikuwa mnajua hizi blunders lakini mlivyokuwa mnamtetea sasa! Tukiwaita wanafiki tunakosea mkuu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Magufuli na Polepole.
Hawa watu wawili walitushambulia sana eti mafisadi yamewakimbia na yamehamia Chadema. Sisi kweli kama Chadema tulibanwa sana kuhusu Lowassa ila tulijikongoja tuu. Kiuhalisia mwaka 2015 tulipoteza uhalisia wetu kichama ingawa Lowassa kweli alikuwa mtu wa watu. Tulilazimika kuwafanya wengine kukaa kimya maana kama chama tuliua agenda zetu kuu. Hatimaye sasa tutapumua.
Nimeshangazwa sana na mapokezi ya kifalme aliyopewa Lowassa huku serikali kuu zaidi ya nusu wakihamia Lumumba kwenda kumpokea mkubwa yule. Ni kwa mara ya kwanza kuona mtu akipokewa na viongozi wote wakuu wa chama na serikali. Mtu ambaye watu hao hao walidai kawakimbia! Leo wao ndiyo waliomkimbilia! Mbaya zaidi Magufuli anampokea Lowassa huku akiwa kasimamiwa na zee la mipango aka Rostam Aziz. Dah kweli dunia ina mambo.
Lowassa najua amerudi CCM ili kulinda fursa zake kibiashara pamoja na hatima yake ya uzeeni. Ni hayo tu.
Nasubiri kuona sasa mapovu ya kina Polepole na Bashiru baada ya madon kujihakikishia kuwa sasa wamemzunguka mkubwa wao. Acha kabisa siasa hizi za kibongo. Pia nasubiri neno la Slaa (Najua hatosema chochote maana anatumikia)
Hapana ili kumpisha Tundu Lissu alifuata Uraisi kaukosa, inebidi arudi huku ili kueka mali zake na afya yake salama, ila siasa ndo basi......Katika kitu nachokiona juu ya huu mpango wakumrudisha Lowassa kuna mambo mawili juu ya siasa za CCM.
Moja ya mkakati huu nikumdhohofisha Cumilius Membe na team yake!kwakutambua Membe ana wafuasi na amekigawa Chama. Pili wanatambua Lowassa anamasalia mengi CCM hivyo kumrudisha nimsaada kwa UMOJA ndani ya CCM pia kudhoofisha CHADEMA kwakuwa wamemfastrate Mbowe kwakujua kesi zinazomkabili. Chama kitadhoofika pia kitakimbiwa na wanachama.
Mytake nikwamba Lowassa si asset tena kwa chama pia kwa taifa ila nachokiona Membe bado ananguvu katika chama hasa CCM hivyo sioni kama wamepiga bao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaaa! Babu ukipulizaga majani ya mpapai huwa unakuwa smart sana kwa nahau na tambo.Bado naendelea kupokea misemo na vitendawili.Endelea kutafakari huku ukikijaza kibubu kwa ajili yako na familia yako. Ishi maisha yako, ukiwatafakari sana wanasiasa utapasuka kichwa bure. Siasa ni ngumu kuliko physics.
Mwanasiasa mzuri zaidi ni yule mnafiki mzuri zaidi asiye na aibu
Yapo mengine CHADEMA walikuwa hawayajui kuhusu LOWASSA. Hebu jikumbushe aliyoyasema Nape Nnauye kwenye kampeni kule Iringa!Lakini CHADEMA ndiyo walianza kumuita Lowasa fisadi, baadae akahamia kwao na akapokelewa kwa heshima kubwa kama mkombozi, gia zikabadilishwa angani,