Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Lowasa alitoka lini ccm? Alirudisha lini kadi ya ccm, na je mmeona amepewa kadi yoyote jana? Lowasa ni mwana ccm mzuri na hajawahi kuwa mpinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna CHADEMA mwenye akili atayepanic, Mimi naona CCM ndio wamepanic, sasa zamu yenu, moja anajinyea hajinyei? Mbili hafai ni fisadi papa au malaika?

Kazi kwenu, naona gia zinakataa kuingia muanzie wapi na mlima ndio huyo mshaufika?
 
Sawa,uko sahihi lakini inammana kweli hakuna impact ambayo ni negative kwa CDM??
Yapo tu tena sana. Kwa mfano wabunge wengine wa viti maalum alipewa nafasi na akapachika watu wake . Hiyo ni hasara kwa Cdm , lakini pia ngome za CCM ambazo zingine zilienda upinzani kwa kumfuata Lowassa huenda zote zikapitezwa na Cdm nk nk.

Kubwa hata CCM haipaswi kutamba, ni kwa sababu inategemea vyombo vya Dola, kufanikisha uwepo wake kwa asilimia kubwa badala ya siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnamu overrate sana Membe. Huyu kimkakati hanusi hata nukta kwa Lowasa. Jipangeni tu upya Chadema ili walau 2025 mrejeshe nguvu yenu ya kuelekea ikulu lakini ya CCM kwasasa hayatowasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini CHADEMA ndiyo walianza kumuita Lowasa fisadi, baadae akahamia kwao na akapokelewa kwa heshima kubwa kama mkombozi, gia zikabadilishwa angani,
Wew pambana na fisadi lenu limewarudia mtatuambia nin sasa hivi mafisadi yameota miziz lumumba.
 
Baada ya mzee Lowasa kurudi nyumbani sasa wapenda mabadiriko tunataka radical politics, kale kazee kalikosema muache siasa za uanaharakati aliwapoteza, Jiwe linahitaji radical politics za jino kwa jino, Mbowe amuondowe sasa Katibu mkuu, na ajihudhuru uenyekiti apewe Lisu na Mbowe arudi kwenye ukatibu mkuu, Mashinji ni mzigo aondolewe haraka, ni Lisu pekee mwenye sifa za kuliongoza jahazi la chadema kwa sasa kuelekea uchaguzi mkuu. Mwisho samahani kwa uandishi mbovu device yangu ina matatizo nimeshindwa kuweka paragraph

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii picha haingii akilini hata chembe. Nianze kwa kuuliza .''HUU KAMA SIYO UNAFIKI WA WATANZANIA ULIOPITILIZA NI KITU GANI...???
Kwamba Watanzania wote wako kwenye musiba mzito wa kifo cha Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa CMG marehemu Ruge Mutahaba anajitokeza Edward Ngoyai Lowassa kutangaza kuhama CHADEMA na kurudi CCM inakuwa ni tukio muhimu zaidi kuliko musiba....!!!Rais wa JMT Mhe. John Joseph Magufuli ame-tweet kwenye mtandao wa tweeter kuelezea masikitiko ya kifo cha Ruge lakini hajafika nyumbani kwao na Marehemu Ruge kuwapa pole wafiwa.

Lakini baada ya Lowasa kutangaza kurudi CCM pale Lumumba Rais Magufuli yuko mbele kushangilia na kusherekea kurudi kwa Lowassa. Makada wa CCM wanashangilia na kufurahi katikati ya musiba mzito wa kijana Mtanzania ambaye amegusa nyoyo za Watanzania wengi.
Je, hili limepangwa au ni bakti mbaya? Kama CCM walikuwa wamepanga Lowassa arejee CCM tarehe ya 1 March, 2019 wameshindwa nini kuahirisha sherehe hiyo ambayo haina tija yoyote kwa Watanzania? Je, haya ni maksudi ya kuumiza nyonyo za Watanzania hasa Wana-media na wale wa vyama vingine vya siasa hususan CHADEMA? Maswali ni mengi kuliko majibu....!!

Nihitimishe kwa kusema hivi, kama Taifa, Tanzania tumeshapoteza mwelekeo wa mambo ya msingi ambayo tuliachiwa na mwasisi wetu Baba wa Taifa JK Nyerere(rip). Ni ubazazi wa hali ya juu kuimngiza siasa katikati ya musina mzito kama huu. Matukio haya mawili: KIFO CHA RUGE MUTAHABA na KUREJEA KWA LOWASSA CCM kwa hakika kimeonesha UNAFIKI WA HALI YA JUU usiozingatia UTU, HESHIMA na USTAARABU katika jamii ya walio HAI na WAFU. CCM wamekuwa ni mafundi sana wa kutengeneza PICHA ZA KINAFIKI ambazo kuna siku zitaleta matokeo HASI ambayo Wanasiasa hasa wa CCM hawajawahi kuzitarajia.

Hivi Rais Magufuli haoni aibu? Rais Magufuli amedhihirisha unafiki wake kwa Lowasa. Hivi yale maneno na kauli aliyoitamka siku ile kuwa WALE WAJUMBE WOTE WA MKUTANO MKUU WA CCM WALIOKUWA WAKIIMBA WANA IMANI NA LOWASSA ANGELIWAPOTEZA ZAIDI YA NUSU YAO... ameyafuta lini? Wahenga walisema ukitaka kuwa mwongo na mnafiki mzuri usiwe msahaulifu...!Je, waliokuwa wanashangilia, kuimba na kusherekea kurudi kwa Lowassa CCM jana pale Lumumba basi Magufuli atuambie atawapoteza wangapi?

Tafakuri.
 
kura za uraisi nipatie mimi na wabunge wengi wa ccm..huyu mamvi huwa simwelewi kabisa.
alimzuia mke wake asiteuliwe viti maalum,akamzuia mtoto wake asigombee kwenye marudio ya uchaguzi kumbe alikuwa na la kwake jambo.
pale ndipo lilikua jibu kwamba yuko upande gani
 
Kwa kweli Lowassa amejijengea heshima kubwa dunia kote kukataa kuwa kibaraka WA mabeberu na kuangalia maslahi mapana ya nchi yake .Mbona Laira na Kenyatta walimaliza tofaut zao Mara baada ya uchaguzi kuisha ,kwanini isiwe Magufuli na Lowassa?
 
Na rostam Mzee wa Mipango ya fedha chafu alikuwepo kuhakikisha mwakani magufuli anapita kwa wizi wa kura za kutosha maana kwa sanduku la kura kawaida hapiti
 
Tulishtuka wakati kila aliyekuwa akikamatwa alitakiwa kupimwa mkojo na hili lilitulia TAL alipowakatalia.Tukashtuka kila aliyekamatwa hata kwa kosa la kutukana kwa mdomo kinachokimbiliwa ni simu.
Mtu anapokuwa na taarifa zako (hasa mbaya) huna ujanja ni suala la muda tu lakini utaucheza muziki anaotaka.
Naam,KIKOMBOZI!
 
Back
Top Bottom