Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

complected, duh.
kuna statement moja alisema Sumaye siku wastaafu walivyoitwa ikulu' kuwa kwangu upinzani ni kwa manufaa ya CCM' hii kauli utata mtupu sijui alijisahau. ila siwaonei huruma wapinzani ni wajinga toka lini mpenzi wa Yanga akahamia Simba halafu na cheo juu. wote ni tamaa tu madaraka hujui wanasimamia nini.CCM watawale tu ila siasa cha uchumi wabadilishe
 
Kinachofurahisha CCM na CHADEMA walimchafua LOWASA kwa kumuita fisadi na wote kwa pamoja wakamsafisha. Safi kabisa hiyo ndiyo akili kubwa.
Usijifarij tuambie lowassa ni asset au liability kwa sasa huko ccm?
 
Hahahaaa nakumbuka wakati yuko chadema alisimama akasalimu kidumu chama cha mapinduzi! Wakamkumbusha sema pipoooozz.
Yeye hakuwahi kuvaa safe za cdm sawa.Nawaomba humu mwenye picha ye-yote ya mwanzilishi wa TANU Na sasa CCM ALIPOVAA SARE ZA HIKI CHAMA Pendwa CCM ATUPIE HUMU.Sio kuhoji safe za Cdm na ma mvi sare za CCM NA Mwl alizovaa TUPIENI PICHA HUMU TUONE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuanzia Ruge,Lowassa na huyo Magufuli a.k.a jiwe ni wanafiki tu.Nchi hii itapata ukombozi kupitia sisi wananchi wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app

Kweli ndugu yangu Mtanzania.
Hapa najaribu kuwaza kwa sauti: Hivi huyu Bashite aliyevamia OFISI ZA CLOUDS na baadaye KUNGIWA KIFUA na JIWE amefika msibani? Hizi akili za kina Bashite na Jiwe kweli zinahitaji UKOMBOZI MKAMILIFU....!!!
 
Hii picha haingii akilini hata chembe. Nianze kwa kuuliza .''HUU KAMA SIYO UNAFIKI WA WATANZANIA ULIOPITILIZA NI KITU GANI...???
Kwamba Watanzania wote wako kwenye musiba mzito wa kifo cha Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa CMG marehemu Ruge Mutahaba anajitokeza Edward Ngoyai Lowassa kutangaza kuhama CHADEMA na kurudi CCM inakuwa ni tukio muhimu zaidi kuliko musiba....!!!Rais wa JMT Mhe. John Joseph Magufuli ame-tweet kwenye mtandao wa tweeter kuelezea masikitiko ya kifo cha Ruge lakini hajafika nyumbani kwao na Marehemu Ruge kuwapa pole wafiwa.

Lakini baada ya Lowasa kutangaza kurudi CCM pale Lumumba Rais Magufuli yuko mbele kushangilia na kusherekea kurudi kwa Lowassa. Makada wa CCM wanashangilia na kufurahi katikati ya musiba mzito wa kijana Mtanzania ambaye amegusa nyoyo za Watanzania wengi.
Je, hili limepangwa au ni bakti mbaya? Kama CCM walikuwa wamepanga Lowassa arejee CCM tarehe ya 1 March, 2019 wameshindwa nini kuahirisha sherehe hiyo ambayo haina tija yoyote kwa Watanzania? Je, haya ni maksudi ya kuumiza nyonyo za Watanzania hasa Wana-media na wale wa vyama vingine vya siasa hususan CHADEMA? Maswali ni mengi kuliko majibu....!!

Nihitimishe kwa kusema hivi, kama Taifa, Tanzania tumeshapoteza mwelekeo wa mambo ya msingi ambayo tuliachiwa na mwasisi wetu Baba wa Taifa JK Nyerere(rip). Ni ubazazi wa hali ya juu kuimngiza siasa katikati ya musina mzito kama huu. Matukio haya mawili: KIFO CHA RUGE MUTAHABA na KUREJEA KWA LOWASSA CCM kwa hakika kimeonesha UNAFIKI WA HALI YA JUU usiozingatia UTU, HESHIMA na USTAARABU katika jamii ya walio HAI na WAFU. CCM wamekuwa ni mafundi sana wa kutengeneza PICHA ZA KINAFIKI ambazo kuna siku zitaleta matokeo HASI ambayo Wanasiasa hasa wa CCM hawajawahi kuzitarajia.

Hivi Rais Magufuli haoni aibu? Rais Magufuli amedhihirisha unafiki wake kwa Lowasa. Hivi yale maneno na kauli aliyoitamka siku ile kuwa WALE WAJUMBE WOTE WA MKUTANO MKUU WA CCM WALIOKUWA WAKIIMBA WANA IMANI NA LOWASSA ANGELIWAPOTEZA ZAIDI YA NUSU YAO... ameyafuta lini? Wahenga walisema ukitaka kuwa mwongo na mnafiki mzuri usiwe msahaulifu...!Je, waliokuwa wanashangilia, kuimba na kusherekea kurudi kwa Lowassa CCM jana pale Lumumba basi Magufuli atuambie atawapoteza wangapi?

Tafakuri.
Who is ruge? Tunashukuru Jiwe kupokea huyo mzee jumla jumla. Ni vema akastaafu tu siasa apumzike umri umesha mtupa mkono
 
Mara zote huwa tunasema upinzani hawana hoja Lowasa ametusaidia tena kuona namna upinzani ulivyo mufilisi kisiasa..siasa zao ni za kilaghai..
 
Raisi utamuona leo,afu kuna wawakilishi pia wa Mh Rais nao nadhani umewaona. kwahiyo kuwa na subira mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Acha longolongo wewe.
Unataka kuniambia pale Lumumba kwenye kumpokea Lowasa hakukuwa na Wawakilishi wa Rais au Mwenyekiti wa CCM(T)?
I'll never buy that cheap and non-sense!
 
Marehemu aligoma kiirusha ile Shilawadu ya kumuumbia Ngwajima wakati mzee akiwa live anaisubiria ...hadi ikapelekea maumivu kwa Nape na wengine wengi....RIP Ruge...kuna wakati mamlaka nazo hucheza faulo za waziwazi.
 
Kama ulifikiria imekujengea historia yoyote ya maana, basi aliyekushauri amekudanganya/amekupoteza. Hata huyo aliyekupokea naye anaingia katika historia za wanasiasa wa hovyo katika historia ya siasa za Tanzania. Kama kuna historia concrete itaandikwa na wana vyuoni, basi jina lako litaandikwa kwnye karatasi za mawe!
Ungeli retire siasa labda ingelikujengea heshima zaidi. Kashifa za ufisadi unaotuhumiwa nao hakuna mwenye ushahidi usiokuwa na mashaka! Hivyo bado heshima yako ingelisimama
Amezidiwa, kila alichokijenga kwa jasho na damu kilikuwa njiani kupotea, ameamua kimwili, kiakili na kiroho hana amani na maamuzi haya, lakini heri maisha yake na kizazi chake kuliko kuishupaza shingo katika vita ambayo hatashinda

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Kwanini unawashangaa akina Polepole kufanya kilekile walichofanya Chadema 2015? Hivi kati ya CCM na Chadema ni nani aliyemuita Lowassa fisadi kwa muda mrefu zaidi? Nitakusaidia jibu: Chadema walianza kumuita Lowassa fisadi mwaka 2006 na waliendelea kufanya hivyo hadi Julai 2015, yaani miaka tisa mfululizo.

And guess what? Wakati CCM haitojihangaisha kumsafisha Lowassa, Chadema ilizunguka nchi nzima kulamba matapishi yake - na kibaya zaidi - kutelekeza flagship policy yake ya vita dhidi ya mafisadi.

Kosa kubwa linaloweza kufanywa na Chadema ni kuendelea kujihadaa kuwa hizi hamahama haziwaathiri.

Swali moja ambalo hakuna mwana-Chadema anaweza kujibu kwa hakika ni hili: WHO IS NEXT?

Sent using Jamii Forums mobile app
NEXT IS MBOWE, LISSU, LEMA NA MSIGWA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom