Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Kwani kuishi tanzania ndio lazima kumjua kila mtu, mbona mimi nimemuona mara moja wakati wa tukio la kuvamiwa clouds na juzi ndio naona taarifa zake kwenye mitandao kuhusu msiba, lakini kabla ya hapo hakuwa kwenye tantion yangu.

Acheni kulazimisha watu kupenda mnachopenda nyinyi.
Wewe unaishi Tanzania na Dunia ya wapi....???
Rugemalira Mutahaba(Boss Ruge)-Mkurugenzi na mzalishaji wa Vipindi vya CLOUDS MEDIA GROUP(CMG).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawataki kabisa Mfalme aguswe


Anaeiua chadema ni mbowe.....!!!!

Ngoja aendelee kusota huko! Akamwekaa katibu mkuu wa ma vyeti, hana ushawishi wowote kwa wananchi....!!! Inabidi wajipange upya! Katibu mkuu kiatu kimewapwaya!
 
Hawataki kabisa Mfalme aguswe


Anaeiua chadema ni mbowe.....!!!!

Ngoja aendelee kusota huko! Akamwekaa katibu mkuu wa ma vyeti, hana ushawishi wowote kwa wananchi....!!! Inabidi wajipange upya! Katibu mkuu kiatu kimewapwaya!
 
Barrick na Acacia are not stupid kumpa asiye na uwezo. Sio tender za serikali au CCM. Advantage aliyokuwa nayo ni kwamba yeye ni major supplier wa heavy machinery za mining.
Tumia akili kijana, kuwa supplier wewe kwa mtazamo wako unaona inahitaji uwe genius..ndiyo maana kwenye kashfa ya richmond kamati ilipokwenda kuongea na waliotengeneza hizo genereta wenye akili waliwauliza mbona nchi nyingine za africa serikali huwa inakuja yenyewe kama inahitaji hizi genereta?? kwenu Tanzania mnahitaji dalali kwa nini??? fikiri vzr kama unadhani Barrick hawawezi nunua hizo equipment toka kwa manufacturer..
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Magufuli na Polepole.

Hawa watu wawili walitushambulia sana eti mafisadi yamewakimbia na yamehamia Chadema. Sisi kweli kama Chadema tulibanwa sana kuhusu Lowassa ila tulijikongoja tuu. Kiuhalisia mwaka 2015 tulipoteza uhalisia wetu kichama ingawa Lowassa kweli alikuwa mtu wa watu. Tulilazimika kuwafanya wengine kukaa kimya maana kama chama tuliua agenda zetu kuu. Hatimaye sasa tutapumua.

Nimeshangazwa sana na mapokezi ya kifalme aliyopewa Lowassa huku serikali kuu zaidi ya nusu wakihamia Lumumba kwenda kumpokea mkubwa yule. Ni kwa mara ya kwanza kuona mtu akipokewa na viongozi wote wakuu wa chama na serikali. Mtu ambaye watu hao hao walidai kawakimbia! Leo wao ndiyo waliomkimbilia! Mbaya zaidi Magufuli anampokea Lowassa huku akiwa kasimamiwa na zee la mipango aka Rostam Aziz. Dah kweli dunia ina mambo.

Lowassa najua amerudi CCM ili kulinda fursa zake kibiashara pamoja na hatima yake ya uzeeni. Ni hayo tu.

Nasubiri kuona sasa mapovu ya kina Polepole na Bashiru baada ya madon kujihakikishia kuwa sasa wamemzunguka mkubwa wao. Acha kabisa siasa hizi za kibongo. Pia nasubiri neno la Slaa (Najua hatosema chochote maana anatumikia)
Mkuu El alisafishwa na chadema kwamba ni mtu safo,kea hiyo sehemu ye yote atakayo kwenda anakwenda na utakatifu kutoka chadema.
Kea vile wamezoea kula matapishi,anzeni Tena kumtukana.
 
Wakati alipojiunga na CDM aliambatana na mke wake kipenzi ,mama Regina Lowassa,na wote wakatamvulishwa hadharani na kupewa kadi.

Swali,kulikoni Jana hatukumona mama Regina Lowassa naye akikaribishwa chamani?

Au safari hii amemsaliti mumewe Mzee Lowassa?
 
Tumia akili kijana, kuwa supplier wewe kwa mtazamo wako unaona inahitaji uwe genius..ndiyo maana kwenye kashfa ya richmond kamati ilipokwenda kuongea na waliotengeneza hizo genereta wenye akili waliwauliza mbona nchi nyingine za africa serikali huwa inakuja yenyewe kama inahitaji hizi genereta?? kwenu Tanzania mnahitaji dalali kwa nini??? fikiri vzr kama unadhani Barrick hawawezi nunua hizo equipment toka kwa manufacturer..
You have no idea mining industry in operate vipi dogo. Waingie tena kununua vifaa? Tender za heavy machinery ni competitive sana. Barrick wanajua kama wanapigwa au la.
Sio tender za serikali hizo. You have to deliver. Siri ni kuwa na capital kubwa. Unaagiza mapema. Wakihitaji, una supply immediately.
 
Karibu mzee, nyumbani ni nyumbani kwa jirani sio kwako....umeshamaliza kazi
 
D
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k

Habari zaidi...

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.

Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.

Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.

Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.

Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.

Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.

Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums

Don't be caught by surprise. Nikiangalia vizuri binafsi sio mtu potential kugombea raisi 2020 licha ya Lowasa au Majaliwa. Ila pia tujue lowasa mpaka kurejea ccm kuna sababu nyingi ila mojawapo nahisi ni ni la uraisi au kupata kitu kikubwa. Ni mtazamo wangu roughly
 
Zawadi B Lupelo

Wanajamvi salamu kwanza!

Samahani najua kuwa kuna msiba. Nimevutiwa na mjadala unaoendelea kupamba moto nchini kufuatia kurudi CCM kwa aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA na CHADEMA kwa upekee mwaka 2015. Kumeibuka kundi la watu ambao wao wameichukulia hatua hii ya Lowassa kurudi CCM kama uthibitisho kuwa CHADEMA ilikosea kumpokea Lowassa.

Watu hawa wanadai kwamba CHADEMA hsikupaswa kumpokea Lowassa mwaka 2015 sembuse kumfanya kuwa mgombea wake wa Urais. Wamekuwa na hoja nyingi sana kuhalalisha maoni yao hayo. Sitazirudia hoja hizo ninaomba niwasilishe mtazamo wangu binafsi kabla sijawakaribisha wanajamvi kwa mjadala.

Kwa maoni yangu siyo sawa kutumia kitendo cha Lowassa kuondoka au kitendo chochote cha Lowassa baada ya uchaguzi wa 2015 kufault uamuzi mzuri wa chama kumpokea Lowassa.

"Kupokelewa" "Kupewa uongozi" na "kuondoka are 3 independent things.

Chama kilifanya assignment zake na kuchanga karata zake baada ya vikao na mashauriano kikafikia uamuzi kuwa kumpokea itakuwa jambo lenye manufaa kwa chama. Akapokelewa na akateuliwa kupeperusha bendera ya chama. Ni ukweli uliowazi kuwa chama kilipata mafanikio kuliko chaguzi zilizopita licha ya kasoro ndogondogo zilizojitokeza.
Chama kiliangalia mazingira ya wakati huo na kikaeleza wazi sababu zake.

Leo hii kitendo cha kuondoka kinakuwaje kigezo cha kudai kuwa uongozi wa CHADEMA ulifanya makosa kumpokea? Ulifanya makosa gani na kivipi? Na je kama asingeondoka wangekuwa wapo sawa?

Vipi leo Mchungaji Peter Msigwa akihama chama itakuwa CHADEMA ilifanya makosa kumpokea na kumruhusu agombee ubunge? Vipi Lissu leo akigombea Urais je itamzuia kuhama siku za mbele? Na je akihama tutakuwa tumekosea kumpa ugombea?

Kuna watu walimezwa na upepo wa Magufuli wakaacha upinzani mwaka 2015 wakampigia kampeni JPM lakini siku hizi wanaona hata aibu kujitambulisha kuwa walikuwa upande wa JPM. Kuhalalisha walichokifanya mwaka 2015 watakwambia hatukusapoti UKAWA kwa sababu ya Lowassa. Leo hii ameondoka yupo CCM wanatumia kuondoka kwake kuhalalisha kuwa chama kilikosea no chama kilikuwa sahihi, mlikosea nyie kusapoti CCM na JPM mwaka 2015.

Mtu akiamua kuhama anahama tu chama hakiwezi kumblock that is democracy. Amehama Katambi ameacha uenyekiti wa BAVICHA je tutumie kuhama kwake kusema kuwa chama kilikosea kumchagua kuwa kiongozi BAVICHA? Hii si sawa na siyo haki kuwalaumu viongozi wa chama kwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mzee huwa namwangaliaga hana charisma as far as i can tell na nikiangalia public persona yake haswa body language anaonekana he is an introvert. Akizungumza hana poise and swagger anazungumza kama introvert. I keep asking myself what makes him think he can win people’s hearts and minds while in reality his personality simply doesn’t correspond with the magnittude of his political ambitions?
 
Aliyesema shukrani ya punda ni mateke hakukosea,Lowassa kawalipa CHADEMA shukrani ya punda.
 
Kurejea kwa Lowassa ndani ya CCM na kupokelewa na uongozi wote wa juu wa nchi na chama tawala, ni ishara ya ushindi mkubwa sana kwake juu ya tuhuma za ufisadi alizokuwa akishambuliwa nazo sana na vyama vya upinzani hasa CHADEMA ambapo mashambulizi ya tuhuma hizo kutoka upinzani yalizima baada ya kujiunga na CHADEMA ili kugombea urais baada ya kutemwa CCM. Ghafla CHADEMA wakabadili kauli kuwa Lowassa hakuwa fisadi.

CCM kuona hivyo wakaibeba ajenda ya CHADEMA kuwa wao wamemtemba kwasababu ya ufisadi na sasa amepokelewa na CHADEMA hivyo ni wapinzani ndio wanao unga mkono ufisadi. Mgombea wa CCM akaenda mbali na kusema kuwa fisadi mkuu amemkimbia na kujiunga na upinzani na akahahidi kuwa akiyakwaa madaraka ataunda mahakama maalumu ya mafisadi lengo likiwa ni kumshughulikia Lowassa. Baada ya kushinda ni kweli aliunda mahakama hivyo lakini hakuna fisadi yeyote aliyepelekwa huko wala Lowassa hakuguswa matokeo yake tuka shuhudia akialikwa ikulu. Kabla ya hapo viongozi mbali mbali wa CCM na vijana wao walipiga kelele kubwa kuwa Lowassa ni fisadi hivyo CHADEMA impoteza mwelekeo kwa kumpokea Lowassa.

Kurudi kwa Lowassa sasa ni wazi mashambulizi ya akina Pole pole, Makonda na rais mwenyewe kuwa Lowassa ni fisadi yamefikia tamati. Lowassa sasa ni safi. Amesafishwa na upinzani ulimtuhumu kwanza na sasa amesafishwa na chama tawala chenyewe kilicho mtema na kumshutumu pia kwa ufisadi. Aidha Lowassa amerejea CCM na rafiki yake mkubwa Rostam ambaye kwa pamoja ndio waliomuweka madarakani JK. Ni wazi huu ni mkakati wa kumasaidia JPM kwa 2020. Lakini kubwa kuliko yote ni kuwa Lowassa ameshinda vita ya ufisadi. Si Mbowe, Lissu, Msigwa, Silaa, Lema, Polepole, Makonda au Rais watako inua midomo yao tena kusema Lowassa ni fisadi. Hongera sana Lowassa!
 
Back
Top Bottom