TEMBO WA SIASA ZA TANZANIA AREJEA CCM.
Leo 13:15pm,03/03/2019.
Mwamba wa siasa za Tanzania,Mwamba wa Siasa katika dunia ya miongo mingi, Laigwanan aliyefikia hadhi ya juu katika Uongozi na kupendwa na Watanzania kulikoleta Mafuriko Mwaka 2015,Mahaba hayo yalichagizwa na kilele cha hali ya juu cha hekima na busara aliyo nayo katika kufikiri na katika Ustaarabu wa Ukomo wa Mwanadamu, Tembo wa Siasa za Tanzania,Edward Lowassa amerejea CCM baada ya kukaa Chadema kwa siku 1,293.
Dhoruba imetulia,Nuru imetamalaki,2020 CCM
Tutaishika tena njia ya Mabadiliko na Hapa Kazi Tu kama kitu kimoja,kuinyanyua tena Elimu kwa kasi isiyo kifani kupata wataalam wa Kitanzania watakao ibeba Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati.Mchapakazi Edward Lowassa aungana na Mchapakazi Rais John Magufuli kuipeleka Tanzania mbele katika uchumi wa kati,Edward Lowassa na John Magufuli wanaotambulika kwa Uchapakazi na Maamuzi magumu wataionyesha dunia kwamba Tanzania ni nchi ya kuheshimika na kamwe si shamba la bibi.
Mafanikio ya sasa ya Rais Magufuli ya kuuinua uchumi,yatanogeshwa na Edward Lowassa kwa fursa kadhaa kwa vijana na kufungua milango ya ajira na kazi.Miaka mitano ya Uongozi wa Rais Magufuli umefanya kazi ya Urais ambayo ilitakiwa kufanywa kwa miaka kumi, Kwa miaka mitano mingine ya Rais John Magufuli atafanya kazi ya urais iliyotakiwa kufanya kwa miaka mingine kumi, hivyo basi miaka 10 ya Rais John Magufuli itakuwa imefanya kazi ya Urais iliyotakiwa kufanywa kwa miaka 20.Kwa lugha ya mabeberu tungesema "A President with a difference " Rais mwenye kuacha alama.
Umuhimu wa Edward Lowassa na mambo yake makuu tunaweza kuyaorodhesha toka Lushoto hadi Sikonge na yasiishe, na Mazuri ya Rais John Magufuli tunaweza kuyaorodhesha toka Tanzania bara hadi visiwani na yasiishe,Niseme tu sasa Chadema, CUF na ACT hawafui dafu,ni wasaka tonge kwa mfano wa Mbowe, Lissu,Zitto,Mwalimu Sefu na Lipumba.Sasa wapinzani watadoda kama chuchunge
Lowassa amewapiga mchana kweupe na siku ya tatu leo wanalala na viatu.
Hakika kupatana na kuungana kwa wagombea Wakuu wawili katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ni Jambo jema na bora kwa Taifa letu la Tanzania,kwa kuwa ni udhihilisho ya kuwa hoja zote za Upinzani zimefanyiwa kazi na Mh Rais John Magufuli hata mpinzani wake Mkuu kumuunga mkono.
Ni historia kuu bara hata visiwani,Siasa zetu zimetia fora kwa kukubaliana katika mambo ya msingi kwa maslahi mapana ya Taifa letu.Taifa linawahitaji watu wengi kama Edward Lowassa na John Magufuli.
-Lowassa aiongezea CCM uungwaji mkono.
Nguzo kubwa ya Chama cha Siasa chochote Duniani ni kuongeza uungwaji mkono kwa maana ya Wanachama wanaomuunga mkono Edward Lowassa kuiunga mkono CCM na kuiacha solemba Chadema.
Edward Lowassa anaungana na wanaCCM wengine kuwa mwanachama sawa na wewe au Mimi na mwingine yeyote awae!
Ujio wa watu maarufu ndani ya chama chochote ni ishara ya kuongeza Uungwaji mkono ndani ya chama na kupelekea chama kuendelea kuaminika kwa Watanzania.
Edward Lowassa karejea CCM baada ya kujihakikishia kuwa ndani ya CCM kuna utulivu na kila mtu anapata haki yake kama ile ya binadamu wote ni sawa, Viongozi wanatenda kazi sawa sawa na hakuna Upinzani nje ya CCM ispokuwa kuna Wanaharakati kuliko vyama vinavyo fikiria kuchukua uongozi wa Taifa {dola} anawaona wanaharakati badala ya wanasiasa kwa namna hiyo kila Mwanasiasa aliyepevuka na kuvuka uanaharakati ni lazima ajiunge na jeshi la wanasiasa halisi na ndivyo alivyofanya Edward Lowassa.
Lowassa amekuja wakati muafaka,Mh Rais Magufuli akitenda sawasawa kwa kila mtanzania, Maelfu ya Wamasai wakipatiwa Maeneo ya kulishia mifugo yao,wakulima wakiendelea kufaidika na Nchi yao kwa kuuza mazao yao hata kufikia wakati Serikali kuamua kununua ili mradi mkulima afaidike na jasho lake na kuepusha matapeli ambao daima walikuwa wakimlalia mkulima.
Edward Lowassa amerejea CCM wakati ambao chama kinaisimamia Serikali na kuhakikisha mnyonge hanyanyasiki,Wakati ambao Mtanzania akijisikia kuwa raia katika Taifa lake,Wakati ambao Rasilimali za Nchi kwa mara ya kwanza zimekuwa mali ya Mtanzania kwa sheria na wala sio kwa msaada,Vivaa Rais John Magufuli.
Mh Edward Lowassa anakuja ndani ya Chama wakati ambapo Taifa linahitaji Umoja zaidi na kupambana na Mabeberu,Mabepari,Mabwenyenye,Makaburu na vibaraka wao popote walipo, Edward Lowassa wakati Taifa linapopiga hatua kuelekea katika Uchumi wa Kati ifikapo 2025.
Karibu sana Mh Edward Lowassa,Karibu sana Tembo wa Siasa za Tanzania, kama kuna wengine wamebaki huko,Karibuni sana Team Lowassa iliyokwenda Chadema, Karibuni sana vijana wa 4u Movement ambao daima mlimuunga mkono Edward Lowassa,Karibuni sana wanamabadiliko ambao mliamini mabadiliko yatatokea Chadema lakini kwa mshangao wenu Mabadiliko yanatokea ndani ya CCM chini ya Rais John Magufuli. tunawakaribisha sana CCM,Daima Chama Cha Mapinduzi kinajengwa na Watanzania wote kwa umoja wetu.
Edward Lowassa maisha yako yote toka ukiwa kijana umekulia CCM kasoro siku 1,293 ambazo ulikuwa mwana mpotevu,Kwa Baba na Mama daima nafasi ya Mwana ipo siku zote, CCM ni kwako karibu ikibidi hata ufike jikoni, we ni sawa na wengine tuliokuwepo hapa uliotuacha na sasa umetukuta, Kwetu hakuna Ubaguzi kama kule Chadema.
-Nani aliyeumia kwa Ujio wa Lowassa ndani ya CCM.
Ni dhahiri shahiri Membe,Makamba,Nape na wanaCCM wale ambao walikua na wapo wanaendesha mikakati ya kumshinda Rais Magufuli 2020.( Tukumbuke, hamna wanasiasa Tanzania ambao ni makachero wa siasa kama Edward Lowassa na Rostam Aziz hata kupata kuitwa King's Maker, rejea uchaguzi wa 2005.) Awa ni Watu ambao kimkakati hawakubaliani na Membe.
-Nani mwingine aliyeumia!?
Chadema ni kitaasisi kingine kilichoumia,Edward Lowassa pekee ni taasisi kubwa kuliko Chadema,Edward huyo huyo ni moja ya vitaasisi vidogo vidogo ndani ya CCM. Kwa hiyo ile taasisi kubwa kushinda Chadema,Taasisi ya Edward Lowassa imeondoka na kura zake Milioni 6 ilizowaletea Chadema 2015,Taasisi hiyo imeondoka na siri ya kambi ya Chadema, hivyo basi Chadema wajiandae kuchunguliwa kama nyani juu ya mti.
Nimalizie kwa kusema Chadema imetiwa chumvini,Chadema imepukutika kwa kutu,Chadema imepotelea pwani,Chadema imebaki kibubutu,Sasa Mpini umegeuka mtukutu,
Mpini umekuwa kifimbocheza,Chadema mtatandikwa mgongoni hadi mjute kuwa wasaliti wa Nchi, Mwambieni Tundu Lissu njia yake ya kuingia ligi kuu imekutana na visiki, Poleni kwa kulala na viatu ikiwa ni siku ya tatu leo tangu Edward Lowassa arejee CCM, Karibu sana Nyumbani, Ndugu Edward Lowassa.Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais John Magufuli.
Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.