Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Aliitwa fisadi na wapinzani kabla ya 2015. Upinzani wakamsafisha. Akaitwa fisadi na CCM baada ya 2015. Kabla ya 2020 nao wamemsafisha. Lowassa katakata pande zote. Ni msafi na hatutarajii makatibu waenezi wa vyama husika watulishe mengineyo. Hongera Lowassa umecheza kiueledi mno!
 
Aliitwa fisadi na wapinzani kabla ya 2015. Upinzani wakamsafisha. Akaitwa fisadi na CCM baada ya 2015. Kabla ya 2020 nao wamemsafisha. Lowassa katakata pande zote. Ni msafi na hatutarajii makatibu waenezi wa vyama husika watulishe mengineyo. Hongera Lowassa umecheza kiueledi mno!

Kweli


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi huwa nashangaa na kupata shida kuwelewa kwa nini Edward Lowassa na suala la ufisadi wa wake huwa linachukua nafasi kubwa sana ya mjadala wa kisiasa kana kwamba yeye ndio fisadi pekee kama kweli ni fisadi au ndiye muasisi wa ufisadi na umaskini katika nchi hii.Kumfanya Lowassa ni muongozo wa kuchagua upande wa kisiasa si kunaonyesha ni jinsi gani siasa zetu zilivyo fukara wa misingi na itikadi ? Si inadhihirisha ni jinsi gani hatujaelewa sawasawa mizizi ya umaskini na shida zetu? Ndio kusema tumebaki tukipunguza matawi tu na kila msimu wa masika huo mti wa uharibifu unachipua tena? Au tukubali tu kwamba Lowassa ni Tembo katika siasa za nchi hii na uwepo wake katika chumba lazima utuliwe maanani na yeyote.
Karibuni mtueleze.

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Aliitwa fisadi na wapinzani kabla ya 2015. Upinzani wakamsafisha. Akaitwa fisadi na CCM baada ya 2015. Kabla ya 2020 nao wamemsafisha. Lowassa katakata pande zote. Ni msafi na hatutarajii makatibu waenezi wa vyama husika watulishe mengineyo. Hongera Lowassa umecheza kiueledi mno!

Ajenda ya ufisadi ilishakufa katakata kote kote apeperushe bendera 2020.
 
Hahahahaha he is genius hana haja ya kujisafisha kacheza na akili ya kila mwanasiasa anafaa kuwa rais sasa maana ni rais wa mioyo ya watu na bado atabaki kuwa ivyo na kuna watu waliimba kbla tunaimani na lowasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila Lisu hawezi itikisa CCM ni mwepesi kama karatasi..hakuna aliyewahi kuwa naye Karibu kwenye mfumo. .Lowasa alitikisa na bado hakufurukuta..
Nakubaliana na ww ila apa naangalia ushawishi na kukubalika kw wananchi. Lissu ana ushawish mkubw na anakubalika pia. Kilichombeba lowassa 2015 na kuitiksa ccm ni mvuto tu wa kisiasa hakuw na ushawish wala hakukubalika kulinganisha na magu. Kw sasa lissu anavyo vyote kuanzia mvuto wake ktk siasa, anaushawish na anakubalika pia. Ila nakubaliana na ww kuhusu mfumo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza sikia mabadiliko kwa ngazi ya urais aliyekua makamu wa rais mama samia hassan amepangiwa kazi nyingine na nafasi yake amepewa mwanachama mpya toka chadema na wazir mstaafu ndugu lowassa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mm binafsi najisikia furaha sana kama viongozi wetu waandamizi wa nchi wanajenga mahusiano mema kwa mustakabala wa taifa letu.

Pale ambapo kunatokea migawanyiko ndipo mwovu shetani naye anaingia bila kupiga hodi na kusambaratisha kile kilichojengwa kw a muda mrefu.

Hongereni viongozi wetu kwa kuiona kasoro hiyo na kuirekebisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yajayo yanafurahisha...uko tayari?
Maendeleo Hayana Chama.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
TEMBO WA SIASA ZA TANZANIA AREJEA CCM.

Leo 13:15pm,03/03/2019.

Mwamba wa siasa za Tanzania,Mwamba wa Siasa katika dunia ya miongo mingi, Laigwanan aliyefikia hadhi ya juu katika Uongozi na kupendwa na Watanzania kulikoleta Mafuriko Mwaka 2015,Mahaba hayo yalichagizwa na kilele cha hali ya juu cha hekima na busara aliyo nayo katika kufikiri na katika Ustaarabu wa Ukomo wa Mwanadamu, Tembo wa Siasa za Tanzania,Edward Lowassa amerejea CCM baada ya kukaa Chadema kwa siku 1,293.

Dhoruba imetulia,Nuru imetamalaki,2020 CCM
Tutaishika tena njia ya Mabadiliko na Hapa Kazi Tu kama kitu kimoja,kuinyanyua tena Elimu kwa kasi isiyo kifani kupata wataalam wa Kitanzania watakao ibeba Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati.Mchapakazi Edward Lowassa aungana na Mchapakazi Rais John Magufuli kuipeleka Tanzania mbele katika uchumi wa kati,Edward Lowassa na John Magufuli wanaotambulika kwa Uchapakazi na Maamuzi magumu wataionyesha dunia kwamba Tanzania ni nchi ya kuheshimika na kamwe si shamba la bibi.

Mafanikio ya sasa ya Rais Magufuli ya kuuinua uchumi,yatanogeshwa na Edward Lowassa kwa fursa kadhaa kwa vijana na kufungua milango ya ajira na kazi.Miaka mitano ya Uongozi wa Rais Magufuli umefanya kazi ya Urais ambayo ilitakiwa kufanywa kwa miaka kumi, Kwa miaka mitano mingine ya Rais John Magufuli atafanya kazi ya urais iliyotakiwa kufanya kwa miaka mingine kumi, hivyo basi miaka 10 ya Rais John Magufuli itakuwa imefanya kazi ya Urais iliyotakiwa kufanywa kwa miaka 20.Kwa lugha ya mabeberu tungesema "A President with a difference " Rais mwenye kuacha alama.

Umuhimu wa Edward Lowassa na mambo yake makuu tunaweza kuyaorodhesha toka Lushoto hadi Sikonge na yasiishe, na Mazuri ya Rais John Magufuli tunaweza kuyaorodhesha toka Tanzania bara hadi visiwani na yasiishe,Niseme tu sasa Chadema, CUF na ACT hawafui dafu,ni wasaka tonge kwa mfano wa Mbowe, Lissu,Zitto,Mwalimu Sefu na Lipumba.Sasa wapinzani watadoda kama chuchunge
Lowassa amewapiga mchana kweupe na siku ya tatu leo wanalala na viatu.

Hakika kupatana na kuungana kwa wagombea Wakuu wawili katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ni Jambo jema na bora kwa Taifa letu la Tanzania,kwa kuwa ni udhihilisho ya kuwa hoja zote za Upinzani zimefanyiwa kazi na Mh Rais John Magufuli hata mpinzani wake Mkuu kumuunga mkono.

Ni historia kuu bara hata visiwani,Siasa zetu zimetia fora kwa kukubaliana katika mambo ya msingi kwa maslahi mapana ya Taifa letu.Taifa linawahitaji watu wengi kama Edward Lowassa na John Magufuli.

-Lowassa aiongezea CCM uungwaji mkono.

Nguzo kubwa ya Chama cha Siasa chochote Duniani ni kuongeza uungwaji mkono kwa maana ya Wanachama wanaomuunga mkono Edward Lowassa kuiunga mkono CCM na kuiacha solemba Chadema.

Edward Lowassa anaungana na wanaCCM wengine kuwa mwanachama sawa na wewe au Mimi na mwingine yeyote awae!

Ujio wa watu maarufu ndani ya chama chochote ni ishara ya kuongeza Uungwaji mkono ndani ya chama na kupelekea chama kuendelea kuaminika kwa Watanzania.

Edward Lowassa karejea CCM baada ya kujihakikishia kuwa ndani ya CCM kuna utulivu na kila mtu anapata haki yake kama ile ya binadamu wote ni sawa, Viongozi wanatenda kazi sawa sawa na hakuna Upinzani nje ya CCM ispokuwa kuna Wanaharakati kuliko vyama vinavyo fikiria kuchukua uongozi wa Taifa {dola} anawaona wanaharakati badala ya wanasiasa kwa namna hiyo kila Mwanasiasa aliyepevuka na kuvuka uanaharakati ni lazima ajiunge na jeshi la wanasiasa halisi na ndivyo alivyofanya Edward Lowassa.

Lowassa amekuja wakati muafaka,Mh Rais Magufuli akitenda sawasawa kwa kila mtanzania, Maelfu ya Wamasai wakipatiwa Maeneo ya kulishia mifugo yao,wakulima wakiendelea kufaidika na Nchi yao kwa kuuza mazao yao hata kufikia wakati Serikali kuamua kununua ili mradi mkulima afaidike na jasho lake na kuepusha matapeli ambao daima walikuwa wakimlalia mkulima.

Edward Lowassa amerejea CCM wakati ambao chama kinaisimamia Serikali na kuhakikisha mnyonge hanyanyasiki,Wakati ambao Mtanzania akijisikia kuwa raia katika Taifa lake,Wakati ambao Rasilimali za Nchi kwa mara ya kwanza zimekuwa mali ya Mtanzania kwa sheria na wala sio kwa msaada,Vivaa Rais John Magufuli.

Mh Edward Lowassa anakuja ndani ya Chama wakati ambapo Taifa linahitaji Umoja zaidi na kupambana na Mabeberu,Mabepari,Mabwenyenye,Makaburu na vibaraka wao popote walipo, Edward Lowassa wakati Taifa linapopiga hatua kuelekea katika Uchumi wa Kati ifikapo 2025.

Karibu sana Mh Edward Lowassa,Karibu sana Tembo wa Siasa za Tanzania, kama kuna wengine wamebaki huko,Karibuni sana Team Lowassa iliyokwenda Chadema, Karibuni sana vijana wa 4u Movement ambao daima mlimuunga mkono Edward Lowassa,Karibuni sana wanamabadiliko ambao mliamini mabadiliko yatatokea Chadema lakini kwa mshangao wenu Mabadiliko yanatokea ndani ya CCM chini ya Rais John Magufuli. tunawakaribisha sana CCM,Daima Chama Cha Mapinduzi kinajengwa na Watanzania wote kwa umoja wetu.

Edward Lowassa maisha yako yote toka ukiwa kijana umekulia CCM kasoro siku 1,293 ambazo ulikuwa mwana mpotevu,Kwa Baba na Mama daima nafasi ya Mwana ipo siku zote, CCM ni kwako karibu ikibidi hata ufike jikoni, we ni sawa na wengine tuliokuwepo hapa uliotuacha na sasa umetukuta, Kwetu hakuna Ubaguzi kama kule Chadema.

-Nani aliyeumia kwa Ujio wa Lowassa ndani ya CCM.

Ni dhahiri shahiri Membe,Makamba,Nape na wanaCCM wale ambao walikua na wapo wanaendesha mikakati ya kumshinda Rais Magufuli 2020.( Tukumbuke, hamna wanasiasa Tanzania ambao ni makachero wa siasa kama Edward Lowassa na Rostam Aziz hata kupata kuitwa King's Maker, rejea uchaguzi wa 2005.) Awa ni Watu ambao kimkakati hawakubaliani na Membe.

-Nani mwingine aliyeumia!?

Chadema ni kitaasisi kingine kilichoumia,Edward Lowassa pekee ni taasisi kubwa kuliko Chadema,Edward huyo huyo ni moja ya vitaasisi vidogo vidogo ndani ya CCM. Kwa hiyo ile taasisi kubwa kushinda Chadema,Taasisi ya Edward Lowassa imeondoka na kura zake Milioni 6 ilizowaletea Chadema 2015,Taasisi hiyo imeondoka na siri ya kambi ya Chadema, hivyo basi Chadema wajiandae kuchunguliwa kama nyani juu ya mti.

Nimalizie kwa kusema Chadema imetiwa chumvini,Chadema imepukutika kwa kutu,Chadema imepotelea pwani,Chadema imebaki kibubutu,Sasa Mpini umegeuka mtukutu,
Mpini umekuwa kifimbocheza,Chadema mtatandikwa mgongoni hadi mjute kuwa wasaliti wa Nchi, Mwambieni Tundu Lissu njia yake ya kuingia ligi kuu imekutana na visiki, Poleni kwa kulala na viatu ikiwa ni siku ya tatu leo tangu Edward Lowassa arejee CCM, Karibu sana Nyumbani, Ndugu Edward Lowassa.Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais John Magufuli.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.
 
E
Nakubaliana na ww ila apa naangalia ushawishi na kukubalika kw wananchi. Lissu ana ushawish mkubw na anakubalika pia. Kilichombeba lowassa 2015 na kuitiksa ccm ni mvuto tu wa kisiasa hakuw na ushawish wala hakukubalika kulinganisha na magu. Kw sasa lissu anavyo vyote kuanzia mvuto wake ktk siasa, anaushawish na anakubalika pia. Ila nakubaliana na ww kuhusu mfumo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuwa akikubalika Ila alikuwa na mvuto tu wa kisiasa? How? Ukishakuwa a mvuto wa kisiasa si ndo kukubalika huko? Nisaidie hapa.
 
kivuli cha Lowasa kinatisha sana, tikisiko la CHADEMA ni kubwa sana, Lissu ajiandae kupambana na CCM yenyewe sasa. Huyo ndio LOWASA, Tanzania political legend
 
Back
Top Bottom