Nimeangalia hoja ya mwanakijiji na michango ya wengi wengine waliochangia na kuna vitu nimeokota humo ndani. Nami nina mtazamo kulingana na uelewa wangu. Hoja ya Mbowe kuachana na uenyekiti kwangu inaendelea kuwa na mashiko bila kujali Utetezi mzuri unaotolewa na wengine. Mimi ni mtu ninayeamini kwenye demokrasia ya kupokezana vijiti. Hivi kama mtu ameshakaa zaidi ya miaka 15 ana uhalali gani wa kuendelea kukalia nafasi hiyo? Ni kweli ndani ya cdm hakuna mtu mwingine anayeweza kuwa mwenyekiti? Hili kosa la kumpokea Lowassa ni kosa la dhahiri la kiongozi kuwajibika na ukizingatia muda aliokaa madarakani ni kipi kinafanya aendelee kukaa madarakani? ni jipya lipi ataleta zaidi ya hayo aliyofanya?
Kuhusu kuondoka kwa Lowassa, ni kweli kutakuwa na kuvunjika moyo kwa baadhi ya watu, kwani kuna ambao walimkubali Lowassa kwa ushabiki na sio nini anachosimamia. Kwenye hili ni rahisi wanacdm waweze kulielezea vyema ili kuwafanya wananchi waliokwazika kuendelea kuwaelewa. Ufafanuzi huo wasiachwe viongozi wa cdm kwani wao watakuwa walionja asali ya Lowassa, hivyo itakuwa ngumu wao kujitetea vyema kwenye hilo. Kwangu mimi kuondoka kwa Lowassa ni faida zaidi kwa cdm kwani hakuwa na msaada wowote zaidi ya kuja kuwafundisha siasa za kikondoo kwa faida ya ccm.
Kuhusu ccm na Magufuli, ni dhahiri ccm inategemea madaraka ya rais kama mwenyekiti wa chama chao kutokana na katiba mbovu kufanya siasa na kujipatia ushindi haramu na halali. Ni ukweli usioacha shaka kwamba Magufuli hawezi siasa za ushindani, na hafichi tabia yake binafsi inapokuja suala la ushindani. Magufuli ni mtu anayependa siasa lakini asiyekubali kushindwa, hivyo kutokana na nguvu zake alizonazo kikatiba anatumia madaraka yake kuhakikisha mamlaka zinajiona zina wajibu wa kumfanya ashinde yeye na watu wa chama chake kwa Hadaa ya uzalendo. Mfano wa tabia ya Magufuli tumejionea kwenye chaguzi za marudio. Na kitakachotokea hiyo 2020 tutaona ccm ikipata ushindi wa kishindo, sio kwa ridhaa kubwa ya wananchi, bali kwa maagizo ya rais. Tatizo litakalotokea ni kuwa na bunge lisilo na upinzani bali bunge la chama kimoja ambalo huenda likamuongezea Magufuli muda wa kukaa madarakani.
Angalizo kwa wapinzani hiyo 2020, iwapo watamsimamisha Lissu kugombea na jinsi alivyo na msimamo, na uhasama wake dhidi ya Magufuli ni dhahiri mauaji makubwa dhidi ya wapinzani yatafanyika kiwazi wazi na nyuma ya pazia. Ukatili wa hali ya juu utafanyika dhidi yao, labda mataifa ya kigeni yatoe tahadhari, na iwapo ukatili utazidi kipimo basi waseme hatua fulani kama kususia bidhaa zetu utafanyika ili kuepusha udhalimu huo.