Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Hili swala linakuzwa sana lakini halina uhalisia, Lowassa alitajwa na Dk Slaa kwenye list of shame sambamba na majina mengine, serikali ya JK mpaka 2015 imekuwa na kashfa nyingi za ufisadi na washukiwa wengi Lowassa hakuwa na uziada wowote labda wewe ndiyo uniambie uziada wa kashfa za Lowassa dhidi ya washukiwa wengine.
Kuna hoja nakubaliana na wewe kwamba Lowassa yeye siyo ndiyo kila ufisadi katika nchi yetu na kuwepo ama kutokuwepo kwake CCM au CHADEMA hakuondoi ufisadi Tanzania.

Lakini lazima tukubali kwamba "Ufisadi" wa Lowassa pia ulikuzwa sana na CHADEMA wakati akiwa CCM na kwenye uchaguzi wa Arumeru ikawa ndiyo kilele cha chanzo cha kampeni za wanasiasa wa CHADEMA kusema kila neno kwamba Lowassa ni Alama ya ufisadi na yeye mwenyewe ndiyo fisadi namba wani.

Sasa kama hii hoja ya CHADEMA kumfanya Lowassa kama ni Alama ya ufisadi na yeye mwenyewe ndiye ufisadi na kisha mtu mwenye sifa hizo kumpokea kwa mbwembwe za "kubadili gia angani" kama inaonekana haina maana basi tukubali kukubaliana kutokukubaliana.
 
Mbowe kupisha wengine ni wao zuri. Ila wazo hilo linatiwa doa na kutia mashaka nia yake pale linapotolewa zaidi na "wapinzani" wa CDM kuliko wanahadema wenyewe.
Hapo ndio panakuwa na ukakasi.
 
Lowasa hakuinunua chadema na wala hakuwa na hiyo pesa huo uzushi propaganda zilitengenezwa makusudi kwa nia ya kuwahujumu chadema lakini wenye Akili walijua na kuzinduka mapema lakini wale vilaza wajinga wasiojitambua hawajazinduka wamekariri mpaka leo wakizani kukariri kwao uzushi wa CCM ni ujanja kumbe ni ujinga uliopitiliza sana, Lowasa alikuwa na nyote kipindi kile popote angekwenda angepokelewa hakuhitaji kununua chochote kwani hata hiyo pesa kubwa hivyo hakuwa nayo acheni kuendelea kukariri ujinga wananchi wanataka maendeleo pia mrudishe trilion 1.5 mlizotafuna mkagawana kimya kimya wenyewe.
Ushuzi!?

Na kweli umeutoa, unanukaa
 
Makosa yalifanyika na kuna ulazima viongozi wa CDM wakae chini na wajitathmini kwa kina, Ni kweli kwamba EL hajawahi kuitetea CDM wala ku support kile ambacho CDM imekua ikipambana nacho.

Ni muda kwa viongozi kujitathmini na kurudi kwa wanachama kukubali kua yalifanyika makosa kumkaribisha EL.
Swali la kujiuliza ni kwamba Je? kama EL angefanikiwa kupata uraisi kupitia CDM angetekeleza kile ambacho CDM inakiamini au angeendeleza yale aliyoyaamini akiwa CCM?
 
Lowassa ndie alikuwa akilipa mishahara ya wafanyakazi wa chadema kuanzia mwezi huu wafanyakazi chadema mtaisoma namba.
 
Na wafanyakazi wa serikali Lowassa ndie alikuwa anawapa mishahara? Maana hadi Leo hawajawahi kuongezewa mishahara tangu Lowassa asepe
Lowassa ndie alikuwa akilipa mishahara ya wafanyakazi wa chadema kuanzia mwezi huu wafanyakazi chadema mtaisoma namba.
 
Nimeangalia hoja ya mwanakijiji na michango ya wengi wengine waliochangia na kuna vitu nimeokota humo ndani. Nami nina mtazamo kulingana na uelewa wangu. Hoja ya Mbowe kuachana na uenyekiti kwangu inaendelea kuwa na mashiko bila kujali Utetezi mzuri unaotolewa na wengine. Mimi ni mtu ninayeamini kwenye demokrasia ya kupokezana vijiti. Hivi kama mtu ameshakaa zaidi ya miaka 15 ana uhalali gani wa kuendelea kukalia nafasi hiyo? Ni kweli ndani ya cdm hakuna mtu mwingine anayeweza kuwa mwenyekiti? Hili kosa la kumpokea Lowassa ni kosa la dhahiri la kiongozi kuwajibika na ukizingatia muda aliokaa madarakani ni kipi kinafanya aendelee kukaa madarakani? ni jipya lipi ataleta zaidi ya hayo aliyofanya?

Kuhusu kuondoka kwa Lowassa, ni kweli kutakuwa na kuvunjika moyo kwa baadhi ya watu, kwani kuna ambao walimkubali Lowassa kwa ushabiki na sio nini anachosimamia. Kwenye hili ni rahisi wanacdm waweze kulielezea vyema ili kuwafanya wananchi waliokwazika kuendelea kuwaelewa. Ufafanuzi huo wasiachwe viongozi wa cdm kwani wao watakuwa walionja asali ya Lowassa, hivyo itakuwa ngumu wao kujitetea vyema kwenye hilo. Kwangu mimi kuondoka kwa Lowassa ni faida zaidi kwa cdm kwani hakuwa na msaada wowote zaidi ya kuja kuwafundisha siasa za kikondoo kwa faida ya ccm.

Kuhusu ccm na Magufuli, ni dhahiri ccm inategemea madaraka ya rais kama mwenyekiti wa chama chao kutokana na katiba mbovu kufanya siasa na kujipatia ushindi haramu na halali. Ni ukweli usioacha shaka kwamba Magufuli hawezi siasa za ushindani, na hafichi tabia yake binafsi inapokuja suala la ushindani. Magufuli ni mtu anayependa siasa lakini asiyekubali kushindwa, hivyo kutokana na nguvu zake alizonazo kikatiba anatumia madaraka yake kuhakikisha mamlaka zinajiona zina wajibu wa kumfanya ashinde yeye na watu wa chama chake kwa Hadaa ya uzalendo. Mfano wa tabia ya Magufuli tumejionea kwenye chaguzi za marudio. Na kitakachotokea hiyo 2020 tutaona ccm ikipata ushindi wa kishindo, sio kwa ridhaa kubwa ya wananchi, bali kwa maagizo ya rais. Tatizo litakalotokea ni kuwa na bunge lisilo na upinzani bali bunge la chama kimoja ambalo huenda likamuongezea Magufuli muda wa kukaa madarakani.

Angalizo kwa wapinzani hiyo 2020, iwapo watamsimamisha Lissu kugombea na jinsi alivyo na msimamo, na uhasama wake dhidi ya Magufuli ni dhahiri mauaji makubwa dhidi ya wapinzani yatafanyika kiwazi wazi na nyuma ya pazia. Ukatili wa hali ya juu utafanyika dhidi yao, labda mataifa ya kigeni yatoe tahadhari, na iwapo ukatili utazidi kipimo basi waseme hatua fulani kama kususia bidhaa zetu utafanyika ili kuepusha udhalimu huo.
 
Lowassa ndie alikuwa akilipa mishahara ya wafanyakazi wa chadema kuanzia mwezi huu wafanyakazi chadema mtaisoma namba.
Dah jamani mbona waonekana fyatu kabisa,mtu mzima na akili zako unaweza kuandika vitu ambavyo hata mtoto wako hawezi kuviandika!!!. Acha kuwaza kwa kutumia mirijaa ya kinyesi
 
Dah jamani mbona waonekana fyatu kabisa,mtu mzima na akili zako unaweza kuandika vitu ambavyo hata mtoto wako hawezi kuviandika!!!. Acha kuwaza kwa kutumia mirijaa ya kinyesi
Subiri mwisho wa mwezi usikie kelele na vilio vya wafanyakazi walioajiriwa chadema .Stay tuned
 
Kuna hoja nakubaliana na wewe kwamba Lowassa yeye siyo ndiyo kila ufisadi katika nchi yetu na kuwepo ama kutokuwepo kwake CCM au CHADEMA hakuondoi ufisadi Tanzania.

Lakini lazima tukubali kwamba "Ufisadi" wa Lowassa pia ulikuzwa sana na CHADEMA wakati akiwa CCM na kwenye uchaguzi wa Arumeru ikawa ndiyo kilele cha chanzo cha kampeni za wanasiasa wa CHADEMA kusema kila neno kwamba Lowassa ni Alama ya ufisadi na yeye mwenyewe ndiyo fisadi namba wani.

Sasa kama hii hoja ya CHADEMA kumfanya Lowassa kama ni Alama ya ufisadi na yeye mwenyewe ndiye ufisadi na kisha mtu mwenye sifa hizo kumpokea kwa mbwembwe za "kubadili gia angani" kama inaonekana haina maana basi tukubali kukubaliana kutokukubaliana.
Brother najua watu ambao hamkupenda yale maamuzi mnafikiri huu ndio wakati muufaka kuonyesha hayakuwa sahihi,lakin unajua kampen za arumeru lowassa alikuwa target kwa sababu na yeye alishiriki zile kampen moja kwa moja,japokuwa hakuna aliyenionyesha ni kwa jinsi ghani chadema waliathirika na uchaguzi wa 2015 kwa kumuweka lowassa kama mgombea
 
Subiri mwisho wa mwezi usikie kelele na vilio vya wafanyakazi walioajiriwa chadema .Stay tuned
Vipi mbona hakuna zile milioni 50 kila kijiji?? Au RA &Edo ndio wamekuwawamekujaa kuokoaa jahazii kuelekea 2020😂😂😂😂😂💰💰💰💰 wapeni Wananchi
 
Back
Top Bottom