Tetesi: Edward Lowassa kuongea na vyombo vya habari kesho kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Status
Not open for further replies.
Mbowe,na uongozi wote wajuu wa chama,achieni ngazi,waingie viongozi wapya,hata kama,CCM,ilifanya ujasusi kupandikiza mamluki,wakakivuruga chama,kitendo cha nyinyi viongozi,kushindwa kulitambua hilo,inabidi muachie ngazi,

Nia yenu aondoke Mbowe, Chadema ife au ibaki kivuli cha ilivyo sasa halafu mtengeneze upinzani katika mfano wenu, hususan ukiongozwa na mnafiki ZZK au Le Profesori. Mwisho mtamleta Bunsen Burner aeleze kuwa eti demokrasia ya nchi imeharibika baada ya Chadema kutegemea uwezo binafsi wa mtu mmoja, yaani Mbowe.

Ukweli ni kwamba Mbowe, kama ilivyo kwa Lissu, ni viongozi wenye uwezo wa kipekee kama wa Mandela hapa TZ. Wanazaliwa viongozi wachache sana wa aina hii duniani, watu wenye misimamo yao thabiti usioyumbishwa.
 
Binafsi sijawai mkubali.lowasa hata tone,na sumaye nae aende anasubiri nini?wabaki makamanda pure.Hawa wafanya biashara sio wa kuwaamini kbsa
Yale mashamba yao walonyanganywa watarudishiwa kwa ahadi ya kurejea FISIEM [emoji196]
 
Lile jina mnalomuita la FISADI je mtalifuta hamtomuita tena?
 
Kuna kundi la vijana wa M4C whatsapp amewatesa sana. Vijana wanasema wenzetu wamefungwa kwa ajili yake leo anafanya hayo tena. Wamesononeka sana.
 
Akienda CCM Chadema wanaweza kusema CCM wamepokea Fisadi.Very crazy politcs ever
 
Huyu mzee kariharibia sana siku leo pamoja kuwa sijawahi kumuunga mkono ila nilikuwa namuona kama labda anaweza kuwa mtetezi wetu kumbe sivyo. Na kauli ya kuumiza zaidi leo ni " Eti anafanya vizuri tumuunge mkono". Hata kama wewe siyo mtafiti utaona direct kuwa Magufuli hafanyi vizuri.
 
Kuna wakati ni kama tunachezewa shere... Yani kuna kaliba ya watu ni mastermind wa kucheza na akili zetu... Jamaa kaleta mtafaruku mkubwa... Mitandaoni pakawa hapatoshi... Jukwaa la siasa likafurika kila aina ya mjadala.....

Kimuhe muhe hiki kimeletwa na Roadman na Fid Q... Kuna mtu kaniambia ilikuwa ni kupoza ishu ya Mr. OLE Sandy... Sijaona uhusiano
Lakini tumechezewa shere... Waandishi walikuwa tayari wameshaandaa vichwa vya habari... Halafu mwana akasepa....!!!! Yani ni sawa na kunywa mchuzi wa pweza karanga mbichi kisha kubugia mkuyati erecto gram 100 halafu goma lisitokee kwenye mtanange kitandani...!!!

Ama goma limejikoki na hamu zake zote lije likususie likwambie leo yote yako halafu na kibermeer chako ndani ya sekunde 59 kwishney kero ya kutofikishwa kileleni

Kila upande umepumua jioni hii.. HAKUONGEA.. Ila haimaanishi HATAONGEA... Kama ni mechi ni ushindi wa mezani lakini ule wa kutoshana nguvu... Hakuna mshindi wala mshindwa.. Mashabiki walie tuu

Bado najiuliza makutano yale hayakuwa ya bahati mbaya.. Yalipangwa kwa makusudi. Ilikuwa ni bypass lakini kwenye lipi?

Mdogo wangu Gambo kajipa credit, kwamba eti roadman kamtuma akamuombee kukutana na Bob! Dah gumbo tuhurumie kwenye hili.. Na waliokuamini wote wanapaswa kupimwa akili... Gumbo siasa umeanza lini mpaka yeye akutume wewe? Another 2018 miracle
Ngoja tusubiri yajayo pengine yatatupa majipu kama si majibu.. Wakati utasema
 
nimezichukia sana siasa za majitaka !siasa za africa !upuuz mtupu !kwakweli Africa ni lazima tutawaliwe upyaa
 
Roadman sio mtu wa kuaminika hata siku moja usije mwekea dhamana
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…