Tetesi: Edward Lowassa kuongea na vyombo vya habari kesho kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Tetesi: Edward Lowassa kuongea na vyombo vya habari kesho kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Status
Not open for further replies.
Huyu akirud alikotoka ni nafuu kubwa kwa sie wanachedema tunaoamini kwenye ukombozi wa pili kupitia harakati na mfumo mbadala wa utawala nje ya watu waliokulia ccm na wanasaka maslahi binafsi tu
 
Mnajiriwaza poleni sana. Endapo hatahama mtamfurahia na kumpongeza sana. Poleni sana, naona furaha zenu ni za msimu. Dah, Polepole mliyemdharau kwa upole kutokana mwendo pole wake naona taratiiiibu anawamalizia watu pumzi. Kazi imebakia kukalia kujiliwaza na Lissu.

Unausemea moyo wako si moyo wangu.Hivyo anavyowaza si niwazavyo mimi.Pole sana huwezi kunisemea ila kikubwa nampa hongera kwa kukaa Muda aliokaa nasi Upinzani na pili ninamtakia kila la kheri aendako.Hakuwahi kuwa role model wangu na hatakuwa role model wangu
 
Lowasa anaakilisana alitaka machadema wamsafishe wenyewe ili wakimaliza kumsafusha arudi Ccm.
Ngoja tuone kama akirudi watasema tena fisadi
 
Wakuu,

Nawaletea taarifa hii kama nilivyopokea.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chadema Edward Lowassa kuongea na vyombo vya habari Jumatano hii kwenye hotel ya Serena Jijini Dar Es Salaam.

Mkutano utafanyika kuanzia saa 5 asubuhi..
Mbowe,na uongozi wote wajuu wa chama,achieni ngazi,waingie viongozi wapya,hata kama,CCM,ilifanya ujasusi kupandikiza mamluki,wakakivuruga chama,kitendo cha nyinyi viongozi,kushindwa kulitambua hilo,inabidi muachie ngazi,
 
Wape faraja kesho... Wanakupenda sana. Kumbuka zile kura million 6 na ushee kumbuka matusi kashfa na kejeli na tuhuma lundo ulizotupiwa... Usije ukawa mwepesi kusahau... Utawaumiza na kuwaliza wengi sana... Usijiwazie wewe... Wawazie hawa watu wanaokupenda sana
Muda unayoyoma watu wamejawa na kihoro kuwa kesho utaongea nini.. Baadhi wanasema maandalizi ya leo kule Pugu hayakuwa ya hasanali bali wewe... Safari yako ya ikulu na matamshi yako yale tayari yameshawasononesha wengi sana... Ni simanzi kila mahali...
Una utashi msimamo na maamuzi binafsi lakini una tafakuri na hekima pia... Kama ukiamua kurudi ccm waweza kwenda.. Hakuna atakayeweza kukuzuia... Lakini utaleta Maumivu kwa mamilioni ya watanzania waliohangaika nawe bega kwa bega usiku na mchana.. Kuna watu si haba wameumizwa kuteswa na kudhulumiwa maisha na mali zao kwa sababu tu ya kukuunga mkono wewe... Usije kuwasahau hawa... Wengine bado wako mahabusu na wengine wanatumikia vifungo usiwasahau pia...
Watanzania wanapitia kipindi kigumu sana.. Wana sononeko na majonzi hawahitaji kuumizwa zaidi.. Wape faraja wafurahi....
Ikishindikana kabisa waweza kwenda.. Watakaobaki wataukomboa wakati...
Kwahiyo mzee na wewe ulikuwa miongoni mwao mliomuamini huyu jamaa?
 
Ninachojua Lowassa hajawahi kuwa mpinzani sembuse kupigania haki za wapinzani ... Lowassa anachojua yeye ni kupigania maslahi yake pekee na hapa ndipo upinzani ulipokosea dira na kusababisha haya yanayoendelea hapa nchini.
 
Binafsi sijawai mkubali.lowasa hata tone,na sumaye nae aende anasubiri nini?wabaki makamanda pure.Hawa wafanya biashara sio wa kuwaamini kbsa
 
Mbowe aliharibu sana kumpokea huyu mzee! kwakweli ametuharibia chama! kitendo cha kumpoteza Dk Slaa ilikuwa ni pigo kubwa chamani! sasa niwakati ws kumuomba Dk Slaa arudi akijenge chama!
Arudi, kwa ujinga upi alionao???
 
Natamani huu ujumbe murua umufikie huyu mzee huko aliko.

Nakumbuka watu walitukanwa, walipigwa, walidhalilishwa, walifungwa, walipewa vilema vya maish, walishinda njaa, walikosana na ndugu na jamaa kisa harakati za 2015 kumusapoti huyu mzee halafu from no where nae awe na price tag yake[emoji27] [emoji27] !!

Upande wangu niliachana na kipenzi cha moyo wangu kisa nilikua upande wa huyu mmasai huku yeye akiwa upande wa huyu wa chato.
Na hatukurudiana kamwe
Na badoooooooooooooo



Utakoma.


Unashabikia ujinga wa chadema????
 
Hato unga mkono ila ata eleza makubaliano kati ya yenye (upinzani) na Magu (chama tawala)
 
Wanachadema huyu Lowassa tumuite nani akihamia ccm?
Fisadi? Mgonjwa?
 
Lowassa ni Great leader.. tatizo CHADEMA wanafanya siasa za utoto na low standards.. Mh. Lowassa nadhani kajaribu kuwarekebisha ila bado hawaelewi..

Hint: Mh. Lowassa kalelewa na kukulia CCM, hivyo akitaka kurudi hakuna shida, CCM tuko tayari kumpokea kwa mikono yote miwili..
Mnampokea fisadi tena!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom