Tetesi: Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM

Tetesi: Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM

Screenshot_20171122-204907.png
JPM
 
Licha ya kuaminishwa, kuna kitu unasahau, COMMON SENSE!
Utendaji kazi pia wa JPM nimeuona kwa miaka kama 10 hivi, UMETUKUKA.

Naona unachanganya mambo mawili: utendaji na matumizi mabaya ya madaraka na mali za umma.

Licha ya kutowahi kukubali wala kuona huo utendaji uliotukuka wa Magufuli; kwani utendaji wa Lowassa una mashaka? Si wana CCM walikuwa wakimsifia kwa kuvunja mkataba wa kifisadi wa City Water? Si alisifiwa kwa ‘kuanzisha’ shule za kata? Si alisifika kama mzee wa maamuzi magumu, ambaye watendaji wa serikali walimwogopa? Kama utatumia karata ya utendaji, Magufuli hatoona ndani kwa Lowassa.

Utendaji uliotukuka wa Magufuli ni upi haswa? Ujenzi wa barabara zilizo chini ya kiwango maeneo yote ya nchi? Ununuzi wa Dar Ferry? Uuzaji wa nyumba za serikali? Ukamataji wa meli ya uvuvi serikali iliyolipa fidia? Uboaji wa kituo cha mafuta Mwanza, ambapo serikali ililipa fidia? Utendaji upi unaouongelea chifu?

Licha ya hiyo karata ya utendaji, wote wawili wana tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya serikali. Lowassa alisemwa hivyo kwenye Richmond; Magufuli kasemwa hivyo kwenye CAG reports.

Tafuta nyuzi za zamani humu jf kabla lowassa hajahamia chadema akiwa sisiemu UNIELEWE nilivyokuwa nampinga, sijawahi mkubali lowassa!

Wapi sasa nimesema nimewahi kumkubali Lowassa? Wana CCM akiwemo Mwenyekiti wenu wa zamani Kikwete walimtetea Lowassa kwa nguvu zao zote! Walifikia kipindi wakasema kwamba kujiuzulu kwa Lowassa ni adhabu tosha, hakuna haja ya kumpeleka Mahakamani. Hivyo ndivyo CCM walisema!

Hata Salary Slip na MUSSA ALLAN toka wakiwa na mzee wao akiwa sisiemu na wao wakimpigia debe na sisiemu niliwapinga!

Hao ni wao, si mimi. Hapa unajadiliana na mimi! Sielewi ni kivipi wanakuwa reference, wakati wao wana maamuzi yao binafsi.

Sio mnafiki kama nyie.

Ona sasa, unanijumuisha sijui na akina nani sasa?
Msimamo wangu kwa Lowassa, upo wazi: Mahakama ndiyo iamue, kwa kuwa tume ya Mwakyembe ilimkuta na hatia, basi serikali imfikishe Mahakamani haraka. Na siyo kuyumbishwa na maneno ya wanasiasa, ambao kutwa kuimba wimbo wa fisadi bila mwisho!
 
abaki huko huko wanakopokea wafisadi!!lakini kama atarudi na kutulia bila kutafuta uongozi wowote hapo sawa!!!apewe masharti kabisa kuwa hamna kuomba uongozi wowote!!!tafadhali sana!!! alikiharibu chama chetu sasa bulldozer anakitengeneza
 
huyo hatutampokea kirahisi, Chama chetu kisije gawanyika tena kwa wenye nacho na wasionacho kama enzi zake. Viongozi wengi walipatikana kutokana na hali zao kiuchumi. Masikini au walala hoi walikuwa hawana nafasi ya kugombea kisa wenye Pesa kukishikilia Chama kwa Rushwa na Ufisadi mkubwa ndani ya Chama.
Sasa Chama letu CCM limesimama wanataka Kurejea Tena Mjengoni.
Kama amebadilika tutamwomba aape mbele ya Wajumbe wote wa NEC na kujadiliwa kwa Nguvu moja.
CCM MBELE KWA MBELEEEE!!!! :✈♿
 
Ehh, Lizaboni umefufuka !. Habari za kuzimu!. Umekuja na polopaganda zako za urongo ambazo ni kama vile kutuambia kuwa kesho jua halitoki.
 
Yo yo yo Chadema walikuwa na matumaini hewa kuwa mgombea uraisi wao hewa Lowasa atashinda na akishindwa atakataa matokeo na atakiinukisha na kuitumbukiza nchi kwenye vita.Wafadhili koko wa Ndani na nje waliamini hivyo kuwa Lowasa na seif Sharif Hamad wakishindwa lazima wakatae matokeo na kuitumbukiza nchi vitani ya wewnyewe kwa wenyewe.Lowasa na seif sharif Hamad wakapiga chenga ya mwili ukawa na wafadhili koko wao wa nje ya nchi hadi Leo hawaamini kilichotokea Tanzania bara na Zanzibar na hawana hamu na CCM wanajua chama CCM ni chama dume kisichosomeka.!!!!!! Lowasa na seif Sharif Hamad wakirudi CCM poa tu .Mission accomplished
 
WEWE NI UCHUMIA TUMBO NDIYO UNAKUSUMBUA NA LAANA YA KUTAFUTIA KUTEGEMEA NA KUCHUMIA TUMBO....NA MZIDI KULAANI KWA KUTEGEMEA VIUNGO VYA MWILI NA WANA WA ADAM ILI MUISHI NA WATU WOTE WASEME AMINA.
Nyinyi ni wabishi kama mashahidi wa Jehova. Kwa taarifa zilizopo ni kwamba hata mwenyekiti wa chama taifa anataka kurudi CCM, hiyo biashara ishamshinda.
 
Namnukuu"""NITAFIA UPINZANI""""""""
BY Edward Ngoyai Lowasa 2015,Dec
 
Lowassa analo jeshi ndani ya CCM ambalo linapambana na kupanga mkakati ea kuhakikisha chama hicho kinakuwa pinzani.
Kuliko wahamie upinzani hao inabidi wabaki kurekebisha mambo huko.
 
hii haiwezi kupingika coz ilikuwa ni game plan kwenda upinzani,Lowasa bado ni ccm. Siku zinakuja kila jiwe litafunuliwa na rangi yake halisi itaonekana
 
Mkuu
Lizaboni
ulipotea sana sana Mkuu Daaaa Mpaka tukasema jamani nani wa kutupa update tena kumbe upo na habari zako motomoto
Usipotee sana Mkuu...
Mkuu kati ya watu ninaowaheshimu sana hapa jukwaani ni wewe kaka...Lizaboni
naomba nikuulize rafiki yako MUSSA ALLAN
Yupo wapi siku hizi?
Hebu teletee huyu Mtu Mkuu tafadhali
 
kuna tetesi kwamba waziri mkuu mstaafu anataka kurudi CCM mimi binafsi sidhani kama kuna mwana CCM anamhitaji mtu kama Sumaye maana hana mvuto wa kisiasa na pia hana upeo wa kupiga siasa za kisasa ,na kwa upande wa CHADEMA sidhani kama itayumba maana siasa za chadema haziwezi mtegemea mtu kama Sumaye.
Anarudi kwa maslah binafsi tuu.
 
Back
Top Bottom