Licha ya kuaminishwa, kuna kitu unasahau, COMMON SENSE!
Utendaji kazi pia wa JPM nimeuona kwa miaka kama 10 hivi, UMETUKUKA.
Naona unachanganya mambo mawili: utendaji na matumizi mabaya ya madaraka na mali za umma.
Licha ya kutowahi kukubali wala kuona huo utendaji uliotukuka wa Magufuli; kwani utendaji wa Lowassa una mashaka? Si wana CCM walikuwa wakimsifia kwa kuvunja mkataba wa kifisadi wa City Water? Si alisifiwa kwa ‘kuanzisha’ shule za kata? Si alisifika kama mzee wa maamuzi magumu, ambaye watendaji wa serikali walimwogopa? Kama utatumia karata ya utendaji, Magufuli hatoona ndani kwa Lowassa.
Utendaji uliotukuka wa Magufuli ni upi haswa? Ujenzi wa barabara zilizo chini ya kiwango maeneo yote ya nchi? Ununuzi wa Dar Ferry? Uuzaji wa nyumba za serikali? Ukamataji wa meli ya uvuvi serikali iliyolipa fidia? Uboaji wa kituo cha mafuta Mwanza, ambapo serikali ililipa fidia? Utendaji upi unaouongelea chifu?
Licha ya hiyo karata ya utendaji, wote wawili wana tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya serikali. Lowassa alisemwa hivyo kwenye Richmond; Magufuli kasemwa hivyo kwenye CAG reports.
Tafuta nyuzi za zamani humu jf kabla lowassa hajahamia chadema akiwa sisiemu UNIELEWE nilivyokuwa nampinga, sijawahi mkubali lowassa!
Wapi sasa nimesema nimewahi kumkubali Lowassa? Wana CCM akiwemo Mwenyekiti wenu wa zamani Kikwete walimtetea Lowassa kwa nguvu zao zote! Walifikia kipindi wakasema kwamba kujiuzulu kwa Lowassa ni adhabu tosha, hakuna haja ya kumpeleka Mahakamani. Hivyo ndivyo CCM walisema!
Hata
Salary Slip na
MUSSA ALLAN toka wakiwa na mzee wao akiwa sisiemu na wao wakimpigia debe na sisiemu niliwapinga!
Hao ni wao, si mimi. Hapa unajadiliana na mimi! Sielewi ni kivipi wanakuwa reference, wakati wao wana maamuzi yao binafsi.
Ona sasa, unanijumuisha sijui na akina nani sasa?
Msimamo wangu kwa Lowassa, upo wazi: Mahakama ndiyo iamue, kwa kuwa tume ya Mwakyembe ilimkuta na hatia, basi serikali imfikishe Mahakamani haraka. Na siyo kuyumbishwa na maneno ya wanasiasa, ambao kutwa kuimba wimbo wa fisadi bila mwisho!