Edward Ngoyai Lowassa anaumwa, alazwa ICU Muhimbili

Nimekuelewa sana.
 
If anyone Dislike or hate Lowassa? Very poor english grammar! Ungesema If anyone dislikes or hates Lowassa.....Kwa nini usingeamua kuandika tu kwa kiswahili? Hapa tuna kazi na lugha ya Malkia jamani, ukute hapo una digrii na upupu wote huu! Dah!
Nashukuru kuwa umeelewa alichoandika...kukosea kwake ndio njia ya kujifunza. Sio jambo la kushupalia
 
Siasa bwana! Nikikumbuka 2015 pale Sumbawanga fomu ya EL ukisaini ulikuwa unapewa cash money 250,000. Ndege mbili, helkopta mbili, v8 za kutosha, mabasi kibao.

Watu kibao walizunguka na mzee kusaka udhamini, wakila wakinywa, kuvuta na kugegedana. Posho mlima. Kweli muda ni hakimu mzuri.
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 

Vyuo vyote Tanzania vinafundisha kwa Kiingereza. Hakuna aliyefikia ngazi ya taaluma bila kusoma kwa kiingereza. Dunia nzima watu walioendelea wanahakikisha wanakijua kiingereza hata kama ni lugha yao ya tatu.

Usione Wachina hawaongei kiingereza ukafikiri hawakijui. Unafikiri wanazurura dunia nzima na kichina tu? Wakongo wanakuja Afrika Mashariki na kifaransa halafu wanajiongeza kwa kiingereza na kuboresha Kiswahili chao. Lugha za kigeni ni nyenzo muhimu kwa mtu anayesaka fursa duniani. Haina politiki za kijinga kama hizi za bongo za “kuenzi Kiswahili” pekee!

Ni aibu kwa Mtanzania anayesoma taaluma yake kwa kiingereza kushindwa kukitumia. Halafu huyo jamaa unayemtetea kashauriwa aandike kwa Kiswahili anachokijua vizuri. Tatizo liko wapi?
 
Tatizo liko hapo mlipomkosoa kwa kumuona kama vile hana akili na kuona ninyi ndiyo mna akili zaidi yake ndiyo nikawaambia kiingereza ni lugha tu wala siyo kipimo cha akili! Na tukumbuke siyo kila mtu anahitaji fursa huko nje ya mipaka kuna watu kiingereza kinawapiga chenga lakini wana akili na wana pesa kuzidi hata wengi wa hao wanaokijua na wakati ni masikini!
 
Sawa kabisa. Sio sisi tu . Afrika hasa mashariki na Kusini ni hivyo hivyo. Tena wenzetu wakiwa nyumbani ni lugha za kikabila tu kama: kichaga, kihaya, kisukuma, kiha, n.k. Lakini hawajilegezi kwenye kujiongeza kwenye kiingereza hata wa primary schools.

Sisi tumefanya kuwa suala kisiasa eti “uzalendo”. Tujivunie Kiswahili tu. It’s not fair. Lugha hasa kiingereza ni nyenzo muhimu ya elimu na fursa za kitaaluma kwa vijana wa kitanzania. Hoja za kushambulia kiingereza ni za kilaghai kutaka kuwajengea vijana masikini false confidence huku wenye pesa watoto wao wanajiongeza mpaka kwenye kifaransa.
 
Tunamuombea uponyaji..kichwa cheupe..njia ya ikulu nyeupe..bila goli la mkono la akina nape huyu ndio angekua ikulu..

Lowassa mabadiliko..mabadiliko lowasa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Tulipoteza wa kutuongoza kwa manufaa ya familia hizi kikwete-riziwani,membe,January makamba, nape mnauye na wengine walijitumbukiza ushabiki wasioujua
 
Namtakia apone haraka Mzee Huyu mwenye busara ZAKE

USSR
Acha Unafiki wewe mbona mlimtukana sana wakati wa Uchaguzi 2015 mkimpigani Mpiga Push Up Eti Ikulu sio ICU leo Yuko wapi yule MZIMA?Dhambi ya kumtukana Mtakufa nayo labda mkamwombe Msamaha hospital
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.

Taarifa kutoka kwa familia hiyo zinasema kuwa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kufanyiwa upasuaji.

Akizungumza leo Ijumaa Januari 28, 2022 na Mwananchi, Mbunge wa jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa ambaye ni mtoto wa Lowassa amesema baba yake alilazwa katika hospitali hiyo alipopatwa matatizo ya tumbo.

"Baba alilazwa kama siku tano zilizopita. Wala haina siri, alifanyiwa upasuaji wa tumbo, lakini bahati mbaya ikaleta complication (hitilafu). Alifanyiwa hapo hapo Muhimbili,” amesema Fredrick.

Amesema wanaomba watanzania, kuendelea kumuombea ili afya yake iendelee kuimarika

"Tunashukuru sana kwa maombi ya Watanzania na tuna imani ataruhusiwa kurejea nyumbani," amesema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…