ONTARIO
JF-Expert Member
- Oct 16, 2013
- 1,884
- 17,096
- Thread starter
- #21
Miaka michache nyuma Marekani walimkamata Saddam Hussein akiwa katika harakati za kutoroka, picha zake zilisambaa dunia nzima. Picha zake akiwa ananyongwa zilichukuliwa na Wamarekani na wakazisambaza kwa maksudi kinyume na sheria. Pia hata mwili wake baada ya kunyongwa uligaiwa kwa ndugu kwajili ya mazishi. Na kama hiyo haitoshi mtoto wa Saddam naye aliuwawa na picha zake zikasambaa kote ulimwenguni. Tukiacha hilo naamini Marekani alikuwa anahusika kifo cha Gaddafi, picha za kuuwawa kwake zilisambaa kote duniani.Kifo cha bin Laden si serekali ya marekani kwa maana ya mashirika ya ujasusi na usalama ama huyu snowden wanazungumza ukweli. Inaweza ikawa ni kweli aliuliwa na c.i.a. lakini wao walitakiwa waionyeshe dunia ushahidi wa picha ya maiti ya Osama.
Snowden naye kwa kuwa alishaamua kuiharibia serekali ya marekani naye alete ushahidi kuthibitisha osama yu hai. Vinginevyo kwa wote wawili inabaki kuwa cospirancy theory.
Mkuu umeandika vizuri na umeeleweka .
Pamoja
Kwanini Marekani walishindwa kusambaza picha za mwili wa adui yao namba moja. Walishindwaje kuutoa mwili wake kwajili ya mazishi. Kama hiyo ilikuwa ngumu walishindwaje japo kutoa DNA proofs za kufo cha Osama.
Bado naamini Osama yupo hai, na kama amekufa basi alikufa kwa sababu za kibaolojia.