Edward Snowden: Jasusi wa Kimarekani alivyopania kumdhalilisha Obama

Edward Snowden: Jasusi wa Kimarekani alivyopania kumdhalilisha Obama

Mkuu Snowden hana njaa kiivo., maana alikuwa na kazi nzuri tu yenye kumuingizia pesa ndefu kila mwezi. Sema jamaa ni jasiri na ni mtu anayeamini katika privacy ya watu. Nahisi kilichomkera ni ile tabia ya US kuingilia kwa siri mawasiliano ya baadhi ya watu kinyume cha katiba yao. Ila sidhani kama Urusi wanamlipa, just kapewa hifadhi tu.
Ukiangali kwa umakini hapa, utaelewa ni uhuni tu wala hakuna kingine.

Snowden hawezi nakataa, kuwa na uchungu na siri za watu, tena wa mataifa mengine ilhali anajua juhudi za taifa lake katika masuala ya kiusalama.huu anaojalibu kuuita yeye ujasiri na kuumizwa ni sarakasi.

Nikashaanga warusi kumpokea, na kumpa hifadhi.
 
Kifo cha bin Laden si serekali ya marekani kwa maana ya mashirika ya ujasusi na usalama ama huyu snowden wanazungumza ukweli. Inaweza ikawa ni kweli aliuliwa na c.i.a. lakini wao walitakiwa waionyeshe dunia ushahidi wa picha ya maiti ya Osama.

Snowden naye kwa kuwa alishaamua kuiharibia serekali ya marekani naye alete ushahidi kuthibitisha osama yu hai. Vinginevyo kwa wote wawili inabaki kuwa cospirancy theory.

Mkuu umeandika vizuri na umeeleweka .

Pamoja
usama alifariki kitambo na ugonjwa wake wa figo na ama kuwa anapokea payroll kwa america sijui anaishi bahamas hapana sio kwl yy kwao peke ktk familia yao wana utajiri mkubwa kuliko hicho tunachoaminishwa kwenye makala
 
Salute!

Siku kadhaa nilibandika uzi hapa kuhusu siri kubwa iliyofichwa katika kifo cha Adolf Hitler. Nilipanga kudondosha mifululizo kadha kujadili ulimwengu wa Hitler, lakini nilipata ombi kutoka mmoja wa wachangiaji kwamba niweke huu uzi ninaouandika sasa. Nami nahisi ni busara kufanya hivyo. Tuendelee...

June 9, 2013 mkurugenzi mkuu wa Nationa Security Agency (NSA) James Clapper akiwa kwenye kikao cha siri na maafisa wa juu wa usalama wa Marekani alifungua kinywa chake na kusema "His crazy operations against our counter espionage has brought us huge grave damage"-- "Oparesheni yake ya kipuuzi dhidi ya usalama wetu wa kijasusi umeleta uharibifu mkubwa mno". Siku chache baadae Katibu mkuu wa Baraza la Wawakilishi (house of representatives) Mike Rogers alitoa maoni yake kwamba "His leaks has put US troops at risk and prompted terrorists to change their tactics, and that most files were related to current Us military operations"-- "Siri alizovujisha zimehatarisha usalama wa askari wa marekani, na imesababisha magaidi wabadili mbinu, hasa ukizingatia taarifa nyingi zinahusu Oparesheni za kivita/kijeshi za hivi karibuni". Wiki hiyo hiyo Mkurugenzi wa Shirika la kijasusi la Marekani (CIA) Dr. James Woosley akiwa kwenye mkutano na vyombo vya habari alisema "If the kid is convicted of treason, he should be hanged to death"-- "Kama huyu mtoto akitiwa hatiani kwa kosa la uhaini/usaliti, yampasa kunyongwa hadi kufa"

Miezi kadhaa baadae Jan 2014, raisi wa Marekani Barack Obama katika hotuba yake alitoa tamko kwa masikitiko "Our nation's defence depends in part on the fidelity of those attributed with our nation's secrets"-- "Ulinzi wa taifa letu kwa namna kubwa unategemea uaminifu wa wale wachache waliopewa majukumu ya kutunza siri za taifa letu". Keshowe mhariri mkuu wa gazeti la New York times aliandika makala ndufu sana ya kuishawishi serikali imsamehe jasusi SHUJAA-MNAFIKI. Mwezi uliofuata Feb 2014, Mbunge (congressman) Ron Paul alifungua malalamiko (petition) kuuomba utawala wa Obama umpe msamaha/kumuonea huruma (clemency) jasusi Edward Snowden.
View attachment 445072

EDWARD SNOWDEN NI NANI?
Alipotokea:
Snowden alizaliwa mjini N. Carolina 1983, babu yake (upande wa mama alikuwa admeri (Afisa darala la kwanza katika jeshi la majini) ambae baadae akawa afisa wa juu FBI, bahati mbaya alikua mmoja wa wahanga wa mlipuko wa Pentagon 9/11. Baba'ke alikuwa mlinzi wa fukwe/pwani (Coast guard), mama'ke alikuwa msaidizi mkuu (chief assistance) mahakama ya jimbo la Maryland. Dada'ke alikuwa mwanasheria wa serikali. Akiwa katika umri mdogo kabisa (13), Snowden alipata alama zaidi ya 150 katika mitihani miwili ya kipimo cha IQ. Akiwa mdogo alipata ugonjwa aliomsababisha asiende shule takriban miezi 10, aliporudi shule alikuta mitihani ya GED akapiga akafaulu kwa wastani wa juu sana. Japo hakupata Bachelor degree, alifanikiwa kupiga Master's ya chuo kikuu cha Liverpool, Uingereza mwaka 2011. Akiwa na miaka 20 alitaja Ubudha (Buddhism) kama dini yake katika fomu za kujiunga na jeshi.

Mtizamo wa kisiasa wa Snowden:
Snowden anadai kua uchaguzi wa 2008 (uliomweka Obama madarakani) alimpiga kura mgombea wa chama cha tatu (3rd-party candidate). Hakuamini katika falsafa za Obama na anadai kwamba alipanga avujishe siri za kijasusi za Nationa Security Agency (NSA) tangu 2009, lakini aliona busara avute subira akiamini kua Obama angetekeleza ahadi zake tofauti na Bw. G. W. Bush.

Baada ya kuvujisha siri nzito za kijasusi na usalama wa Marekani mwaka 2013, jukwaa la kijamii la Ars Technica lilithibitisha kuwa Snowden alikua active member wa jukwaa hilo na kwamba mwaka 2009 katika uzi unaohusu kulinda usalama wa taifa, Snowden alipost kwamba "I think leakers of classified information should be shot in the balls"-- "Nafikiri kwamba wavujishao siri nzito za taifa wapigwe risasi za korodani".

Ajira:
May 2004, Snowden akiwa na miaka 21 aliorodheshwa kwenye kikosi cha akiba (US Army reserve). Alitamani sana kupigana vita ya Iraqi akiamini kwamba kupigana vita hivyo ni ishara ya ukombozi kwa watu wanyanyaswao, bahati mbaya hakufanikiwa kwakua alivunjika miguu akiwa kwenye mafunzo ya kijeshi.

2005 aliajiriwa kama mtaalamu ya maswala ya usalama katika chuo cha Maryland. Mwaka 2006 aliombwa ajiunge na CIA, ambapo aliwekwa kitengo cha mawasiliano ya kimataifa na upelelezi wa mtandao (network surveillance) makao makuu ya CIA Virginia. Mwaka huo alipost kwenye jukwaa la Ars Technica kuwa "siwezi kuhangaika kutafuta/kupata ajira kwakuwa mimi ni mchawi wa kompyuta", akiwa kijana mwenye umri mdogo zaidi katika timu ya wataalamu wa usalama wa mtandao, alipelekwa masomoni katika shule ya siri ya CIA kwajili ya kupata utaalamu wa hali ya juu ya kompyuta, ambapo aliishi hoteli yenye hadhi ya nyota 5 mwaka mzima akipata mafunzo hayo maalumu.
View attachment 445089

Mwaka 2007, CIA walimwagiza Snowden Geneva, Uswisi pamoja na jopo la wanadiplomasia kwajili ya kuchunguza na kuoperate usalama wa mtandao wa vikao vya siri. Alipewa pasi ya kusafiri ya Marekani daraja la diplomasia na alikabidhiwa apartment ya vyumba vi4 karibu na ziwa Geneva. Akiwa kwenye hiyo trip, Snowden alishuhudia kwa macho jinsi CIA walivyoweza kuwahonga kwa rushwa kubwa mno maafisa wa benki ya dunia, maafisa wa ulinzi na wanasheria ili CIA waweze kudua siri za ndani za World Bank. Snowden alipigwa butwaa, kivipi Marekani ilikuwa inahubiri uwazi na kupinga vikali rushwa lakini kumbe ndani ya tundu la sungura wao wanatenda kinyume. Snowden alikasirishwa mno na tukio hilo.
Mwaka 2008 Snowden alichaguliwa na CIA aongozane na raisi Obama katika mkutano wa NATO huko Romania.

Feb 2009, Snowden alimua kujiuzuru kua agenti wa CIA tayari akiwa na siri nyingi sana za ndani.View attachment 445095

March 2009, alianza kazi kwenye kampuni binafsi la Dell ambapo alikua na wajibu wa kutoa maelekezo juu ya kuhakikisha usalama wa mitandao ya wateja wa Dell kuepuka cyber attack. Wateja wa Dell wakubwa walikuwa Yokota Air Base, Shirika la kijasusi la China, mashirika ya serikali na wizara mbali mbali za Marekani, CIA pamoja na kusimamia mifumo ya mawasilia ya National Security Agency.
View attachment 445099

Upelelezi wa kitaalamu unaonesha kwamba Akiwa Dell, kuanzi April 2012, kutumia ujuzi wake wa hali ya juu ya kompyuta, Snowden alianza rasmi kupakua mafaili ya siri za kiusalama za marekani ambazo inakadiriwa kufika zaidi ya documents million 1.

Akiwa analipwa mshahara wa mil. 420 tsh kwa mwezi, Snowden aliamua kuacha kazi katika kampuni ya Dell. Alikua na msukumo wa kumwaga siri zilizomchukiza za usalama wa dunia, lakini alisubiri apate pa kuanzia "breaking point". Siku ambayo kiongozi mkuu wa NSA Alipolidanganya Bunge la marekani (congress) na kula kiapo feki ndipo ilikuwa breaking point yake.

Mwezi mmoja baadae alitoroka marekani kuelekea Urusi ambapo alipewa hifadhi ya maficho (asylum) na Raisi Putin. Baada ya kujihakikishia kuwa ana ulinzi imara ndipo Snowden alipoanza kurusha makombora, alivujisha siri nzito sana za uwezo wa kivita wa marekani, silaha za kivita, tecknolojia, mbinu za kijeshi za marekani, oparesheni chafu za marekani. Katika historia ya ulinzi na usalama wa Marekani hajatokea mpuliza filimbi (whistle blower) aliyeweza kutoa siri nzito, za ndani zaidi na nyingi. Mwaka huo pekee Snowden alimpa mwandishi wa The Gurdian mafaili 10,000 ya siri. Pia njia nyingine aliyoitumia ni kufanya mahojiano na mwanahabaru sehemu ya siri na kisha kurushwa kwenye vyombo vya habari.
View attachment 445101

Snowden amekua akikutana na maafisa wa juu wa usalama wa nchi mbali mbali duniani kama Urusi, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Israeli na mshirika makubwa kama UN, World Bank, IMF na kuwaleza mipango ya Marekani kwa mataifa / mashirika hayo.

Kwasasa Snowden ni mmoja ya watu wanaoohitajika zaidi na Marekani, lakini ni ngumu kumdaka maana hata Mkurugenzi wa FBI James Comey aliwahi kusema "Snowden akiwa CIA na NSA aliishi na magenius lakini wote kwake walikuwa ni taka taka". Jamaa ana verified twitter account na huwa anarusha makombora mara chache chache.

LENGO/DHUMUNI KUU LA UZI HUU:

Mnamo mwaka 2011 serikali ya Marekani kupitia raisi wake Barack Obama ilithibitisha kwamba May 2 ya mwaka huo kikosi maalumu cha maangamizo kilifanikiwa kumtoa kwenye uso wa dunia adui namba 1 wa Marekani, Osama Bin Laden. Aliuwawa akiwa kwenye makazi yake Abboltabad, Pakistan kupitia oparesheni mkuki wa Neptune (Neptune spear) na mwili wake kuzamishwa baharini.
View attachment 445104
Daily mail waliandika kwenye kichwa cha habari "Kaoze kuzimu- Obama: Timu ya Wamarekani imemuua Osama kwenye pambano la moto"

May 2014, Snowden mpuliza filimbi, msaliti_shujaa anaibuka kwenye mahojiano ya siri na kituo cha Moscow Tribune na kusema "The famous terrorist and former leader of Al-Qaeda is ALIVE and receives benefits from central intelligence Agency, CIA"-- "Gaidi maarufu na kiongozi wa Al-Qaeda YU'HAI na anapokea fadhila kutoka Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA). Anadai taarifa za kifo cha Osama zilighushiwa ili kumuongezea sifa na mvuto wa kisiasa raisi Obama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2012. Snowden anaendelea "I have classified documents showing that Osama is still on CIA's payroll"-- "Nina document murua zinazoonesha kwamba Osama bado yupo kwenye malipo ya CIA".
"He still receives more than $100,000 a week which are being transferred through some front businesses and organisations directly to his Nassau bank account, I am not certain where he is now, but in 2013 he was living quietly in Bahamas in his Villa with his 5 wives and many children"-- "bado anapokea zaidi ya mil 209 tsh kwa week kutoka CIA, ambayo inahamishwa biashara na mashirika moja kwa moja kwenye akaunti yake ya benki ya Nassau. Sina uhakika alipo sasa, lakini mwaka 2013 alikuwa anaishi maisha ya kifahari sana Bahamas yeye na wake zake wa5 pamoja na watoto wake wengi"
View attachment 445107

Snowden alidai kwamba "Osama bin Laden ni mshirika (operative) mtiifu na makini wa CIA kwa muda mrefu sasa. Je tukio la Marekani kumuua Osama lingefikisha ujumbe gani kwa washirika pandikizi wa CIA? Kwamba nao wajiandae kuuwawa? Anaendelea kudadavua kwamba Marekani ilipanga shambuluo la bandia la kumuua Osama kushirikiana na Pakistan Secret service na hili tukio limemkumbatia Osama na kumfanya awe salama zaidi, kwasababu kila mtu ameamini Osama ameuwawa, hivyo hakuna mtu atakayejishughulisha kumsaka.

Leo hii Snowden akiwa na makosa yenye kifungo cha jumla ya miaka 120 yupo mafichoni katika nchi za Urusi na Brazil. Baadi ya watu wanamuona kama Msaliti wa usalama wa taifa na baadhi ya watu wanamuona ni mwananchi mzalendo.View attachment 445109

UKWELI UNAOTHIBITISHA KUWA OSAMA HAKUUWAWA KWENYE OPARESHENI GERAMINO.

☆Kivipi Osama afe mara mbili, ni lini alifufuka?
Wachambuzi wa maswala ya kijasusi, viongozi wa nchi, wakuu wa taasisi za usalama waliwahi kuzungumza kwamba Osama alifariki miaka mingi iliyopita (2001). Afisa veterani wa CIA Robert Beir, kiongozi wa zamani wa FBI kitengo cha kupambana na ugaidi (counter - terrorism, waziri mkuu wa zamani wa Pakistani Banazir Butto, Alex Jones wa CIA wote walidai Osama alifariki 2001. Katibu mkuu msaidizi wa Marekani Dr. Steve Pieczenik aliwahi kuthibitisha kwamba Osama alifariki kwa Marfan Syndrome na kwamba daktari wa CIA walifika kuupima mwili wa Osama akiwa hospitalini Dubai.

☆Mkanganyiko wa matukio ya oparesheni Geramino.
Kwanza tunaambiwa kulikuwa na majibizano ya risasi ya dakika 40, tena tunaambiwa hakukuwa na majibizano yoyote (kwamba mlinzi m1 wa Osama alitandikwa mkwaju akafariki na kisha kikosi cha FBI kikamfikia Osama.)
Tunaambiwa Osama alijeruhiwa vibaya, mara tena tunaambiwa Osama hakujeruhiwa bali alimtumia mkewe kama ngao.
Tunaambiwa makazi ya Osama yalikuwa ya ghali zaidi ya $1 million, ukweli ni kwamba kilikuwa ni kakibanda cha ovyo hata hakifiki robo ya huyo pesa.
Taarifa alizotoa Obama na maafisa wa usalama na intelijensia zilikuwa zinapishana sana.

☆Kutupa mwili wa Osama baharini.
Baada ya watu kushambulia kitendo hiko, Obama aliibuka na kusema kwamba walifanya hivyo kufuata utaratibu wa Ibada ya mazishi ya kiislam. Lkn wanazuoni wa kiislam wakapinga vikali hoja hiyo wakidai kwamba muislam anaweza tu kuzikwa baharini endapo alifia baharini.

☆Uchunguzi wa sayansi wa vinasaba na sura.
Viongozi wa usalama walidai kwamba vipimo ya DNA na uchunguzi wa sura (facial recognition) vilifanyika ili kuhakiki pasi shaka kuwa mwili ule ulikua ni wa Bin Laden. Je ni kwanini vithibitisho hivi havijawahi kuwekwa popote hadharani?

☆Kughushi picha ya chumba cha matukio (situation room).
Ikulu ilitoa picha ya ikulu ikimuonesha Obama, H. Clinton, Joe Bide na staff wengine wa ulinzi wakifuatilia shambulio lililomuuwa osama. Lakini baadae mkuu wa CIA, Leone Panette alikiri wazi kuwa Obama na team yake wasingeweza kushuhudia shambulio hilo 1 kwa 1 (live feed) kwani mitambo ya kurekodi tukio hilo ilizimwa ili isiingiliane na mawasiliano eneo la tukio.
Picha hii iliundwa mahsusi kumpa obama kiki ya kihistoria.View attachment 445114

☆Tamko la Al-Qaeda.
Vyombo vya habari viliripoti kua Al-Qaeda wenyewe wamethibitisha kuuwawa kwa Osama. Lakini mchezo huu ulisukwa na shirika liitwalo SITE ambao ni mtandao maalumu wa kupika propaganda za shambulio la Pentagon. SITE ipo chini ya binti wa shushushu wa Israel mara kadhaa wamekuwa wakidakwa kutengeneza video kwa kutumia utaalamu wa juu kulingana na matakwa ya serikali.

☆Majirani wa mjengo wa Osama.
Majirani wa Osama ktk kijiji cha Abboltabad hawajawahi kuhisi tetesi zozote juu ya uwepo wa Osama hapo. Hata jeshi ya Pakistani ambalo lipo jirani walishindwa kung'amua uwepo wa Osama pia. Obama pia alithibitisha kua hawakuwa na uhakika 100% kuwa Osama alikuwa ndani ya lile jengo (ni kama kamari). Yawezekana waliuwa mtu tofauti kabisa na kuamua kuutangazia ulimwengua kuwa wamemuuwa osama ili kuficha aibu.

☆Osama alikuwa ni asset.
Asset katika dunia ya kiinteligensia ni kitu chochote chenye thamani/value ya kuweza kudukua taarifa muhimu. Gaidi aliyekamatwa porini ndiye aling'amua wapi Osama alipo, alikamatwa na kuhojiwa kwa mateso (torturing interrogation) ndipo akafunguka. Iweje Osama ambaye alikuwa gaidi most wanted na biggest asset asikamatwe ahojiwe ili kung'amua taarifa za ugaidi wa ulimwenguni. Moja kwa moja aliuwawa wakati lengo la Marekani lilikuwa kumkamata akiwa hai (kwanini walimuuwa wakati kulikuwa na uwezekana wa kumkamata akiwa hai).

☆Mbinu ovu za serikali ya Marekani.
Mara kadhaa serikali ya marekani imeshtukizwa kusuka mipango ya kijeshi ili kujiongezea sifa za kivita kimataifa mfano tukio la kumuokoa Jessica Lysch walipika mpango kufanya kama alitekwa na wanamgambo wa Iraqi na kisha jeshi la marekani likamwokoa (sawa na kujitekenya) pia hata kifo cha Pat Tillman yote ni mbinu za kughushi. Pia siku za usoni nitazungumzia moja ya matukio ya aina hii yaliyoidhalilisha marekani (oparesheni Misitu ya kaskazini).

☆Pia naandika uzi huu najiuliza je ni kweli Osama alikua na ulinzi dhaifu kiasi kile? Ni kwanini marekani walifanya shambulio hili bila kuwashirikisha viongozi wa usalama wa Pakistan.

HITIMISHO:
Obama, ikulu ya marekani, taasisi na mashirika ya ujasusi ya marekani na viongozi wa usalama wa Marekani hawajawahi kutoa tamko la kupinga/kukanusha filimbi aliyopuliza Bw. Snowden (Obama alijitahidi kujibu baadhi ya hoja za Snowden lkn suala la kifo cha Osama hajawahi kuligusa).

Niseme tu, taarifa za kuuwawa kwa Osama na kikosi maalumu cha Navy SEAL unit 6 ni jambo la kutiliwa wasiwasi na ni vizuri tujiulize kwa mapana zaidi.
Snowden kwanza alitoa Siri zake akiwa Hong Kong na kulikuwepo jitihada kubwa sana kumkamata na kumpeleka marekan lakin china walikataa kumkamata ndio urusi ikatoa ofa ya kumpa hifadhi ya muda na c kwamba alitorokea urusi kutoka marekan nilikuwepo Hong Kong wakat wa hilo saga. Na kwa kipande hicho kidogo cha uongo siiamin tena story yako yote.
 
Kuhusu Osama kuwa hai ,snowden kalishwa maneno

Kama kweli angesema basi vyombo vya habari duniani vingesimamia kidete kutangaza na ingekuwa hot news

Lakini chanzo cha taarifa hyo ni blog ambayo hata haijulikani

Kwahyo Snowden hakuwahi kusema Osama yupo hai ,alilishwa tu..hoax
Mkuu sidhani kama ni kweli kuwa leak ya Snowden kuhusu kifo cha Osama ilitokea kwenye blog ya uchochoroni. Mimi nahisi Marekani iliingilia kati utata huo usisambae sana, kwasababu ukifuatilia kwa karibu vituo vikubwa vya matangazo kama cnn, snopes, world daily news, daily mail, independent, huffpost, bbc nk walireport, lakini baada ya Marekani kuintervene haikusambaa.
 
Snowden kwanza alitoa Siri zake akiwa Hong Kong na kulikuwepo jitihada kubwa sana kumkamata na kumpeleka marekan lakin china walikataa kumkamata ndio urusi ikatoa ofa ya kumpa hifadhi ya muda na c kwamba alitorokea urusi kutoka marekan nilikuwepo Hong Kong wakat wa hilo saga. Na kwa kipande hicho kidogo cha uongo siiamin tena story yako yote.
Ila kunukuu habari yote hiyo ni uhuni.
 
upo vizuri mkuu....
the bold
complex
mnanichkulia muda wangu mwingi,kunipa manufaa ya ulimwengu wa kijasusi....nawakubali sana..
 
Hapa kama vile naangalia movie napenda sana issue za kiintelijensia ila mimi nina maswali zaidi wakuu wangu....Hivi huyu kijana Snowden Urusi ndio inampa kiburi au?Je anauza information anzotoa na kama anauza basi atakuwa millionaire...Sijajua mwisho wake utakuwa ni nini na sipati picha makazi yake yalipo dahhh labda pangoni au keshafanya plastic surgery......wakuu tuekimishane
tatizo hadi mifumo na logistic za kijasusi za ufuatiliaji wa kina kwa anaehitajiwa na US kwa udi na uvumba....zipo kwa kichwa chake....
maana yake hapo...mitego na mbinu zote edo anazujua....kumbuka jamaa ni most genious ktk vijana wa hivi karibuni waliowahi kutokea marekani...!!..NSA.. walimbaini wakamuongezea maujuzi zaidi......kapita cia,fbi,nas na secret service kote huko tena idara zote ni nyeti......ni kazi kdg ifanyike mpaka wamtie mikononi hao us....
 
MKUU hongera kwa uzi mtamu, umetoa maelezo yanayoeleweka

Ila ktk haya mambo kiukweli naona kuujua undani inakuwa kitendawili hasa kwa mtu wa nje. Unapogusa suala la USALAMA wa taifa flani, operations za kijeshi/usalama + siasa haya ni mambo yanayobeba usiri wa hali ya juu sana. Kuna operations nyingi sana za kiusalama zinaweza kuandaliwa ila hata hao wanajeshi wanaoenda ktk hiyo operations wasijue kitu mpaka siku ya tukio.

Maana yangu nin nin basi..
Kuna vitu vinawezafanyika ktk Taifa na vikahusisha idara nyeti sana lakini nyuma yake ni vitu ambavyo vinafanywa kwa maslahi ya Taifa, inawezekana pia ikawa ni kwa maslahi ya kiongozi flani au hata chama flani ila waliopewa order wasijue au wakajua wachache sana.

Unaweza kujiuliza kama ulimwengu umeaminishwa kuwa aliyeaminika ni Gaidi tishio OSAMA BIN LADEN aliuwawa ktk Operation Neptune Spear then mtu wa ndani kabisa aje na vielelezo kuwa yu hai, huoni kama kuna maswali mengi na ukweli umefichika..!?

Kitu kingine Edward Snowden alikuwa kijana mdogo sana ndani ya Intelligencer ya marekani na alikuwa nacheo ktk upande wa IT, alikuwa analipwa vizuri sana na alipelekwa course tofauti tofauti kumjengea uwezo wa kazi kwa maslahi ya Taifa so unadhani ni rahisi tu kuasi na marekani itulie tu!??

NOTE:
Taifa kama marekani linataka kujiimarisha katika kila idara kila kukicha
Marekani pia inawapinzani kila pande ya dunia...
Je haiwezekani kuwa kuasi kwa Snowden pia ikawa ni mpango wa marekani kumtumia ktk nchi anazokuwepo aweze kuchukua information na kuzituma marekani?
(Usisahau kuhusu double Agent, sleepers Agent nk)

HITIMISHO
Siri ya mtungi aijuaye Kata..!!
 
Hizi story za ki spy ni za ajabu kweli. Inawezekana akawa kaambiwa na C.I.A/FBI atorokee huko Russia nao Russia bila kujua wakampokea na sasa yupo kazini kwa ajili ya marekani.

Au Russia wao ndio waliomwandaa na kumwezesha kujiunga na mashirika ya kijasusi ya marekani. Na sasa baada ya kupata taarifa zote muhimu kuhusu marekani kakimbilia kwa jamaa waliomtuma kufanya aliyotakiwa kuyafanya.

jamaa ataishi kwa shida sana aisee.
daahh...nimekuelewa sana mkuu....yawezekana edo anawafanyia counterintell warusi..??....inawezekana pia edo alitumwa na warusi mapema kabisa...!!..hii vita ni ya kiufundi sana....
ngoja tuendelee kufuatilia haya mabandiko..... naenjoy sana..
 
Ila hata mimi nliwah kusoma article flan inaelezea kuwa osama alikufa kwa ugonjwa wa figo mwaka 2001,tena akiwa chini usimamizi wa maafisa wa marekani kwenye kambi ya kijeshi ya marekani nchin saudia..
 
Back
Top Bottom